Kilichopo Manyara ni humanitarian crisis. Saidia familia hata moja na utazidishiwa zaidi

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,311
4,019
Watu 50 labda zaidi wamefariki. Miundo mbinu haswa ile ya familia masikini imeharibika vibaya mno. Majeruhi wengi wapo hospitalini.

Nyakati kama hizi Sadaka yako inaweza kubadilisha mustakabali wa maisha yako. Sadaka yako inaweza tumika kuwapa faraja masikini walioathirika na naamini Mungu hatokuacha 2024 inayokuja.

Achana na akaunti za michango kama unahofia ubadhilifu, unaweza ifikia familia direct hata na gunia la nafaka yoyote ile.

Muwe na siku njema, poleni Wanamanyara.
 
Ni vizuri kuchangia tu na kama hazitafika kwa mlengwa Mungu atakubariki tu na huyo atakayeiba Mungu atashughulika naye lakini kwako utakuwa umepata baraka ya utoaji.
Kwanini zisifike lazima jitahada wafanye zifike
Haya mambo ya kusema sijui mungu atakubariki ,kama umetoa na zisifike
Wale waroho walaji hata hawajali
Msemo huo
Pesa kama zitachangwa lazima zifike

Ova
 
Viongozi waliokwenda kurundikana huko, wametoa mchango gani, na posho za safari usikute wanalipwa na marupurupu mengine wanachukua, nchi ya kisenge saana hii.

Na bado tukichangia, michango mnaifinyia kwa ndani.

Tukubaliane hapa, michango tunatuma kwa nan? Apatikane wa kumshika shati hela zetu zikienda ndivyo sivyo.
 
Back
Top Bottom