Boss,
Sheraton hawakuondoka. Walibadilisha tu jina la kampuni lakini wamiliki ni wale wale.
Una uhakika na unalolisema, Swala la Sheraton lilipotoshwa saana na watu tulivyo wavivu wa kufuatilia mambo tunashabikia tu. Ukweli ni kwamba, aliyejenga jengo la iliyokuwa Sheraton alikuwa hana ujuzi wowote na uendeshaji wa hoteli, waliingia mkataba na Sheraton ili waiendeshe ile hoteli, ukumbuke hii mikataba hususani na hotel chain zenye majina inalipiwa pesa nyingi saana, miliki aliona hapati faida akahamua kuwatimua sheraton baadae akawachukua Royal palm ambayo ni hotel chain kutoka south africa, mwana wa mfalme wa Soudia akatembelea tanzania akalipenda jengo akamtafuta miliki akamshawishi amuuzie kwa kuwa jamaa alitoa pesa nzuri jamaa kakubali kuuza, Mwarabu yeye anaaamahoteli sehemu mbalimbali duniani yanayoendeshwa na Movenpich hotels and lodges ya Uswis nda kawaajairi wamuendeshee, na ndio wanaendesha mpaka leo. hiki ndo kitu kilichotokea
Kwa biashara ya mahaoteli hili ni jambo la kawaida saana kwakuwa wabongo hatuko so used na haya mambo ndo maana tunaona ni kitu cha ajabu,, swala la kodi ni kweli serekali ilikuwa inatoa vivutio kwa wawekezaji ila nadhani kwa sasa wameondoa baadhi ya hivyo vivutuo,
kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo, utakumbuka HOLIDAY INN na wao walikuwa wanaiendesha Southern san hotel , walitofautiana miliki wa jengo kawatimua kahamua kuliendesha peke yake wao wakatafuta wahindi wakaindgia maktaba nadhani kwa sasa wanaendesha hoteli karibu na posta mpya. haya ni mambo ya kawaida saana mkubwa
cha msingi ni serekali kujaribu kuwashawishi hizi chain kama Marriots, Hilton, holiday inn, waje wajenge property zao wenyewe hapa nchini kwa kufanya hivyo hutaona kila baada ya muda wanaondoka.

Maelezo haya matamu ni cover up tu ya kujisafisha machoni mwa wadanganyika wengi. Nina uhakika na ninachokisema. Hata Andrew Chenge nae ana maelezo matamu tu ya kumfanya Attorney General ama Takukuru wasimkamate.
Kila aina ya ufisadi ufanywao Tanzania una cover up yenye maelezo matamu kama hayo ulioyatoa lakini tunaujua ukweli na ukweli ndio huo wa TAX EXEMPTION.
Kwa nani kawafukuza Kilimanjaro Hotel Kempinski?
mkuu prodigal son asante saana...
tatizo wabongo wengi tunaamini ufisadi kiasi kwamba hata logic hatutaki kuitumia
hizo hoteli za sheraton mfano
zipo dunia nzima,sasa iweje tanzania tu ndo ziwe za kifisadi??????
na zipo katka nchi zingine ambazo kodi ni kubwa kuliko zetu........
ukweli ni kuwa hizo brand hotels nazo zinakuwa makini mno na kuchafuka majina
iwapo zitahusishwa na ufisadi
wabongo wengi hatutaki kutazama matatizo ya sekta ya utalii kwa upana wake
mfano hakuna airport ya kiwango huko serengeti,
na gharama za kutoka dar kwenda arusha au mwanza ni kubwa mno kuliko
gharama za kutoka london kwenda amsterdam,au beijing kwenda kuala lumpur
hatutazamii hayo
MKUU BOSS
uko sawa kabisa, hata majuzi hoteli iliyoshambuliwa Kabul ni Hilton ya wamarekani, mkuu sekta ya utalii kutokana na rasilimali tulizonazo ingeweza ikalisha nji nzima. Tatizo kubwa kuna umafia mkubwa saana unaoendelea mkubwa mpaka hizi chain kubwa zinaogopa kuja na kuwekeza. kuna ma king makers lazima utimize masharti yao lasivyo huwezi fanya lolote mkubwa. kutokana na hii hali ndo maana tunaambulia wawekezaji uchwara. Kinachosikitisha wakati watawala wanapigania kujenga barabara serengeti ili kurahisisha usafiri kwenye mahoteli yao yaliyopo ndani ya hifadhi, Sudan sasa wanajitahidi kuanzisha mbuga ambayo wanyama wanahama kama waserengeti
hebu angalia hii link In Sudan, an Animal Migration to Rival Serengeti - New York Times soon tutakuwa nawashindani, wanasiasa wetu wanapigania matumbo yao tu
mkuu inasikitisha mnno
utalii ungetosheleza bajeti yetu tungekuwa makini
south africa wanapata dola bilioni kumi kila mwaka kwa utaliii
na wanatumia zaidi ya dola milioni 50 kwa matangazo kila mwaka
sisi hatujawahi kutumia hata dola milioni mbili tu kwa matamngazo
na bado utaliii ndio sekta inayoleta fedha za kigeni kuliko sekta zote
yaani tunababaisha na bado tunapata faida,
jiulize tungekuwa serious?????????
mkuu prodigal son asante saana...
tatizo wabongo wengi tunaamini ufisadi kiasi kwamba hata logic hatutaki kuitumia
hizo hoteli za sheraton mfano
zipo dunia nzima,sasa iweje tanzania tu ndo ziwe za kifisadi??????
na zipo katka nchi zingine ambazo kodi ni kubwa kuliko zetu........
ukweli ni kuwa hizo brand hotels nazo zinakuwa makini mno na kuchafuka majina
iwapo zitahusishwa na ufisadi
wabongo wengi hatutaki kutazama matatizo ya sekta ya utalii kwa upana wake
mfano hakuna airport ya kiwango huko serengeti,
na gharama za kutoka dar kwenda arusha au mwanza ni kubwa mno kuliko
gharama za kutoka london kwenda amsterdam,au beijing kwenda kuala lumpur
hatutazamii hayo
Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 25th July 2011
HOTELI kubwa mbili za kitalii jijini Dar es Salaam zenye hadhi ya juu nchini zitabadilishwa majina yake ya sasa kwa mara nyingine kutokana na kuuzwa kwa mojawapo na nyingine kwa sababu ya kubadilisha kampuni inayosimamia masuala ya uongozi.
Hoteli hizo, Kilimanjaro Kempinski na Royal Movenpick ndizo zinazoelezwa kuwa mbioni kubatizwa majina mapya ifikapo Agosti mosi mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Utalii nchini, Ibrahim Musa alisema taarifa rasmi alizonazo ni za kubadilishwa kwa jina la Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kuwa Kilimanjaro Hyatt mwezi ujao.
Musa alisema suala la Movenpick bado lipo mikononi mwa wenye hoteli wenyewe na kwamba ni vigumu kwake kulizungumzia kwa sasa kwa sababu taarifa rasmi hazijaifikia meza yake.
"Nitazungumzia Kempinski pekee kwa sasa kwa sababu hiyo ya Movenpick bado wenyewe hawajatuletea taarifa rasmi kuihusu. Nina taarifa ya kuwepo kwa mazungumzo kati ya wanaoendesha Movenpick na wadau wengine, lakini siwezi kuyasema kwa kuwa sio rasmi," alisema Mkurugenzi wa Utalii.
Hata hivyo, pamoja na maelezo hayo ya Mkurugenzi wa Utalii, gazeti hili lilipata taarifa za kuwepo kwa mpango wa kubadilishwa jina kwa hoteli hiyo ya Movenpick kuwa Serena endapo wauzaji (Movenpick) na wanunuzi (Serena) watafikia makubaliano.
Aidha, imefahamika kuwa pande hizo mbili zipo katika mazungumzo ya mwisho kuhusu kuuziana hoteli hiyo ili utekelezaji wake ufanikishwe ifikapo mwanzoni mwa mwezi ujao.
