Full Text: Hotuba ya Msemaji wa kambi ya Upinzani, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
HOTUBAYA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NAUSHIRIKA MHESHIMIWA MESHACK JEREMIAH OPULUKWA (MB) KUHUSU MAKADIRIOYA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

(InatolewaChiniya Kanuni ya 99(9) toleo la mwaka 2013



  1. [*=center] UTANGULIZI
Mheshimiwaspika, Awaliya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema nakuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako tukufu kuwasilisha maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani kususu Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha2015/2016. Kwa namna ya pekee napenda kutoa shukrani nyingi kwaKiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freema Mbowe,kwa kuniamini na kunipa fursa ya kuitumikia Kambi Rasmi ya Upinzaniana UKAWA kwa ujumla.

MheshimiwaSpika, Kwamasikitiko makubwa, napenda kutoa salaam za pole kwa Watumishi waHalmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa kusimamishwa kazi siku ya jumamosiya tarehe 18.05.2015 kwenye kikao walichokaa na Mbunge wao ilikumwelezea kero zao kwa lengo la kuziwakilisha Bungeni. Hakika hakiya walimu hawa haitapotea kamwe ila yaweza kucheleweshwa tu.

MheshimiwaSpika,Aidha kabisa na kwa namna ya kipekee kabisa, napenda kuwashukuruwananchi wa Jimbo la Meatu kwa ushirikiano mkubwa na imani waliyonayokwangu kama mwakilishi wao. Niliwaahidi kuwatumikia kwa moyo wanguwote na naendelea kuwaahidi kuwa imani yao kwangu haitopotea bure naMungu aendeele kuwabariki,

MheshimiwaSpika,Kumekuwana mipango mbalimbali inayoandaliwa na Serikali kuhakikisha kwambaKilimo kinakuwa cha kisasa na hivyo kuzalisha chakula cha kutosha napia mazao mengi ya biashara hivyo kuongeza kipato kwa mwananchi mmojammoja, kukuza pato la Taifa na kuongeza thamani ya mauzo yetu nchi zanje. Lakini matokeo yake hayaakisi thamani ya fedha zinazowekwakatika sekta hiyo, kwani wakulima wameendelea kuwa masikini.

MheshimiwaSpika,Umoja wa Afrika kupitia NEPAD’s waliasisi program ya kuendelezaKilimo mwaka 2003 (CAADP) kwa kikao kilichofanyika Maputo nchiniMsumbiji kwa Viongozi wa nchi za Afrika kukubali na kuchukua dhamanaya kutoa utaalamu na msaada wa fedha kwa sekta ya kuendeleza kilimokwa nchi zao kwa kutenga asilimia 10 ya bajeti ya nchi zao kuelekezwakwenye sekta ya kilimo na maendeleo vijijini. Hadi sasa lengo hilo lakutenga 10% ya bajeti halijatekelewa na serikali hii.

KambiRasmi ya Upinzani inataka kujua, lini serikali itaanza kutenga 10% yabajeti yake kwenye sekta ya kilimo kama ambavyo maazimio ya viongoziwa nchi yaliyofikiwa huko Maputo yanavyotaka?


MheshimiwaSpika, Wadaumbalimbali wa kilimo wamekuwa tukiishauri Serikali kuyapatia ufumbuzimatatizo ambayo tayari watafiti walishayatolea suluhu ya ninikifanyike lakini kutokana na udhaifu wa kiutendaji wa Serikali ya CCMimeshindwa. Hivyo basi sasa ni muda mwafaka kwa vyama vinavyoundaUKAWA kuongoza Serikali ili kuyaweka kwa vitendo yale yote ambayotumekuwa tukishauri kuyatekeleza.

MheshimiwaSpika, Hakunasuluhisho ambalo halijulikani kwa Serikali,tatizo kubwa ni kwambawatendaji waandamizi wa Serikali wanafaidika binafsi kutokana namatatizo hayo, hivyo basi KambiRasmi inawataka wananchi watuunge mkono ili kuondokana na madhirahayo ya miaka mingi yaliyosababishwa na utendaji usiojali wa Serikaliya CCM.




  1. [*=center] MIGOGORO KATI YA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAWEKEZAJI
MheshimiwaSpika, Migogorobaina ya wakulima na wafugaji itaendelea kudumu kwa muda mrefu zaidiendapo haitapatiwa ufumbuzi, ikiwemo jitihada za viongozi kutengamaeneo mahususi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji. Hali yasasa ya migogoro hiyo ni mbaya zaidi na inatishia kutoweka kwa amani,umoja na utangamano wa wananchi katika maeneo yenye migogoro na taifakwa ujumla.

MheshimiwaSpika,Hivi sasa katika maeneo yenye migogoro, uhasama baina ya wakulima,wafugaji, wawekezaji na watumiaji wengine wa ardhi umefikia kiwangocha juu; ambapo imekuwa vigumu kwa jamii hizo kukaa pamoja katikamikutano, kushirikiana katika shughuli za ujenzi wa taifa au zakijamii, kutumika kwa lugha za kibaguzi na ukabila na hivyokusababisha mapigano ya mara kwa mara na hata mauaji miongoni mwaokama ilivyo sasa katika mikoa ya Morogoro, Manyara, Arusha Shinyanga,Simiyu na maneo mengi nchini.

MheshimiwaSpika, Matatizoya migogoro ya ardhi baina ya wakulima/wafugaji na wawekezajihayawezi kupatiwa ufumbuzi kwani inaonekana watendaji waandamizi waSerikali ni sehemu ya matatizo hayo.

MheshimiwaSpika,Kambi Rasmi ya Upinzani inasema kuwa Serikali hii ya CCM haina nia yadhati kumaliza migogoro hiyo, kwani kamati zote ambazozilikwishaundwa na Serikali na pia asasi binafsi zilikwishatoasuluhisho lake, lakini imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya kamatihizo. Hivyo basi, Serikali makini ijayo ya vyama vinavyounda UKAWAinaahidi kutekeleza yale yote ambayo tayari yalikwishafanyiwa utafitiwa kina na kutoa suluhisho.



  1. [*=center] MAZAO YA BIASHARA

Ai): Pamba
MheshimiwaSpika,Zao la pamba ni la pili kwa uingizaji wa fedha za kigeni baada ya zaola kahawa, likichangia asilimia 40 ya ajira nchini, limekuwalikikabiliwa na changamoto mbalimbali pamoja na mambo menginezikiwemo tija ndogo, bei ndogo ya pamba yenyewe kwa kulinganisha nagharama za uzalishaji, kilimo cha mkataba, uchafuzi wa pamba, uuzajinje wa pamba ghafi kwa asilimia 75, zana na pembejeo duni, utegemeziwa mvua, mabadiliko ya tabia nchi,udanganyifu katika mizani na kutokuwa na taarifa zinazohusumabadiliko ya bei. Ushurumkubwa unaoongeza mzigo kwa mkulima; Uwezo hafifu wa viwanda vyakuchambua pamba; Ruzuku ndogo kutoka katika bajeti ya Taifa;Ushindani usiozingatia Kanuni; Kulegea kwa Miongozo na Kanuni za zaola pamba n.k.

MheshimiwaSpika,Suluhisho la matatizo haya yote yamefanyiwa utafiti, na Serikali yaCCM inaelewa lakini inashindwa kusimamia utekelezaji wake. Matatizoya zao na biashara ya Pamba hapa nchini hayawezi kumalizwa naSerikali hii ya CCM kwani Wasimamizi wakuu wa Sekta hii ya Pamba ndiowanaofanya biashara ya Pamba. Hivyo sio rahisi kwa watu hao kutoasuluhisho la kudumu.

ii)Pembejeo

MheshimiwaSpika,Kwa miaka mingi kabla ya soko huria kulikuwa na mfumo maalumu wauzalishaji wa mbegu hali iliyofanya kuwepo na mbegu ya kutosha nabora kwa ajili ya kupanda. Baada ya mfumo wa uzalishaji wa mbegukukoma, hali ya ubora wa mbegu za kupanda ilianza kuwa ya mashaka nahasa baada ya soko huria kuanza hadi sasa.

MheshimiwaSpika,Mfumo wa upatikanaji wa mbegu za kupanda kwa sasa ni wa mbeguinayotokana na pamba iliyolimwa na mkulima wa kawaida katikamazingira duni ya utunzaji yasio na usimamizi wa kitaalamu. Katikamfumo huu limekuwa ni jukumu la Bodi ya pamba kuhakikisha kuwa kilakampuni ya uchambuaji iliyo nunua pamba kutoka kwa wakulimambalimbali katika msimu husika inahifadhi sehemu ya mbegu iliyotokanana pamba hiyo, kisha kampuni hiyo kuzisambaza mbegu hizo katikaWilaya mbalimbali hadi vijiji kwa maelekezo ya Bodi ya pamba kwakushirikiana na kamati za mazao za Wilaya husika. Mfumo huuunajulikana kama mfumo wa mbegu mzunguko (recycled seed system).

MheshimiwaSpika,Ikiacha mfumo nilioutaja hapo juu, ulikuwepo mfumo mwingine (rasmi)wa kuzalisha mbegu za pamba. Fedha zote zilikuwa zinatolewa naserikali kwa lengo la kuwasaidia wakulima kupata pembejeo. Hivikaribuni Serikali ilifanya juhudi za kuanzisha mfumo rasmi wauzalishaji wa mbegu za kupanda ambapo kampuni ya Quton (T) LTDilipewa kazi hiyo ya kuzalisha mbegu tangu Mwaka 2009 hadi leo.

Kambirasmi ya upinzani inahoji yafuatayo;



  • [*=center] kwa nini Quoton ambayo siyo taasis ya Serikali ipewe jukumu kubwa kama hilo wakati hawawezi kukaguliwa na Serikali?



  • [*=center] Kwa nini kazi ya kuelimisha wakulima ifanywe na quoton badala TCB?



  • [*=center] Kwa nini serikali isianzishe mfuko kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa taasis zote TOSC, UKIRIGURU, TCB, kwenye bajeti ya wizara?

iii)Kilimo cha Mkataba

MheshimiwaSpika,Lengo la kuanzishwa kilimo cha mkataba nchini ni kuweza kumsaidiamkulima wa pamba kupata pesa nyingi kwa kuzalisha kwa tija wakatiakitumia pembejeo anazokopeshwa na huduma za ugani, kumhakikishiamnunuzi, mchambuaji upatikanaji wa pamba nyingi na ubora na kuongezasoko la pamba ya Tanzania.

MheshimiwaSpika,Kinyume na matarajio ya wengi, kilimo hiki kimeendelea kulalamikiwana wakulima katika maeneo mbalimbali yanayolima pamba ukiwemo mkoa waSimiyu ambao unaongoza kwa kulima zao hilo, kutokana na mikatabawanayoingia na makapuni kutoweka wazi kiasi cha fedha atakachokatwamkulima wakati wa kuuza, ili kulipa mkopo wa pembejeo za mbegu,viuadudu na huduma za ugani alizokopeshwa.

MheshimiwaSpika,Kilimo cha mkataba siyo kibaya ni mikataba mibovu ambayoinamgandamiza na kumnyonya mkulima na kumpendelea mchambuaji wapamba. Mkulima hajui bei ya pamba yake wakati wanapoingia mkatabakitendo ambacho Kambi Rasmi ya Upinzani inapingwa kwa nguvu zote.



  1. [*=center] Korosho

MheshimiwaSpika,Tanzania inatajwa katika Bara la Afrika kuwa katika nafasi ya pilikwa uzalishaji wa zao hilo, ikifuatiwa na Nigeria. Lakini kilimo chakorosho kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mengi ambayo mpaka sasahayajatatuliwa. Wakulima wa zao la korosho nchini wako hatarinikupoteza soko duniani kufuatia udanganyifu unaodaiwa kufanyika katikamaghala ya kuhifadhi zao hilo wakati zikisubiri kusafirishwa kwendanje.

MheshimiwaSpika,Takwimu zinaeleza kuwa mahitaji ya korosho duniani yanakuwa kwa 8%kila mwaka, ikiwa ni ishara kwamba Tanzania inapaswa kuimarishauwekezaji wa zao hilo. Hivi sasa Tanzania inakadiriwa kubangua 2%i tuya korosho yote nchini na kiasi kinachobaki kinauzwa nje kama malighafi.

MheshimiwaSpika,Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na the Agricultural Non State ActorsForum (ANSAF) mwaka 2008, kuuza korosho nje ya nchi bila kubanguliwakuna hasara zake kwani wakulima wamekuwa wakipata kipato kidogo hukuserikali ikikadiriwa kupoteza dola 110 milioni, kila mwaka. Utafitihuo ulipewa kichwa cha habari. “Uboreshaji wa Mazingira ya Biasharaya Korosho Tanzania”. “Vikwazo vya kujenga viwanda vya kubanguakorosho nchini, vimesababishwa na udhaifu wa sera, ukosefu wa fedhana kutokuwapo kwa uzoefu katika soko la kimataifa,” sehemu yautafiti, inaeleza.

MheshimiwaSpika,Mnamo miaka ya 70 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, mikoa yakusini ilijenga viwanda 12 vya kubangua korosho(processingindustries) ili kuongeza ubora wa mazao hayo lakini viwanda hivyovimefungwa na vimekuwa vikitumika kama maghala (godows) tu. Aidhainasemekana viwanda vingine vimeuzwa kwa watu binafsi wakiwemowaliokuwa viongozi waandamizi wa Serilakali ya na CCM na wale CCM kwakiwanda cha Lindi, Mtama na Nachingwea.

KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwaeleza watanzania kwa niniiliuza viwanda hivyo ili hali vilikuwa ni muhimu sana katikauongezaji wa thamani ya zao la korosho ili kuwaongezea kipatowakulima?

PiaKambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuviruddisha viwanda vyoteilivyoviuza kinyamela kwa watu binafsi kwa faida wa wakulima yaKorosho nchini.

MheshimiwaSpika,imebainika kuwa wizi mkubwa wa export levy ambapo korosho zilizouzwanje mwaka 2012 ni tani 140,000. Cha kushangaza ni tani 80,000 tundizo zilizolipiwa ushuru wa forodha katika bandari ya Mtwara, natani 60,000 zilizobaki fedha hazikulipiwa ushuru. Jambo hililimezisababishia halmashauri zinazolima korosho kukosa mapato.

Kambi Rasmi ya Upinzani inahoji, kwa nini korosho isafirishwe kupitiabandari ya Dar es Salaam badala ya bandari ya Mtwara ambako ndipokituo kikubwa cha usafirishaji wa korosho kwenda nje?


MheshimiwaSpika,Zao hili linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefuwa viwanda vya kubangulia korosho na kusababisha wakulima kuuzakorosho ambazo hazijabaguliwa. Changamoto nyingine katika zao lakorosho ni mfumo wa stakabadhi ghalani. Mfumo huu umewaathiriwakulima kwa kiasi kikubwa kwani umeshindwa kukidhi mahitaji ya sokohuria na wakulima kushindwa kunufaika na soko.

MheshimiwaSpika,Utafiti huo wa ANSAF unaonesha kuwa bei anayopewa mkulima ni asilimia46% tu kati ya 100. Makato yanayokula kwa Mkulima yako kamaifuatavyo;
1. Gharamaza soko yaani vyama vya msingi na ghala ni shilingi 286/kg sawa na asilimia 34%
2. Kodianayotozwa mkulima ni 4%
3. Mchakatowa gharama za kusafirisha nje 6%

KambiRasmi ya Upinzani inahoji kama kwa makato haya ni kweli Mkulimaanaweza kujikomboa kutokana na zao la Korosho?

MheshimiwaSpika,Hali halisi ilivyo katika matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani nitofauti kabisa na sheria inavyotaka. Kwani wananchi wanalazimishwakuuza mazao yao kwenye vyama vya msingi badala ya wakulima kwendamoja kwa moja kwenye Ghala. Na katika kuuza kwenye vyama vya msingiwanatozwa ushuru na wakipeleka kwenye ghala wanalipishwa ushuru.Aidha bei inayotolewa na vyama ni ndogo sana ambayo sio shindani. Hiiinapelekea kukosa maana kwa uanzishwaji wa mfumo huu.

Kambi Rasmi ya Upinzani inasema, kwa kuwa sheria iko wazi na Serikaliya CCM imeshindwa kuisimamia ni muda mwafaka kukaa pembeni naSerikali ijayo ya UKAWA ikaitekeleza sheria hiyo kwa maendeleo yawakulima na kilimo husika.


C)Kahawa

MheshimiwaSpika, Kahawani zao la pili kwa mauzo ya nje nyuma ya Tumbaku kwa mazao ya kilimona linachangia asilimia 4% ya jumla ya mauzo ya nje kwa kipindi chamwaka 2004-2011. Uzalishaji wa zao la kahawa umekuwa ni wastani watani 40,000 kwa mwaka na takriban asilimia 100 ya uzalisahaji huo nikwa mauzo ya nje. Mnada wa Kahawa yote inayozalishwa hapa nchinihuuzwa kwa mnada Mjini Moshi.

MheshimiwaSpika,zaidi ya asilimia 90% ya kahawa yote inayozalishwa hapa nchiniinazalishwa na wakulima wadogo. Sekta ndogo ya Kahawa inatoa kipatocha moja kwa moja kwa zaidi ya familia 80,000 na kutegemewa na zaidiya watanzania 2.5 million kuendesha maisha yao (URT-Coffee Boardand TACRI, 2010).

MheshimiwaSpika,Tanzania imegawanyika katika maeneo makuu matatu ya kanda zauzalishaji wa Kahawa, ambazo ni; 1. Nyanda za Kaskazi yenye mikoa yaKilimajaro na Arusha: 2. Nyanda za Kusini yenye mikoa ya Mbeya,Ruvuma na Wilaya ya Ludewa; 3. Ukanda wa Ziwa Viktoria wenye Mkoa waKagera na Mara hasa wilaya ya Tarime. Pia kuna maeneo mengine yenyefursa kubwa kwa uzalishaji wa Kahawa ambayo ni: Tanga, Iringa,Manyara, Morogoro, Kigoma, Mwanza, Rukwa na Mara.

MheshimiwaSpika,Mikoa ya Kaskazini ambayo ndiyo mkulima mkubwa wa Kahawa nchiniwameamza kung’oa miche ya kahawa na badala yake kuanza kupandambogamboga na matunda kwa sababu ya gharama ya pembejeo kuwa kubwa.

MheshimiwaSpika,Miti mingi ya Kahawa imezeeka na inatakiwa ibadilishwe na miche mipyailiyo bora zaidi. Kasi ya ubadilishaji wa miche hii ya zamani nakupanda mipya ni dogo sana.

KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iziwezeshe kituo cha utafitikilichopo Lyamungo (TACRI) ili wafanye kazi ya kubadilisha micheiliyozeeka kwa kasi.


MheshimiwaSpika,KNCU inalalamikiwa kwa kuuza magari, mashamba na nyumba za ushirikabila kufuata utaratibu.

Kambi
Rasmiya Upinzani inaitaka Serikali kuingilia kati swala hili harakaiwezekanavyo ili kulinusuru zao hili la kahawa na sharia ichukuemkondo wake kwa wale wote ambao wametumia madaraka yao vibaya nakufuja mali za Ushirika.



  1. [*=center] HUJUMA ZINAYOFANYWA NA MAKAMPUNI MAKUBWA KATIKA MNADA

MheshimiwaSpika,Katika mnada wa kahawa kuna kitu kinachoitwa “buy back-system”mfumo huu umebuniwa na makampuni makubwa ambayo yanasajili vikampunividogo vinavyonunua kahawa ya wakulima moja kwa moja na kuipelekakatika mnada wa kahawa na kwakuwa kampuni hizo ni mali ya Kampunimoja kubwa. Jambo hilo hushusha kwa makusudi bei ya mnada na hivyoKampuni Mama ununua kahawa hiyo kwa bei ambayo vyama vya ushirikahushindwa kuinunua.

MheshimiwaSpika,Hujuma hii inayasaidia makampuni hayo kununua kwa bei ndogo ya mnadana wanapata bei kubwa wanapouza nje (Export price).Hapa waowanavizuia vyama vya ushirika kupata bei nzuri kwenye mnada (premiumprices at auction)

MheshimiwaSpika,Hujuma hizi Serikali ya CCM na vyombo vyake husika inazifahamu lakinihaichukui hatua za kulinusuru zao hili ili wakulima waweze kupata beiinayoendana na gharama za uzalishaji, badala yake inakaa kimya maanayeke ni kuwa wahusika nao wananufaika binafsi mfumo huo wa“buy-back”.

KambiRasmi inasema kwakuwa ukweli wa hujuma hizi na suluhisho upo kwenyemakabrasha basi suluhisho ni rahisi pale UKAWA utakapopata ridhaa yawananchi kuendesha Serikali.




  1. [*=center] MATUMIZI YA KAHAWA KWA SOKO LA NDANI

MheshimiwaSpika, Kwa mujibu wa takwimu za FAO inaonesha kuwa ni asilimia 4.2%ya Kahawa yote inayozalishwa nchini ndiyo inayotumika katika soko laNdani. Aidha tawkimu zinaendelea kusema kuwa tangu mwaka 2003 kiasicha kahawa inayotumika nchini inaendelea, Jambo hili linatokana nakupungua kwa utamaduni wa unywaji wa kahawa kwenye jamii zetu. Hivyobasin i jukumu la watanzania wote hasa vyombo vyenye thamana yakuendeleza zao hili kuhamasisha watanzania kunywa kahawa suala hililitaongeza uwezo kwa wazalishaji wa ndani na si kutegemea soko la njeambalo tayari limekwishahujumiwa.

