Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by C.K, Feb 19, 2011.

 1. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Jamani habarini za wikiendi, naomba kujua mche wa tikiti maji unaweza kuvunwa mara ngapi matunda yake?

  Kwa mfano embe zinavunwa kila mwaka, ndizi unavuna mara moja tu na mche unakwisha kazi yake. Vipi kwa matikiti maji, unavunwa mara ngapi na kwa kipindi/interval gani?

  Nataka kulima, yanalipa sana nisaidieni tafadhali.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  mkuu ... water melon inafanana kabisa na mzao wa maboga .... unaotesha mbegu na hakuna transplantation ..... huwa linaota na ktambaa kama maboga na kutoa maua jinsi linavyokua ..... linaanza kuzaa matunda na kuvunwa kadiri yanavyokomaa ..... msimu ukiisha linakufa
   
 3. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Asante sana mkuu kwa response nzuri
   
 4. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,584
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  Wakubwa mimi nina swali moja, jee mbegu kutoka north america zinaweza kumea vizuri hapa nyumbani?
   
 5. Mzee Dogo

  Mzee Dogo JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 377
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Haina shida, uwe na maji ya kutosha lakini pia uwe makini na timing ya mvua si nzuri sana kwayo hasa kipindi cha mavuno yakinywa maji sana huwa yanapasuka yenyewe
   
 6. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,351
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  chonde chonde kaka,usizilete hizo mbegu,it may cause GM contamination,wasiliana na wataalam wa kilimo watatoa ushauri mzuri.ila bora uziache huko huko,hizi za kwetu ni poa sana tu.
  wajapan wametengeneza watermelon la square kama box ili iwe rahisi kusafirisha matunda hayo,Mh! madhara yatajulikana baadae,ktk cancer na magonjwa mengineyo.
   
 7. G

  George Upina Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Matikiti ni matunda, japo tunasema ni mboga kutokana na njia zinazotumika kuyazalsha kwan siyo tofaut na mboga.

  Matunda yanaanza kukomaa kuanzia siku 80-120 kufuatana na aina, kama sugarbaby inakomaa mapema. Na il kupata matunda makubwa na yenye ubora, tunashaur kwa mti mmoja usiwe na matunda zaidi ya matano ambayo interval ya kuvuna ni siku hadi 10 kwani uvunaj ni had miezi miwil kwa mti mmoja. Hector 1=8-12 tan za matunda.

  Kwa maswali zaidi kuhusu kilimo cha mazao tuwasiliane.
   
 8. G

  George Upina Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aksante kwa swal lako, mbegu hizo zitaota vizuri kwani tunatoa mbegu kutoka huko na tunakuja kuzizalsha Tz halafu zinaenda kuuzwa huko tena, lakini hakikisha unaziotesha kitalun kwanza kabla ya kuzpeleka shamba kwan zaweza zisiote vzr.

  Tumia samadi kuziotesha na zipe joto la kutosha kwa kufunikia kitalu, maji yasiwe meng maana zaweza kuoza, na baada ya siku saba mpaka 14 miche itakuwa tayar kwenda shamban.

  Aksante.
   
 9. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Naombeni msaada kwa watalaam wa kilimo! Nataka kuotesha miche ya tikiti maji 10,000/= mkoani Shinyanga je,
  1. Itanigharimu kiasi gani kuitunza hadi ikue na kufikia mauzo??
  2. Shamba ninalo ekari 3 je litatosha??
  3. Mbegu zake zinapatikana wapi zaidi??
  4. Soko la tikiti maji sasa zuri liko mkoa gani?
  5. Angalau kwa kiwango cha chini tikiti moja naweza kuiuza kwa shliingi ngapi??
  Asanteni wapendwa!
   
 10. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,049
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Bila shaka hata tikiti lenyewe hulijui. Laiti ungelikuwa unalijua usingehangaika pa kupata mbegu.
  Matikiti yanahitaji maji mengi na mbegu zake waweza zipata kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.
  Soko lake haswa ni pale wewe ulipo. Ukitoa matikiti Shinyanga na ukiyapeleka Dsm kuna uwezekano mkubwa yakaharibikia njiani kwa sababu ya mkandamizano na joto.
   
 11. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Asante ndugu yangu ka jibu lako zuri licha ya kwamba umeanza kwa kunisaga kidogo sina shida! Ubarikiwe
   
 12. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ninayo business plan ya kilimo cha water melon!.. Ila iko planed zaidi kwa infrastructure za Dodoma cjui kama itakufaa!..
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,774
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 180
  we mwaga maujanja. Isipomsaidia yeye itasaidia wengine.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,824
  Likes Received: 19,334
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono mia kwa mia.
   
 15. Niko

  Niko Member

  #15
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ushasikia mtu ametajirika kwa ukulima?
   
 16. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu itanifaa sana tena napenda mkuu nisaidie pliz mkuu!
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,824
  Likes Received: 19,334
  Trophy Points: 280
  Zaidi ya 80% ya matajiri duniani ama wametajirika kwa ukulima ama wametajirika kwa mazao ya ukulima.
   
 18. Z

  Zahor Salim Member

  #18
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Tunaisubiri kwa hamu hiyo business plan
   
 19. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,394
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Tikiti ni zao la bustani(horticultural crop) hivyo uangalizi wa karibu ni muhimu linastawi maeneo mengi ya nchi laki i linastwi vizuri udongo wa kichanga. linakomaa baada ya 56Days. Kwa Shy Bukombe na Kahama kuna soko kubwa sana maana wanachukua tikiti kutoka Ruanda na burundi kwa maelezo ya kina na Business Plan kama utahitaji unakaribishwa kunipm
   
 20. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Thank you check my Pm
   
Loading...