Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Chief, Mar 2, 2012.

 1. C

  Chief JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Msaaada tafadhali wajemeni. Nina shamba mahala ambapo nataka kupanda miembe. Ushauri? Wapi ntapata miche ya miembe?

  Nipo Dar
  Imeboreshwa zaidi:
   
 2. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nenda maeneo ya kurasini zilipo ofisi za WAPO REDIO nyuma ya chuo cha maafisa wa Polisi nasikia kuna miche inauzwa hapo. Thanks
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ukipata hii mifupi ni mitamu na ina soko sana!

  MAEMBE.jpg MAEMBE TENGA.jpg
   
 4. B

  Bobby JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  PJ thanks! Hii inapatikana wapi?
   
 5. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,042
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Panda miembe ya kawaida inayokubali eneo ulipo halafu ndo uwaite jamaa wakufanyie cross-pollination. Hii ni cost effective and sustainable pia. Mimi nimefanya hivyo
   
 6. C

  Chief JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nakushukuru sana Fmewa:

  Nyati: Wewe ulipata miche wapi au ulipanda mbegu (kokwa) za embe?
   
 7. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,549
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu salam u nyingi na karibu kwenye kilimo

  Wauza miche ni wengi sana Dar es Salaam na kwingineko lakini wauzaji miche bora ni wachahche sana.
  Hivyo ni vema ukafahamu mahali pa kupata miche bora( ya kiisasa ama ya kienyeji iliyoboreshawa)

  Kwanza kabisa Tambua mbegu bora: Kuna aina kama 17 ya mbegu bora za embe kwa ajili ya matumizi na masoko
  tofauti. Hivyo tambua kwanza soko lako linataka nini kisha chagua mbegu iendanayo na soko/matumizi yako.

  Kuna mbegu kama sita ivi kwanza BOLIBO (ya kienyeji lakini iliyoboreshwa), Kuna alfonso, Keit, Kent, Apple ambazo
  ni tamu hazina nyuzi nyuzi nyingi, zina zaa sana kati ya tunda 400 - 3000, ukubwa wake ni 0.25kg - 1.3kg nk.

  Hivyo kabla hujaenda kununua hizo embe ni vyema ukatambua sifa ya kila mojawapo (hata ukigoogle utapata).

  Wauzaji kama nilivyosema wapo wengi ila kuna association of Mango growers (AMAGRO) wapo mtaa wa Mkurumah karibu petrol station wale wanawajua wadau wenye vitalu vyenye mbegu za uhakika nchi nzima. Mimi nafahamu wachache
  1. Dr. Diwani anacho kitalu Kinondoni karibu na makaburini na ni Mkulima mkubwa sana wa embe wilayani Mkuranga hivyo yeye anazo mbegu za Uhakika.

  2. Kuna kitalu Rufiji - Kibiti kinamilikiwa na kikundi cha wakulima (Rufiji Environmental Group) ambao walipata tuzo mwaka jana Nanenane ukifika kibiti karibu na kituo cha polis utaona bango lao

  3. Chambezi Research Sub station kipo bagamoyo 5km kabla hujafika bagamoyo kuna kibao chao on the left hand side uningia ndani about 3km wana aina karibu zote 17 za embe za kisasa

  4. SUA wanazo hizo mbegu pia unaweza ukazipata ingawa zitakua ghali kidogo

  5. Mkuranga Research substation nao wana mbegu bora za miche ya miembe wapo few km (3-5) kutoka njia ya kwenda halmashauri ya wilaya ya mkuranga.

  Angalizo: Wapo wajasiriamali wengi wanauza micha ya embe wengine kweli ni nzuri na za uhakika lakini wengine wameiga tu na kuingia kwenye hiyo fani.

  Mfano: ukiotesha kokwa la embe yeyote linalozaa sana halafu ukaweka kikonyo cha embe bora halafu ikatokea chipukizi chini ya sehemu iliyoungwa(grafting) kama lisipokatwa na kuachwa na ikitokea kikonyo kilichoungwa kimekauka mche utaendelea kuwa wa kienyeji na sio wa kisasa.

  Nawakilisha
   
 8. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,042
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Miembe ipo maeneo mengi. Kwa upande wangu, kwangu kulikuwa na mwembe unaozaa sana hivyo nikaomba ushauri wa mbegu mzuri toka kwa mtaalamu aliyekuwa anapajua kwangu. yeye ndo aliyenipa ujanja huo. Hiyo kokwa nilichukua pale pale kwangu na vile vile miche yote iliyokuwa inajiotea pale chini ya ule mwembe nayo iligeuzwa miche ya kisasa.
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  watembelee sua kuna kila aina ya mbegu na ushauri
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wakuu, hivi ni wapi soko kubwa la embe? Mahitaji ya soko yako vp, zinazopatikana ni kiasi gan na zinatoka wapi?
   
 11. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  soko ni ubunifu tu, kama unataka soko la uhakika ingia contract na hotel kubwa kama mimi ili uwe unasupply matunda (may be kwa mwaka mzima) vinginevyo itakuwa ni hasara kwako coz msimu wa embe ukifika bei huwa inashuka sana
  pia tumia artificial ways ambazo zitakufanya uwe unavuna matunda kipindi ambacho si cha msimu wa embe [bei uwa ipo juu sana kipindi hiki]
   
 12. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  bei ya mche ikoje Mkuu?
   
 13. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,549
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Bei inarange kati ya 2000 na 3500 mkuu
   
 14. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,549
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Wakuu

  Nimepita Kibiri kwenye kile kikundi cha wakulima wa kitalu cha embe. I tell you wako vizuri saaaaaaana kuliko hata nilivyo tarajia.

  Wameanzisha kampeni yao ya '' Lima miti kumi ya embe upate Shillingi millioni moja. Kampeni yao ni kwamba nunua miche kumi (30,000) chimba mashimo na kuweka samadi (5,000x10= 50,000), mwagilia kwa mwaka ni assumption dumu moja miche 5 na dumu moja la maji ni TZS 300 na kwa wiki nyeshea mara 2 (2x2x300x52 = 62,400) na garama nyinginezo 30,000. Jumla 172,400

  Mapato: kila mti unayo potential ya kuzaa hadi embe 3,000 kwa msimu lakini wao wamechukua average ya 500/tree
  hivyo unaweza kupata embe 5,000 kwa miche kumi na kila mmoja unaweza kuuza kwa sh 300 = 1,500,000 ukitoa garama laki 2 unapata faida ya sh 1.3million minimum.

  Eneo kwenye compaign yao wanasema hata kama kuna eneo la bustani kima 5 meters kuzunguka nyumba yao unaweza kuotesha embe utapata kivuli lakini pia matunda yake ni fedha.

  Naomba tuwaunge mkono. wao ni wakulima wadogo wa miche bora ya embe (Dodo, bolibo, Tommy, Keit, Kent, Alfonso, red Indian, Palmer, n.k) pia wanatoa ushauri kwa kweli nimevutiwa nao saaaaaaaaaaaaaana.
  sikutarajia kama ningeweza kupta elimu niliyopata kwao, ukipata nafasi ya kuwa KIBITI

  please pita kwenye hiki kikundi ujionee.
   
 15. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Inachukua muda gani tangu kupanda hadi kuvuna miembe ya kisasa?
   
 16. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  google mango growing in kenya, utapata pdf document ya page 122, Itakusaida sana kujua aina za maembe na uzalishaji. Kwa bahati mbaya kwa tz ni 2 pages only na hazina details nyingi. Thanks
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  this is a great opportunity indeed, for those who have land, i have 14 acres on a flat land in moshi and i have witnessed mangos doing very good yields around this region

  changamoto ni maji kwa ajili ya kunyeshea miembe hii ikiwa bado midogo kipindi cha kiangazi, maji ya mto mdogo yapo about 1.5kilomenters

  i have no any worry about the market ..... naomba ushauri
   
 18. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  hata mkuu wangu hapa ana bonge la shamba la miembe huko bagamoyo,
  ukinitafuta pembeni nitakupa namba ili uweze kucommunicate naye.
   
 19. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiki kilimo ni kizuri, pia waweza anza na hata miche michache hata 20 kisha ukaendelea taratibu.

  tunaweza, anza kwa kuwasiliana na hizo contact ulizopewa.
   
 20. n

  ngoshas JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Miaka mitatu, hapo utapata kiasi tu, miaka mitano ndo unaanza kupata faida kamili, hapo ndo unaweza kupata hadi matunda 3000 kwa mti mmoja
   
Loading...