Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Huyo n mchungaji uchwara, siwez acha kupariria kaburi la mama yangu kamwe, uniambie sijui biashara ya mapepo sijui upepo. Na ndo kwanza nikiendaga kijijini nikirud mjini ndo natusua. Wewe kuna jambo uliwauzi wenye makaburi yao sio siri, kaa utafakari.
Wanasemaga mwisho wa siku jini lazima litoke kwenye chupa sasa wewe lisubirie msipobadilishana makazi
 
Mpaka uwe na jicho la tatu ndio utaweza kuunganisha hizi doti.
 
MBONA WALE MALAYA WANAOFANYA MAPENZI MAKABURI YA KINONDONI KILANSIKU WATEJA WANAJAZANAAA.....NAO UANWASHAURIJE

Unaniuliza mimi au mleta hii mada??
Mkuu we endelea tu kupenda vya mteremko kwa hao madada poa siku ukangengeda juu ya kaburi na siafu wakakuingilia huko kwenye difu yako
Na imani utatoka baruti kuelekea maskani huku ukirukaruka juu juu ma ukiimba wimbo wa MIMMASAI BANA NASEMA MIMMASAI NADUMISHA MILA[emoji443][emoji443][emoji3]
 
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.
Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.
Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .
Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .
Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.
Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.
Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.
Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.
Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.
Kabla yakuanza kufagilia makaburi ulifanya sala ??nabaada yakumaliza pia ulifanya sala ??pia watoto hawatakiwi kwenda makaburini huwa wanaona.
 
Huyo n mchungaji uchwara, siwez acha kupariria kaburi la mama yangu kamwe, uniambie sijui biashara ya mapepo sijui upepo. Na ndo kwanza nikiendaga kijijini nikirud mjini ndo natusua. Wewe kuna jambo uliwauzi wenye makaburi yao sio siri, kaa utafakari.
Hakufanya sala huyo yakuwaombea .
 
Huyo mch alikushauri vizuri. Mtu anapokufa Mungu huondoa ulinzi wake kwasababu imeandikwa Mungu si Mungu wa wafu... Hivo baada ya mtu kufa malaika huondoka na shetani huleta wa kwake na kufanya maskani tulivu kwao. Ndo maana wachawi, washirikina maeneo ya makaburi ni sehem muhimu sana kwao kwasababu ni maskani ya mashetani, ni maeneo ambayo hakuna roho wa Mungu wala malaika watakatifu, ni maeneo huru kwa shetani.
 
Mkuu huenda ukawa ulikosea masharti ya MGANGA au ulidhulimu....makaburi hana uhusiano wowote na hyo MIKOSI ULIYOPATA....vuta picha tu...hyo pesa uliipata vp? huenda hyo madini uliyopatia pesa ndy MIKOSI...ieleweke unaweza ukapata Kitu....au ukanunuwa kitu...ikawa kumbe umenunuwa MIKOSI....na mtu AKIFA NI KWELI anabaki mwili tu ila hata ROHO YAKE IPO PALE..
 
Sasa unaposema tusiyazoee makaburi kuna mapepo huko na wachawi. je.? sisi ambao nyumba zetu zipo upande wa pili ambapo njia lazima ukatize makaburini unatuambuaje.. mbona tushazoea kila siku tunapita usiku na mchana hayo mambo hayatupati..huwenda ulikuwa na mapepo yako tu binafsi..muulize mchungaji vizuri asikudanganye..
huyo mchungaji ni mchungaji njaa
 
Aiseee..pole mkuu sasa uhusiano wa mtoto kulia, wewe kupata ajali na kufilisika ni upi?
Hata kama ni 1st to reply,, just soma nyuzi polepole, mbona jamaa kafunguka vizuri tu. Anyway avatar yako inasadifu uelewa wako
 
ungemalizia tu, mambo ya kuweka kiporo ka hadhithi za shigongo wakati unasema ni kisa kimekutokea, haileti ladha ya story yako
 
wengne tukitoka kupalilia makaburi ya wazazi mambo yananyooka.
huyo mchungaji atakuwa wa hivi vimakanisa vinavyochipua kama uyoga
 
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.

Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.

Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .

Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .

Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.

Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.

Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.

Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.

Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.

Huyo mchungaji wako hana uelewa wa kutosha juu ya Taalimungu. Mapepo ni Malaika walioasi na pamoja na shetani(malaika mkuu,wakati ule). Sasa kama nia ya hao mapepo ni kumsaka binadamu inakuwaje wakamvizie tu huko makaburini? Ndio kusema hao mapepo hawawezi kum-deal binadamu nje ya eneo la makaburi? Au ndio kusema binadamu hai akiwa sehemu za makaburini anaishiwa nguvu na hivi inakuwa rahisi kwake kushughulikiwa na hao mapepo?
 
nashangaa watu wanaenda makaburini kutembelea!je wao marehemu wakija kututembelea mbona tunakimbia?!
 
Aiseee..pole mkuu sasa uhusiano wa mtoto kulia, wewe kupata ajali na kufilisika ni upi?
hivi wewe ni kilaza kiasi gani?
Umeshaambiwa kule kunakuaga na mapepo au wachawi hutumia maeneo hayo sasa huelewi nn tena hapo?
 
Back
Top Bottom