Kikwete siyo safi! - yes I said it! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 22, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 22, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijui kwanini tunazungushana na kudai watu wote walioatajwa kwenye orodha ya Ufisadi wanastahili isipokuwa Rais Kikwete! Hata viongozi wanaotambua baadhi ya uzito wa tuhuma zilizotolewa na wanaodai kuwa zitiliwe maanani hujikuta wanajing'ata ng'ata kuhusu Rais Kikwete. Baadhi ya watu wamefikia mahali pa kulaumu kina Dr. Slaa kumuweka Kikwete katika kundi hilo kwani JK ni safi! Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!

  a. Mkataba wa IPTL ulisainiwa yeye akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Hakuna mkataba mbovu kama huo. Kushindwa kwake kutetea maslahi ya nchi akiwa Waziri na kulisababishia Taifa hasara kubwa ilikuwa ni kilele cha kutokuwajibika na kushindwa kuongoza. Akiwa Waziri mwenye dhamana ya nishati Ndg. Kikwete alitakiwa kuhakikisha kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inaingia kwenye mkataba ambayo inaweza kujitoa pasipo kupata adhabu kubwa. Alishindwa hivyo na hivyo kuoneshe kutokuweza kusimamia maslahi ya nchi.

  b. Wakati Rada ya bilioni 50 inanunuliwa, Ndg. Kikwete alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa na wakati sakata lenyewe linaanza alikuwa ni Waziri wa Fedha. Akiwa Waziri mwenye dhamana hiyo alishindwa kabisa kufuatilia ukweli kuwa kampuni ya BAE siyo mali ya serikali ya Uingereza na ya kuwa rada yenyewe ilikuwa imeongezwa kwa asilimia 24. Kiasi hicho kinakaribiana kabisa na wastani wa asilimia 20 za fedha za umma zinazopotea katika manunuzi ya serikali (public procurement).

  Alishindwa kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa letu yanalindwa na alipopata nafasi ya kuonesha busara aling'aka na kusema "kwanini sisi ni idara ya Benki ya Dunia? ni kututukana kudai kuwa tusubiri Benki ya Dunia kutuamulia nini kinatufaa".

  Ndio maana leo hii anapokuja na kuzungumza kuwa hawezi kuamini kuwa nchi kama Uingereza inaweza kuacha kampuni "yake" kurusha rada hiyo kwa bei hiyo wengine tunamshangaa kwani alikuwa na nafasi zaidi ya 20 ya kuweza kupinga ununuzi huo lakini alikuwa ni kinara wa kutetea tenda hiyo ya rushwa! Ni kuelewa hilo ndio utaona ni kwanini hakutaka watu wamuulize Rais Mkapa juu ya suala la rada, kwani miongoni mwa wahusika wakubwa ni yeye mwenyewe Kikwete.

  c. Kama nilivyoonesha hapo juu kuwa Rais Kikwete aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Kwa hivyo nina uhakika kabisa alikuwa anajua kabisa jinsi mikataba inavyoingiwa na alikuwa na kila sababu ya kuhakikisha kuwa mikataba inalinda maslahi ya nchi na kunufaisha nchi wakati inawapatia wawekezaji faida ya kibiashara. Kwa kitendo chake yeye mwenyewe kuwa ukaribu na wafanyabiashara hao hasa swahiba wake ambaye ni mmiliki mkubwa wa ardhi yenye vito na madini Bw. James Sinclair, Rais Kikwete tangu akiwa Waziri wa Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje amekuwa mtu aliyetiwa upofu na "dhahabu".

  Wakati Rais Mkapa na Yona wanajipatia tenda ya Kiwira, Rais Kikwete na Msabaha walikuwa wanajisogeza karibu na Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration ambapo kuna madai (yanayothibitishwa na taarifa za SEC na EDGAR) kuwa Msabaha na Kikwete walikuwa na "hisa" za kiasi fulani. Kampuni hiyo ya TRE iliingia mkataba na Barrick Gold kuwa inapovumbua madini katika ardhi inayomiliki basi Barrick wanakuwa wanunuaji wa kwanza.

  Ni wao TRE waliouzia Buzwagi kwa Barrick na maeneo mengine kadhaa kwa makampuni mengine. TRE inaponufaika kwa mikataba mibovu ambayo serikali inaingia na makampuni ya uchimbaji kuna watanzania wawili ambao nao wananufaika (ni wazi wapo wengine na wengine ni vigogo wengine) na dili hizo.

  Ni kwanini Barrick walikuwa wa kwanza kukubali mabadiliko ya vipengele vya mikataba yao? jibu ni ushawishi wa James Sinclair na Kikwete ili kutetea kilicho chao. Kwa yale makampuni ambayo hayana ukaribu wa James Sinclair na Kikwete (JK alimualika JS kwenye kuapishwa kwake na mara nyingi amekuwa mgeni wake akija US, na binti ya JS aliyeko Tanzania ni rafiki wa karibu...) basi imekuwa vigumu kuwashawishi kubadili vipengele hivyo.

  Ndio maana hadi leo hii si kweli kuwa kupitia vipengele na kuzungumza na "wakubwa" hao kuhusu mikataba kumekoma kama alivyodai mjasiriamali mwingine Nazir Karamagi alipokuwa akijaribu kupangua hoja za Zitto. Ukweli ni kwamba kamba waliitundika wenyewe serikali na ni wenyewe walioziweka shingo zao humo! wawekezaji wanatishia kuondoa kigoda!! Serikali inabembeleza!!

  Anapozungumzia matatizo ya mikataba Rais Kikwete anazungumzia kana kwamba tatizo ni kipengele kimoja tu! Hajachukua muda kufuatilia uzito wa hoja hizo kwani kwake ni kelele!

  d. Kikwete si Safi kwani amewalinda watu wachafu! Waswahili walisema ukiwa na urafiki na wezi, usishangae watu wakakuhisi na wewe mwizi! Rais Mkapa anapomlinda mjasiriamali Mkapa, aliposhindwa kumsimamisha kazi mara moja Ditto na kuamua kumuacha ajiuzulu huku akiendelea kupata mafao yake alionesha udhaifu mkubwa wa uongozi!

  Rais Kikwete amekuwa mtetezi wa wabadhirifu akikesha kutoa vitisho hewa akijaribu kutetemesha mabua na kuangusha vichuguu huku milima ikiendelea kuganda theluji! Ukimya wake kama ule wa Mkapa ni ishara wazi kuwa walifeli darasa la Mwalimu!

  Anapoona kuwa madai ya ubadhirifu Benki Kuu, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, n.k kuwa "kelele za upinzani" na kuwa "ndiyo demokrasia" anaonesha udhaifu mkubwa usiomstahili kiongozi wa nchi. Haiwezekani upotevu wa mabilioni ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka kuwa viwe ni "kelele" tu!

  Rais ni lazima we mtu ambaye hapuuzii masuala mazito na hayafanyi kuwa ni ya kijinga. Kwa mtu kuwa mpinzani hakuifanyi hoja yake kuwa "kelele". Leo hii wana CCM wenzake wanazungumza wazi kuhusu tuhuma hizi na kudai kuwa wanaotuhumiwa (akiwemo yeye mwenyewe) wajibu siyo suala la kupuuzia!

  e. Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote. Hivi hadi nini kitokee ndipo Rais Kikwete atajua kuwa mambo haya si ya kupuuzia? Wakati Lowassa ameenda kukutana na Karamagi kule London na mkataba wa Buzwagi ukasainiwa je Rais Kikwete alifahamu ujio wa Waziri wake Mkuu? Je walikutana? Kama Rais hakujulishwa kutiwa saini kwa mkataba mkubwa namna hiyo na Waziri Mkuu anakutana na Waziri mwingine pasipo ujuzi wa Rais je haoni ni ukosefu mkubwa wa kiutawala!? Lowassa alifuata nini London na kukutana na Karamagi badala ya kukutana na Rais?

  Leo hii watu wakihoji mazingira ya kusainiwa mkataba huo kwanini hiyo iitwe kelele!

  Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka miwili baadaye watanzania walishika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....

  Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!
   
 2. p

  princejafari Member

  #2
  Oct 22, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  As. usual you are right on the spot. nakumbuka maneno ya marehemu Sembene Ousmane katika kitabu chake cha God's Bits of Wood, "mother what is it that washes the water'? kwa maana nyingine huwezi hata siku moja mtu ukatumia maji machafu kufulia nguo. In short ni kwmaba JK na watu wake wa karibu wamenufaika na ubadhirifu uliopo tanzania long kabla hajaingia ikulu. JK can not bite the hand that feeds him without implicating himself. Taifa limeingia hasara.
   
 3. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2007
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuliishauliza hapa; ni mambo gani ya maana sana ambayo rais huyu katika utumishi wake wa siku nyingi serikalini yanayojionyesha kwake yeye kuwa kiongozi wa kutumainiwa?

  Hatukupata jibu.

  Lakini ya ufisadi naona hakuna aliyeyategemea pia!
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Hii makala yako ina madai mapya, naomba kama unaweza fafanua juu ya hili suala la Lowassa kukutana na Karamangi London. Mimi sijawahi kulisikia, kama ni kweli basi huenda hapo sio tu kuna moshi mkubwa bali hata moto wenyewe unawaka. Kwanini Lowassa akutane na Karamangi kinyemelea?

  Pili hili la Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration, je ni kweli Msabaha na JK wana hisa? Kama ni kweli basi pia hapa
  patakuwa na moto mkali.

  Kama madai yako yote haya Mwanakijiji ni sahihi, basi nchi yetu imekwisha. Huyu JS amefikaje mpaka kuwa karibu na JK?

  Manyang'au yanatunyang'anya sisi maskini hata kile kidogo tulichopewa na mungu kwa kuwatumia watu ambao tumewaweka madarakani kwa mbwembwe zote na kuwapa kila tulicho nacho ili waishi vizuri na wasipate tamaa, lakini wao wameamua kutusaliti na kuwa mafisadi.

  Kweli inasikitisha sana!
   
 5. Bi. Senti 50

  Bi. Senti 50 JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 291
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!
   
 6. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2007
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mungu wangu tuhurumie tupe ujasiri. tutatendwa hivi mpaka lini jamani!
   
 7. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #7
  Oct 22, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Halafu hawa ndio wanataka award ya MO!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 22, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yote niliyoyasema ni kweli tupu! wao wanajua na wanajua ninajua.. na wapo watu wengine ambao wanajua.. Lowassa anasema "waligongana kwa bahati mbaya na Karamagi pale Hotelini"...
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Oct 22, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Waafrika bwana! Yaani tumefikia kiwango cha kuwazawadia fedha viongozi wetu tunaoona wamefanya vizuri ktk utawala wao. Halafu akina Watson wakisema akili zetu finyu tunakuja juu. Mimi binafsi sioni umuhimu wa hiyo zawadi ya MO
   
 10. m

  mwana siasa Senior Member

  #10
  Oct 22, 2007
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sisis tusubiri 2010,
   
 11. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2007
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  My God naomba usamehe EL na Karamagi(FISADI) kama wanasameheka.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji katoa hoja yake na kuipembua, wewe unachomoza kichwa una pinga hoja unazama ardhini bila kuumba hoja yako mwenyewe kueleza kwa nini unapinga. Mimi sikuelewi hata chembe.

  Umeanza tena! Maana yake nini? Hapa katikati MWKJJ alikuwa kimya?
  Je MWKJJ kwa siri alikubali kukaa kimya? Wewe nani wa kumzuia mtu asipumue Tuhuma ,Ukweli, Hisia na mwelekeo wake?

  Naona hujipendi. He!Maana yake nini tena jamani? MWKJJ kavaa vinyambu na suti kaziacha sandukuni? Unamtisha? Unamwonya? Au unamwekea hofu moyoni?

  Waache wala wali wale wali wao! Wala wali ndo akina nani? Kwa nini wachwe?

  Una maana waachwe wale wali wa kwao? Au waachwe waendelee kuwala waliwao?
   
 13. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ukiona Tai wengi basi ujue kuna mzoga.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 22, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwenye toleo la Jumatano nitapanua kidogo hoja hii kuwa "Kikwete naye si safi - Yes I said it!"
   
 15. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji there is no point of return.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 22, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unajua naona tunazungushana tu hapa.. watu wanalaumu inaction ya JK kwa vile na yeye kajumuishwa.
   
 17. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 272
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wewe mbona unatishia mtu hajipendi umekuwa mganga wa kienyeji? Badala ya kujibu hoja unaleta vioja. Mzee Nyani Ngabu said it best, "Wenyekushindwa Hoja...Huleta Vioja". Somo la bure hili bi Mkubwa.
   
 18. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hawa ngedere wasikusumbue, tunawataka nyani wajibu maswali wanayoulizwa huwezi kukimbilia Ikulu kwa sababu ya kulinda interest binafsi na kutumia pesa za walipa kodi kama vile hazina mwenyewe. Ingekuwa sio hivyo tusingemuona Karamagi wala EL kwa muda wote huu na uvurundaji wao bila kuwasahau genge lote la mafisadi toka Balali etc. na Kiongozi lao BWM.
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo umenena Mkijiji, kumbe ndo kigugumizi chote hicho?? kwa hakika maiti hawezi ucheka mzoga!

  Kumbe ndio woga wa kuondoa vibanzi vya mafisadi! anachelea boriti jichoni kwake!

  Swali moja la msingi najiuliza, yote haya tumeisha yajua, tumeisha jutia uchaguzi wetu, uovu wote na jinsi jahazi letu linavozidi kwenda mrama vipo wazi, ninacho baki nikijiuliza hivi hamna namna nyingine ama njia nyingine fupi ya kutuepusha na zahama hii hadi hapo 2010?? miaka 3 mingi sana tutakuwa tumezama kabisa!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Oct 22, 2007
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Naona sasa wakati umefikia wa mimi kubadili jina....maana hii misamiati yenu mnayotumia neno/jina "nyani" saa ingine hunipa shinikizo...
   
Loading...