Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Nanjilinji kwa mzee Lipetelo.
 
Vp ulifanikiwa kupata mashine ya kupandia ufuta mkuu?
 
Mwaka huu nimefanya majaribio ya kulima ufuta wilaya ya Malinyi. Nimelima hekari 10, sijalima kitaalamu badala yake nimelima kama wakulima wa maeneo hayo.

Gharama za uendeshaji kuanzia December 2019 hadi sasa March 2020 ziko kama ifuatavyo;

Kukodi eneo hekari 10@30000 = 300000
Kufyeka/Kusafisha eneo hekari 10@15000 = 150000
Mbegu debe 1 = 100000
Kulima hekari 10@ 50000 (Phase1: 30000@hekari, phase2: 20000@hekari) = 500000
Kupalilia hekari 10@25000 = 250000
Dawa ya kupulizia wadudu, kopo 5@5000 = 25000
Gharama za matumizi ya msimamizi hadi sasa 100000.
Jumla ya gharama zilizotumika kuhudumia hekari 10 hadi sasa ni Tsh 1425000.
Pia kuna gharama za uvunaji zitaongezeka msimu wa kuvuna ukifika.

NB: Sikutaka kuanza na kilimo cha kitaalamu kutokana na changamoto za usimamizi kwani usimamizi uko chini ya watu ambao mostly wanalima kilimo chetu cha kitanzania. Hivyo kwa majaribio nimeona nianze hivyo kwanza ili tuweze kuzungumza lugha inayoendana na wenyeji wangu walioko mashambani then huko mbele ndio ninaweza kulima kwa kufuata kanuni za kitaalamu kama nitaona inafaa.
 
Vp maendeleo yapoje mkuu?
 
Vp maendeleo yapoje mkuu?
Tunamshukuru Mungu maendeleo ya mazao yanatia moyo, tuna matumaini ya kupata.

Kwa hali ya hewa bado inasapoti kulingana na nature ya maeneo niliyolima, japokuwa mvua zinanyesha sana ila maeneo niliyolima hayatuamishi maji ni maeneo ya juu kidogo hivyo athari za mvua hazijaonekana sana hivyo matumaini ya kupata yapo.

Changamoto ninayoiona saivi ni wadudu wameanza kuonekana kwenye ufuta ila ni wachache na nimeshanunua dawa na wiki hii nitapulizia ili kuwadhibiti.
 
Kila la kheri mkuu
 
Mkuu,kwa makadirio ekari Mona inaweza kutoa kias gan(debe ngapi) Cha ufuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upepo huu wa Corona ufuta utalipa kweli mwaka huu? Mana wanunuaji wakubwa ndo hao wanapata tabu.
 
Mkuu,kwa makadirio ekari Mona inaweza kutoa kias gan(debe ngapi) Cha ufuta?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwangu hii ni mara yangu ya kwanza kufanya kilimo hiki. Ila niliambiwa kuwa inaweza kutoa debe 12-18. Jibu sahihi kabisa nitakalokuwa na uhakika nalo nitalipata nitakapovuna maana hayo ndio yatakuwa matokeo halisi ya kutoka field kwa experience yangu mwenyewe.

Labda kwa wadau wenye experience na kilimo hiki wanaweza kutusaidia kupata jibu la uhakika zaidi maana wakati mwingine hali ya hewa, aina ya ulimaji pia inaweza kuchangia kupungua/kuongezeka kwa mazao.
 
Nimekuwepo lindi- Liwale huko wanapata debe 24- 36 kwa heka pia huku songwe maeneo ya mkwajuni napo kipato kipo hivyo pia ukienda maeneo ya bonde la ziwa rukwa napo wengi huwa kipato kina range kwenye debe 18-36

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…