Kilichomfelisha Tundu Lissu ni kuongea ukweli mbele ya Umma uliozoea uongo, shortcut, unafiki na propaganda

Mtu na nusu

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
636
1,115
Habari wakuu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Hakuna ubishi kuwa hoja zote alizokuwa anaziwasirisha Mhe. Tundu Lissu kipindi cha kampeni zilikua Ni ukweli mtupu.

Ingekuwa anagombea nchi zenye watu wenye uwezo wa kupambanua mambo Basi angeibuka mshindi mapema Sana

Hakuna ubishi nchi yetu imejawa na wimbi kubwa la watu wajinga waliozoea unafiki , uongo , chuki , shortcut , na roho mbaya

Pole mh Tundu Lissu
Badili uraia ukagombee USA.
 
waliomfelisha tundu lisu ni aliokuwa anawatumikia, kutowajua watanzania vizuri, na ndio hao waliopigania mpaka kaondoka
Screenshot_20201110-170347_Twitter.jpg
 
Atafute mwalimu mwenye elimu ya darasa la tatu amfundishe siasa!
Siasa ni kutimiza mategemeo na shida za wananchi.
Angalia kokote wanakopita viongozi kilio cha wazi cha wananchi ni maji, umeme, ajira, hospitali, madawa, barabara, rushwa.
Magufuli anatimiza hayo kwa kasi ya ajabu, na bado anaahidi kutimiza zaidi hayo mahitaji. Anakuwa amewagusa watu moja kwa moja, bila hata kupiga longolongo.

Sasa ndugu yangu Lissu!
Magufuli kapambana na korona kwa kutumia malimao, tangawizi na nyungu, kisha kawambia wananchi India hofu piga kazi, watu wakashangilia korona ikawa siyo tishio. Lissu kabla harudi anamtukana Magufuli kwamba ni idiot na superstitious! Watanzania wanakufa kwa mamilioni kwa korona, na wasipovaa barakoa ndiyo wataisha! Kaja Tz kavaa barakoa kwa masaa machache tu, baada ya hapo kaitupa kule akachanganyikana na umati wa watu wakati alisema tusifanye hivyo! Ni unafiki na kutojielewa kuliko pitiliza!

Kisha akaanza kuponda maendeleo ambayo watu wamekuwa wakiyalilia na wanayafurahia yaliyokwisha letwa lama barabara, hospitali, maji, umeme, na kuyaita maendeleo ya vitu! Sijui akiwa Rais atafanya nini?

Akaanza kuzungumzia vitu superficial ambavyo si mahitaji ya wananchi. Mara tunataka uhuru. Watu wanamshangaa tu, kwa uhuru wote tulio nao tena bila vitisho vya ujambazi wala vibaka Kama ilivyokuwa siku za nyuma!

Mara kuzusha uongo Rais anakutana na wakurugenzi Dodoma muda huu ili kupanga kuiba kura, wakati wananchi wako na hao wakurugenzi 'site' wanapiga kazi! Mara bajeti ya ununuzi wa ndege haukupitishwa na Bunge, wananmwonyesha hansard anasakizia anashangaa! Na uongo mwingine mwingi kama deni la taifa, vitambulisho vya wamachinga nk

Wakamalizia na matukio ya kubumba siku ya kupiga kura kwa kusingizia kuibiwa kura. Wamechapisha vikaratasi vyao feki vya kura, kisha wakaonyesha kisanii na kuvichoma moto haraka haraka ili watu wasigundue vikarasi feki vya kura!

Akamalizia drama kwa kuitisha maandamano yasiyoisha nchi nzima. Wananchi wakabaki wanamshangaa tu, bila kumpa support japo kidogo tu.

Baada ya hapo kakimbilia balozini na Leo amekwea pipa!

Hii move angeifanya "Commedy" toka mwanzo angalau wachache wangemwelewa na kumpa support. Sasa wewe unacheza ustar kwenye muvi ya "No Surrender, no retreat" wakati wewe ni Charlie Chaplin!
 
Wewe mtoa mada kwenu kwenye kupiga kura mawakala wa upinzani waliruhusiwa kusimamia uchaguzi!? Tanga nzima walikataliwa wote
 
Aliibuka mshindi. NECCM wakamtangaza Magufuli msindi. Kura za wananchi hazikuhesabiwa kabisa. Kura zilitoka Ofisi Kuu ya NEC Dodoma zikionyesha Magufuli kashinda kila kituo cha kupigia kura.
Ingekuwa anagombea nchi zenye watu wenye uwezo wa kupambanua mambo Basi angeibuka mshindi mapema Sana
 
Back
Top Bottom