Kilimanjaro: Mhandisi wa Kilimo apewa usimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesikitishwa na kitendo cha Mhandisi wa kilimo (agricultural engineer) kapewa usimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Kisingizio alichopewa ni eti kumekosekana mhandisi hivyo wakaona ni bora Mhandisi wa Kilimo angalau alete kaujuzi kake pale kwenye mradi unaohitaji Mhandisi wa Ujenzi (Civil Engineer)

Mpango amesema tayari ameagiza Waziri wa Tamisemi kupeleka timu kwa ajili ya uchunguzi na kurekebisha ili hospitali hiyo iweze kukamilika na kuanza kazi, na kwamba kwa watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua.

Nchi ya vibweka!

Akiwa katika ziara Wilayani Mwanga, Makamu wa Rais wa JMT, Dkt. Philip Mpango ameiagiza TAMISEMI kuchunguza Matumizi ya fedha za Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo baada ya kutoridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa Mradi huo

Ni katika ziara hiyo Dkt. Mpango alipobaini kuwa aliyepewa kazi ya Usimamizi wa Ujenzi wa Hospitali hiyo ni Mhandisi wa Kilimo. Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Zahara Msangi amesema kutokana na Changamoto ya uhaba wa Wahandisi Wilayani humo aliona huyo anafaa
 
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesikitishwa na kitendo cha Mhandisi wa kilimo (agricultural engineer) kapewa usimamizi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Kisingizio alichopewa ni eti kumekosekana mhandisi hivyo wakaona ni bora Mhandisi wa Kilimo angalau alete kaujuzi kake pale kwenye mradi unaohitaji Mhandisi wa Ujenzi (Civil Engineer)

Mpango amesema tayari ameagiza Waziri wa Tamisemi kupeleka timu kwa ajili ya uchunguzi na kurekebisha ili hospitali hiyo iweze kukamilika na kuanza kazi, na kwamba kwa watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua.

Nchi ya vibweka!

View attachment 2941644
Unajua maana ya Koneksheni ?
 
Back
Top Bottom