Hongera mkuu kwa kufichua matapeli kama haya...!NAMAINGO chini ya umiliki wa bi UBWA ni utapeli mtupu.Huyu mama alianza na taasisi aliyoipa jina la AMSHA na hatimae aliwatapeli wakulima wengi wa mkoa wa Pwani na mikoa ya kusini katika zao la ufuta.Aliwahadaa wakulima wengi kwamba atawasaidia kupata ardhi na masoko ya zao la ufuta na hatimae aliingia mitini.Kwa ushuhuda zaidi nenda katika wilaya ya Kilwa kwa kuanzia kijiji cha Somanga mpaka Lindi vijijini maeneo ya Kiwalala jimbo la Mtama ulizia wananchi kuhusiana na taasisi ya AMSHA.Baada ya plan yake ya kwanza kufeli amerudi tena na NAMAINGO BUSINESS AGENCY na kuweza kuzishawishi taasi kama PSPF,NHIF,NMB na kuweza kuzishawishi kwa kuwa anakundi kubwa la watu analoliongopea ameamua kulitumia kundi hilo kuliunganisha na hizi taasisi kwa kuwapelekea wateja(wadanganyika)na hatimae kunufaika na hizi taasisi kwa kupata commission na ufadhili wa safari zake katika kupitia shughuli za uhamasishaji.Huyu mama bi UBWA amefika mbali hata na kuweza kuwa karibu na viongozi wakuu wa nchi kama makamu wa rais mama Samia Suluhu na kutumia nafasi hiyo kuonyesha ni jinsi gani taasisi yake ilivyopewa baraka zote na serikali.Huyu ni tapeli na shughuli zake alianzia kama mganga wa kienyeji maeneo ya UKONGA lakini ameweza kulishawishi kundi kundi la watu wakiwemo wasomi kwa kuamini atawakomboa kwa kuwapatia ardhi,biashara na fursa za masoko na hatimae anawatumilia kupiga dili.
Kilimo cha mnyororo wa thamani hakipo hivyo utoe laki 7 waache utani nahisi uwo ni upatu wa kilimo,na pia ni eneo gani unafanyia na kutoka chanzo kipi cha maji maana sasa hivi pampu zinanyanganywa uchelewi kulaza mtaji ukabaki na deni la bank au saccos ref. kilimo cha vitunguu ekari 200 klm.Mkuu nimeenda ili uwe mwanachama inakughalimu si chini ya 700,000,
September 30 2016 unazungumzia UJIO wa Namaingo? Mbona ipo muda mrefu sana!Mwana jf ,karibu katika fursa kubwa ya kilimo chenye tija. Ni kilimo cha kisasa kijulikanacho kama vijiji biashara, ni chini ya ujio wa kampuni liitwalo Namaingo Bussness Agency ambapo utasaidiwa utaalam pamoja na soko la bidhaa au mavuno yako! Kwa mawasiliano 0769635970
Kwa ujumla kazi ya kuendeleza wakulima mmeshindwa kabisa, mmekalia kuwavuna kidogo walichonacho kupitia malipo ya semina na vipeperushiMwana jf ,karibu katika fursa kubwa ya kilimo chenye tija. Ni kilimo cha kisasa kijulikanacho kama vijiji biashara, ni chini ya ujio wa kampuni liitwalo Namaingo Bussness Agency ambapo utasaidiwa utaalam pamoja na soko la bidhaa au mavuno yako! Kwa mawasiliano 0769635970
jamaa njoo utoe maelezo maana tangu ulipotoka hujarudi kulikoni? tangu mwaka juzi.Hallo, si kweli kama unavofikiria naombeni kuandika Maelezo kama ifuatavyo
Safi sana kiongozi kwa maana umewaumbua wahusika. Huo ni utapeli wakipuuzi, tatizo wabongo tunapenda sana vitu vyepesivyepesi ndio maana wanawalizwa wengi, sasa mtu kuelezea biashara yake tuu anavunga, eti apigiwe sim kwa maelezo zaidi,Mimi niliwahi wafuata hawa watu wakanipa mpaka vipeperushi na muhudumu niliyemkuta alionekana hajajipanga nilipokua namuattack na maswali..ila hata hcho kipeperushi waliniuzia kwa shilingi 1000 na nilianza kuwaamini lakini nilishtushwa nilipoambiwa mrejesho wa faida kwa hesabu zangu za haraka hazipungui milioni 60 yani 60,000,000 na hapo hapo kwa hyo laki saba uliyo toa wanaahidi kukupa hekari nne huko rufiji zenye nyumba na mabanda yaliyojengwa tayari kwa hyo laki7 yako pia kuna mashirika makubwa ya kijamii wanadai wanaubia nayo kama pspf,NHIF, NSSF Kuwa eti ndo wanajenga hzo nyumba wa watu ambao wamesha fanya projection watu 2000 watakao toka kila kaya nikajiulizaaaaaa...nikasema ngoja ipo siku nitaujua ukweli
Kama ifuatavyo....mpaka Leo mwaka na nusu,heee heeee kweli JF kibokoHallo, si kweli kama unavofikiria naombeni kuandika Maelezo kama ifuatavyo
NASHUKURU LEO BAADA YA MUDA MREFU WATU KUIBIWA NA NAMAINGO KWA MIAKA MINGI WAMEJUA SASA KUWA NILICHOSEMA NI KWELI IMEPIGWA MARUFUKU RASMI KWA WIZI WALIOWAFANYIA AKINA MAMAhuu ni ulaghai kama utapeli mwingine wowote unaoendelea hapa bongo. Hawa wanaitwa wakulima wa keyboards au kwa jina lingine wauza maneno. watakuambia utoe 100000 tsh ya form wanapiga bla bla nyingi hakuna jipya. wao interest yao no hiyo laki moja ya kingilio. wao wapo ukonga mombasa. jiulize huko kuna Mashamba? Waambie wakuonyeshe Mashamba yao yako wapi ili ukajifunze huko. wakikuonyesha natembea uchi toka kariakoo hadi mbezi. Mtu anaambiwa eleza vizuri anasema piga simu. kueleza si rahisi kwa kuandika hapa kuliko watu elfu moja kupiga simu? Watu wengi wamedanganyika na hawa wauza maneno. Huwezi kuwaongoza watu kwenye kitu ambacho wewe mwenyewe ufanyi. wanakuambia tutakuanzishia shamba. jiulize kwanini wao wasianzishe ya kwao? Hawa na Amsha ni ndugu moja. Wanaongea kama wahubiri wa kilokole waulize maswali sasa ndiyo utachoka. Mimi sina mengi ni hayo tu.