Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

...Ulofa ni pale unapo muita Kinara wa Ufisadi hapa Nchini kuwa Kamanda wa Mabadiliko!

Ulofa ni kwamba mtu anapokuwa kwako akaitwa fisadi mnatumia nguvu kubwa kupinga, huyohuyo akienda upande wa pili mnatumia nguvu kubwa kumwita fisadi

Kinachonishangaza wazito wote ambao wametoka kwenu mnawapa kashfa, hamuoni kuwa kwa kufanya hvyo mnachafua ccm yenu? Nasema hvi kwa sababu mnawazito wengi au to be honest mnaweza mkawataja baadhi ambao mkonao kuonyesha mnachukia ufisadi na ubadhirifu wa mali za uma?

JEYKEY AMEMWELEWA SUMAYE?
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.

anamuelewa sana ila anaogopa kusema ukweli maana ni zaidi ya maumivu
 
Kinara wa Ufusadi nchini ni yule mgombea alie enda haja kubwa kwenye mkutano wa hadhara Geita ikabidi Mr zero ampeleke chooni akabadilishwa na suruali,akapanda jukwaani na suruali nyingine

Mmmh! inawezekana kweli!!?? au ndiyo mtindo wenu tu wa kukashifu watu mnao waona ni athari kwa maslahi yenu?
Ni bora kuacha akiba kwa kesho yako huijui utakuwa wapi! Be good man.
 
Hahahah hii kali sasa!!

Kenge na mamba macho yao yamejeukia juu matone ya mvua yanawaumizaga machoni ndio maana wanakimbilia kwenye maji kuficha macho. Naomba huyo bwana atufafanulie amehusishaje hilo sisi wengi ni mawe jamani
 
Lusungo wewe ndie Mfugaji Bora wa Kahawa kwa mjibu wa Fisadi Lowassa

Hapana mimi siye...

atakuwa yule aliyewaambia wenzake wanye kisha wasambaze kinyesi kiwe lami...

Na aliyesema Sadam alikuwa Rais wa Libya baadae Kuwait ...

Ni yule aliyesema asiye na 200 ya nauli apige mbizi...
 
Kenge na mamba macho yao yamejeukia juu matone ya mvua yanawaumizaga machoni ndio maana wanakimbilia kwenye maji kuficha macho. Naomba huyo bwana atufafanulie amehusishaje hilo sisi wengi ni mawe jamani

Hahahahah subiri atakuja...
 
Ulofa ni kwamba mtu anapokuwa kwako akaitwa fisadi mnatumia nguvu kubwa kupinga, huyohuyo akienda upande wa pili mnatumia nguvu kubwa kumwita fisadi

Kinachonishangaza wazito wote ambao wametoka kwenu mnawapa kashfa, hamuoni kuwa kwa kufanya hvyo mnachafua ccm yenu? Nasema hvi kwa sababu mnawazito wengi au to be honest mnaweza mkawataja baadhi ambao mkonao kuonyesha mnachukia ufisadi na ubadhirifu wa mali za uma?

JEYKEY AMEMWELEWA SUMAYE?

Hao watu ni sifuri.
 
Ni kiburi cha dola tu, ukweli alimuelewa akaweka dharau sasa ausubiri mwiba umchome
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.

Aliyemuelewa/anaemuelewa Sumaye hana tofauti na Sumae mwenyewe, mwenye akili timamu hawezi kumuelewa Sumae mtu ambae amekuwa PM kwa kipindi cha miaka 10 halafu mtu huyo huyo leo anasema serikali (ambayo yeye alikua sehemeu yake) imewatelekeza wananchi wake kwa miaka mingi (including miaka ambayo yeye amekua PM)!!

Naamini waliomuelewa/wanaomulewa Sumae ni lile kundi alilolitaja Ben Mkapa siku ile ya uzinduzi wa kampeni za ccm pale jangwani - malofa na wapumbavu!!! Kweli baadhi ya watanzania ni wavivu wa kufikiri, hasa wale wanaomuelewa Sumae!!
 
Back
Top Bottom