Miundo ya utawala wa Tundu Lissu na Magufuli inaweza kufanana, tofauti ndogo ni kwenye matumizi ya sheria na diplomasia

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Nimejaribu kwa muda mrefu kuwafananisha hawa viongozi wawili ambao mmoja ametangulia mbele za haki kwa mapenzi ya Mola, Hawa viongozi wawili ni Energetic na Ni wakali sana kwenye rasilimali za nchi na ni wazalendo wa kweli.

Tofauti ya ndogo iko katika vipande hivi;
1. Tundu Lissu ni mwanasheria na Marehemu JPM ni mwanasayansi, ndio maana moja alisimama kiutendaji zaidi na mwingi ukali wake ni wa kiuanaharakati zaidi.

2. JPM alikua hasubiri na wala haangalii jambo flani linazuiwa na katiba au sheria ya nchi ili miradi tu ameona lina maslahi na taifa, Tundu Lissu yeye anataka kila kitu kifuate sheria ya nchi na katiba.

3. Lissu anaamini zaidi katika itifaki lakini JPM aliongeza zaidi kwenye matumizi ya nguvu ikiwezekana na wanajeshi wanatumika kwenye tawala za kiraia.

4. Tundu Lissu ni mwanadiplomasia na ana Expusure kubwa kwenye masuala ya kigeni lakini JPM hakua mwanadiplomasia na zaidi aliwatumia waandamizi wake kwenye masuala hayo.

5.JPM alielekeza nguvu nyingi katika kundi moja la watu wanaoitwa Wanyonge, Tundu Lissu yeye anaamini kila mtanzania ana haki sawa na wengine.

6.JPM alikua na uwezo wa kukasirika haraka sana penye jambo ambalo lina ubishani ndani yake na ikiwezekana anatumia mamlaka yake kulimaliza, Tundu Lissu yeye anapenda ubishi na hakubali kushindwa katika jambo.

7.JPM alikua muumini wa maendeleo na ustawi wa vitu lakini Tundu Lissu yeye ni muumini wa maendeleo na ustawi wa watu.

Tabia ziingine zote zilizobakia wanafanya kwa kila kitu wala hakuna ubishi.
Hawa Viongozi kwenye uzalendo sina shaka nao. Kwenye mapenzi yao juu ya taifa hili hakuna shaka.
Anayesema kua JPM mwingine hatokaa atokee katika taifa hili ni waungo na wana maslahi yao. Kiuongozi JPM na Tundu Lissu kwa kiasi kikubwa sana wanashabihiana katika Characters zao.
 
Unasahau TL si mzalendo kama unavyoonesha bali maslahi (tumbo lake kwanza) bila itikadi
 
Tundu Lissu atafaa sana akija kuwa rais . Mana utawala wa sheria ndo muhimu zaidi kuliko ule ambao wengine wako juu ya sheria , Ni mpango wa Mungu kumuacha hai mpaka leo, pia ni mwananchi mzalendo sana na mpambania katika mpya , kwenda ulaya sio kosa ni harakati za kuokoa maisha na naimani Mungu alimwambia akimbie Kama Daudi alivyoambiwa akimbie , kwenye Bible.
 
Binafsi nilikua mpiga kura wa TL ila nilivyoona tweet zake za hivi karibuni anavyoshabikia mambo kama kina Kigogo nikaona huyu jamaa si presidential material inabidi abaki kuwa mwanaharakati na mpiga kelele makoridoni.....

Useless kabsa simpi tena kura yangu akigombea tena. Ameni dissapoint sana....
 
Hivi unaelewa maana ya mtu kukoswa kuuawa?
 
Alikuwa raia wa Tanzania Akapata rafiki anaitwa Robert Amsterdam akaenda kuishi nae ubelgiji.
Acha ujinga, upuuzi na chuki zako hazikusaidia ila ukweli ndio huu. Lissu amenusurika kuuawa na watesi wake anawahisi. Unataka abakie ili amalize? Bahati nzuri Mungu si athumani..
 
3. Lissu anaamini zaidi katika itifaki lakini JPM aliongeza zaidi kwenye matumizi ya nguvu ikiwezekana na wanajeshi wanatumika kwenye tawala za kiraia.

....

Hiyo namba 3. Naomba akazikwe nayo amevuruga morali na ubunifu kutokana na uoga aliopandikiza miongoni mwa watumishi
 
Tundu Lissu atafaa sana akija kuwa rais . Mana utawala wa sheria ndo muhimu zaidi kuliko ule ambao wengine wako juu ya sheria , Ni mpango wa Mungu kumuacha hai mpaka leo, pia ni mwananchi mzalendo sana na mpambania katika mpya , kwenda ulaya sio kosa ni harakati za kuokoa maisha na naimani Mungu alimwambia akimbie Kama Daudi alivyoambiwa akimbie , kwenye Bible.
hayo ni mawazo yako.. but he does not deserve to be the President.
 
Tl will never be the prezda, the closest he got was TLS presida, kama ana hizo attributes azitumie ktk familia yake.
 
Back
Top Bottom