Akifafanua kuhusu Hoteli ya Kempinski, Mkurugenzi huyo alisema kitakachofanyika hakitakuwa na athari zozote katika uwekezaji wala ulipaji wa kodi kwa sababu umiliki unakuwa bado ni wa mhusika wa awali.
"Tuliliangalia suala la kodi kwa kina na kujiridhisha kuwa halitaathiriwa kwa namna yoyote kwa kubadilishwa jina kutoka Kempinski kwenda Hyatt. Kitakachobadilika ni kampuni inayoshughulika na masuala ya uongozi wa hoteli hiyo kutokana na kumalizika kwa mkataba wake na wamiliki," alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema kampuni hiyo mpya iitwayo Hyatt ni ya Kimarekani na kwamba wamekubaliana nao wasiondoe jina la Kilimanjaro ili kulinda historia ya Mlima wa Kilimanjaro ambao ni fahari ya Tanzania.
"Pamoja na kuangalia masuala ya kodi, pia tuliwaomba wahusika wasiliondoe jina hilo Kilimanjaro kama njia moja ya kulinda historia ya mlima wetu. Walikubali kwa kweli na kutufahamisha kuwa jina hilo litaendelea kutumika kwa kuwa ndio linalowavutia wateja wengi wanaofika kupata huduma katika hoteli hiyo," alisema.
Juhudi za kumpata Meneja wa Hoteli wa Kempinski aliyejulikana kwa jina moja la Trevo, ziligonga mwamba baada ya Ofisa wa Mapokezi aliyejitambulisha kwa jina Oswald Akyoo, kumzuia mwandishi wa habari hizi kumwona kwa maelezo kuwa haikuwa siku ya kazi. Kuhusu uwezekano wa kuwepo athari katika makusanyo ya kodi kutokana na kuuzwa kwa Hoteli ya Movenpick endapo suala hilo litatekelezwa, Mkurugenzi wa Utalii nchini alisema itakuwa vema likizungumzwa wakati litakapotokea.
"Kwa kuwa wapo kwenye mazungumzo, hatuwezi kusema imeuzwa, tusubiri watupe taarifa ndio tuzungumzie suala hilo. Lakini kwa vyovyote, Serikali haiwezi kuruhusu athari katika uchumi wake hivyo sitegemei zitokee," alifafanua Musa.
Kumekuwa na hofu miongoni mwa Watanzania kuhusu kubadilishwa kwa majina ya hoteli nchini huku wengi wakidhani ni njama za kukwepa kulipa kodi katika miaka mitano ya uwekezaji wa kwanza.
Lakini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA), Dk. Adelhelm Meru aliwahi kusema mabadiliko ya majina ya uwekezaji pekee hayana athari katika kodi.
Kwanini Mahoteli ya Kenya - Kama Nairobi Hilton haijabadilisha Jina - Toka nikiwa mtoto hadi sasa na Uzee bado ni Nairobi Hilton... kwanini Hoteli zetu tunazowapa wawekezaji zinabadilishwa badilishwa?Couple of things:
The so called GREAT THINKERS wa JAMII FORUMS watakuja hapa na allegations kuwa kodi itapotea hawa jamaa wakibadilisha majina pasipo kuleta ushahidi wowowte ule wa ku substantiate hizi conspiracy zao
Nawahikikishia thread itafika pages 4 na kitakachoongelewa ni theories na hisia tena kwa ku refer habari zilizoandikwa na mwandishi ambaye hawezi kuandika jina la TREVOR!
I cant wait kuwaona GREAT THINKERS wa JAMII FORUMS watakavyokuja kujadili hili jambo tena najua wengine wata refer majina ya makampuni ya simu yaliyobadilishwa lakini hakuna takaye leta ushahidi wowote toka TRA au mamlaka yoyote ile husika
JF ya 2011 imejaa wababaishaji tuu ambao hawana tofauri sana na akina John Mashaka na yule "DR" feki SHAYO.
lakini it takes all sorts to make this forum ya GREAT THINKERS