Masoko ya mazao ya kilimo

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
MIFUMO YA MASOKO YA MAZAO YA KILIMO

Masoko ya mazao na bidhaa za kilimo ni muhimu kwa ajili ya kuchochea uzalishaji na kuendeleza Sekta ya Kilimo. Aidha, ubora wa miundombinu wezeshi katika uzalishaji, usafirishaji, hifadhi na usindikaji wa mazao ya kilimo ni muhimu katika kuwezesha ukuaji wa masoko. Vilevile, ubora wa mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini ni kigezo muhimu cha kufikia mahitaji ya masoko na hatimaye kupata bei nzuri.

Kuna mifumo mikuu mitatu inayotumika hapa nchini katika kuuza mazao ya wakulima ambayo ni mfumo wa vyama vya ushirika au vikundi; Mfumo wa mikataba na mfumo wa soko huria.

•Mfumo wa vyama vya ushirika au vikundi huwawezesha wanaushirika kukusanya bidhaa/mazao yao pamoja kupitia vyama vya ushirika kwa lengo la kutafuta soko la pamoja ili kupata nguvu ya kujadiliana bei yenye tija na wanunuzi.

•Mfumo wa Mkataba huwakutanisha wazalishaji na wanunuzi kabla ya msimu kuanza na kuingia makubaliano ya uzalishaji na bei. Katika mfumo huu baadhi ya wanunuzi huwakopesha wazalishaji
pembejeo zinazohitajika na baadaye kuwakata gharama hizo wakati wa mauzo.

•Mfumo huria huwapa fursa wanunuzi/wafanyabiashara kukutana na wakulima pale walipo na kununua mazao yao kwa bei wanayokubaliana ambapo mara nyingi mwenye nguvu ya kupanga bei huwa ni mnunuzi.

Kati ya mifumo hii mitatu mfumo wa vyama vya ushirika au vikundi umeonesha kuwa bora zaidi kuliko
mingine katika kuwanufaisha wadau wote yaani wauzaji, wanunuzi na Serikali.

Masoko ya mazao ya Kilimo

Masoko ya mazao ya kilimo nchini yapo, bali hushindwa kuhudumiwa na wakulima kitu ambacho husababisha wauuzaji wa rejareja kutafuta bidhaa hizo kutoka masoko ya nje ya nchi au kutumia mawakala kununua mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima.

Matumizi ya mawakala husababisha wakulima kupata bei za chini. Bei za mazao huwa ndogo sana kipindi cha kuvuna kwani kipindi hicho mazao ni mengi kuliko wanunuzi. Hivyo, ni vizuri wakulima kuuza mazao yao baada ya kipindi cha kuvuna hususani kwa mazao yanayoweza kuhifadhika kwa muda mrefu. Ili kupata masoko ya mazao ya kilimo ni muhimu kufanya utafiti wa masoko mara kwa mara juu ya mahitaji ya soko la zao husika kabla ya kuzalisha

Mambo yanayoathiri masoko ya mazao ya kilimo

Kabla ya kuzalisha mazao, mkulima anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo: -

•Bei za washindani
•Gharama za uzalishaji
•Upotevu baada ya mavuno
•Ubora
•Mfumo wa malipo (fedha taslim au mkopo)
•Soko lililolengwa
•Upatikanaji na mahitaji ya mazao sokoni
•Umbali kutoka eneo la uzalishaji hadi sokoni
•Kiasi kinachohitajika sokoni

Maandalizi ya Mpango wa Uzalishaji na Taarifa za Masoko

Kabla ya kuzalisha mkulima anapaswa kuandaa mpango wa uzalishaji kulingana na mahitaji ya soko. Mpango
huo unapaswa kujibu maswali yafuatayo:-

•Zao gani na kwa kiasi gani
•Viwango gani vya ubora wa mazao unaohitajika
•Nitauza katika soko gani
•Nitauza kwa bei gani (wastani)
•Nini mahitaji ya soko kwa zao husika
•Upatikanaji wa zao husika ni wa kiasi gani sokoni
•Gharama za uzalishaji ni kiasi gani
•Kuna changamoto gani za uzalishaji kwa zao husika
•Kuna ushindani kiasi gani katika soko

Ili kujibu maswali haya kwa ufasaha mkulima anapaswa kuwa na taarifa sahihi za masoko. Taarifa hizi
hupatikana kwa kuwekeza muda wa kutosha katika kufanya utafiti wa masoko. Utafiti huu hufanyika
kwa kwenda moja kwa moja sokoni na kuongea na wanunuzi sambamba na kuangalia mwenendo wa
soko (upatikanaji na mahitahi ya mazao). Vilevile, taarifa hupatikana kupitia vyama vya ushirika, vyombo
vya habari, wakala za serikali, wabia wa maendeleo, maonesho ya wakulima na teknolojia ya habari na
mawasiliano (mitandao, simu).
Ufahamu kuhusu soko humsaidia mkulima kuzalisha kulingana na mahitaji na hivyo humhakikishia soko la bidhaa yake na kupata faida.Vilevile husaidia kupunguza upotevu wa mazao. Inampasa mkulima kuelewa kwamba uzalishaji usio na faida ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo yake binafsi, kaya na jamii nzima.

Wakati wa uzalishaji, ni muhimu kuzingatia uzalishaji wa bidhaa zenye viwango bora kulingana na mahitaji
ya soko

NJIA ZA KUUZA MAZAO YA KILIMO
Kuna njia kuu mbili ambazo mkulima anaweza kuuza mazao yake. Njia hizo ni: -

i.Njia ya moja kwa moja – Mkulima anapeleka mazao yake moja kwa moja kwa mlaji pasipo kupitia kwa wafanyabiashara/madalali. Njia hii humpatia mkulima faida kubwa.

ii.Njia isiyo ya moja kwa moja – Mkulima anauza mazao yake kupitia wafanyabiashara/madalali. Njia hii humpatia mkulima faida kidogo.

Wakulima wengi hupendelea kuuza moja kwa moja kwa watumiaji ili kupata faida kubwa. Pamoja na
ukweli kwamba uuzaji wa moja kwa moja una faida kubwa, wakulima wengi bado wamekuwa wakipata
hasara kutokana na upotevu wa mazao haya baada ya kuvuna.

Sababu kubwa za upotevu ni pamoja na:-
•Vifaa na miundombinu duni ya kuhifadhi na usafisishaji
•Umbali kutoka eneo la uzalishaji
•Kiasi cha mazao anachozalisha (hakikidhi mahitaji ya soko)
•Elimu duni kuhusu utunzaji wa mazao hayo baada ya kuvuna
•Matumizi ya vifaa duni katika kuhifadhi
•Usimamizi mbovu wakati wa uzalishaji, uvunaji, ufungashaji, usafirishaji na uuzaji wa mazao

Ni vema mkulima akaelewa kwamba uuzaji wa moja kwa moja unahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo elimu
kuhusu mbinu na teknolojia bora za utunzaji wa mazao hayo baada ya kuvuna, masoko, namna ya utunzaji
wa mazao sokoni na vifaa kwa ajili ya hifadhi na usindikaji wa mboga mbichi. Lengo la uwekezaji huu ni kutunza ubora, kudhibiti upotevu wa mazao hayo na kuleta faida si tu kwa mhusika (mfanyabiashara) bali kwa wadau wote katika mfumo.

Cc: Wizara ya kilimo
IMG_16858596614406209.jpg
 
Cc: Wizara ya kilimo View attachment 2645489
MPYA HII,hapa mfanyabiashara na mtumiaji wa viazi mviringo,,,,,,,,,,(kiepe)
Msimu umewadia.tenaaaaaa,
KARIBU,mkoa wa
NJOMBE,kusini mwa Tanzania, ujipatie viazi mviringo aina zote,unazotaka wew kwa bei nafuu,kabs,....
Wewe dalali na mfanyabiashara mnakaribishwa,....
bei maelewano,
Mawasiliano 0620743697.
FB_IMG_16964051229546339.jpg
View attachment 2773009View attachment 2773008
 
Back
Top Bottom