Story of Change Kilimo cha Alizeti ni Utajiri

MTEGULE

Member
Jul 16, 2021
15
45
PATA FAIDA KUBWA KUPITIA KILIMO CHA ALIZETI. KWA MTAJI WA LAKI MOJA NA AROBAINI (140,000) KWA HEKALI MOJA NA KUPATA ZAIDI YA MILLION MOJA NA LAKI NNE (1400,000/=) KWA SIKU TISINI (90).

Ndugu Wapendwa hapana shaka ya kuwa mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.Ikiwa ni tofauti basi Mungu akufanyieni wepesi na mrudi katika hali zenu njema za awali.

Leo ningependa kuwapa mbinu au njia bora ya kuongeza kipato kwa kulima zao la alizeti kwa kutumia kiwango kidogo mnoo cha pesa ambacho ni laki na arobaini tu (140,000/=) na kuweza kupata faida zaidi ya millioni moja na nusu (1500,000/=) kwa siku tisini (90).Natambua kuwa una hamu na shauku ya kutaka kufahamu ni kwa namna gani kilimo hichi kinafanyika.

Alizeti ni miongoni mwa zao muhimu sana ambalo hutoa mafuta mazuri yasiyo na lehemu kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu ya kila siku. Alizeti ni zao linalolimwa hasa maeneo ya ukanda wa kati hapa Tanzania kama vile Dodoma, Singida, Manyara na hata Tabora.

Alizeti ina sifa ya kustahimili ukame na ndiyo maana utaona hata mikoa ambapo hulimwa zao hilo haina sifa ya uwepo wa mvua nyingi.

Zao la alizeti limekua na soko kubwa mnoo hapa Ulimwenguni kutokana na uhitaji wake mkubwa, sambamba na hayo mwaka 2017 Tanzania ilitangazwa kuwa ni nchi ya pili katika uzalishaji wa zao la alizeti hapa barani Afrika.

Moja kwa moja nielekee na nieleze ni kwa namna gani unaweza kutumia mtaji kidogo sana na kuongeza faida maradufu ndani ya siku tisini.

Katika jimbo la Kibakwe, wilaya ya Mpwapwa iliyopo mkoani Dodoma..hii fursa adhimu ndipo inapatikana.Kwanza ifahamike kwamba katika vijiji mbalimbali vinavyopatikana jimbo la Kibakwe mfano.Chamtumile,ikuyu,chogola,winza,makose n.k) ardhi kwa ajili ya kilimo cha alizeti inapatikana ya kutosha na ni kwa bei rahisi mnoo.

Mchakato wenyewe uko hivi:

(i)Mbegu nzuri lita 2 ni Tsh 20000/=

(ii) Kukodi shamba hekali moja ni Tsh 20,000/=

(iii) Kusafisha shamba(Kuberega) hekali moja ni Tsh 10,000/=

(iv) Kulima na jembe la plau (Kutifua) hekali moja ni Tsh 20,000/=

(v)Palizi ya kwanza na ya pili..ni Tsh 20,000/= kwa hekali moja.

(vi) Kukata, kuzipiga, usafirishaji mpaka mashineni ni Tsh 50,000/=.

Jumla ya gharama zote ni Tsh 140,000/= .

Kwa kawaida hekali moja ya alizeti hutoa gunia 12 hadi 15 kwa makadirio ya chini. Na katika maeneo ya huko huko zipo mashine maalumu kwa ajili ya kukamua alizeti na bei yake huwa ni chini sana na kama unayaacha mashudu huwa hakuna tozo yoyote.

Lakini pia, ifamike kwamba Gunia moja la alizeti ambazo huwa ni debe 6 tu. Hutoa mafuta kuanzia lita 18 hadi 25(Kwa makadirio ya chini) kutokana na vile alizeti ilivyokomaa.

Hivi sasa lita moja ya alizeti ni Tsh 7000/=kwenye maeneo mengi ya mjini lakini tujaalie wewe utauza kwa Tsh 5000/= kwa lita kwa sababu ni mali yako toka shamba.

Ikiwa umepata gunia 13 kwa hekali moja, kila gunia ukapata lita 22 za mafuta(Kwa makadirio ya chini) utakuwa na lita jumla 286 ukizidisha kwa (5000/=) utapata Milioni moja laki nne na elfu thelathini TSH 1430,000/=

Tsh 140,000/= Hadi Tsh1430,000/=

Faida iliyopatikana ni milioni moja laki mbili na tisini Tsh 1290,000/= kwa siku tisini (90).

Naomba kuwasilisha.
 
Upvote 8

mazagazagatza

Senior Member
Jul 15, 2021
104
225
Mkuu Mtegule,mbona kama uko too theoretical?

Be honest,umeshawahi kufanya hiki kilimo cha alizeti au unasoma kwenye makaratasi na kusikia stori?

Hizo mbegu za kupima kwenye plastic ukamue upate lita 22/60kg gunia la alizeti ni aina gani?

Je, unapata wapi labour ya kupalilia ekari moja kwa shilingi 10,000/=? Mtu mmoja anaweza kutumia masaa managi kupalilia ekari moja?
 
harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,971
2,000
Hapo kwenye Lita moja ni 7000 ndio nmegundua we ndio mwanzilishi wa kilimo Cha matikiti kwenye makaratasi.

Kwanza hujui nn maana ya kilimo na biashara.

unaweza ukaingia shambani Lita ikiwa 10,000 ukatoa mzigo shambani ukakuta Lita ni 1500,Cha kufanya wape watu mbinu za kulima lakini swala la bei achana nalo labda Kama mnunuzi utakua wewe!
 
MTEGULE

Member
Jul 16, 2021
15
45
Mkuu unafanya hii biashara? Ingekuwa na uwalisia kama ungetoa mfano wa wewe binafsi,hiki kilimo cha makaratasi huwa si aliasia sana
Ushauri wako mzuri kaka..shukrani sana ndugu Yangu..ila ningependa kukuweka wazi kuwa mimi ninaishi kwenye hiyo jamii na mimi ni shuhuda wa hayo.. nimefanya hivyo kwanza watu watumie fursa katika kilimo hicho hasa maeneo ya huku kwetu maana gharama za Ukodishaji,uandaaji na michakato yote ya shamba ni chini sana..
 
MTEGULE

Member
Jul 16, 2021
15
45
Hapo kwenye Lita moja ni 7000 ndio nmegundua we ndio mwanzilishi wa kilimo Cha matikiti kwenye makaratasi.

Kwanza hujui nn maana ya kilimo na biashara.

unaweza ukaingia shambani Lita ikiwa 10,000 ukatoa mzigo shambani ukakuta Lita ni 1500,Cha kufanya wape watu mbinu za kulima lakini swala la bei achana nalo
Maneno yako ya mwanzo si sahihi cha kusema mimi ndiye mwanzilishi wa kilimo cha matikiti kwenye makaratasi dai hilo si sahihi.

Lakini pia, Shukran sana kwa kunipa ushauri hapo mwishoni..Mungu akubarik sana Mkuu.
 
mkombengwa

JF-Expert Member
Dec 4, 2011
2,401
2,000
PATA FAIDA KUBWA KUPITIA KILIMO CHA ALIZETI. KWA MTAJI WA LAKI MOJA NA AROBAINI (140,000) KWA HEKALI MOJA NA KUPATA ZAIDI YA MILLION MOJA NA LAKI NNE (1400,000/=) KWA SIKU TISINI (90).

Ndugu Wapendwa hapana shaka ya kuwa mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.Ikiwa ni tofauti basi Mungu akufanyieni wepesi na mrudi katika hali zenu njema za awali.

Leo ningependa kuwapa mbinu au njia bora ya kuongeza kipato kwa kulima zao la alizeti kwa kutumia kiwango kidogo mnoo cha pesa ambacho ni laki na arobaini tu (140,000/=) na kuweza kupata faida zaidi ya millioni moja na nusu (1500,000/=) kwa siku tisini (90).Natambua kuwa una hamu na shauku ya kutaka kufahamu ni kwa namna gani kilimo hichi kinafanyika.

Alizeti ni miongoni mwa zao muhimu sana ambalo hutoa mafuta mazuri yasiyo na lehemu kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu ya kila siku. Alizeti ni zao linalolimwa hasa maeneo ya ukanda wa kati hapa Tanzania kama vile Dodoma, Singida, Manyara na hata Tabora.

Alizeti ina sifa ya kustahimili ukame na ndiyo maana utaona hata mikoa ambapo hulimwa zao hilo haina sifa ya uwepo wa mvua nyingi.

Zao la alizeti limekua na soko kubwa mnoo hapa Ulimwenguni kutokana na uhitaji wake mkubwa, sambamba na hayo mwaka 2017 Tanzania ilitangazwa kuwa ni nchi ya pili katika uzalishaji wa zao la alizeti hapa barani Afrika.

Moja kwa moja nielekee na nieleze ni kwa namna gani unaweza kutumia mtaji kidogo sana na kuongeza faida maradufu ndani ya siku tisini.

Katika jimbo la Kibakwe, wilaya ya Mpwapwa iliyopo mkoani Dodoma..hii fursa adhimu ndipo inapatikana.Kwanza ifahamike kwamba katika vijiji mbalimbali vinavyopatikana jimbo la Kibakwe mfano.Chamtumile,ikuyu,chogola,winza,makose n.k) ardhi kwa ajili ya kilimo cha alizeti inapatikana ya kutosha na ni kwa bei rahisi mnoo.

Mchakato wenyewe uko hivi:

(i)Mbegu nzuri lita 2 ni Tsh 20000/=

(ii) Kukodi shamba hekali moja ni Tsh 20,000/=

(iii) Kusafisha shamba(Kuberega) hekali moja ni Tsh 10,000/=

(iv) Kulima na jembe la plau (Kutifua) hekali moja ni Tsh 20,000/=

(v)Palizi ya kwanza na ya pili..ni Tsh 20,000/= kwa hekali moja.

(vi) Kukata, kuzipiga, usafirishaji mpaka mashineni ni Tsh 50,000/=.

Jumla ya gharama zote ni Tsh 140,000/= .

Kwa kawaida hekali moja ya alizeti hutoa gunia 12 hadi 15 kwa makadirio ya chini. Na katika maeneo ya huko huko zipo mashine maalumu kwa ajili ya kukamua alizeti na bei yake huwa ni chini sana na kama unayaacha mashudu huwa hakuna tozo yoyote.

Lakini pia, ifamike kwamba Gunia moja la alizeti ambazo huwa ni debe 6 tu. Hutoa mafuta kuanzia lita 18 hadi 25(Kwa makadirio ya chini) kutokana na vile alizeti ilivyokomaa.

Hivi sasa lita moja ya alizeti ni Tsh 7000/=kwenye maeneo mengi ya mjini lakini tujaalie wewe utauza kwa Tsh 5000/= kwa lita kwa sababu ni mali yako toka shamba.

Ikiwa umepata gunia 13 kwa hekali moja, kila gunia ukapata lita 22 za mafuta(Kwa makadirio ya chini) utakuwa na lita jumla 286 ukizidisha kwa (5000/=) utapata Milioni moja laki nne na elfu thelathini TSH 1430,000/=

Tsh 140,000/= Hadi Tsh1430,000/=

Faida iliyopatikana ni milioni moja laki mbili na tisini Tsh 1290,000/= kwa siku tisini (90).

Naomba kuwasilisha.
Bado nazitafakari sana hizi gharama zako mkuu
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,958
2,000
Gharama zako ni za chini sana kuliko uhalisia, bei yako ya mafuta kutoka shamba ni kubwa sana kuliko uhalisia. In fact nimenunua mafuta ya alizeti lita kwa shilingi 5500 hapa Dar, sasa iweje wewe shambani uuze kwa 7000?

Itoshe kusema hakuna uhalisia katika kilimo hiki. Tutarajie kilio kwa atakayefuata mwongozo huu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom