Kikwete to announce stimulus for economy

Kikwete to announce stimulus for economy

Ndo mmeshtuka?! Toka mwanzo tulijua ile pesa inaenda kutumika katika kampeni 2010! Sio kitu mpya hii. Same game, same players, different playing style but same result!
 
Naweza sema tunaongozwa na NSYUKA hawa watu hawana tofauti na pepo NSYUKA yaani mtu alieinadi kwa nguvu na kuitetea pale bungeni huku akicheka kumbe alikua anatucheka sisi wadanganyika hii ni hatari. Sasa tushamjua lakini je wote tunaona? au wengine ndo mimacho vidondaa? Lakini kama huyu mtetezi wa stimulus package si mroho wa madaraka anatakiwa ajiuzuru kila kitu kilicho mikononi mwake ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji, vinginevyo natilia shaka huu mtandao wa mafisadi unaweza kuwa mkali kuliko hata ule wa mihadarati ulioongozwa na CARLOS.

Na sasa wanataka tuwachangi bil 40 nyingine kwa ajili ya kampeni! Hizo za stimulus package ziakuwa kwa ajili ya tshirts, skafu, kanga, pilau, posho kwa wanahabari na timu ya kampeni, pi na hongo kwa kwa wapiga kura!
 
who cares!!! tuliwaambia toka mwanzo..hawakusikia..

Kuna Kilimo kwanza

kuna Kashfa ya Pembejeo..

na watu bado katika akili zao timamu wataendelea kuchangia ili kiendelee kuwa madarakani!!!


Sitachangia hata kama wataamua kunishusha katika pipa la mafuta yanayochemka kama walivyofanyiwa waamini wa mwanzo!!! Kama nina fedha za ziada basi nitanunua chakula niwapelekee yatima na kule kijijini kwangu hawana hata huduma muhimu, nitachangia kununua hata panadol zitulize maumivu ya kilimo cha jembe la mkono.
 
Most of the money will find route back into CCM for campaign. And into individuals accounts. One of these days tutaambiwa pia kuhusu EPA nyingine, lets wait and see. We will always be doing mactime. No forward movement we can achive execpt for few scripulous individuals protected by politicians.

Ndio maana evaluation for payments zilikuwa zinaonyesha kampuni nyingi kufidiwa zaid ya hasara yao waliopata. Hata hiyo hasara unaweza kukuta watu wamechezea tu mahesabu ili wapate hela and in the end irudi CCM kupitia kwao kama michango etc ....
 
mai wasuu!!!

nchi hii inaniudhi sana

yeye nduru anaweza kuongelea mambo hayo
halafu anakwepa
 
Wakati uchumi wa dunia unaanza kudorora, Gavana wa BoT Ndullu alituhakikishia uwongo wake kwamba Tanzania kamwe haingeweza kuathitrika kwa sababu ilikuwa imewekeza fedha yake kwa kile alichokiita "bonds" za nchi ambazo uchumi wake haungeweza kuyumba au kudodrora bila kuzitaja nchi hizo! What a lie!"

"Economic stimulus" (kutia damu ya fedha katika mishipa ya uchumi wa nchi) ilikiuka "the very tenet" ya ubepari" - "the magic of the market economy"! Nchi za ma-bepari wakubwa (Amerika na Ulaya ya Magharibi) zikatii amri ya u-soshalisti. Na sisi, akina popo, tukafuata; bendera fuata upepo!

Wanauchumi wetu, ma-Prof waliobobea: Ndullu, Mkullo, Wangwe, Lipumba na Bukuku (kwa kuwataja wachache tu), mlikuwa wapi kutoa misimamo yao kuiacha Tanzania iselee-ki-"market value"?

· Amerika lifanya hivyo kwa sababu mabenki yaliyoathirika yalikuwa ni ya wa-Amerika wenyewe!
· Iceland ilikataa kufanya hivyo kwa sababu mabenki yalikuwa ni ya wageni (Denmark na Ujerumani)!

Tanzania mabenki si yetu; ni ya wageni. Yamevuna, ki-BoT EPA! Je, yatarudisha lini hizo pesa za wakulima wa Tanzania? Ama ni kwa sababu wakubwa (viongozi wa serikali, vyama vya siasa na wabunge) wana hisa katika mabenki hayo?
 
Wakati uchumi wa dunia unaanza kudorora, Gavana wa BoT Ndullu alituhakikishia uwongo wake kwamba Tanzania kamwe haingeweza kuathitrika kwa sababu ilikuwa imewekeza fedha yake kwa kile alichokiita "bonds" za nchi ambazo uchumi wake haungeweza kuyumba au kudodrora bila kuzitaja nchi hizo! What a lie!"

"Economic stimulus" (kutia damu ya fedha katika mishipa ya uchumi wa nchi) ilikiuka "the very tenet" ya ubepari" - "the magic of the market economy"! Nchi za ma-bepari wakubwa (Amerika na Ulaya ya Magharibi) zikatii amri ya u-soshalisti. Na sisi, akina popo, tukafuata; bendera fuata upepo!

Wanauchumi wetu, ma-Prof waliobobea: Ndullu, Mkullo, Wangwe, Lipumba na Bukuku (kwa kuwataja wachache tu), mlikuwa wapi kutoa misimamo yao kuiacha Tanzania iselee-ki-"market value"?

· Amerika lifanya hivyo kwa sababu mabenki yaliyoathirika yalikuwa ni ya wa-Amerika wenyewe!
· Iceland ilikataa kufanya hivyo kwa sababu mabenki yalikuwa ni ya wageni (Denmark na Ujerumani)!

Tanzania mabenki si yetu; ni ya wageni. Yamevuna, ki-BoT EPA! Je, yatarudisha lini hizo pesa za wakulima wa Tanzania? Ama ni kwa sababu wakubwa (viongozi wa serikali, vyama vya siasa na wabunge) wana hisa katika mabenki hayo?

Hizo pesa zitapelekwa kwenye uchaguzi...CCM!
 
Tanzania is not yet born.
Let me keep quite, because JF will be the Victim of my word.

"The country is led by learned ignorants"
This is the situation there is no mind for changing people lives in power, We had only one guy and is no more because he was made off by Economic Hit Men"
 
Nyanza yalia na taratibu {Raia Mwema 11 Augost}

lC.gif
Waandishi Wetu, Mwanza​
Agosti 11, 2010
rC.jpg

bul2.gif
Kampuni binafsi zapendelewa

bul2.gif
Hata ahadi ya Serikali imekwama

WAKATI kampuni nyingi za binafsi za ununuzi wa pamba katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa zikiwa zimenufaika na mabilioni ya fedha zilizotolewa na Serikali kama fidia kwa hasara ambayo kampuni hizo zilipata katika mtikisiko wa uchumi wa dunia, Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU) hakikulipwa chochote licha ya kupata hasara ya zaidi ya Sh milioni 141, imefahamika.
Mbali na fedha hizo, NCU pia hakijapewa na Serikali zaidi ya shilingi milioni 48 ambazo ni nyongeza ya bei ya kununulia pamba kwa mkulima musimu uliopita ambamo Serikali iliongeza Sh 80 kwa kila kilo moja ya pamba baada bei ya kununulia kuporomoka hadi kufikia Sh 360 kwa kilo moja.
Habari za uhakika kutoka ndani ya NCU zinasema kuwa baada ya Serikali kutangaza mfuko maalumu kwa ajili ya kuhami uchumi, maarufu kama Stimulus Package, katika bajeti ya mwaka wa fedha uliopita, walifuata taratibu zote zilizotakiwa ili kupata fidia hiyo.
“Kama ilivyokuwa kwa wanunuzi wengine tulifuata utaratibu uliowekwa. Benki ya CRDB ambao ndio waliotukopesha, walitufanyia mchanganuo wa hesabu na kuonyesha kuwa tulipata hasara ya Sh milioni 141, tukawatumia Hazina lakini mpaka sasa hatujapata. Jambo la kushangaza hapa ni kwamba kampuni binafsi ndizo zililipwa haraka haraka huku ushirika kama sisi ambao ndio tuna hali ngumu, mpaka sasa hatujalipwa.
“Tumejaribu kuandikia Hazina mara kadhaa kuwakumbushia madai yetu hayo lakini hatujajibiwa. Hatujui tatizo liko wapi? Tuna kila sababu ya kudhani kwamba ni kwa sababu sisi ni chama cha ushirika ndiyo maana hatujalipwa.
“Wanunuzi binafsi hawako katika hali mbaya kifedha kama ushirika. Na hata wengine hawakupata hiyo hasara kubwa kama inavyodaiwa lakini ndio wamekuwa wa kwanza kulipwa, tena mabilioni ya fedha,” anasema kiongozi mmoja wa NCU ambaye kwa sababu za wazi aliomba jina lake lisitajwe.
Matumizi ya fedha hizo za Stimulus Package ambazo ni Sh trilioni 1.7 kwa ajili ya kuhami uchumi dhidi ya mtikisiko wa kiuchumi duniani ulioathiri kampuni za ununuzi pamba yamezua utata, huku baadhi ya wakubwa wakitajwa kuwa sehemu ya walionufaika na fedha hizo.
Uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizokwishakutolewa na Benki Kuu (BoT), chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa fedha hizo ni takriban Sh bilioni 870.8 ikiwa ni sehemu tu ya Sh trilioni 1.7 zilizopitishwa na Bunge mwaka jana.
Kwa mujibu wa utaratibu wa BoT, fedha hizo hutolewa kutoka benki hiyo kwenda katika benki ambazo zilikopesha kampuni zinazostahili kufidiwa, ambazo zimeathiriwa na mtikisiko wa uchumi duniani, hivyo NCU ilipaswa kulipwa na CRDB.
Raia Mwema limepata kuripoti kuhusu utata uliopo katika benki hizo katika kufidia kampuni husika ikibainika kuwa baadhi ya michanganuo ya hesabu za kampuni husika inaonyesha hazikupata hasara lakini baadhi ya benki zilipendekeza kampuni hizo zilipwe fidia ya mabilioni.
Mbali na baadhi ya kampuni kulipwa fidia pasipo kupata hasara kwa mujibu wa taarifa zao za kihasibu zilizowasilishwa katika benki husika, zipo kampuni nyingine ambazo zimebainika kupata hasara ndogo lakini ikapendekezwa zilipwe fedha nyingi zaidi kama fidia.
Kwa upande wa nyongeza ya bei ya kununulia pamba, kiongozi huyo wa NCU anasema kuwa mpaka sasa Serikali imeshindwa kuwalipa zaidi ya Sh milioni 48 ambazo chama hicho kilitumia kuongeza bei ya kununulia musimu uliopita.
“Labda hapa niweke sawa kwamba hizi fedha (Sh 80) tulizoongeza wakati wa kununulia pamba si pesa za Nyanza, ni fedha za mkopo kutoka benki (CRDB) ambao una riba kubwa. Kwahiyo kadri Serikali inavyochelewa kutulipa hizo sh milioni 48 na riba ya benki nayo ndivyo inazidi kuongezeka. Sasa serikali inabidi itulipe pamoja na hiyo riba ya benki,” aliongeza kiongozi huyo wa NCU.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo anasema utaratibu wa mkopo ulioweka na benki ya CRDB kwa chama hicho unakiweka katika hali ngumu ya kumudu ushindani katika ununuzi wa pamba hasa katika kipindi hiki cha soko huria.
Anafafanua kuwa benki hiyo inataka NCU iwe imekusanya na kufikisha kwenye viwanda vyake vya kuchambua pamba, asilimia 65 ya pamba iliyonunuliwa kwa kutumia mkupuo wa kwanza wa mkopo uliotolewa kabla ya kupewa mkupuo wa pili.
“Kwa mfano katika musimu huu tumepata mkopo wa Sh. bilioni tatu ambazo zitatolewa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza wametoa Sh. bilioni moja ambazo tunanunulia pamba. Baada ya hapo inabidi kwanza tusombe angalau asilimia 65 ya pamba hiyo yote tuliyonunua mpaka kwenye ginnery zetu za Kasamwa na Magu ndipo waje kuhakiki na kutoa awamu ya pili ya mkopo ambayo ni Sh. bilioni moja tena, vivyo hivyo mpaka utakapomaliza mkopo wako. Wanasema hii ni kwa ajili ya ‘loan security’ (usalama wa mkopo).
“Lakini hali hii inatuathiri sana katika ununuzi. Ukiangalia mlolongo wote huo wa kununua, usombe ndipo tena upewe fedha nyingine, ni mrefu sana. Hii inafanya tushindwe kushindana na wanunuzi wenzetu, hasa binafsi, na hivyo kushindwa kufikia malengo.
“ Kwa mfano, musimu uliopita tulipanga kununua kilo milioni 10 lakini tukaishia kununua kilo milioni 3.7 tu kwa sababu wakati wewe unahangaikia usombaji, usubiri benki waje wahakiki, usubiri tena watoe fedha zingine, wenzio wanaendelea kununua, hawakusubiri. Kwa kweli huwa tunapigwa bao la kisigino,” anasema.
Alipoulizwa, Meneja Mkuu wa NCU, Donat Gabagambi, alisema kwa kifupi kuwa chama hicho hakijalipwa fedha zilizoahidiwa na Serikali kwa ajili ya wanunuzi wa pamba waliopata hasara kutokana mtikisiko wa uchumi duniani na hata zile za nyongeza ya bei.
“Hayo ya stimulus package na nyongeza ya bei ya kununulia mwaka jana yapo lakini siwezi kuyazungumzia kiundani. Lakini hilo la masharti magumu ya benki ni kweli linatuathiri sana katika ununuzi maana hatufikii malengo tunayojiwekea.
“ Lakini ndiyo hali hali, bila kufuata masharti hayo hatupewi mkopo, hivyo hatuwezi kununua pamba. Kwa lugha nyingine ni kwamba bila kufuata masharti ya benki, ushirika huu ndio utakuwa umekufa maana hatutaweza kununua pamba na wala ushirika kujiendesha,” alisema.
Meneja huyo anaongeza kuwa itachukua muda mrefu kwa NCU kujitegemea kwani hivi sasa inakabiliwa na deni kubwa la zaidi ya Sh bilioni 5.6 huku vyanzo vya mapato vikizidi kupungua hivyo kusababisha mapato kidogo yanayopatikana kutumika kulipia madeni.
Ubadhirifu mkubwa na hujuma za mali za chama hicho uliofanywa na uongozi uliopita hasa kati ya mwaka 1999-2005 umefanya chama hicho cha ushirika mkoani Mwanza kuwa katika hali ngumu kifedha huku kikikabiliwa na mzigo wa madeni.
Kamati Maalumu iliyoundwa na uongozi wa sasa wa NCU imebainisha wazi namna viongozi hao walivyohujumu mali za chama hicho lakini tangu kutolewa kwa ripoti hiyo Julai mwaka 2006 na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Habari zilizotufikia wakati tukienda mitamboni zinasema kuwa Serikali imelipa wiki hii Sh. Milioni 27 ikiwa ni sehemu ya deni la Sh. milioni 48 ya nyongeza ya bei iliyotoa katika musimu wa ununuzi wa mwaka jana.
Aprili mwaka huu, gazeti hili liliandika kuhusu malipo ya Stimulus Package na kubainisha kuwa baadhi ya kampuni ambazo hazikustahili zililipwa na baadhi zilizostahili kulikuwa na njama za kuzilipa malipo makubwa.
Gazeti hili lilipata nyaraka zinazoonyesha taarifa za benki na michanganuo ya kampuni husika. Baadhi ya benki ziliteuliwa na Benki kuu kwa ajili ya kuhakiki hesabu za kampuni husika kama zimepata hasara ili zifidiwe.
Benki ya CRDB ilipendekeza kampuni 26 zilipwe mabilioni kadhaa na mbili zikitupwa nje ya mgawo, wakati benki ya TIB ikiidhinisha malipo kwa kampuni moja ya Al-Adawi, kupewa fidia ya Sh milioni 405.6 ambazo mapendekezo ya awamu ya pili hayakuridhia malipo hayo.
Benki nyingine ni Kenya Commercial iliyokagua mchanganuo wa kampuni ya Birchand Oil Mills Ltd na kupendekeza kampuni hiyo ifidiwe Sh bilioni 1.66, lakini mapendekezo mbadala ya watalaamu yalitaka kampuni hiyo ifidiwe Sh bilioni 4.642, Exim Bank Tanzania Ltd imependekeza kampuni ya Bio Sustain kufidiwa Sh milioni 597.7 lakini baada ya uhakiki mwingine kampuni hiyo ikapendekezwa kulipwa milioni 458.1 na Stanbic Bank ilipendekeza kampuni ya S & Ginning Co. Ltd kufidiwa Sh bilioni 5.69, lakini ikabainika inastahili kufidiwa Sh bilioni 2.86.
Katika Benki ya CRDB utata unazidi miongoni mwa kampuni ambazo zimeomba fidia kupitia benki hiyo. Kampuni ya Badugu Ginning ya Musoma, ambayo hesabu zake zinaonyesha katika shughuli zake imetumia Sh bilioni 4.41, ikipata mapato ya Sh bilioni 2.94 kwa mauzo ya pamba na Sh milioni 727.6 kutokana na mauzo ya mbegu za pamba na pato lake la jumla ni Sh bilioni 3.7, ikiwa imetengeneza hasara ya milioni 742.2.
Licha ya mchanganuo huo unaoonyesha kampuni hiyo kupata hasara ya Sh milioni 742.2 ilipendekezwa na Benki ifidiwe Sh bilioni 1.4, hata hivyo mapendekezo ya awamu ya pili yalipinga taarifa hizo na kutaka kampuni hiyo ifidiwe Sh milioni 742.2 tu.
Kampuni ya Chesano Cotton Ginning Ltd ya Bariadi, Shinyanga imebainisha CRDB kuwa matumizi yake (ununuzi na uendeshaji) ni Sh bilioni 2.6, mapato yake kutokana na uuzaji nyuzi za pamba ni bilioni 1.99 (bilioni 2), mauzo yaliyotokana na uuzaji mbegu za pamba ni Sh milioni 586 na kwa hiyo mapato yake ya jumla ni sh bilioni 2.6.
Utata unaojitokeza ni kwamba kwa mchanganuo huo wa Benki ya CRDB kampuni hiyo imepata faida ya Sh milioni 6.4, lakini benki hiyo hiyo ikapendekeza kampuni ifidiwe Sh milioni 580. Hata hivyo, ukaguzi zaidi wa hesabu ulipofanyika, kampuni hiyo haikupendekezwa kulipwa chochote. Kampuni nyingine ambayo fidia yake inaonyesha utata ni Gaki Investment Ltd ya Shinyanga.
Gaki Investment Ltd imebainika kununua kilogramu takriban milioni 19.8 za pamba, ikitumia Sh bilioni 12.9, mapato yake baada ya biashara ya nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.15, mapato yaliyotokana na kuuza mbegu za pamba ni Sh bilioni 1.727 na kwa hiyo mapato yake ya jumla kwa msimu husika ni Sh bilioni 13.9, ikijizolea faida ya Sh bilioni 1, lakini ukaguzi wa kibenki (CRDB) ukionyesha imepata hasara milioni 146 na ifidiwe kiasi hicho, lakini ukaguzi wa pili huru ukapendekezwa kampuni hiyo kutolipwa chochote.
Kampuni ya Igunga Cotton Ltd yenye makao yake makuu Dar es Salaam, hesabu zake zilizowasilishwa CRDB ambazo gazeti hili limepata mchanganuo wake zinabainisha ilinunua kilogramu milioni 2.8, ikitumia Sh bilioni 1.9, mapato kutokana na mazao ya pamba iliyonunua Sh bilioni 1.43, mapato kutokana na mauzo ya mbegu za pamba ni Sh 300.5, mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 1.7, ikitajwa kupata hasara ya Sh milioni 205.
Lakini licha ya kampuni hiyo kupata hasara ya Sh milioni 205, ilipendekezwa na watalaamu wa benki ya CRDB ifidiwe Sh milioni 839, hata hivyo uhakiki huru wa awamu ya pili ulipofanyika, kampuni hiyo ikatakiwa ifidiwe hasara yake halisi ya Sh milioni 205.
Ipililo AMCOs Ltd ambayo katika msimu husika ilinunua pamba kilogramu milioni 101, ikitumia Sh milioni 82, na mauzo yake ya nyuzi za pamba yakiwa Sh 54.5 na mauzo ya mbegu za pamba yakiwa Sh milioni 10.8, mapato yake ya jumla yakiwa Sh milioni 65.35, ikitajwa kupata hasara ya Sh milioni 16.7 lakini ikapendekezwa na benki ifidiwe Sh bilioni 51, ukaguzi wa pili ulipofanyika ikapendekezwa ifidiwe hasara halisi tu, ambayo ni Sh milioni 16.7.
Jambo Oil & Ginneries Ltd ya Shinyanga, katika msimu husika ilinunua kilogramu milioni 22.08, kwa gharama ya Sh bilioni 13.9. Mapato ya kampuni hiyo katika uuzaji wa nyuzi za pamba ni Sh bilioni 12.51, mauzo kutokana na mbegu za pamba yameiingizia kampuni hiyo Sh bilioni 2.4 na kwa hiyo mapato yake ya jumla ni Sh bilioni 14.9, ikijipatia faida ya Sh milioni 927.1, utata unaibuka pale benki baada ya kupitia mchanganuo huo wa hesabu kupendekeza ifidiwe Sh bilioni 1.06.
Kahama Oil Mill Ltd ya Kahama yaShinyanga, ilinunua kilogramu milioni 24.9 na mchanganuo wa kampuni hiyo uliowasilishwa benki ukionyesha kuwa imetumia Sh bilioni 19.8, ikipata Sh bilioni 14.6 kutokana na mauzo ya nyuzi za pamba na Sh bilioni 2.7 za mauzo ya mbegu za pamba na kujipatia mapato ya jumla, Sh bilioni 17, ikipata hasara ya Sh bilioni 2.3, lakini benki ikipendekeza ifidiwe Sh bilioni 4.4.
Kampuni ya Kisumwa Machinery Ltd, ambayo nyaraka zilizopo hazibainishi kama imewasilisha mchanganuo wake lakini wakati huo huo imependekezwa ilipwe fidia ya Sh milioni 377. Mbali na kampuni hiyo, kampuni nyingine ambayo ingawa mchanganuo wake haukubainishwa lakini ikipendekezwa kulipwa fidia ni Morogoro Canvas Mills (1998) Ltd, iliyopendekezwa na benki ilipwe fidia ya mtikisiko wa uchumi duniani, Sh bilioni 1.612.


------------------------------------------------------------

Wadau, hii imekaa vipi???
 
Back
Top Bottom