Kilimanjaro Kempinski yabadilishwa jina

Movenpik ilianza kama SHERATON bado wakasema hailipi! hapa ni ujanja ujanja tu! Mbona Sheraton Uganda mpaka leo bado ni ileile?
 

...hii imekaa vizuri japo haijatupa picha halisi. Jambo la kujiuliza ni je?...Kwanini Serikali inatoa hizo Tax Exemptions za miaka mitano mitano kwa wawekezaji wa kigeni?

Hebu turudi kwenye suala zima la uwekezaji. Je uchumi wa Tanzania unaruhusu muwekezaji kutochambua risks mfano; Competency ya waajiriwa, Raw materials i.e Upatikanaji wa Mazao ya chakula, nyama na samaki Vilivyo kwenye Viwango na ubora wa kimataifa kulingana na matakwa ya wateja wao? Vipi suala la upatikanaji Maji safi, Umeme, nk? Investments sio kuleta jina la Kempinski/au Grand Hyatt pekee.

Kempinski/Sheraton/Hilton/Grand Hyatt/Movenpick/Marriot/Serena... zote hizo ni "BRAND" tu zinazotambulisha huduma zinazopatikana kwenye hoteli husika. Brand sio jina pekee useme labda ni kama Coca Cola, au AZAM, nk...
A Brand is your customers' experience and the expectation you set when doing business with your company. Brand is a promise. No wonder utakuta wana aina fulani ya vitanda, mito, Linen, aina fulani ya Restaurants, Service,...management nk..

Dar es salaam tunahitaji hizo Reputable chain of hotels wawekeze, hata kama mapato tutakuwa tunagawana 50:50. Kuna faida kubwa kuwa na mahoteli yenye hadhi hizo in a long term, faida zake zitakuja jionyesha baadae.



'Exposure' ya kufanya kazi na wageni hao kunaongeza ujuzi na ari kwa wenye mioyo na vichwa vya kujifunza. Kujifunza na kujiendeleza si lazima kuwe darasani pekee. Mara nyingi, 'wataalamu' hao huja kwa mikataba ya muda mifupi, wazawa ni jukumu letu kujifunza ili tumudu kuendeleza huduma kama zinavyotakiwa zisimamiwe kwa mujibu wa miongozo ya kazi (Work Ethics and Standards) lakini wapi... Wabongo utawaambia nini na visingizio vya "Nimefiwa na shemeji yake jirani yake dada!"...almuradi tu asije kazini.

Kuna classes za Watalii, watalii ambao watatafuta mlo kwa mama Ntilie ni wale wanaokuwa classified as Drifters/ Backpackers. Hao huna la kuwaambia kwenye cost control, tofauti na Leisure travellers ambao hawaoni tabu kulipa chumba $380 na kuendelea kwa usiku mmoja, mlo wa $25 na kuendelea...
Mtu wa aina hiyo ana demands zake kwamba anataka Red Wine ya Burgundy, sio Red Port ya Dodoma...
nk, nk....huwezi mkatalia.
 
Reactions: EMT
WIZI MTUPU!!! Na hawa nao ikifika 2016 wataamua "kuiuza" kwa "mwekezaji" mwingine kumbe wanakwepa kulipa kodi. Hawa wanaojiita Viongozi wanauona wizi huu wa mchana kweupe lakini hawachukui hatua zozote!!!

Mkuu ukiona hivyo fahamu kuwa viongozi wetu wamenunuliwa, kila mwezi wana mgao wa dola kadhaa kwenye akaunti zao. Mahoteli makubwa kwenye beach za Zanzibar na hata huku bara hasa mahoteli makubwa ya mbugani watu wanalipia online au huko huko kwao. Ina maana kodi hatupati na wakubwa wanalifahamu sana hilo lakini wako kimya kabisa. Inauma sana kwa kweli.
 
...hii imekaa vizuri japo haijatupa picha halisi. Jambo la kujiuliza ni je?...Kwanini Serikali inatoa hizo Tax Exemptions za miaka mitano mitano kwa wawekezaji wa kigeni?

Serikali itakuambia misamaha ya kodi huchochea ukuaji wa uchumi, huongeza uwekezaji, ajira, ukuaji wa pato na hivyo kuleta mapato zaidi ya kodi katika muda mrefu. Lakini ukweli ni kwamba sababu mojawapo ya Tanzania kuwa na utegemezi mkubwa wa misaada toka kwa wahisani na kushindwa kuwekeza kwa haraka zaidi katika maendeleo yake ni ukusanyaji mdogo wa mapato yatokanayo na kodi.

Ukweli utabakia kuwa misamaha ya kodi Tanzania ni mikubwa ukilinganisha na ile ya jirani zake, Kenya na Uganda na kwa kiasi kikubwa inawafaidisha wawekezaji wakubwa wenye vyeti vya kupatiwa motisha kutoka vituo vya kukuza uwekezaji. Manufaa tunayoyapata kutokana na misamaha ya kodi ni madogo mno.



Una maana kuwa madhumini ya tax exemptions ni kusaidia wawekezaji kwenye hayo uliyoyataja? Kuwa watatumia hizo fedha walizo save kwenye tax exemption kupata nyama na samaki wenye ubora wa kimataifa, nk? Nyama na Samaki wa Kilimanjaro hotel wananunuliwa wapi? Ukienda kuagiza wali maharage pale, unafikiri yanatoka wapi? Mbona Kenya na Uganda nchi ambazo tuko eneo moja, hawatoi misamaha mikubwa kama tunayotoa? Ina maana upatikanaji wa raw materials huko ni rahisi zaidi kuliko Tanzania?

Kuhusu suala la upatikanaji maji safi na umeme kwani wawekezaji ndio pekee wanaoathirika? Kwa nini wawekezaji wa ndani nao wapiwe hizo exemptions? Wao pia wanaathirika na tatizo la umeme. In deed, kila mtu anaathirika na tatizo la umeme whether or not ni muwekezaji. Huoni kama hizo fedha tunazopoteza kwenye tax exemption zingeweza kutumika na kutatua tatizo la umeme altogether kwa faida ya wawekezaji na wasio wawakezaji?


Heri hata tungekuwa tunagawana mapato 50/50. But kwa sasa we get nothing because of tax exemption. Kila mwezi tuna lose out sh 700 billion kwenye tax exemption. Ina maana unataka kusema kuwa faida tunayopata kwa mwezi kutokana na tax exemption ni sh 700 billion na ushee? Sijui una maana gani kwa long term, lakini unajua tax exemptions zimeanza lini? Tokea zianze mwanzoni kabisa ya miaka ya 1990s tumenufaika na nini? Angalia kwa mfano kwenye migodi, what benefits are we getting from them kama sio haya makampuni kutuachia ardhi tupu iliyojaa mashimo baada ya miaka mitano?

Tatizo lingine ni usiri ulioko kwenye hii misamaha. Ni vigumu kujua ni kwa kiasi gani viwango vikubwa vya misamaha inayotolewa vinawafaidisha wananchi. Kwa kuwa na uwazi zaidi, kwa mfano, kwa kuweka bayana taarifa kuhusu makampuni yanayopokea misamaha ya kodi na viwango vya msamaha kwenye mtandao, uchambuzi kama huu unawezekana. Taarifa hizi kwa sasa hazipatikani kwa ukamilifu kwa umma, pamoja na kwamba misamaha ya kodi ni sawa tu na aina nyingine ya matumizi ya serikali. Kama ilivyo kwa matumizi ya afya, maji au elimu, inatakiwa misamaha ya kodi ipitiwe na kuchanganuliwa na Bunge, pamoja na walipa kodi.
 
Reactions: Mbu

...umejibu hoja vizuri sana. Nitarudi na maswali zaidi juu ya hiki "kichwa cha mwendawazimu!"
 
Reactions: EMT
EMT, hebu upitie tena huu ukurasa halafu tuangalie "siri-kali" yetu imefungwa wapi mikono
kwenye suala zima la uwekezaji wa kigeni.
Tanzania


Bado naamini utegemezi wetu ndio unaotulazimu kukubaliana na masharti ya World Bank,
IMF na donors wengine ambao indirectly wana recoup fedha zao through hizo channels za wawekezaji.
Au wewe unaonaje? ...tulishalikoroga since zama za ujamaa na kujitegemea. Kwenye zama hizi za soko huria, tunalazimika kumeza 'some bitter pills' tupate unafuu. Miongoni mwa hizo tembe ndio hizi Exemptions kwa Foreign Investors.

JK alipata kutamka, "ukitaka kula lazima uliwe!..."
Hivi, bora ni nini? Kuwa na Investors wenye tax Exemptions na kufaidika angalau na kipato cha ziada,
au kukosa kabisa Investors kwa sababu ya mazingira yetu?

Nazungumzia zaidi kwenye hii sector ya Mahoteli na Utalii.
Tunanufaika vipi na wawekezaji hawa?
 
Reactions: EMT
badala ya kulalama ni vema mgepiga kelele serekali iwasiadie wajasiriamali wa ndani kama Ndugu Mfugale na Peacock Hotel, Mrema wa Impala wapanua mahateli yao. Hii itasaidia walau kwenye swala la kodi.Na mahoteli hayatabadilishwa majina baada ya miaka mitano. Kuna uzembe, rushwa, kutokuwasikiliza wataalam, na ubinafsi mkubwa ndani ya wizara ya utalii. hili ndio linaifanya hili taifa kuwa kama shamba la bibi

Mataifa mengine yanawashawishi hawa brand OWNER Kama Hilton na wengine kuwekeza nchini kwao na sio kupitia kwa mtu wa pili kama wanavyofanya hapo Tanganyika. Wakijenga hotel yao wao wenyewe hawataweza kuondoka kurahisi, baadhi ya maofisa serekalini wakipewa rushwa kidogo tu wanakubali huu upuuzi wa kubadilishwa majina na uuzwaji wa haya mahoteli kiholela bila kuangalia faida na hasara.

Imefika mahali sasa wananchi tuamke tuwaambi basi. Sekta ya utalii inazo changamoto nyingi saana, na wamekuwa wakizifumbia macho mfano, hatuna wataalamu wa kati. Chuo Cha Taia Cha Utalii, kilitakiwa kiwe mstari wa mbele kuzalisha hawa wataalamu, Kwa kuwa Luhanjo tangu akiwa maliasili kwa sababu anazojua mwenyewe wamewachanganya wafaransa waliotoa msaada wa kujenga chuo kimpya mpaka leo hakijaanza ilihali pesa walitoa tangu mkapa akiwa madarakani( SOmeni Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 1995 na ya 2000). ndio maana hata leo ukiwaambia watupe mchango wa haya mahoteli hawawezi. Ni haya haya mahoteli yanaagiza sukari, chumvi, maji kutoka nje wakati hivi vitu vinaweza kupatikana hapa nchini kama watu watawezeshwa

Swala la Kilimanjaro kempinski na Movenpick kubadili jina subirini baada ya miaka mitano mtasikia tena wamebadili majina. Binafsi naamini hili taifa lingekuwa chini ya Ukoloni wa Waingereza tungekuwa na maendeleo zaidi. kuliko hawa watawala weusi ambao wanajali matumbo yao na familia zao. naamini ipo siku watafikishwa mahakamani kama Mubarak
 
Jamani Nimesikia pia MOven Pick imeshauzwa kwa watu wengine na soon the name will be changed to certain arabic name, HUU NI WIZI.

.....................Haha inaitwa taking advantage of realities.

Mie ninaomba mwenye hiyo policy/regulation au sijui nini kuhusu hiyo tax holiday atuwekee hapa sie vilaza wengine tuisome tuelewe maana haiingii akilini eti mtu afanye bashara miaka mitano pasipo kulipa kodi kisha akaacha wakati we all know kuwa biashara za hotel kama hiyo inalipa hapa nchini kwetu. Naingiwa na hisia kuwa kuna kitu ambacho hakiko wazi as to why serikali yetu (ingawa Mh. Nyalandu alisema kuwa hii tax Holoday haifanyiki Tanzania peke yake) inalifumbia macho suala hili.......... Najiuliza maswali makuu mawili
1. Hawa wawekezaji wanapokuja kuwekeza nchini mwetu hawanaga masharti yoyote ambayo kwa namna moja au nyingine yanatufunga kuwabana ipasavyo? (Ukizingatia tunawabembeleza kuja kuwekeza andn knowing the poor negotiation sills we have na marushwa - inawezakana nao wanatubanaga kona flani ambayo mwisho wa siku tunajikuta hatuna la kufanya zaidi ya kuwa wapole kama tunanyolewa nywele na kinyozi)

