Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
Kwani Lowassa, Membe na Sitta siyo wapinzani wa JK?
Mzee Mwanakijiji hawa sio wapinzani wa JK kwa sababu JK hagombei 2015!.

Kama Chadema itaendelea kucheza makida makida ya hide and seek kwenye urais wa 2015, then rest assured, rais ajaye yuu miongoni mwa watatu hao na tutaindandika Malawi immediately there after kama itashikilia msimamo wa kung'ang'ania mpaka bandia wa mkoloni Mwingereza aliyeupoka Tanganyika!.

Leo ni tarehe 20 Agosti, 2012, take note ya hii tarehe, nitakukumbusha haya maneno 20 Agosti 2015!.
 
hata mi nimesikia aibu sana anaacha kujitetea anasingizia wapinzani,mbona sijasikia hata kiongozi mmoja wa upinzani akisema tuingie vitani,nazni membe ,lowassa ndio wapinzani.
 
Source: BBC..anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.mytake Lowassa,membe,Sitta ni Wapinzani?

Hakupepesa macho???? Inasikititisha ukweli usimamiwe KWA ukweli Jamani SO SAD!!!!, kweli Siasa ni mchezo Mchau, nimeamini DUUUUU!!!!! Hata Nyasa Times limunukuu hivyo, so sad, Uwongo mkavu
 
Walichosema Membe na EL ndicho sahihi and in fact ndicho kilichotakiwa kusemwa na JK yeye kama Amiri Jeshi Mkuu!.

Kazi ya jeshi ni kulinda nchi na mipaka yake 24/7. Nchi jirani inajimegea pande la Tanzania kwa kuhamisha mpaka halali huku Amiri Jeshi wetu akiponda maraha kwenye trips bila kusema chochote na badala yake anafunguka pale tuu alipokutana na she wa Malawi ndipo anapojitangaza yeye ndie Amiri Jeshi!.

Mpaka halali ni katikati ya Ziwa Nyasa, Baada ya kushindwa vita kuu ya Kwanza, Waingereza waliipoka Tanganyika ule mpaka na kuukabidhi kwa Malawi. Ilitakiwa ile siku tunapata Uhuru na mpaka urudishwe, haukurudishwa hadi sasa Wamalawi wanajiona ni halali yao na wamejiapiza kufa nao!.

Msimamo wa EL na Membe ndio msimamo thabiti, mpaka ni pasu pasu na hakuna mjadala wala diplomasia chini ya hapo!.

Kwa vile tayari kuna dhana ya "Dhaifu" kushindwa kufanya maamuzi magumu na kuopt kubembeleza, na tumesha subiri mpaka halali kwa kipindi cha miaka 50, hatuwezi kushindwa kuvumilia miaka miwili na nusu iliyobakia ambapo nchi itatwaliwa na amiri jeshi ambaye sio dhaifu ataurudisha mpaka halali mahala pake!.

Niungeni mkono 2015 kwe CCM asimame ama EL, ama Membe tupate ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Pasco.

Hapo kwenye RED, ni mkataba gani ulio-revoke Anglo-Germany Treaty of 1890 kwa kuuondoa mpaka kwenye eastern cost of Lake Nyasa na kuupeleka katikati ya ziwa. Heligoland treaty haikuipa Dautch East Africa hata tone moja la ziwa hilo.

Pasco, wewe ni mwandishi, kama huna facts you better keep deep silence than acting otherwise.
 
hivi jk anamamlaka gani ya kubadilisha mipaka ya nchi.? Kisa amiri jeshi mkuu ndio afanye upuuzi namna hii. Wakati anaapa kulinda mipaka alijua ni mipaka ya mikoa na wilaya...Naona aibu kuwa na riasi kama huyu ila sina jinsi.!
 
Aliyetamka kuhusu vita najua alikuwa Amri Jeshi Mkuu mr Lowasa sasa wapinzani gani anasemelea hapa. wapinzani ndani ya CCM au?

Manake hakuna wapinzani wa nje waliotamka kuhusu vita.
 
Source: BBC..anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.mytake Lowassa,membe,Sitta ni Wapinzani?

Ni kweli Lowassa, Membe, Sitta et al ni wapinzani. JK anajua kuwa serikali ijayo si ya ccm, na kwa hakika mgogoro huu hautamalizwa na ccm bali chama kingine, CHADEMA. Hivyo wote waliotoa kauli ile ni wapinzania.
 
