- Tanzania wakati mwingine inaudhi kweli, Wamarekani wamefanya mambo ya stimulus package kwa sababu uchumi wao ulikuwa bomba, lakini ukaharibika na matatizo ya bad credit, sasa sisi bongo yametukutia wapi hayo? Lini uchumi wetu uliwahi kuwa bomba sasa eti tunataka kuurekebisha ili urudie tena aaaahhhhgrrrrrr?
- Hapo kuna ka-mchezo ka-EPA kanataka kuchezwa, halafu wananchi tukishituka basi wachezaji wataambiwa warudishe tu serikalini,
Mungu Ibariki Tanzania.
William.
Mkuu nadhani lugha inayotumika hapa ndio somo zima.. Hili neno BAIL OUT Na STIMULUS limekuwa mbiu ya kiuchumi kila mtu hata maskini ombaomba anatumia siku hizi..
Lakini pamoja na yote haya Tanzania ni lazima itakuwa affected na Depression! hilo wazi kabisa sii leo wala kesho lakini tutakuja ipata itachukua muda kama Hurricane Category 5 ilopitia India tunaweza pata mafuriko yake pwani yetu ambayo ni tosha kabisa kuteketeza vibanda vyetu vya uchumi...kwa sababu hata wakati wa Nyerere mwaka 1982 tulifikiria hilo haliwezi kutukuta kwa sababu ya mfumo wetu wa uchumi chini ya Ujamaa hatukuwa karibu kabisa na hizo biashara walizokuwa wakizungumzia..
Kitu kimoja tu tufahamu ni kwamba mashirika yote ya nje yanayochukua cocontracts nchini ama kuwekeza nchini wamekuwa Bailed out from day one..Tumeona Richmond, TRC, ATC na mashirika mengine mengi tena binafsi yaliyonunua mashirika ya Umma yakitegemea serikali kulipa baadhi ya matumizi makubwa ya mashirika haya tena basi bila serikali kuchukua share kutokana na ongezeko la mtaji huo ndani..Hivyo,bail out ipo siku nyingi tu ila tulikuwa na lugha yetu wenyewe..
Sasa tunapokuja kutazama hali ya Uchumi huu wa sasa nadhani ni muhimu sana kwa rais wetu kuangalia mchango wa vyombo hivyo ktk uchumi wetu, huwezi ku bail Out bank ambayo haitowi mikopo kwa mashrika wala sii kazi ya serikali ku bail out mashirika yanayoanguka kwa sababu kwanza hayapo ktk soko letu la Taifa..Hatufahamu chanzo na sababu ya mashirika au viwanda hivi kuanguka..Na muhimu zaidi hatujawahi kuliweka kitimoto hata shirika moja kutazama uzembe unatoka wapi.
.
Tusipoangalia tunafanya nini tutarudi kule kule alipoangukia Nyerere..swala halikuwa soko pekee, bali uzalishaji wenyewe ulipungua kiasi kwamba viwanda vingi vilizalisha chini ya kiwango chake na uzembe ulitokana na sisi wenyewe wananchi..Tunajua sote tumefanya kazi wakati wa mwalimu. Mtu anaamua lunchtime ya masaa mawili, Break hazina hesabu kwenda kununua mboga au kukutana na mshakaji alokuja mtembelea ofisini.. Gari la serikali unalitumia kwenda jirusha, kwa siku mtu anakaa kazini masaa matano, nayule aliyekaa siku nzima kazalisha kazi ya masaa mawili wakati mshahara haubadiliki kulingana na uzalishaji..Kweli mkuu tungeweza kupona?..
Hapo hata wahisani walishindwa kuingia fedha yao kwani mikopo wanayoitoa ilikuwa inatazama possibility za kurudisha fedha yao na hata Bail Out inatakiwa kutazama uwezekano mkubwa wa kuzalisha na ku supply kulingana na demand inayotegemewa..
Nchi zote za kijamaa zilizalisha mali kulingana na mahitaji yao wao wenyewe, horticultural products ni zile tulizoachwa na soko la mkoloni miaka 50 iliyopita. Vitu kama Pamba, Kahawa na Katani ni mazao ambayo kwa miaka zaidi ya 70 yametupa kula tu, yameshindwa kukuza uchumi wetu wala hakuna nchi dunaini inategemea mazao haya tena..Tunaposema kilimo ni pamoja na mbinu mpya, mazao mapya kwa kuzingatia soko na wapi dunia ya kesho itategemea kutoka ktk kilimo..Huko ndiko unakowekesha nguvu na mtaji wako..
Katika mahojiano ya JK na CNN niliposikia Kikwete akizungumzia Pamba na anguko la bei duniani akasema anataka ku stimulate zao hilo nilishtuka sana kwa sababu amesema sababu ni bei kushuka kisha wewe ndio kwanza unaingiza fedha yako mahala ambapo demand yake imeshuka na sii swala la kwamba tumeshindwa kukidhi demand ya mali hiyo kutokana na hali mbaya ya wakulima ktk mtaji..hapo si tunapika chakula wakati hakuna walaji jamani?.
Kwa hiyo unaongeza ajira au fedha kwa mkulima ambaye anajua mali yake haina soko...tunafanya kitu gani hapa! Kisha basi kibaya zaidi ni kwamba hizo bank hazikopeshi wakulima nazo zinakuwa bailed out na hapo hapo it's only less than 20% ya Watanzania wafanya biahsra hupata mikopo ya Banks hizi...Hiuzi hizi banksa zilikataa kuwakoppesha wananchi kwa sababu hawana creditline wakati wa mabillioni ya Saccos... leo kimebadilika kitu gani..Na kibaya zaidi ya yote ni kwamba mabillioni ya fedha za Banks zatu ziko mikononi mwa watu wanaokataa kulipa hadi wafikishwe mahakamani..Billions of dollar zimechukuliwa kwa mtindo wa uhisani yaani unachukua mkopo lakini kulipa ni hadi siku utakayopenda!..
Ni hatari kubwa, kuna hatari kubwa sana ya kupoteza mabillioni mengine kwa sababu maneno mawili hapa yanatumika.. Stimulus na Bail Out..haya ni maswala mawili mazito sana kiuchumi na yanatofautiana sana ktk utekelezaji wake na hasa ktk kupanga vipaumbele..
Kama kikwete ataweza kunambia mafanikio ya yale mabillioni aliyogawa SACCOS zimeweza vipi kukuza uchumi wetu ama hali ya wananchi, laa sivyo sidhani kama kuna haja ya kutoa mabillioni mengine kwa njia sawa na zile zilizotumika ktk kugawa yale mabillioni...Kwa sababu yale mabillioni ni sawa na zawadi toka kwa ndugu au rafiki aliyerudi toka Ulaya..Ni utamaduni wa kumpa mwenye njaa samaki badala ya kumfundisha kuvua samaki..