2. Mkataba/sijui sheria inasemaje juu ya hii 'tax-holiday' thing? sababu gani inakubalika kwa mwekezaji ambaye amepewa grace period ya kutokulipa kodi anaruhusiwa kukubaliwa kiutoendelea kuwekeza? je ni biashara kuto kulipa (Kwamba biashara haina faida ndo maana nimeamua kuuza mtaji baada ya kumaliza grace period ya tax free au?)

Mtanisamehe pengine yalishajibiwa haya na hiyo sheria kuwekwa but naombeni mnitoe tope hili la macho,
 

lol,...kaka kweli umechoka. Hivi muingereza alitufanyia lipi la maendeleo? Upande wa kilimo na infrastructures nyingi zililetwa/zilianzishwa na mjerumani.

Waingereza ndio wameturudisha nyuma hawa!



...Mwj1, maswali yako yana akili sana. Tunaweza kuwalaumu wawekezaji buree
ilhali loopholes 'tumetoboa' wenyewe...

“Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded.” -Mwl Julius Nyerere.
 

Mkuu wakati Chief Economist and Senior Vice-President for Development Economics of the World Bank, Mr Justin Yifu Lin alipotembelea Tanzania mwaka huu alisema kuwa World Bank itaunga mkono MKUKUTA II kama kama serikali itaongeza source ya vipato including kupunguza misamaha ya kodi.

Pia ukisoma Joint IMF-World Bank Staff Advisory Note (JSAN) ina ten conditions ambazo Tanzania must meet kabla ya kupata support toka World bank/IMF. Condition mojawapo ni serikali kurekebisha sheria na sera yake ya kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwa wawekezaji. It says, in addition to better use of public resources, the JSAN emphasizes the need to increase domestic revenues, including by reducing tax exemptions and other measures to expand the tax base.

Ilichofanya serikali ni kujaribu kufuta tax exemptions kwa kwa religious organisations na NGOs ambayo ili backfire kwa sababu hizi NGOs zina-target providing essential services to wananchi. Ndio mama unaona serikaki sasa inahaha kupitia sheria husika. Kwa hiyo unaposema kuwa World bank inaunga mkoni misamaha mikubwa ya kodi sikuelewi.

Mkuu hii ya JK kusema "ukitaka kula lazima uliwe" mbona wenzetu Wakenya na waganda wanakula bila kuliwa? Hata kama msemo wake una maana yoyote, tunakula kidogo sana kuliko tunavyoliwa.
 
Reactions: Mbu
Mkuu MBU

Uko sawa kabisa kwa miundombinu, waingereza hawakuleta kitu, lakini naamini wangekuwa wanatutawala KUNGEKUWA NA UTAWALA wa Sheria, tungekuwa tunalipa kodi hata kama ni ya kichwa lakini, ingetumika kusafisha mitaa, kutupatia maji safi ya kunjwa, kujenga barabara,( Huduma za jamii kwa ujumla wake)

Inasikitisha saana, nii hii hii serekali ya wakolini weusi mtu hana vigezo, hana uelewa, hana elimu kwa kuwa ni nyumba ndogo ya Mkubwa anapewa majukumu na kufanya maamuzi ambayo yanaligarimu hili taifa kwa miaka

Kuna uzembe, ufisadi, kupendeleana, kutojali katika idara ya utalii, bodi ya utalii, TIC, Huwezi amini mkuu wa Idara anaweza kuwa na nguvu kuliko katibu mkuu, kuna jamaa moja kwa kuwa alikuwa analinda mslahi ya wazee alikuwa anampiga Mkwara waziri, Haikuchukua Muda waziri yule alibadilishwa. Sasa hapa huu upuuzi wa kubadilisha majina kila baada ya miaka mitano

Wizara ya Utalii na idara zake zingesimamiwa kwa uadilifu na umakini ingeweza kutokaribia robo ya mapato ya serekali lakini kinachofanyika ni usanii mtupu, Kuna wakuu wa idara na vitengo wanawapeleka ma secretary ulaya, madereva kwa kisingizio cha kwenda kutangaza utalii, vitalu wanagawa kwa rushwa ya hali ya juu. Kama tungekuwa na mkoloni sidhani kama wangeruhusu huu upuuzi
 
Huwa najiuliza ni kwa nini hata magoteli makubwa ya kitalii kila ikifika miaka 5 ya kufanyakazi hufunga virago na kuwauzia wengina ambao nao wakichuma shamba la bibi baada ta miaka 5 nao huwapa wengine ni kama vile mbio za kupokezana vijiti kila baada ya miaka 5 hupokea wengine au kuna ujanja fulani ndani yake ,au hawa jamaa hupata holiday tax ya miaka 5,wenye kujua tujuzeni hii si bure bana
 
Reactions: EMT

...inasikitisha sana mkuu, it's all about accountability na watu kuwa held responsible kwa majukumu waliyokabidhiwa.
Nidhamu ya kazi, utendaji na utiifu imepungua kwa asilimia kubwa sana. Fitna, majungu na Uzembe umekithiri na kukumbatiwa kwenye vitengo vingi, hata kwenye sehemu nyeti. Mifano ipo mingi na ya kusikitisha.

Kiukweli, tunahitaji Authoritarian Prez mwenye vision kama ya Kagame. Tatizo mpaka akubalike na apitishwe na Chama chake.
 
Kuna sehemu nilisikia kuwa hii tax- holiday (ambayo ndio inafahamika zaidi kwa watanzania wegi-kuhusiana na mahotel) kuwa iko more linked na uanzishaji wa 'Enterprises" ambazo hazitambuliki au haziko katika level ya 'invenstment' ....sikuelewa pengine ina maanisha hotels kama Kempinski, Moven Pick zinafall kwenye Enterprises zaidi ya Investments kama kina Barrick............kama kuna mtu anaeelewa juu ya tofauti hii naombeni msaada pengine itanipa mwongozo kwenye kutoa hoja juu ya 'wawekezaji ' wanvyootunyonya na hasara tuipatayo maana kwenye haya mambo mie ni mweupe kabisa ingawa napenda kuyafahamu kwa undani.
 
Ndo matunda ya chama legelege cha magamba ambacho kimezaa serikali legelege ambayo inakomaa na wenye viosk kukusanya kodi kumbe kuna matajiri wanakwepa kodi kwa kujiita wawekezaji na kubadili majina kila baada ya miaka 5
 

MwanajamiiOne nitaweza information kuhusiana na uliyouliza baadae. In mean while tafakari haya.


IMF/World Bank ambao wana support foreign investment wanasema hii misamaha ya kodi kwa wawekezaji ni too much. Mpaka Mr John Wakeman-Lynn, the IMF resident representative, mwenyewe amekiri kuwa it would be in the public interest to scale down the level of exemptions. Anasema "we think it should be part of the new government's agenda."What the government did ni kujaribu kufuta misamaha ya kodi kwa NGOs na vyombo vya dini bila kuwagusa wawekezaji. NGOs na vyombo vya dini vinafanya biashara gani ya kutozwa kodi?

Nikupe mchanganuo wa utafiti mmoja juu ya misamaha ya kodi. Kwa mfano, mwaka 2008/9, misamaha ya kodi ilikuwa asilimia 2.8 ya GDP na mwaka 2009/10, asilimia 2.3. Ukilinganisha na Kenya na Uganda misamaha ya kodi ilikuwa ilikuwa asilimia 1 (Kenya) na asilimia 0.4 (Uganda) ya GDP. Mwaka 2008/09 and 2009/10, serikali ilishindwa kufikia target ya makusavyo ya kodi kwa kiasi cha Tsh453 billion ($302 million) kwa wastani. Katika kipindi hicho hicho, misamaha ya kodi kwa wastani ilikuwa Tsh724 billion ($483 million) kwa mwaka. Kama tungefuata system ya misamaha ya kodi Kenya tunge save Tsh484 billion ($323 million) kwa mwaka 2008/9 na Tsh302 billion ($201 million) kwa mwaka 2009/10.
 

Yep, kwa nini wasifungashe virago baada ya miaka minne au sita? How come is so coincidence kila hoteli kufungasha virago baada ya miaka mitano?
 

EMT aksante sana sasa umenifungua macho pamoja na kunichanganya hapo kwenye mahesabu.....mwe najuta kukimbia hisabati.

Sasa kwa uelewa mdogo nilionao bado ninaamini kabisa kuwa tuna tatizo sehemu. Kwani naelewa kuwa hizi tax incentives ambazo zimekuwa zikiwekwa lengo na nia ni kuvutia wawekezaji sawa, lakini tax holiday pekee ni muhimu but haitoshi kuwavutia........ kuna swala zina la miundo mbinu ambalo imfortunately bado linalega lega (sijui serikali yetu ni vivu kwa kukimbilia njia rahisi ya kuvutia wawekezaji na ku'minyia' nyingine??
2. Kitu muhimu kinachotakiwa ni kujiuliza tangu hii tax-holiday imeanza kutolewa, je imetimiza lengo?? i.e. lengo ni kuvutia wawekezaji - je wawekezaji wengi wameongezeka (na wamekuwa wakiinvest kwenye sustainable investments?? yaani investment ambayo inadumu?- sasa sijui hizi za miaka mitano mitano tunawezaita ni za kudumu au vipi?
3. Tax-holoday inatakiwa kutolewa iwapo the targeted Investment (Investor) ana contribute in one way or another (sio kwa njia ya tax) in country's development- sasa hawa investors wanacontribute nini na vipi kwenye maendeleo yetu ya nchi mfano employment ni;
-% ngapi ya walioajiriwa wako kwenye hizi tax-fee enterprises/investments??
- je mishahara yao, inakatwa kodi?
-kodi hiyo inatumikaje kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla??

Najua kuna kil ekitu kinaitwa Corporate Social responsibility ( ambayo nayo ina makasheshe kibao) but najiuliza maswali mengi sana juu ya utendaji kazi wa serikali yetu, systems gani tunatumia kumonitor na kuevaluate impacts za sheria zetu- nakumbuka recently nilitembelea Hotel ya The Double Tree by Hilton pale Masaki, kusema ukweli ile barabara ya kuingilia pale ilinipa mtihani mkubwa but kwa kuwa haya mambo siyajui sana nikaishia kunyamaza tu.
 
Reactions: Mbu

Hiyo report iliwakilishwa kwa watawalala lakini wameweka masikio yao gundi

Mbali na hiyo report Mfano Kuna baadhi ya wataalamu wa idara ya Utalii walishauri Watawala kwamba kwakuwa vivutio vyetu vya utalii ni vya hali ya juu, hususan Ngorongoro, Serengeti serekali iondoe kabisa Misamaha ya kodi kwa wanaoitwa wawekezaji kwani hayo maeneo yanajiuza yenyewe. Hawa wapuuzi walichokifanya ni kuwahamisha wengine wakashushwa vyeo. Haya mambo saanyingine yanakatisha tamaa saana.mijitu hii hii imesoma kwa kodi za watanzania, badala ya kulitumikia hili taifa wamehamua kuliuza
 
Reactions: Mbu

lol...kwakweli mambo kama haya ukiyajua undani wake waweza kujikosesha raha za maisha.
Ni sawa na mahoteli ya TTC, TAHI, mashirika ya Umma Kuanzia Mabasi, viwanda vya nguo,
viwanda vya kusindika vyakula etc yalivyokufa. Mismanagement ya nchi hii ilianza zamani jamani
acheni tu!

hii post ya leo https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-wa-trilioni-3-apata-mshtuko-na-kuzirai.html imenimaliza nguvu kabisa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…