Kilichotokea ANC, hakiwezi kutokea CCM - Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichotokea ANC, hakiwezi kutokea CCM - Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 10, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara) Bw. Pius Msekwa amesema kuwa mgongano na hatimaye kumeguka kwa chama cha ANC kabla ya uchaguzi wao Mkuu wa Rais na Wabunge hakiwezi kutokea kwenye Chama cha Mapinduzi.

  Ameyasema hayo akiwa Afrika Kusini kusherekehea kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo Bw. Jacob Zuma. Vyama vya ANC na CCM vina historia ya muda mrefu ya ushirikiano na urafiki kwa miongo mingi sasa.

  Wakati huo huo; Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz naye alikuwa Afrika ya Kusini siku ya Jumamosi katika kile kilichoelezewa kuwa ni shughuli zake binafsi. Hata hivyo vinzi vinavyoruka ruka vimeelezea pia ilikuwa ni nafasi kwa RA kukutana na Rais Kikwete ambaye naye alikuwa SA katika sherehe ya kuapishwa kwa Bw. Zuma.

  Baada ya sakata lake na mfanyabiashara Mengi na hasa mwelekeo wa kisheria ambao sakata hilo limechukua kuna mambo ambayo Bw. RA alitaka kuhakikisha mkuu wa nchi anayasikia na kuyafahamu na vile vile kufahamu msimamo wake.

  Rais Kikwete inadokezwa kuwa alifanya safari toka Uskandinavia kuelekea Afrika Kusini kwenye sherehe ya Zuma na anatarajiwa kuelekea Marekani ambako kuna uwezeekano pia wa kukutana na Rais mpya wa Marekani Bw. Barack Obama..
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Duh! Kama ni kweli sasa huyu bwana itabidi afokewe ili akae nyumbani kwa angalau siku 120 bila kusafiri. Yaani yeye kila kukicha safari safari tu...anaenda kufanya nini kwenye hizo safari? Gotdamnit
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  ana watendaji kibao, wacha atembee tu!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  for once tumekubaliana.. wiki iliyopita gazeti la Uhuru lilikuwa na kichwa cha habari "Kikwete apewe kazi Denmark" ... nusuru nipige magoti kushukuru!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 10, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Oh really?
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ina maana hujui hilo?
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa nchi zilizo makini hicho cheo kinaitwa Roving Ambassador lakini hapa bongo anajulikana kama President of the United Republic of Tanzania. Tatizo la akina Kibunango ni kuwa hamwezi kutofautisha which is which. This is really sad.
   
 8. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanini wasikutane oceanroad/kivukoni, kulikoni-TISS wana vyombo vya kunasa ufisadi?:D
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Duh! Kumbe ni kweli RA hakupata nafasi ya kuwasiliana na JK? No wonder ushahidi na nyaraka za siri vinaibiwa huko kwa kina IGP Mwema na mkemia mkuu!
  JK kaoa ndugu ya RA na Said Mwema naye kaoa kwakina JK kama sijakosea,sasa haya ni mambo kifamilia ama?
  Kama kweli RA kaamua kumfungia safari JK hadi SA...Basi mambo si mambo kwa mafisadi.
  Tusubiri tuone huu mkorogo matokeo yake ni nini,lakini kuna watu hawataki kuachia utamu kwani umenoga.
  Tulishauri tume ya ukweli na maridhiano hapa JF,na Zitto na yeye aliiwakilisha huko,hawakusikiliza,sasa naona kama imefikia stage ambayo ni irreversible kwasababu ya kiburi.
  Ama kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha na hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho....Kelele za mlango hatimaye zimemkosesha usingizi mpangaji. lol!
  Kwa anayedhani kupanga ikulu=usingizi mnono amekosea!
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa nchi kama hii, yenye wasifa wa umatonya unategemea nini?
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Saafi sana Mkulu Mushi, tupo pamoja sana hapa.

  FMEs!
   
 12. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Msekwa akiwa ndani ya S. Africa, katika ujumbe wa Rais wa TZ, mgeni wa ANC, hakutakiwa kuongea hivyo. Ki-diplomasia hilo ni sawa na kujigamba au kukosoa siasa za ndani za wengine. ANC bado wana hasira, hawakupenda huo mpasuko, umesababisha Zuma akose super majority bungeni aliyoitegemea kusaidia agenda zake, kama kufumua mfumo wa judiciary. Msekwa anafyatua tu bila clue ya state of affairs ugenini. Viongozi wetu kidiplomasia ni taabani vilaza. Ambacho kinasishangaza sana, huyu Msekwa alianza kuwa Katibu Mkuu Mtendaji wa chama toka mwaka 1967, mpaka leo hapati clue?

  Au ni hawa waleta habari wetu ni watupu choka hawasemi mazingira, mada, context, ya maongezi ilikuwa nini.
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  tehe tehe hilo wese toka uskandi mpaka bondeni kisaha pipa hiloo linakata wingu mpaka majuu kudadadeki na akitoka huko atapitia UK kukagua matangazo ya juma pinto kwa siku 3.......

  .....sijawahi kuona taifa ambalo kiongozi wake mkuu anaongoza nchi akiwa ndani ya ndege.....zaidi ya tanzania..
   
 14. m

  mkama Member

  #14
  May 10, 2009
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hamna marefu yasiyo na ncha.

  Rashidi alisema,yanamwisho(kitabu cha Kuli)

  Kama kazomewa busanda,tena na Tingatinga,basi asiwe na imani mgando,abadilike.Lolote laweza kutokea na kumeguka ni uwezekano mmojawapo
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ulipaswa kujua kwanza Msekwa ameongelea katika mazingara gani kabla hujakurupuka na uncalled accusations ambazo huna uhakika aliposemea ni wapi, haiwezekani Msekwa amesema hayo mbele ya public, ni lazima alikuwa anaongea na waandishi wa bongo akaulizwa kuhusu the ishu, lakini mtu hahitaji kuwa Professor ku-figure that out!

  Resepct.

  FMEs!
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi ni nchi gani huyu Kikwete ambayo hajafika?
   
 17. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama Msekwa anaongea na waandishi wa Bongo, chochote kile unachokitoa mdomoni mwako kwa waandishi kinakuwa ni public declaration, hakuna siri kwenye siasa na waandishi. Sio lazima uongee jukwaani ndio iwe gaffe. Sasa hivi Balozi wa South Afrika Tanzania akisoma press ya Bongo akaona hii na ikamsumbua, Msekwa hawezi kudai oooh, ilikuwa ni siri yangu na waandishi wa Kibongo. Hizi ni a-be-che za diplomasia.

  Aidha waandishi wetu taabani wanapotosha context au ni gaffe la Msekwa kuingilia ya ANC ndani ya S.Africa
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  huwa naona viongozi kadhaa wanaongea au kuajdiliana na viongozi wenzao kwa simu badala ya kufunga safari kwenda kuongea nae huko.....kwanini muungwana asimpandie heani obama wakalonga wamalizane kwenye simu?
   
 19. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kikwete hajafika Tanzania huru isiyo na ufisadi, inayoendelea kiuchumi bila porojo, inayojari generation inaykkuja, yenye rais anayejua hali halisi ya maendeleo nchini kwa macho yake na si kaumbiwa, yenye rais anayekaa ofini kwake na kufanya maamuzi ya mambo magumu ya kimaenddeleo, ninakuhakikishia Kikwete hajafika hiyo Tanzania
   
 20. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Anyway mdau hapo juu kasema JK ni Roving Ambassador, wacha atalii
   
Loading...