William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,376
mpaka kieleweke
Washauri wa huyu Mama tafadhali mshaurini kuwa hapa watu hawaangalii ni nani kaleta hoja ama imetoka wapi ,ila la msingi ni kuangalia jinsi ambavyo masilahi ya taifa yanazingatiwa.
Nawashauri pia wamshauri kuwa kitendo cha Dr.Slaa ,kuendelea kusema juu ya haya mambo ni kuweka msisitizo wa kina ili serikali ilete majibu ya kina na sio vinginevyo.
Ashauriwe kuwa hoja sio imeletwa na nani na yeye alipaswa kujua kuwa,Import Support Commodity ,ilianza mwaka 2006 bunge la mwezi April na liliwekwa bungeni na Dr.Slaa ,natafuta Hansard husika na nitaliweka hapa kwa ushahidi.
Mama ashauriwe kuwa sasa jamii inamfuatilia kila jambo ambalo analifanya na kulizungumza hivyo kauli zake zinachukuliwa kwa uzito mkubwa kuliko ilivyokuwa hapo awali, nisingependa huyu na yeye awekwe kwenye kundi la wasanii ........
Naamini kuwa washauri wake watampa ushauri ili aweze kutoa clarification ya alichosema ili aweze kueleweka, we still need her please.
Mkuu Kieleweke,
Hili lako ndio tunaita darasa la elimu ya siasa kwa wananchi, haya ndio maneno ambayo yanaweza kumuelimisha mwananchi, safi sana angalau once for a change.