Tunahitaji rais mwanamke. Malawi wameweza, nasi tutaweza. Nimeipenda hii kasi ya malawi!
 
Ni kweli wapinzani kama chama hakuna hata mmoja aliyeongelea kuhusu vita na Malawi. Na ukiyasoma matamko yote ya wapinzani hayakosi neno "international arbitration".

Hii maaana yake ni nini? Maana yake ni kwamba through international arbitration kila mmoja yaani Tanzania na Malawi will lay her facts on table.

Ni wazi Malawi wataweka Heligoland Treaty ambayo inajulikana duniani kote ilisema kwamba mpaka haukuipa Tanzania hata tine moja la maji.

Tanzania tutaweka nini kama facts zetu. Hakuna.

Hivyo, wapinzani wanajua kwamba Tanzania hatuna kitu hapa na ndiyo maana hawawezi kutamka tofauti na walivyotamka.

Tuje kwenye matamshi ya watu binafsi. tena tuje humuhumu JF. Chukua ID za wote humu waliotaja neno kuitwanga Malawi na kuishawishi Tanzania ipuuzie Heligoland Treaty of 1890.

Ukiweza kukusanya ID zao basi angalia trend au history yao humu ya ushabiki wao wa vyama yaani CCM au CHADEMA. Hata kama mtu hatoi contribution basi angalia huwa anatoa LIKE kinaposifiwa au kupondwa chama gani.

Mimi siipendi CCM na nimeutetea ukweli kwamba Tanzania hatuna hata tone moja la ziwa na sijaona comment ya kunizidi uelewa ili nijifunze.

Lakini ukifanya niliyosema na kama hata JK alikuwa anachughulia humu JF kwa kufanya nilivyosema basi alikuwa na haki ya kusema ni wapinzani waliopandwa na jazba. Kama siyo jazab kwa nini umponde mtu anayetetea ukweli bila kuleta vigezo vyako kana kwamba shuleni hukujifunza kuleta vigezo bali ulijifunza kudesa.

Hivyo, JK yuko sahihi kwa hili.
 
Source: BBC..anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.mytake Lowassa,membe,Sitta ni Wapinzani?
Nimesikiliza hata mimi. Kwa staili ya Urais wa JK hata mimi naweza kuongoza nchi vizuri zaidi kuliko yeye. Walioweka kipengere cha kuwa na miaka 40 ili uwe Rais hawakutarajia mtu mzima kama JK awe na mambo ya hovyo kama haya. Hajui kwanini Tanzania ni maskini, hajui mmiliki wa Dowans. Huyu ndio Jk ambaye kazi yake ni kuhudhuria misiba na kuwaona wagonjwa! Nchi ipo likizo kwa miaka 10. Ole wetu!!!
 
Source: BBC..anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.mytake Lowassa,membe,Sitta ni Wapinzani?

Sijawahi kuona raisi thaifu kama JK yaani anawaonyesha kua nchiyake inauthaifu wauongozi.
Kulikua na hajagani yakumwambia kua niwapinzani wana sema

JK asiwe anaongea navyombo vyahabari vyanje hata sikumoja abakina wahariri wetu wabonho tu

Huu niujinga na huuuthaifuutatupeleka mbali
Je kama malawiwakiendelea na kutafuta mafutaleo nani atawauliza?
 
sipendi kabisa kumuongelea huyu bwana, lakini saa nyingine unashindwa kujizuia, unafki umemzidi mno, yeye ujifanya mzuri kwa kila mtu, lakini kitu muhimi ni wapinzania wamuulize aeleze kinaga ubaga kuhusu hili kuendelea kumcheka atatutia vidole machoni
 
kama Malawi jirani yetu nchi ndogo tena ya Africa wanatushinda.! Sipati picha akikaa na akina Obama Cameroon, sijui huwa anaongea nini zaidi ya ndio mzee na kuchekacheka tu.!
 
80% ya watanzania ndio mlimuweka madarakani. Sasa mnajuta nini? Hamkujua kuwa "majuto ni mjukuu". Let him finish his term, no mistakes again.
 
...labda reference yake ni JF hapa...hahaaaahaaaaa....
Daudi alitenda dhambi sababu ni mwanamke..
Samson nae.......
Suleimani kadhalika...
Jk ooooh...oooooh.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom