Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Kikwete unamuogopa Mwakyembe

Yeye pia ni binadam kuna mda anaweza kwenda tofauti,yeye sio mungu!!!! Mbona hatusemi wizara zingine?!,ujue hadi tunaongea inamaana kuna kitu hakijaenda sawa!!!!

TAMISEMI imeenda sawa kwa mfano? Maswali ni mengi kuliko majibu
 
Mto ngana na songwe, kila mwaka mafuriko, kwanini, asigeboresha kama mkapa alipojijengea daraja la kwao masasi?
 
Mwakyembe alienda Marekani na kutia saini ya makubaliano ili kuleta reli ya uwanja wa ndege wa Dar es Salaam. Muwekezaji aliyehusika inadaiwa ni tapeli anayefahamika duniani. Ndugu Shumake. Ni vizuri wamemuhamisha kuepusha hili dili lisiendelee.

Labda kama sababu ni hiyo. Wazee wa vetting labda kuna kitu wamekiona kwake. Ila ilipaswa tu wamwambie hiki usifanye. Zee la viwango tusubiri kama ataweza
 
Khaa!! Kuna akili za ajabu sana humu. Ndiyo maana tulishauri waziri asiwe mbunge kwa sababu ya ujingaujinga kama huu. BTW sasa hivi lahamia wizara mpya labda ataipigania Kyela ihamie Nairobi au Kigali
 
Jamani tumwache rais afanye kazi yeye ndo mwenye dhamana

Nawachukia sana watu wenye mawazo kama yako. Yawezekana hujawahi hata kulipa kodi ndani ya nchi hii. Lakini hata vocha hununui? Maana hata mawasiliano yako juu kwasababu ya watu wachache wezi. Pole ndugu jitathimini saaana
 
mkashitaki ikulu,kwani lazima atumikie uchukuzi? rais kafanya vile ili kuleta ufanisi
 
Nilikuwa.sifahamu.kuwa.kwenda wizara ya.afrika.mashariki ni.adhabu na.kwamba kuna.watu.hawafai.kuitumikia ile.wizara

Huwezi kujua kwasababu hutaki kujua, ila ukitaka kujua utajua
 
Kumbe sitta huwa anaigiza na akina wolper,na ray

Nilikuwa namuheshimu sana yule mzee, ila amekuwa akifanya juhudi za kujisafisha kwa boss wake. Kwenye katiba ndo heshima zote ziliisha na hii inadhihirisha kuwa jamaa ni bonge la acter, yuko kwa masilahi yake na kutaka heshima ambazo hadi sasa keshazikosa kwa wananchi. Miez hii ilobaki itakuwa balaa pale bandar na airport
 
Tatizo sio uwaziri alionao, tunachosema hata ubunge aliopewa bado hajaitendea haki wilaya yake, jimbo lake linarudi nyuma badala ya kwenda mbele, Huyu mwakyembe katurudisha enzi za kasyupa, barabara ni vumbi kiasi kwamba umatakiwa utembee na ndoo ya maji ya kunawa ukifika uendapo, kyela ninayoijua mim umeme haukuwahi kukatika wakati tunahudumiwa na kiwika coal mine, lakin siku hzi umeme unaweza kukatika hata siku 3 bila maelezo ya msingi, kwel kyela imechakaaa sana si kyela niliyokulia.
Kwakeli inasikitisha sana kuona mbunge hajali jimbo lake.
Pia kitendo chakumchagua mtu ambaye familia yake inaishi Dar ni kosa kubwa, kwasababu si rahis kujua adha mnazopata wananchi, kasafisha kibarabara cha ikolo kwa kua mama yake yupo kule,
Abhandu bha kukyela mungamleka umundu hujhu, tukatele na loli.
 
Kyela bado haijapata mbunge. Na Mijitu ya kyela ni mibonafsi sana
 
Kama huijui Kyela nyamaza tafadhali
Kyela tuna bandari HAJAWAHI igusa hata kwa miundo mbinu kila siku tunaona anaimarisha bandai ya Dar,Mwanza na Tanga
Kyela tuna meli chakavu zinazo zima katikati ya ziwa kila siku lkn ni Mwakyembe aliyeipa Mwanza hela za meli mpya!

Mwakyembe ni mbunge wa hovyo hovyo kupata kutokea ktk Wilaya ya Kyela na hawezi shinda hata kura za maoni
achilia mbali kupambana na CHADEMA
Malafyae unamuonea tu MWAKYEMBE, huko Mwanza hajapeleka meli wala kujenga bandari! Hata Dar bandari hajajenga. Labda useme huko anakutembea sana kila mara na huko kwenye bandari ya kwenu haji mara kwa mara. Hiyo ni kwa vile anakufahamu sana huko haitaji kuja kufahamu matatizo yake.
 
wananchi wa jimbo la kyela tulipata faraja kubwa baada ya kukabidhiwa wizara hii, umeshindwa kuiga kwa mawaziri wenzio,

Uwaziri sio kupindisha mipango ya serikali kwa faida ya jimbo lako, usimlinganishe Harisson na vibaka ktk siasa, alilitumikia taifa sio kyela pekeee
 
100% hujawahi fika Kyela!
100% hujawahi iona Kyela ya Mbunge Mwakipesile na Mbunge Mwakyembe
100% hujui kama Kyela nayo ina bandari na ina meli mbovu na Mwakyembe kama Mbunge wetu hajawahi hata fika bandarini kuona tatizo wanalopata wapiga kura bandarini hapo
100% wala hujui Mbunge kwanza ahudumie matatizo ya wapiga kura wake kingine ndiyo kinafuatia

Kama mmnampenda Mwakyembe mshaurini agombee kwenye majimbo yenu,huku anajua hapiti hajafanya lolote kwa miaka yake hii 10

Then unapoleta hoja ACHA KUTUMIA LUGHA ZA KUKERA,tumia lugha nyoofu utaeleweka zaidi!Neno una akili wewe sidhani kama hapa ni mahali pale

Kitendo cha kusema 100% hajawahi fika kyela wakati unakumbuka kuwa hata wakati wa janga la mafuriko alikuwepo kyela,hapo umeshanikatisha tamaa kujadili mada.au ulitaka aache ofisi Dar aje kulala kyela?Hata hivyo tunataka mlalamike kwa ubunge wake,sio mnakuja kulalamika eti Mwakiembe hakuifanyia kitu kyela kwa nafasi yake ya uwaziri.je kama hakupata loophole ya kuipendelea kyela?afanye tu?c ndio?
 
Mkuu

pixel 23:58 Today
Mleta mada ana ujasiri wa ajabu sana kuleta mada
kama hii public.ni hatari sana kustimulate waziri
apendelee kwao,yani waziri asipeleke meli
iliyoahidiwa na mhe.Rais/chama wakati wa
kampeni ila aipeleke kyela kwao?

Yaani ungejua jimboni kwake ambako ni kwetu kulivyo wala hata usingemponda mleta maada...ndugu yangu hali ni mbaya sana...baada ya kupata dhoruba ile iliyompelekea kuugua...aliwahi ahidi (NASIKIA) kuwa jk akimchagua uwaziri hata kubali tena..kumbe ilikuwa ahadi ya buree...tu!! sasa hilo ni tisa...

Matatizo tuliyokuwa nayo miaka ya 1995 mpaka leo yapo umeme maeneo ya mabunga, kisale mpaka leo kimya lakini alituahidi mda mrefu ssaaaaana, huduma za jamii bado hatuna kwa hiyo

mtoa maada hajakosea kabisa kuleta maada hii hapa..

pia tukumbuke kuwa wanainchi tunataka mabadiliko saaa hivi...kwa hiyo tunamkaribisha 2015 aje kupumzika huku mabhunga kisale...baada ya kulitumikia taifa huko.

Mkuu mimi nakuelewa vizuri,ila kutaka upendeleo bila sifa stahiki ni kosa kubwa sana.Haiwezi kupelekwa Meli ambayo kimsingi Rais aliahidi iende ziwa victoria halafu Mwakiembe aipeleke kyela.hivi hapo unapaonaje?
 
Kama huijui Kyela nyamaza tafadhali
Kyela tuna bandari HAJAWAHI igusa hata kwa miundo mbinu kila siku tunaona anaimarisha bandai ya Dar,Mwanza na Tanga
Kyela tuna meli chakavu zinazo zima katikati ya ziwa kila siku lkn ni Mwakyembe aliyeipa Mwanza hela za meli mpya!

Mwakyembe ni mbunge wa hovyo hovyo kupata kutokea ktk Wilaya ya Kyela na hawezi shinda hata kura za maoni
achilia mbali kupambana na CHADEMA

Yapasa kuwa waangalifu. Mnaweza kudhani hafai kiasi hicho mkaja mkampata mwingine ambae ni taizo zaidi mkaishia kunyang'anywa hata kidogo mlicho nacho.
 
Mleta mada ana ujasiri wa ajabu sana kuleta mada kama hii public.ni hatari sana kustimulate waziri apendelee kwao,yani waziri asipeleke meli iliyoahidiwa na mhe.Rais/chama wakati wa kampeni ila aipeleke kyela kwao?
Si lazima alete meli , lakini ukumbuke kwamba Mwakyembe kama mbunge alikuwa na ahadi za kuboresha miundo mbinu kwenye jimbo lake , sasa kama ameshindwa akiwa jikoni ataweza akiwa bafuni ? Lingine ni kwamba hakuna waziri yeyote aliyekatazwa kutimiza ahadi jimboni kwake , hakuna andiko la namna hiyo ! Bali ukweli ni kwamba Mwakyembe ameshindwa kutimiza kile alichoahidi kyela na ATAVUNA ALICHOPANDA , HAKUNA CHA MSWALIE MTUME WALA YESU NI JIBU .
 
Mkuu bandari ya Kyela maarufu kama Itungi Port ipo ktk kata ya Kajunjumele nyumbani kwa mama yake Mwakyembe!Ni Bandari ya asili ambayo haijachimbwa kina chake na ina mchanga mweupe unao anzia Mwaya kutambaa hadi Ikombe kwa upande wa pili!Ni bandari inayohudumia nchi za Msumbiji na Malawi lkn biashara imedorara sababu ya uchakavu wa meli zake MV Iringa na MV Songea!

Mwakyembe hapatani na wapiga kura wa kata hiyo sana kwa sababukuu 2: Kwanza ilikuwa ngome kuu ya Mwakipesile na walimnyima kura Mwakyembe uchaguzi wa 2005 na sababu ya pili ni uchafuzi wa mazingira wa meli za Malawi zinazoleta makaa ya mawe toka Mchuchuma na malori ya Mbeya Cement yana pakua makaa hayo toka pale kijijini yanaharibu sana mazingira!Wananchi wamemuomba Mwakyembe aingilie kati bila majibu

Wakati wa Mwakipesile bandari hii ilikuwa chanzo kikubwa sana cha ajira kwa wazawa
MUNGU akulinde sana mkuu .
 
Abhandu bha Kyela na gwa kutukujhu bha ka na mahala kabisa. Mwakyembe ikubhuja na Mwakyusa jhope ikubhuja mwi bunge
Nakamo nakamo , kangi ngubhula ukuti mwakyembe mma imbombo jake mwa kyela jimalike , ngasimanya isya mwakyusa .
 
Back
Top Bottom