D)Miwa/ Sukari

MheshimiwaSpika,Tasnia ya sukari ni muhimu katika Nyanja zote za kijamii na kiuchumi,sekta inazalisha ajiraza moja kwa moja kwa watu takriban 14,000 nainategemewa na familia zipatazo 30,000. Wastani wa nguvu kazi ya watu2-3 katika familia kwenye maeneo ambayo yanalima Miwa, tasnia hiiinatoa ajira ambazo sio za moja kwa moja (secondary employment) zaidiya ya watu 80 000.
Aidha,tasnia hii inawaingizia wakulima kiasi cha shilingi bilioni 4 kilamwaka, takriban USD 2.7MILIONI, pia shughulizi zingine zinazohusianana tasnia hii ya sukari zinaliingizia taifa mapato ya takribanshilingi 12.2 bilioni (1.7%of total tax revenue) kwa mwaka.

MheshimiwaSpika,Mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 590, 000, viwanda vya ndanihuzalisha tani 300,000, sukari inayoagizwa kwa ajili ya viwanda nitani 170,000, hivyo mahitaji yanayobaki huagizwa nje ya nchi.Sikuchache kupita baada ya Wamiliki wa Viwanda vya Sukari nchini kusemaviwanda Vyao viko hatarini kufa kutokana na serikali Kuendeleakuagiza sukari ya nje ya nchini na kupelekea Sukari ya ndani kukosasoko nakuvifanya Viwanda hivyo kupunguza wafanyakazi.

MheshimiwaSpika,Serikali imeshasema kwamba kamwe haitoacha kuagiza Sukari toka njenchi kutokana na Viwanda Vilivyopo nchini kukosa uwezo wa kuzalishaSukari za Matumizi ya Viwandani kwani Viwanda vya ndani vinauwezo wakuzalisha sukari za majumbani peke yake. Serikali imekiri kwambatatizo inalokumbana nalo ni Uingizaji wa Sukari Kinyemela kutoka njeya nchini ambao ndio limekuwa kikwazo katika Viwanda hivyo.

MheshimiwaSpika,Malalamiko ya wamiliki wa viwanda vya sukari yanayotolewa kutokana nasoko la ndani kutekwa na sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi nawafanyabiashara wakubwa. Hata Serikali inakiri kwamba sukari nyingiinayopitia bandari ya Dae rs Salaam kwenda nchi jirani (trasit)imekuwa ikishushwa na kutumika hapa nchini kiasi cha viwanda vyandani kushindwa kushindana na sukari hizo kwenye soko la ndani.
Hiiinadhihirisha jinsi gani Serikali ya CCM ilivyochoka kiasi kushindwakutekeleza majukumu yake ipasavyo.

E)Tumbaku
Kuwepokwa viongozi wa kisiasa kwenye uongozi wa ushirika kuliletamanung’uniko mengi kwa wana ushirika wa Tumbaku. Kwa mfano,viongozi wa CCM wa Mkoa na Madiwani wa CCM walikuwa ndiyo viongozi waushirika wakiacha wakuklima wakiibiwa na kudhulumiwa fedha zao.Sheria mpya ya vyama vya ushirika iliyopitishwa katika Bunge lakotukufu mwaka jana imewaweka nje lakini mpaka sasa hatua zakuwafikisha mahakamani viongozi wa ushirika walioshiriki ubadhilifubado zinasuasua.

Kambi Rasmi ya Upinzania inatitaka Serikali kuwafikisha mahamani maramoja wale wote walioshiriki katika ubadhilifu wa mali za wanaushirikana itoe taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo.




  1. [*=center] Chai

MheshimiwaSpika,Tanzania inaweza kuongeza uzalishaji wa zao la chai na kuliingiziaTaifa fedha za kigeni kama nchi nyingine za Kiafrika, iwapo Serikaliitaweka mazingira mazuri kwa kutumia fursa zilizopo. Uzalishaji wazao la chai duniani umeongezeka katika kipindi cha miaka mitanokutoka tani milioni 4.6 mwaka 2009 hadi tani 4.91 mwaka 2013 wakatikwa Tanzania imechangia kidogo, huku kukiwa na fursa nyingizinazopotea.



  1. [*=center] BODI YA MAZAO MCHANGANYIKO (COPB) + WAKALA WA CHAKULA (NFRA)


MheshimiwaSpika, Vyombohivi ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii ya watanzania, na hasa jamiimasikini ili kuhakikisha usalama wa chakula. Hata hivyo, kwa sehemukubwa, kuna muingiliano wa kiutendaji, na hasa Cereals and OtherProduce Board (CoPB) na uwepo wa wafanyabiashara wadogo na wakati.

MheshimiwaSpika, Uwepowa CoPB unaweza kudidimiza jitihada za vijana kujikwamua na umasikinikutokana na kununua, kutunza, kuchakata na kuuza bidhaa baada yakuziongezea thamani. Kwa kuwa nchi hii inalenga kutengeneza ajirasawa ilivyo kwenye FYDP, MKUKUTA na TDV2025, kuna haja ya kuhakikishashughuliza za Bodi ya mazao mchanganyiko inaunganisha vijana na fursabadala ya kuwaondoa vijana kwenye ajira.

MheshimiwaSpika,Pia ni bora serikali ikaweka wazi kuwa siku hizi imengia kufanyabiashara na kushindana na wananchi wake kwenye ufanyaji wa biashara.Vinginevyo wizara za kilimo, viwanda na kitengo cha uwezeshaji(commission of planning and empowerment) ziweke mikakati ya kuibuamakampuni ya kizalendo (madogo na ya kati) ili yaweze kuchangiakuleta ajira na kuboresha uchumi.

MheshimiwaSpika,KambiRasmi ya Upinzani inajiuliza kama Serikali inafanya biashara ya mazaohasa ya nafaka ni sababu zipi iliviuza viwanda vyake vyotevilivyokuwa vinaongeza thamani ya mazao? Hii ni sababu ya kwambaSerikali ya CCM imechoka kufikiri na inasahau upesi maamuzi yake,hivyo basi tunawataka watanzania waiweke pembeni na Serikali mpyaijayo ya Upinzani ifanye kazi.



  1. [*=center] UINGIZWAJI WA MCHELE NA SUKARI


MheshimiwaSpika,Bidhaaza Sukari na Mchele ni miongoni mwa bidhaa zinazotengeneza sehemukubwa ya kapu la mlaji (consumer’s basket) wa kitanzania. Hatahivyo siku za karibuni uingizaji wa bidhaa hizi umetekelezwa kwamfumo ambao unadidimiza jitihada za wakulima masikini wa kitanzaniana hivyo kuwanyang’anya kipato chao. Mfano, wakulima wa miwa kuleKilombero wamefikia kushindwa kumwuzia mwekezaji miwa kwa kuwamwekezaji ameshindwa kuuza sukari iliyoko kiwandani kutokana nauingijzaji wa sukari yenye ruzuku ya hali ya juu kutoka nje ya nchi.

MheshimiwaSpika,Sualala mchele pia, halina tofauti na sukari, kwa kuwa, mwaka 2014/15wakulima wengi wameshindwa kuuza mchele kwa bei ya faida (baada yakutoa gharama za uzalishaji) kutokana na uingizwaji wa mchele kwanjia za panya na ukwepaji wa soko. Wakulima walishindwa kuuza mchelekwa mwaka 2014/15 wakajikuta wanauza gunia kwa Tzs 30,000 badala yaTzs 90,000 kwa miezi ambayo bei huwa ni ya kawaida. Kwa kuwa wengi wawakulima hawa wamelima kwa mkopo (trekta ama madawa), inakuwa ngumukuweza kurudisha gharama za uzalishaji, na hivyo wametumbukizwakwenye lindi la madeni.

MheshimiwaSpika, KambiRasmi ya Upinzani inauliza, kama soko la mazao ya wakulimalinahujumiwa na Serikali hii ya CCM ikielewa fika bila ya kuchukuahatua, ni kwa vipi jitihada za wakulima kukopa mitaji zitaweza kuinuawakulima hao na sekta nzima ya Kilimo? Kambi Rasmi ya Upinzaniinasema sasa ni muda mwafaka Serikali chovu ya CCM ikakaa pembeni nakuona jinsi gani kilimo kitakavyoweza kulikomboa taifa letu.



  1. [*=center] MAZAO YA CHAKULA


i)Kilimo cha muhogo kwa chakula na biashara

MheshimiwaSpika,Nchini Tanzania, muhogo unatajwa kuwa zao la pili kwa kuchangia patola taifa kwa asilimia 19 baada ya mahindi. Pamoja na hayo. Zao hililina faida nyingi kijamii na hata kiuchumi na kwa maendeleo ya nchi.

MheshimiwaSpika, Nizao ambalo linaweza kuzalisha bidhaa zaidi ya 300, zikiwemo zile zachakula na ambazo si za chakula viwandani. Majani yake hutumika kamamboga na dawa pia. Katika viwanda, mazao yanayopatika katika mziziwenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi nivifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu, naplastiki. Vilevile wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa zamadoa, gundi katika samani, rangi za awali katika kuta za nyumba nasukari (Sugar syrup).

