Majangili wajeruhi Askari wawili wa TANAPA katika Hifadhi ya Burigi Chato

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Uhifadhi -TANAPA wakitekeleza majukumu yao ya Ulinzi wa Rasilimali za Taifa katika Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato walibaini ujangili wa nyama na kufanikiwa kukamata majangili wawili kati ya watatu waliokuwa wakiwinda hifadhini.

Aidha, katika jitihada za kuwakamata majangili hao askari CRIII Wilson Lucas Mwita alishambuliwa kwa mkuki na kupata jeraha la mkuki kiganjani, na askari mwenzake CRI Pele Malima Taraba akijeruhiwa kwa mkuki tumboni.

Majeruhi wote wawili walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu ya haraka (Emergency Care) ambapo CRIII Wilson Lucas Mwita alipatiwa matibabu na kuruhusiwa wakati mwenzake CRI Pele Malima Taraba amefanyiwa upasuaji, na anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.

Watuhumiwa wawili, Jumba Pascal (38) na Amos Nyanda (18) wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi na jitihada za kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka zinaendelea.

TANAPA inatoa Onyo kali kwa majangili kuacha mara moja vitendo vya ujangili kwani kwa kufanya hivyo inawadhulumu watanzania wengine haki ya mapato yanayotokana na rasilimali hizi. Aidha, kwa wale wanaojeruhi na kuua askari wanaopambana usiku na mchana kutunza Maliasili hizi tunawapa salamu: Tutawatafuta popote walipo na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

Tanapa.jpg
 
Natoa pole kwa askari waliojeruhiwa na kuwaombea wapone kwa haraka.

Vinginevyo, taarifa hii imekosa kitu muhimu kajisansijui ji kwa makusudi au vipi: kwa nini kipengele cha eeneo mahususi ambako tukio limetokea halikutajwa?

Inaweza kutusaidia kwwhye kutunza kumbukumbu au kuondoa fikra kuwa inawezekana hao " majangili" wamekutwa kijijiji wakiendelea na shughuli zao lakini ....
Kingine, taarifa haielezi ni wanyama wa aina gani na kiasi ambacho " majangili" wamekutwa navyo.
 
Jeshi la Uhifadhi -TANAPA wakitekeleza majukumu yao ya Ulinzi wa Rasilimali za Taifa katika Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato walibaini ujangili wa nyama na kufanikiwa kukamata majangili wawili kati ya watatu waliokuwa wakiwinda hifadhini.

Aidha, katika jitihada za kuwakamata majangili hao askari CRIII Wilson Lucas Mwita alishambuliwa kwa mkuki na kupata jeraha la mkuki kiganjani, na askari mwenzake CRI Pele Malima Taraba akijeruhiwa kwa mkuki tumboni.

Majeruhi wote wawili walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa matibabu ya haraka (Emergency Care) ambapo CRIII Wilson Lucas Mwita alipatiwa matibabu na kuruhusiwa wakati mwenzake CRI Pele Malima Taraba amefanyiwa upasuaji, na anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.

Watuhumiwa wawili, Jumba Pascal (38) na Amos Nyanda (18) wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi na jitihada za kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka zinaendelea.

TANAPA inatoa Onyo kali kwa majangili kuacha mara moja vitendo vya ujangili kwani kwa kufanya hivyo inawadhulumu watanzania wengine haki ya mapato yanayotokana na rasilimali hizi. Aidha, kwa wale wanaojeruhi na kuua askari wanaopambana usiku na mchana kutunza Maliasili hizi tunawapa salamu: Tutawatafuta popote walipo na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

Mengine yapo Loliondo. Ngorongoro na Bungeni wakayamate pia
 
Jangili sio mtu mzurii kbs..
Ukiona jinsi wanawatega wanyama utalia kwa mateso ya yule mnyama!!jangili akishikwa na kizibo dawa ni kutupa kwenye mto wa mamba tuu.
 
Hii ni aibu. Hivi unapigwaje mshale wa tumbo afu una silaha na risasi kisha unatutangazia kuwa umewakamata majangili hao wawili na niwazima? Hizo silaha na risasi ulipewa kama manati ya kuwindia ndege? Kwa nini hukuwalenga tena risasi za kufumua ubongo? Sasa ngoja ufe wewe familia yako iteseke majangili wakale maisha hadi uzee
 
Back
Top Bottom