Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,657
- 218,145
Pamoja na juhudi zake binafsi , za serikali anayoiongoza na za chama chake za kuunda kesi za kizushi dhidi ya Wapinzani wake wa kisiasa kwa kushirikiana na ofisi ya DPP pamoja na Jeshi la Polisi huku wengine akiwafunga jela, lakini bado ameshindwa kuumaliza upinzani na sasa amekiri hadharani kwamba hali ya CCM si shwari huku akiunadi hadharani upinzani kwamba una nguvu kubwa ambapo amewaomba viongozi wa chama chake kutobweteka.
Siri ya Upinzani kupenya kwenye siasa za Tanzania ambazo zimepigwa marufuku kwa miaka minne sasa ni mshikamano miongoni mwa viongozi wake na kuondoa uoga (NO HATE NO FEAR), mbinu za kisasa za kufanya siasa ambazo zimeamsha wananchi kote nchini kutambua haki zao , kwa kipindi kirefu sasa ni wabunge wa upinzani pekee wenye uwezo wa kuitisha mikutano ya hadhara japo ndio walengwa wakuu wa mabomu ya Polisi , Uchunguzi mpya umebaini kwamba Jeshi la polisi nchini Tanzania limekamata zaidi wanasiasa wa upinzani ( hasa Chadema ) kuliko lilivyokamata wavuta bangi na majambazi kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ( hii ni rekodi ya dunia )
Cha kushangaza sasa wabunge waCCM ambao wanalindwa na kuheshimiwa na jeshi la polisi hawajawahi kuwa na uwezo wa ushawishi wa kuitisha mkutano hata wa nyumba kumi tu ! hawajawahi kuwa na hoja wala kuwa na mvuto wa kushawishi hata watu wa 5 wa kuhudhuria mkutano , kwa mfano wabunge kama Waitara , Mwakyembe au Mtolea hawana ushawishi wowote kwenye majimbo yao kiasi hawawezi kuitisha hata kikao cha kujadili harusi ya mtu na ikafanikiwa .