Kikwete: Nimeshindwa Sekta ya Kilimo

Kikwete: Nimeshindwa Sekta ya Kilimo

Kenge ndo wewe na hayo MAUKAWA yako nimeeleza uhalisia. Tanzania tunazalisha chakula cha kutosha mpaka tunasafirisha nje ya nchi. Utatulinganishaje na hawa wakenya ambao hawana hata ardhi ya kutosha?

Wewe buku saba ngoja nikupe mfumo wa chakula haitegemei unazalisha au hauzalishi na kumbumba kenya nao hutoa msaada wa chakula somaria wakati huo kenya huomba chakula kutoka tanzania.nenda tu huko katafute buku 7 hili swala tuachie sisi tuliokwenda shule.buku 7.

Swissme
 
Hizi Takwimu za FAO zina mashaka. Kenya wanaomba chakula kwetu na sisi tunazalisha chakula kingi kuliko mahitaji ya nchi.

Kenya hawaombi chakula kwetu bali wananunua, usishangae kuona sehemu wanaolima sana wana njaa kuliko ambako hawalimi, mfano rahisi jiji la mwanza hatuna hata mashamba ya kulima lakin hamna njaa, lakin kwimba ambako wanalima wanakumbwa na njaa
 
Swali la msingi aliloshindwa kujibu ni kwa nini Kilimo kimefeli kipindi chake despite all the efforts made to improve the sector?
Hili ndo swali la msingi sana.
 
idoyo

Hizi Takwimu za FAO zina mashaka. Kenya wanaomba chakula kwetu na sisi tunazalisha chakula kingi kuliko mahitaji ya nchi.

idoyo

Nadhani kuna mushkeli katika hizo takwimu.
ni mara ngapi tumekuwa tunasikia watu wanakabiliwa na njaa? waziri mkuu akiagiza bungeni watu hao wapatiwe msaada?
https://www.jamiiforums.com/habari-...kutokana-na-ukosefu-wa-mvua.html#post12377900
https://www.jamiiforums.com/habari-...ilaya-za-tarime-na-same-taabani-kwa-njaa.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ja-dear-mr-president-on-a-serious-note-6.html
Tanzania hatarini kukubwa na baa la njaa - MVIWATA | East Africa Television
 
mwenyekiti wako amekiri kuwa sera za chama chenu zime-fail kukuza kilimo.

Kikwete hakushindwa kusimamia kilimo tu bali ameshindwa kutawala nchi katika kila nyanja na akahitimisha kwa kushindwa kusimamia nchi kupata katiba wananchi waipendayo!!

A president who failed because of sharing a bed with drug traffickers,Poachers, bandits, tax evaders and all manner of crooks!!
 
Siku wakiweza kukirudisha chama chao kwa wenye nacho (wakulima) ndo siku hiyo wataweza kuiendeleza sekta ya kilimo na kupambana na umaskini dhahiri, hatutegemei kwa vyovyote vile sekta ya kilimo ikue wakati si sera ya chama tena.

Sera ya chama kwa sasa hivi ni biashara na ndo maana chama kimejaa wafanyabiashara, wachuuzi, wezi na vibaka. Leo mmeamua kufanya biashara mpaka ikulu na kufuga magenge ya "Vibaka" wachache huku walalahoi wa nchi hii wakisalia kapuku. I

rudisheni CCM kwa wenye nayo walio wengi ili muihepushe nchi kuingia vitani vinginevyo balaa linakuja, mmeua being na masoko ya mazao mpaka viwanda mmeshindwa kuanzisha mmebaki kuangalia sekta ya mawasikiliano kila mmoja awe na simu eti ndo maendeleo,

maisha ya wakulima yanategemea kilimo na si kumikiki simu. Namuona kinana anazunguka anaagiza bei za kahawa zipande sijuhi anatoa wapi kauli hizo na wakati bosi wake anakiri kilimo kimewashinda, upuuzi tu.
 
Japo alijitahidi kkwenye kuweka bajeti ambayo ingeweza kuwasogeza mbele watanzania lakini kutokana na kushindwa kuwawajibisha watendaji wezi na wabovu fedha nyingi za miradi kama DADPs zimeishia kuwatajirisha wezi. Miradi ilofika kwa wananchi imekosa usimamizi na imekufilia mbali. Yote hiyo ni matokeo ya kuwakumbatia mafisadi. Miradi ya umwagiliaji japo ilitengewa pesa nyingi lkn bado mafisadi hawakuiacha ama haikukamilika au iko chini ya kiwango.
Rais alipaswa kuwaomba radhi watanzania kwa hilo na si kukimbilia kupiga magoti kwa wazungu. Sisi ndio wahanga wakuu japo akiomba msamaha hatutomsamehe lkn tutautambua uungwana wake. Na wataokuja baada yake watajifunza kitu.
 
Sio kilimo tu,ameshindwa kila kitu!
 
Hizi takwimu sijui wanazipima kwa kuangalia vigezo gani ndiyo ziweze kupitishwa.
 
Shida ni JK amezungukwa na VIBAKA ambao yeye wakati wote anawakenulia.<br>Rais lazima uwe mkali kidogo katika mambo serious.<br>Hatukuwahi kumwona huyu bwana akiwa serious katika lolote lile.<br>Aondoke tu kwakweli.
 
Hizi takwimu sijui wanazipima kwa kuangalia vigezo gani ndiyo ziweze kupitishwa.
takwimu weka kando, fuata kauli ya JK. kama JK amekubali hivyo, basi na takwimu ni sahihi. :lol::lol::lol:
 
I bet asingekiri haya kama angekuwa na muhula mwingine.
Ingekuwa vizuri akakiri kuwa chama chenye nembo ya jembe na nyundo kimeshindwa kuinua moja ya alama yake
 
Kingereza ni shida sana kwa Watanzania wengi na unaweza kutafsiri hata kwa kupotosha na utaonekana wa maana.
 
idoyo

Za Kuambiwa Changanya na Zako.
Kushindwa Kilimo + Kilimo ndio Uti wa Mgongo wa Taifa + Maisha Bora kwa Kila Mtanzania

= Total failure of Kikwete kukuza uchumi na kutupatia Maisha bora
 
Last edited by a moderator:
Dhamira alikuwa nayo. Ila kwa mfumo corrupt kama huu wa kwetu inakuwa ni shida kutimiza mahitaji ya wananchi. Rushwa inakwamisha maendeleo ya nchi nyingimza Afrika. Hiyo inatokea Angola, Malawi, Zambia, Uganda, South Africa nk

Sidhani kama upo sahihi kusema kuwa ameliangamiza taifa. Ila nadhani hajafikia malengo yake ipasavyo. Alifanya jitihada nyingi ila ilikuwa inaonekana ni kama yupo peke yake. Matrekta mengi yameletwa na watu wameshindwa kuyasimamia
Lizaboni hapa ndipo utakapokubaliana na mie na wadau wengine kwamba inabidi tubadilishe mfumo mzima kwenye uchaguzi mkuu ujao.. Kama unakiri raisi ambae tulimchagua awe juu ya kila kitu lakini mwisho wake ameangushwa na wa chini yake na yeye kama raisi kushindwa kuwachukulia hatua hao waliomuangusha, basi hawa ambao wako kwenye mfumo wana nguvu nyingi kuliko mamlaka ya uraisi..! Tuwatoe hawa wote na mfumo huu uliojikita kwa zaidi ya miaka 50 na kuingiza mfumo mwingine ambao itakuwa rahisi kuuondoa ndani miaka mitano kama ukishindwa kutatua shida za watanzania..!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom