Tangu 2006 kuna mengi yametokea kuhusiana na utendaji na uongozi wa Rais Kikwete. Kuna imani ambayo imejengeka kuwa Rais "anashauriwa vibaya" na hivyo huwa anasema au anafanya vitu kwa sababu 'wasaidizi' wake wamemuelekeza vibaya n.k Kuanzia sakata la mapanki na mwitikio wake kuhusu filamu ya Darwin's Nightmare hadi hii ziara ya Marekani kuna vitu vinafanyika na mara zote watu wote hulaumiwa isipokuwa rais mwenyewe.
Tumeona kwenye CCM kama ilivyo kwenye serikali wanalaumiwa watu wengine wote isipokuwa mtu pekee ambaye anastahili kulaumiwa. Mawaziri mara nne wamelaumiwa na wananchi na mara nne ndani ya miaka sita Rais amelazimika kufanya mabadiliko. Lakini mara hizo zote wanalaumiwa ni mawaziri na watendaji isipokuwa mtu pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.
Sasa itachukua muda gani kwa watu wengine kuelewa na kukubali kuwa tatizo yawezekana ni Rais mwenyewe na namna (manner) ya uongozi wake wa kukaa pembeni (hands off approach)? Yawezekana amekuwa akiachilia vitu vitokee kwa sababu hataki kubeba lawama na hivyo watu wengine kabisa walaumiwe? Kwa mfano la Lowassa analaumiwa Mwakyembe, la mawaziri wanalaumiwa watendaji wa chini, la watu kuwajibishwa wanalaumiwa wabunge n.k? Yeye mwenyewe mara zote anakuwa mtu wa kunung'unika asiyekubali kosa lolote au kuwajibika kwa lolote?
Inawezekana pia ni jitihada ya kumuonesha kuwa ame-delegate power na hivyo haitaji kujishughulisha na mambo hayo yote?
...unafananisha Rais aliye mfu na aliye hai?Tatizo ni watu kama wewe, msioelewa tatizo halisi liko wapi. Rais kama Rais anatekeleza majukumu yake zaidi ya Rais yoyote yule wa kabla yake.
Nyerere alifanya nini cha maana kwa miaka 24 aliyokaa madarakani? kutuwacha masikini wa mwisho duniani!
...unafananisha Rais aliye mfu na aliye hai?
...kama anatekeleza majukumu yake kwanini basi hayatekelezeki wala kuonekana yakitekelezwa na watendaji wake?
...Railway kunanuka, Ports kuchafu, Nishati giza, Miundombinu kumepinda, Makazi kumebomoka, NEC CCM makundi, n.k., n.k... au mpaka afikishe miaka 24 ya uongozi ndiyo tupate tathmini?!
Tatizo ni watu kama wewe, msioelewa tatizo halisi liko wapi. Rais kama Rais anatekeleza majukumu yake zaidi ya Rais yoyote yule wa kabla yake.
Nyerere alifanya nini cha maana kwa miaka 24 aliyokaa madarakani? kutuwacha masikini wa mwisho duniani!
So kwa kifupi JK ndiye tatizo kubwa, na ndiye chanzo cha hayo mengine (ktk awamu yake hii mbovu kabisa)!