Kikwete: Nimeshindwa Sekta ya Kilimo

Kikwete: Nimeshindwa Sekta ya Kilimo

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
jkkk.png

Rais Jakaya Kikwete amekubali - na kujuta - kushindwa kwake kubadilisha na kukuza sekta ya kilimo katika kipindi cha miaka yake kumi Ikulu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ulosambazwa kwa vyombo vya habari jana, rais, ambaye yupo katika ziara rasmi ya siku tatu Uholanzi, alikiri katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje (Uholanzi), Bert Koenders.

"Inasikitisha kwamba nimeshindwa kubadilika na kufanya sekta ya kilimo kukua na hivyo watu wengi wameendelea kuwa maskini," Rais alikiri. "Ni sekta inayohusisha watanzania wengi na inahitaji juhudi kubwa," alikiri.

"Watu wengi wanategemea sekta ya kilimo lakini haijakua kwa kasi inayohitajika na wala haijapewa kipaumbele kinachohitajika," Rais aliendelea kukubali. Alisema katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake, wakati sekta nyingine zimekua, hali imekuwa tofauti kwenye kilimo.

President Jakaya Kikwete has conceded - and regretted - his failure to change and grow the agricultural sector over the course of his ten years at the State House.

According to a statement from the Directorate of Presidential Communications circulated to the media yesterday, the president, who is on a three-day official visit to the Netherlands, admitted to the fact in his talks with the country's Minister for Foreign Affairs, Bert Koenders.

"It is sad that I have failed to change and make the agricultural sector grow and hence many people have continued to be poor," the president admitted. "It is a sector that incorporates many Tanzanians and needs much effort," he acknowledged.

"Most people rely on the agriculture sector but it has neither grown at the required pace nor has it been given the required priority," the president went on to admit.

He said over the past ten years of his leadership, while other sectors have grown, that has not been the case for agriculture.

"We need modern agriculture and farmers need loans," he said and pledged that even after he retires from office, he would continue to fight for agricultural development so as to reduce poverty.

"In addition to the continuous growth of the economy, we need to increase efforts to reduce poverty," the president said.

The President said Tanzania utilises well all the assistance it gets from development partners since to a large extent, efforts to ensure economic growth have been successful.

He mentioned examples of such achievements as reduction of the inflation rate from 18.6 per cent during the economic downturn in 2011 to the present 4.5 per cent.

The Netherlands Foreign Affairs Minister, Bert Koenders, pledged his country's continued assistance to Tanzania following the President's appeal.


SOURCE:
THE GUARDIAN
Dokezo: kwa wale watia nia mnaojitamba na #KilimoKwanza mnyamaze sasa, mkuu wenu kashakubali yaishe!
 
kwa mujibu wa 'The FAO Hunger Map 2015'
United Republic of Tanzania
Proportion of undernourished in total population
2014-16: 32.1 %

Number of people undernourished (millions)

1990-92: 6.4 (millions)
2000-02: 13.0 (millions)
2005-07: 14.1 (millions)
2010-12: 16.1 (millions)
2014-16: 16.8 (millions)

Kenya
Proportion of undernourished in total population
2014-16: 21.2 %

Number of people undernourished (millions)

1990-92: 7.9 (millions)
2000-02: 10.4 (millions)
2005-07: 10.4 (millions)
2010-12: 10.0 (millions)
2014-16: 9.9 (millions)

FAO4.png

The Hunger Map, 2014

Ukilinganisha takwimu hizi za FAO, inaonekana 'proportion' ya watu wenye njaa Tanzania inaongezeka ukilinganisha na 2013 ambapo Kenya na Tanzania zilikuwa zinalingana (angalau) kwa 'proportions' za watu wenye njaa katika 'population'! Kenya wamekuwa wakinunua chakula kutoka Tanzania yenye njaa (ni kituko uh)

ed9ea3bfa2.jpg

The Hunger Map, 2013

 
At least amekubali mapungufu

Lakini haitakiwi kuishia hapo

Kuna mabilioni mengi sana yameibiwa kwa mgongo wa kukuza kilimo...mfano ile kampeni ya kilimo kwanza

Tunahitaji kupata mrejesho

Haiwezekani watu watumie madaraka vibaya alafu waachwe tu...They must be held accountable
 
idoyo

Hizi Takwimu za FAO zina mashaka. Kenya wanaomba chakula kwetu na sisi tunazalisha chakula kingi kuliko mahitaji ya nchi.
 
Last edited by a moderator:
idoyo

Nadhani kuna mushkeli katika hizo takwimu.
 
Last edited by a moderator:
Kauli mbiu yake ilikuwa kilimo kwanza, kwa hiyo angesema tu ameshindwa kuongoza taifa, ameliangamiza.
 
Angekiri maisha bora kwa kila mtanzania yameshindikana na kwamba ilikuwa ni porojo tu za majukwaani.
Dhamira alikuwa nayo. Ila kwa mfumo corrupt kama huu wa kwetu inakuwa ni shida kutimiza mahitaji ya wananchi. Rushwa inakwamisha maendeleo ya nchi nyingimza Afrika. Hiyo inatokea Angola, Malawi, Zambia, Uganda, South Africa nk
 
Kauli mbiu yake ilikuwa kilimo kwanza, kwa hiyo angesema tu ameshindwa kuongoza taifa, ameliangamiza.
Sidhani kama upo sahihi kusema kuwa ameliangamiza taifa. Ila nadhani hajafikia malengo yake ipasavyo. Alifanya jitihada nyingi ila ilikuwa inaonekana ni kama yupo peke yake. Matrekta mengi yameletwa na watu wameshindwa kuyasimamia
 
Sidhani kama upo sahihi kusema kuwa ameliangamiza taifa. Ila nadhani hajafikia malengo yake ipasavyo. Alifanya jitihada nyingi ila ilikuwa inaonekana ni kama yupo peke yake. Matrekta mengi yameletwa na watu wameshindwa kuyasimamia
nini kifanyike katika serikali ijayo? cha tofauti kabisa!
 
Mkapa naye alisema hayo hayo. Sasa ni miaka ishirini kilimo kumetupwa wakati asilimia kubwa ya watanzania ndiyo tegemeo lao.

Hao ndiyo viongozi wetu.

Njia ya kuendeleza kilimo iko dhahiri - hakikisha wakulima wanapata masoko. Weka mazingira ya watu kufungua viwanda vya usindikaji (hawa ndio wa kusamehewa kodi). Karne hii bado tunauza pamaba ghafi kwa mfano.

Soko likiwepo watu watalima bila kushurutishwa. Ikifikia hatua hiyo hakikisha upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, ushauri wa kitalaamu, umwagiliaji nk
 
Sidhani kama upo sahihi kusema kuwa ameliangamiza taifa. Ila nadhani hajafikia malengo yake ipasavyo. Alifanya jitihada nyingi ila ilikuwa inaonekana ni kama yupo peke yake. Matrekta mengi yameletwa na watu wameshindwa kuyasimamia

Sawa kama alijua yuko peke yake kwa nini hakuwawajibisha hao aliokuwa amewaweka kwenye hayo madaraka? Kaliangamiza taifa kweli maana maisha yamekuwa magumu sana, amewabeba sana acha abebe lawama.
 
Mkapa naye alisema hayo hayo. Sasa ni miaka ishirini kilimo kumetupwa wakati asilimia kubwa ya watanzania ndiyo tegemeo lao.

Hao ndiyo viongozi wetu.

Njia ya kuendeleza kilimo iko dhahiri - hakikisha wakulima wanapata masoko. Weka mazingira ya watu kufungua viwanda vya usindikaji (hawa ndio wa kusamehewa kodi). Watu likiwepo watu watalima bila kushurutishwa. Ikifikia hatua hiyo hakikisha upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, ushauri wa kitalaamu, umwagiliaji nk
Bora ya Kikwete alithubutu. Lowasa katika hotuba zake hajawahi hata kutamka neno mkulima
 
Sawa kama alijua yuko peke yake kwa nini hakuwawajibisha hao aliokuwa amewaweka kwenye hayo madaraka? Kaliangamiza taifa kweli maana maisha yamekuwa magumu sana, amewabeba sana acha abebe lawama.
Kwani tangu aingie ameweka mawaziri wangapi kwenye sekta ya kilimo na bado mambo hayaendi?
 
Bora ya Kikwete alithubutu. Lowasa katika hotuba zake hajawahi hata kutamka neno mkulima

Kama umewahi kufuatilia hotuba zake, ana kila dalili ya kuonyesha kwamba wafugaji wanaonewa. Akipata urais wafugaji watalisha mifugo kwenye mashamba ya watu! Huo wote ni ubinafsi kunufaisha wafugaji wenzie.
 
Kwani tangu aingie ameweka mawaziri wangapi kwenye sekta ya kilimo na bado mambo hayaendi?

Kuwabadilisha tu haitoshi wangewajibishwa kwa ubadhirifu walioufanya, angepeleka mahakamani washtakiwe kama wahalifu na sheria ichukue mkondo wake wangetia akili lakini kuwekwa pembeni tu haitoshi ndio maana walimchezea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom