Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
kama hii habari ni ya kweli sasa nimeamini kuwa Jk naye ni empty head chap! ni kiongozi yupi wa upinzani hata mmoja aliyewahi kuchochea vita na malawi? halafu anaposema katu hatutapigana na malawi maana yake hata wakiingia ndani ya mipaka yetu tutawaacha tu? hiyo kweli ni kauli ya amiri jeshi mkuu,? sikuwa naamini tuna amiri jeshi mkuu muoga! kidiplomasia alitakiwa kusema Tanzania haikusudii wala haina mpango wa vita na Malawi au Jirani yoyote ila ni jukumu lake kama rais na amiri jeshi mkuu kulinda mipaka ya nchi na raia wake! hiyo ingepeleka ujumbe tosha kuwa sio kwa malawi tu ila jirani mwingine yeyote akituchokoza hatutakaa kimya!

Mkuu endelea kuamini hivyo kwani mimi pia nimesikia BBC wakisama eti JK kasema wapinzani wanachochea vita na Malawi kwa Uroho wa Madaraka! Ukishangaa ya Nape Utakutana na JK. Kwa JK kauli za Sita, Membe na Lowassa ni za wapinzani! Leo usiku Lowassa atkuwa akihijiwa na ITV dk 45 anakanusha kuwa na kusema watu walipotesha kali yake. Angalia dk 45 ITV leo.
 
Dah!kweli rais tunae!kumbe Mwalimu alikua na vigezo vya msingi sana kumkataa huyu mtu by then,haikua umri peke yake bali hata thinking capacity!kauli hii ni aibu kwa nchi nzima,bora 2015 ifike na aondoke tu maana kwa sasa nchi ni auto pilot,inajiendea tu,hatuna kiongozi kwa aina ya mtu wa namna hii,empty head chap!
 
Tukisema anacopy na kupest je,
Siku akiwa peke yake utasikia,
Najua kesho Rais Jk akiulizwa atasema hajasema
 
Mkuu endelea kuamini hivyo kwani mimi pia nimesikia BBC wakisama eti JK kasema wapinzani wanachochea vita na Malawi kwa Uroho wa Madaraka! Ukishangaa ya Nape Utakutana na JK. Kwa JK kauli za Sita, Membe na Lowassa ni za wapinzani! Leo usiku Lowassa atkuwa akihijiwa na ITV dk 45 anakanusha kuwa na kusema watu walipotesha kali yake. Angalia dk 45 ITV leo.

Wanatapatapa tu,Watanzania sasa wanaamka na wameazimia 2015 c.c.m kua history,akanushe aseme kweli aliongea hvyo kauli zao hazina tija kwetu,wametudanganya na kutuibia for 50 yearz then tuje kuwaamini kwa uongo wao wa siku moja?inahitaji kua na phd ya u.j.i.n.g.a kuweza kua supporter wa magamba,au labda uwe unafaidika moja kwa moja na mirija ya dhuluma na uporaji inayofanywa na magamba!their days are numbered!wajiandae kutujibu haya majumba ya kifahari kila kona,na hotel zinazojengwa milimani na kuvuka mipaka ya mali asili kama kule Bigwa Morogoro kwa kivuli cha umiliki wa Mbena Malumbi wakati wake zao na watoto zao tunawaona wakienda kukagua ujenzi,hizo pesa wanapata wapi,lazima waje kutujibu!
 
Ni kweli wapinzani kama chama hakuna hata mmoja aliyeongelea kuhusu vita na Malawi. Na ukiyasoma matamko yote ya wapinzani hayakosi neno "international arbitration".

Hii maaana yake ni nini? Maana yake ni kwamba through international arbitration kila mmoja yaani Tanzania na Malawi will lay her facts on table.

Ni wazi Malawi wataweka Heligoland Treaty ambayo inajulikana duniani kote ilisema kwamba mpaka haukuipa Tanzania hata tine moja la maji.

Tanzania tutaweka nini kama facts zetu. Hakuna.

Hivyo, wapinzani wanajua kwamba Tanzania hatuna kitu hapa na ndiyo maana hawawezi kutamka tofauti na walivyotamka.

Tuje kwenye matamshi ya watu binafsi. tena tuje humuhumu JF. Chukua ID za wote humu waliotaja neno kuitwanga Malawi na kuishawishi Tanzania ipuuzie Heligoland Treaty of 1890.

Ukiweza kukusanya ID zao basi angalia trend au history yao humu ya ushabiki wao wa vyama yaani CCM au CHADEMA. Hata kama mtu hatoi contribution basi angalia huwa anatoa LIKE kinaposifiwa au kupondwa chama gani.

Mimi siipendi CCM na nimeutetea ukweli kwamba Tanzania hatuna hata tone moja la ziwa na sijaona comment ya kunizidi uelewa ili nijifunze.

Lakini ukifanya niliyosema na kama hata JK alikuwa anachughulia humu JF kwa kufanya nilivyosema basi alikuwa na haki ya kusema ni wapinzani waliopandwa na jazba. Kama siyo jazab kwa nini umponde mtu anayetetea ukweli bila kuleta vigezo vyako kana kwamba shuleni hukujifunza kuleta vigezo bali ulijifunza kudesa.

Hivyo, JK yuko sahihi kwa hili.
Nikupateje usiwe na akili kama za wanasayansi wa kale walioamini kuwa dunia iko kama meza wakaweka na sheria kuzuia mtu/mwanasayansi yeyote kufikiri ama kutamka vinginevyo.

Wakati unajifungia kwenye uelewa huo, chungulia kwenye ufa uyasome maandiko.

Jumuiya ya kimataifa (UN) ilipitisha sheria isiyohitaji utapeli wa namna yoyote wala nguvu ya ushawishi wa pesa za kirushwa rushwa. Na haihitaji lot of paper works,

NCHI MBILI ZIKIPAKANIA ZIWANI, AUTOMATIC MPAKA NI KATIKATI YA HILO ZIWA.

Sheria hii imetungwa na kukubaliwa na member states huku wahusika wakijua fika kuwa lengo lake ni ku-neutralise hizo old fassioned treaties.
Kumbuka hakuna nchi mpya imeanzishwa zaidi ya sudani kusini, uujue ukweli uliobebwa kimantiki na sheria hii. Ni uelewa tu utawafanya wamalawi kugundua ukweli huu.
 
Last edited by a moderator:
Ivi hiyo deligation ya tanzania inayoelekea MZUZU ktk meza ya wine ndo akina nani..wasije wakapelekwa vjizee ilimradi posho inaingia kumbe hawana skills za diplomac.
 
we are ready to defend our sovereignty at any cost," said Committee Chairman, Edward Lowassa (CCM).

Mr Bernard Membe, strongly warned Tanzania’s southern neighbour, Malawi. He ordered an immediate stop to all gas and oil prospecting activities on the portion of Lake Nyasa that falls on the Tanzania side.

Prof Abdallah Safari(CDM), a lawyer and expert in international relations, urged both countries to respect the international laws which show boundaries between countries

Prof Mwesiga Baregu(CDM) warned both countries not to engage in military confrontation. Rather, said the Professor in Political Science and International Relations, the two countries should resolve the dispute diplomatically. “Both countries should not be drawn into military action because the consequence of doing so is very dire not only to Tanzania and Malawi but for the entire Sadc (Southern Africa Development Community) region,” warned Prof Baregu
haya hapo mpinzani yupi ccm yupi????

Inasikitisha sana tunapokua na Raisi Mwongo na asiyejiamini.Sote tulisikia kauli za Membe na Lowasa, tukasikia pia kauli za upinzani toka kwa Prof Safari,Baregu na Lipumba.Je! Ni wepi hapo walokua wakihimiza vita? Au ndio yale anapewa taarifa potofu? Mie binafsi naona aibu kuwa na Rais wa namna hii
 
Nikupateje usiwe na akili kama za wanasayansi wa kale walioamini kuwa dunia iko kama meza wakaweka na sheria kuzuia mtu/mwanasayansi yeyote kufikiri ama kutamka vinginevyo.

Wakati unajifungia kwenye uelewa huo, chungulia kwenye ufa uyasome maandiko.

Jumuiya ya kimataifa (UN) ilipitisha sheria isiyohitaji utapeli wa namna yoyote wala nguvu ya ushawishi wa pesa za kirushwa rushwa. Na haihitaji lot of paper works,

NCHI MBILI ZIKIPAKANIA ZIWANI, AUTOMATIC MPAKA NI KATIKATI YA HILO ZIWA.

Sheria hii imetungwa na kukubaliwa na member states huku wahusika wakijua fika kuwa lengo lake ni ku-neutralise hizo old fassioned treaties.
Kumbuka hakuna nchi mpya imeanzishwa zaidi ya sudani kusini, uujue ukweli uliobebwa kimantiki na sheria hii. Ni uelewa tu utawafanya wamalawi kugundua ukweli huu.

Hujasoma hata sentensi moja ya sheria hiyo, la sivyo usingesema hilo ambalo tumelieieza vizuri na hatuna haja ya kurudia kwa anayekurupuka na kudandia treni kwa mbele.
 
Nikupateje usiwe na akili kama za wanasayansi wa kale walioamini kuwa dunia iko kama meza wakaweka na sheria kuzuia mtu/mwanasayansi yeyote kufikiri ama kutamka vinginevyo.

Wakati unajifungia kwenye uelewa huo, chungulia kwenye ufa uyasome maandiko.

Jumuiya ya kimataifa (UN) ilipitisha sheria isiyohitaji utapeli wa namna yoyote wala nguvu ya ushawishi wa pesa za kirushwa rushwa. Na haihitaji lot of paper works,

NCHI MBILI ZIKIPAKANIA ZIWANI, AUTOMATIC MPAKA NI KATIKATI YA HILO ZIWA.

Sheria hii imetungwa na kukubaliwa na member states huku wahusika wakijua fika kuwa lengo lake ni ku-neutralise hizo old fassioned treaties.
Kumbuka hakuna nchi mpya imeanzishwa zaidi ya sudani kusini, uujue ukweli uliobebwa kimantiki na sheria hii. Ni uelewa tu utawafanya wamalawi kugundua ukweli huu.

Mkuu tumia akili pia katika kufikiri, Ziwa Nyasa limepakana na nchi tatu, kama Tanzania na Malawi watachukua nusu kwa nusu, Msumbiji nao watachukua nini?
 
Last edited by a moderator:
Upea wa kufikiri wa kiongozi ni mdogo. Mgogoro wa mpaka siyo wa kisiasa, ni wa kitaifa. Hapa ni kuweka pembeni tofauti zetu za kisiasa na kujiunga kuwa kitu kimoja kutetea taifa la Tanzania.
 
Source: BBC..anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.mytake Lowassa,membe,Sitta ni Wapinzani?

Source ni BBC au Nyasatimes?Hebu tunaomba utuwekee link mkuu tukashuhudie wenyewe maana nakuwa mgumu kidogo kuiamini hii post!Samahani lakini.
 
Mkuu tumia akili pia katika kufikiri, Ziwa Nyasa limepakana na nchi tatu, kama Tanzania na Malawi watachukua nusu kwa nusu, Msumbiji nao watachukua nini?

Hv mgawanyo wa lake Victoria upo vipi mkuu?
 
Inasikitisha sana tunapokua na Raisi Mwongo na asiyejiamini.Sote tulisikia kauli za Membe na Lowasa, tukasikia pia kauli za upinzani toka kwa Prof Safari,Baregu na Lipumba.Je! Ni wepi hapo walokua wakihimiza vita? Au ndio yale anapewa taarifa potofu? Mie binafsi naona aibu kuwa na Rais wa namna hii

simply usione aibu miaka saba sasa nchi haina rais yupo mtalii fulani tu hivi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom