Kilimo: nilichoona kiteto

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
nilipata fursa ya kwenda Kiteto hivi karibuni.. nimejifunza yafuatayo:

  • Ardhi ya kule ni karibu sawa na bure na bado ipo virgin --ekari inauzwa Tsh 10,000 kwa ekari.. cha kushangaza zaidi kukodisha shamba inakuwa 10,000 kwa ekari vilevile
  • watu wanajitahidi kulima mahindi, maharage, choroko na sunflowers (alizeti) na soko la mazao hayo lipo sana
  • tatizo kubwa la kiteto ni upatikanaji wa maji. Msimu wa mvua mara nyingi ni mmoja. kwa hiyo ukipatia mvua ikanyesha kwa wingi unakula bingo. ikigoma inakula kwako
  • kama mtu upo tayari kucheza na risk unaweza kujaribisha kulima huko (kilichonitia moyo wapo watu wengi wanalima na wamefanikiwa-- MIMI NITAWEKEZA KIDOGO kwanza ili kuona nitapata nini!!!
 
  • Thanks
Reactions: A2G
Asante Kanyagio kwa taarifa.

Hata nami nilipata taarifa za huko hivi karibuni na nimekuwa nikifuatilia uwezekano wa kulima kwa mwaka huu, lakini mpaka sasa sijapata shamba hata la kukodi kwani ninayemtumia ananipa hadithi kila siku. Nategemea kwenda mwenyewe weekend hii; vipi kuna mtu unayemfahamu ambaye anaweza kunisaidia upatikananji wa shamba even la kukodi. Je kwa jinsi ulivyoona itkuwa ni wakati muafaka kwangu kulima mwaka huu au nitakuwa nimechelewa kutokana na msimu wa mvua.
 
Mgombezi, nitakupa feedback as soon as possible, kama kulima ni kipindi hiki ambapo kuna mvua!!
 
je elfu kumi kwa eka,hii unauziwa na kijiji au ni mtu binafsi,angalizo kuna baadhi ya mashamba yalishalimwa sana huko kiteto so rutuba yake ipo chini,hii taarifa nilipewa na rafiki yangu ambaye yupo dodoma na alishawahi kulimisha alizeti
 
Mhh kilimo cha kuvizra mvua hakina tija!bora ununue mazao wakati wa mavuno uyahifadhi ikifika jan au feb unauza bei maradufu!
 
Bongolala,ahsante kwa ushauri

new mzalendo--- ni kweli kuna mashamba ambayo yameshachoka!! ahsante kwa angalizo!! kwa shamba ambalo nimepanga kununua halijatumika kabisa ila lile la kukodisha ndo linaweza kuwa limelimwa sana!!. nitazingatia ushauri wako!!.
 
kilimo cha hukonilikisikia ni chenye mafanikioo sana,lakini kilimo ni kilimo tu ni kucheza na pata-potea,....................
 
mbwamweusi (BLACKDOG) ndo maana na mimi nilisema Kiteto unacheza na risk.. ila kama ukienda sehemu ukakuta katika kijiji kimoja kuna matrekta yasiyopungua 3 na mashamba yanalimwa basi mimi naona ni kiashiria cha kwamba kilimo kinakubali... kwa kweli niliona matrekta 3 hapo katika kijiji kimojawapo hapo kiteto (about 14 km from Kiteto mjini).
 
Je ulidadisi gharama ya kukodi tractor ni kiasi gani kwa heka,na mazingira ya mtu kuja na Tractor lake yakoje?msimu kwa kilimo unaanza mwezi gani.kuna uwezekano nikaja kusurvey kipindi hicho kwa kuja na ka-massey ili kulimisha and the same time kuona uwezekano wa kununua japo ekari70 hivi ,na kwa bei uliyotaja ya elfu 10 itakuwa around 700,000.
 
newmzalendo, [URL="https://www.jamiiforums.com/members/mgombezi.html"]Mgombezi na wengineo[/URL]https://www.jamiiforums.com/members/newmzalendo.html: kulima kwa trekta inaenda Tsh. 30-40,000 kwa ekari kutegemeana na sehemu. ila kumbuka kabla ya kulima na trekta ni lazima ufyeke na kungoa visiki. ekari moja wanafyekea Tsh 10,000/= na unaongezea fedha kidogo ya kung'oa visiki.. msimu wa kulima ndo huu kwa sababu mvua ndo zimeanza.. hutakiwi kuchelewa kwa sababu mvua kiteto ni msimu mmoja (mara nyingi).
 
Asante Kanyagio;

Kama nilivyosema ninaelekea huko weekend hii na tutapashana zaidi.
 
Mhh kilimo cha kuvizra mvua hakina tija!bora ununue mazao wakati wa mavuno uyahifadhi ikifika jan au feb unauza bei maradufu!

Yeah ni wazo zuri lakini ni vizuri kujaribu uwekeza kwenye kilimo pia - Mwaka jana nililima hekari 50 matokeo hayakuwa mazuri.

Kipindi cha mavuno May 2010 Debe la mahindi lilikuwa linauzwa 3,000 had 3500. Sikuwa na pesa za kununua na kuweka stock na kama ningefanya hivyo basi ningepata maradufu kwani kwa sasa debe linauzwa 7000 hadi 7500 Tshs.

Kwa sasa nitayauza mahindi kidogo ambayo nilipata msimu uliopita ili nijiweke sawa kwa msimu huu kwa kupunguza makosa yaliyojitokeza msimu uliopita kama kuchelewa kupanda na kutumia mbegu zisizo bora zaidi.

Kilimo cha Umwagiliaji kinahitaji mtaji mkubwa sana, hatuna njisi kwa sasa ni kutumia tu hizi hizi mvua na neema ya mwenyezi mungu. Kununua mazao na kuweka stock kipindi cha mavuno ni jambo zuri pia ingawa linahitaji mtaji mkubwa ili kupata mafanikio kwa mfano ukinunua mazao ya thamani ya Tshs 50m basi baada ya miezi 8 utapata 100m bila ubishi.
 
Asante Kanyagio;

Kama nilivyosema ninaelekea huko weekend hii na tutapashana zaidi.

Mkuu,
ukirudi toka shamba njoo utumwagie data zote, mimi naomba uangalie vitu vifuatavyo huko porini uendako.

Kaangalie aina ya wadudu wote walioko huko porini
Kaangalie aina ya ndege wanaoishi huko
kaangalie aina ya wanyama wa porini na wafugwao
Kaangalie na aina ya matunda gani yako huko
Na ukiweza tuletee picha za misitu au vipori vya huko

Unaweza kupata haya kwa kuuliza pia.

Asante na safari njema.
 
Yeah ni wazo zuri lakini ni vizuri kujaribu uwekeza kwenye kilimo pia - Mwaka jana nililima hekari 50 matokeo hayakuwa mazuri.

Kipindi cha mavuno May 2010 Debe la mahindi lilikuwa linauzwa 3,000 had 3500. Sikuwa na pesa za kununua na kuweka stock na kama ningefanya hivyo basi ningepata marafufu kwani kwa sasa debe linauzwa 7000 hadi 7500 Tshs.

Kwa sasa nitayauza mahindi kidogo ambayo nilipata msimu uliopita ili nijiweke sawa kwa msimu huu kwa kupunguza makosa yaliyojitokeza msimu uliopita kama kuchelewa kupanda na kutumia mbegu zisizo bora zaidi.

Kilimo cha Umwagiliaji kinahitaji mtaji mkubwa sana, hatuna njisi kwa sasa ni kutumia tu hizi hizi mvua na neema ya mwenyezi mungu. Kununua mazao na kuweka stock kipindi cha mavuno ni jambo zuri pia ingawa linahitaji mtaji mkubwa ili kupata mafanikio kwa mfano ukinunua mazao ya thamani ya Tshs 50m basi baada ya miezi 8 utapata 100m bila ubishi.

Wakuu msisahau kulima migomba. soko la ndizi linapanuka sana kwa sasa.
 
Mkuu,
ukirudi toka shamba njoo utumwagie data zote, mimi naomba uangalie vitu vifuatavyo huko porini uendako.

Kaangalie aina ya wadudu wote walioko huko porini
Kaangalie aina ya ndege wanaoishi huko
kaangalie aina ya wanyama wa porini na wafugwao
Kaangalie na aina ya matunda gani yako huko
Na ukiweza tuletee picha za misitu au vipori vya huko

Unaweza kupata haya kwa kuuliza pia.

Asante na safari njema.

Mkuu Malila pamoja na wadau wengine.

Ni kweli nilitoa ahadi ya kwenda Kiteto weekend iliyopita lakini kutokana na majukumu mengine yaliyojitokeza nilishindwa kutekeleza ahadi hii; hata hivyo kutokana na taarifa ambazo nimekuwa nikizipata kutoka huko ni kwamba msimu wa kulima umekaribia au umekwisha na sasa mahindi yapo kwenye hatua ya kupalilia, nami lengo langu ilikuwa ni kupata uwezekano wa kulima mwaka huu. Hivyo basi najiandaa kufanya ziara ya huko kwa wakati mwingine na ninajiandaa kwa mwakani. Samahani sana kwa wadau waliokuwa wanategemea kupata taarifa za huko, bali kama kuna yeyote mwenye taarifa zaidi tuendelee kujuzana. Vilevile kikao chetu tutakachokutana punde naamini tutapeana taarifa zaidi.
 
hivi kikao ni lini Vile and wapi?inabidi sasa tuwe na email groupe for updates za vikao
 
Wakuu naomba moto tuliouanzisha usipoe kabisa, napendekeza tarehe 5february siku ya jumamosi,tukutane pale Lunch time Hotel, Hotel hii iko opposite na Mabibo hostel barabara ya Mandela, pale pana nyama choma,ulinzi wa kuaminika, parking ipo, kuna kumbi zaidi ya mbili zenye viyoyozi kabisa, kuingia na kutoka kwa wenye magari na waenda kwa miguu ni rahisi sana. Muda uwe saa kumi na mbili jioni ili wengi waweze kufika baada ya kazi zao za mchana.
 
Back
Top Bottom