MheshimiwaSpika, Hivisasa zao la muhogo limezidi kupata umaarufu zaidi, ambapo kadri sikuzinavyokwenda linabadilika na kuwa zao la kibiashara. Katika nchinyingi za Afrika kama vile Afrika ya kusini, Nigeria, Ghana, nakwingineko, kuna viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika mihogo nakupata bidhaa mbalimbali. Mojawapo ya bidhaa kubwa zinazotengenezwakatika viwanda hivyo ni pamoja na wanga, madawa, kiungo cha kuongezaladha kwenye vyakula, pamoja na glucoseinayotokana na muhogo.

MheshimiwaSpika, Kwahivi sasa wakulima walio wengi wanajipatia kipato kizuri kutona naumaarufu na umuhimu wa zao la muhogo duniani kote, ambapowafanyabiashara kutoka bara la Asia kama vile uchina, wana mahitajimakubwa ya zao la muhogo kwa ajili ya viwanda nchini mwao. Kwamantiki hiyo unaweza kuona ni kwa namna gani zao hili lilivyo naumuhimu mkubwa tofauti na linavyochukuliwa na jamii nyingi zawakulima barani Afrika kuwa ni zao la kimaskini.

KambiRasmi ya Upinzania inasema Serikali ijayo ya Upinzani itatilia mkazozao hili kwa faida ya wakulima na Taifa kwa ujumla. Kwani Serikaliiliyoshindwa kuona fursa ya CCM itakuwa kando.


ii)Teknolojia ya GMO katika Kilimo

MheshimiwaSpika, GMOni kifupi cha maneno ya kiingeraza yani Genetically ModifiedOrganisms. Viumbe hivi nizao la teknolojia mpya ya kibaliojiaijulikanayo kama Biotechnology.Wanasayansimbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki wamekuwa wakitafiti juuya uwezekano wa kutumia teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) katikakilimo. Hatua hii inatokana na teknolojia hiyo kuwa na upinzani kwakile kinachoelezwa kuwa ikitumika inaweza kusababisha athari zakiafya na kimazingira.

MheshimiwaSpika,Hata hivyo, watafiti mbalimbali duniani wamekuwa wakiiteteateknolojia hiyo kuwa ni salama na tayari baadhi ya nchi kama vileMarekani, India na China zimeshaanza kutumia teknolojia hiyo katikakilimo.

MheshimiwaSpika, Niukweli usiopingika kwamba teknolojia ya GMO inaweza kumsaidia mkulimakuvuna mazao mengi katika eneo dogo, kutotumia au kutumia kidogo dawaza kuulia wadudu na mazao kumea vyema kwenye maeneo yenye mvuakidogo. Nchi mbalimbali zimekuwa zikitamani kuona wananchi wakewanazalisha chakula cha kutosha na pengine kuwa na ziada kwa ajili yakuuza, lakini zimekuwa na hofu ya kujiingiza kichwa kichwa kwa kuwani teknolojia mpya.

MheshimiwaSpika, Mfanomzuri ni Rais Jakaya Kikwete alipotembelea Taasisi ya Tafiti zaKilimo ya Mikocheni (MARI), Machi mwaka 2013 na kuhimiza wanasayansikuharakisha utafiti wa teknolojia ya GMO, ili Watanzania waanzekuifaidi.

KambiRasmi ya Upinzani inataka kujua lini tafiti hizi zitakamilika na ninikauli Serikali kuhusu GMO.




  1. [*=center] MAPITIO YA BAJETI KWA MWAKA 2015/16

MheshimiwaSpika,Wizara katika mwaka wa fedha 2015/2016 katika vifungu vyote vitatu(43, 24 na 05) inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi353,150,873,000ambapo shilingi 95,387,647,000ni kwa ajili ya maendeleo sawa na 27%.Fedha nyingine yote inayobaki ni kwa ajili ya matumizi ya kawaidakitendo ambachoi kinaonyesha dhahiri kwamba serikali haina utashi wakuendeleza kilimo nchini pamoja na kwamba zaidi ya 80%ya watanzania wanategemea kilimo.

MheshimiwaSpika,Kwa kuwa serikali imeshindwa kabisa kusimamia kilimo nchini nakuwaacha watanzania wakihangaika ovyo.

KambiRasmi ya Upinzani inawaomba wanachi kuunga mkono juhudi zinazofanyawa vyama vinavyounda UKAWA ili kukiweka chama cha mapinduzi pembenikwa ajili ya mstakabali wa nchi.

MheshimiwaSpika,Baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naombakuwasilisha.

……………………………………………………

MeshackJeremiah Opulukwa (Mb)MsemajiMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani – Wizara ya Kilimo Chakula naUshirika23.05.2015

 
Back
Top Bottom