Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

...Ulofa ni pale unapo muita Kinara wa Ufisadi hapa Nchini kuwa Kamanda wa Mabadiliko!
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.

Mleta mada ni mtoto wa nje wa Mr Zero
 
Unapokaa mahali kusikiliza hadithi za Pwagu na Pwaguzi usitegemee utapata kitu chochote cha maana, katika uzi huu mleta mada ni Pwagu, waonamuunga mkono ni mapwaguzi.

mh,jk atakuwa amemuelewa sana waswahili wana msemo zimwi likujualo halikuli na kumaliza ,hii bahati ya mtende walionayo ccm wasiogope kukabidhi kijiti ukawa ,ukawa ipo tuli,mbwembwe ziko kwa kina bulembo anapayuka huyu hafikiri kuna maisha ya kesho
 
...Ulofa ni pale unapo muita Kinara wa Ufisadi hapa Nchini kuwa Kamanda wa Mabadiliko!


Kinara wa ufisadi nchini ni nani?

Hata angekuwa yeye kwani hawezi kubadilika?

Mbina Sauli alikuwa Muuwaji baadae akageuka mhubiri injili ambaye ndiye mtume Paulo?
 
Anamili kihalali au kiharamu?

Kama ni kiharamu CCM si bado mna dola why msilichukue?

Lile shamba la miembe la Mwinyi pale Mkuranga lililogeuzwa mavuno ya mkaa vipi anamiliki kihalali au kiharamu?
Hahahaaa.... Mr. Clean naye atueleze kile kipande kilicho kilichozungukwa na miti ya mkonge alikipataje upande ule wa Vikawe kuelekekea Bagamoyo.
 
Kinara wa ufisadi nchini ni nani?

Hata angekuwa yeye kwani hawezi kubadilika?

Mbina Sauli alikuwa Muuwaji baadae akageuka mhubiri injili ambaye ndiye mtume Paulo?
Kinara wa Ufusadi nchini ni yule mgombea alie enda haja kubwa kwenye mkutano wa hadhara Geita ikabidi Mr zero ampeleke chooni akabadilishwa na suruali,akapanda jukwaani na suruali nyingine
 
...Ulofa ni pale unapo muita Kinara wa Ufisadi hapa Nchini kuwa Kamanda wa Mabadiliko!

Vipi yule wa kule Bariadi aliye nyanyuliwa mkono na kuombewa kura na Magufuli? Huyo si ndio shujaa wenu wa dili kubwa kubwa?
 
Back
Top Bottom