Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,132
- 2,681
Nimevutiwa sana na kilimo cha alizeti hasa ukizingatia mafuta yake ni miongoni mwa mafuta yanayopendwa na watumiaji wengi japokuwa yanauzwa bei ghali
Kwa msimu huu nimefanya majaribio ya kilimo hiki kama sehemu ya kupata uzoefu
Nimeweza kubaini yafuatayo na hapa nitafurahi kama wengine mtaweka uzoefu wenu ili tuendelee kujifunza zaidi;
1. Kilimo cha Alizeti ni rahisi sana kwani kina hitaji kuandaa shamba, kupanda, kupalilia na kuvuna tu
2. Ni kilimo kinachotumia pesa kuanzia stage ya mwanzo hadi unapopeleka kukamua mafuta mashineni
3. Kama kilivyo rahisi, pia ni rahisi kupoteza pesa nyingi sana na zisirudi kwasababu kila hatua inahitaji pesa
4. Soko lake ni zuri lakini bado bei ya mafuta haikidhi kumpa faida mkulima
Kwa mfano, walio wengi niliovuna nao tumepata wastani wa gunia 4 hadi 7 (za debe sita) kwa heka moja ambapo baada ya kukamua mafuta unapata wastani wa lita 16 hadi 20 kwa gunia moja
Kwa bei ya jumla lita 20 inauzwa Tsh.80,000/= hadi Tsh.85,000/=
Kwa mahesabu haya ni vigumu sana kutoboa japo wenye mashine wengi wanakupa option ya kukwepa gharama za ukamuaji kwa kuwaachia mashudu
Je, nyie wenzetu mnapataje faida kwenye kilimo cha Alizeti?
Karibuni mtupe uzoefu weni