Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,219
- 40,456
Zitto Kabwe, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuwa Rais wa Tanzania anasema kuwa Jakaya Kikwete amemwambia yeye na Mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila, kuwa anapendelea Rais wa 2015 awe kijana. Kikwete amewataka Zitto, Kafulila na vijana wengine wajiandae kumrithi.
Source: Post ya Zitto kwenye account ya JF ya kwenye facebook yenyewe hii hapa:
"Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu. Kizazi chenu sasa kijiandae"-JK to David Kafulila and I when launching construction of Malagarasi Bridge.
JK hamteui mtu kushika nafasi kwa kuangalia uwezo wa anayemteua kuweza kuleta mabadiliko katika utendaji bali humteua kwa ushwahiba, na uwezekano wa mtu huyo kumwongezea watu wa kumwunga mkono au kumpunguzia maadui. Ni kwa vigezo hivyo aliwateua kwenye nafasi za uwaziri marafiki na ndugu zake. Alipoona maadui wameongezeka kiasi cha kushindwa kuhimili, kwanza aliweza kufanya jitihada za kumpa Msekwa umakamu M/Kiti wa CCM, akawateua Sita na Mwakyembe. Ili kujiongezea watu wa kumwunga mkono alimteua Mchungaji Rwakatare kwa kudhania atawavuta wafuasi wake wa kiimani kumwunga mkono yeye na CCM bila kujali mtu huyo atakuwa na msaada gani katika Taifa. Nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa na Rais ziliwekwa kwa nia maalum, hasa ikiwa kuwapata watanzania wenye uwezo wa pekee wa kumsaidia Rais katika serikali yake, lakini watu hao hawapendi kuingia kwenye vurugu za uchaguzi, lakini yeye hajaweza kuzitumia vizuri.
Hoja ya kusema Rais ajaye lazima awe kijana, haina msingi wowote maana haina uhusiano na utendaji mzuri tunaoutaka. Kwa sababu JK hakuwahi kuwa na vigezo vya kiutendaji katika teuzi zake, ni dhahiri hata pendekezo lake la Rais ajaye haliwezi kuwa na vigezo tunavyovitaka. Yeyote atakayependekezwa na JK kuwa Rais ajaye, hiyo pekee yake itakuwa ni disqualification, maana kuna uwezekano mkubwa wa JK kupendekeza jina mtu ambaye atakuja kuwa kama yeye. Tulifanya makosa wakati wake, hatutaki kurudia tena.