Kikwete: Msamaha wa kodi utolewe; Lengo ni kupunguza makali ya maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Msamaha wa kodi utolewe; Lengo ni kupunguza makali ya maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 16 March 2011 19:49


  RAIS Jakaya Kikwete ameingilia kati bei ya bidhaa kupanda nchini, hivyo kuiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi kupunguza mfumuko wa bei. Amesema ikiwezekana, wizara itoe msamaha wa kodi ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha. Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana, mjini Dar es Salaam, alipotembelea makao makuu ya wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake, ambapo alizungumza na watendaji. Alisema licha ya wizara kufanya vizuri katika makusanyo ya kodi, inapaswa kuangalia namna ya kupunguza mfumuko wa bei, ili kutoa nafuu ya maisha kwa Watanzania.[​IMG]
  "Ikiwezekana angalieni namna ya kupunguza kodi, ingawa hilo linaweza kutupunguzia mapato lakini inafaa kufanya hivyo ili kutoa ahueni ya maisha kwa wananchi," alisema.
  Katika ukusanyaji kodi, alisema wizara imefikia lengo la serikali, ambapo Desemba, mwaka jana ilikusanya zaidi ya sh. bilioni 500. Hata hivyo, alisema ni vyema ikageukia katika kuinua uchumi wa nchi, hususan kupunguza mfumuko wa bei ili mwananchi wa kawaida apate nafuu ya maisha.
  Aliitaka pia wizara kujikita katika kuzipa nguvu sekta zenye mchango mkubwa katika ukuaji uchumi.
  MADENI YA WASTAAFU
  Rais Kikwete ameitaka wizara hiyo kumaliza malipo ya madeni ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), ili serikali iondokane na mzigo wa kudaiwa na wazee hao.
  Alisema juhudi kubwa zimefanywa na wizara katika kuwalipa wastaafu hao na kwamba, waliosalia ni wachache.
  Kutokana na hilo, alisema ni vyema wakalipwa haraka ili kuondokana na mzigo wa kudaiwa.
  "Hili la wastaafu wa Afrika Mashariki nalo limalizeni, hatuwezi kuendelea nalo siku zote, walipeni," alisema.
  MALIPO YA WALIMU
  Akizungumzia malipo ya walimu, rais Kikwete aliitaka wizara kuwa na utaratibu mzuri wa kuwalipa, hususan wanaoripoti vituoni kwa mara ya kwanza, ili kuepusha usumbufu wa kudai stahili zao.
  Kwa mujibu wa rais Kikwete, wizara imeweza kurekebisha kwa kiasi kikubwa kasoro ya ucheleweshaji mishahara ya watumishi wa umma.
  Hata hivyo, alisema bado tatizo la walimu wapya kutolipwa kwa wakati linaendelea, hivyo linapaswa kushughulikiwa ili lisijirudie.
  Alirejea agizo la kuzuia uhamisho wa watumishi, pale inapokuwa hakuna maandalizi, ikiwemo fedha. Alisema ofisa yeyote wa serikali atakayehusika kufanya hivyo bila maagizo achukuliwe hatua za kinidhamu, ikiwemo kukatwa mshahara.
  Kuhusu maslahi ya watumishi wa serikali, aliiagiza wizara hiyo kuangalia uwezekano wa kuwadhamini wafanyakazi katika taasisi za fedha ili wapate mikopo kwa urahisi.
  Rais Kikwete alisema ili kuwasaidia watumishi hao kujiongezea kipato, ni vyema wizara ikaandaa utaratibu wa kuwadhamini katika taasisi za fedha, hususan wale wenye muda mrefu wa kuendelea kuitumikia serikali.
  Aliagiza kuharakishwa mchakato wa kupatikana Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali, atakayehusika na usimamizi wa fedha za halmashauri, ili kukabiliana na ubadhirifu.
  Rais Kikwete alisema Naibu Mhasibu Mkuu atahusika moja kwa moja katika usimamizi wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri.
  Wizara pia imetakiwa kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani na idara za serikali, ili wafanye kazi kwa uhuru bila kuingiliwa.
  "Wakaguzi wa ndani wasiwe wanawajibika kwa makatibu wakuu, kwa kuwa wao nao ni miongoni mwa wanaochunguzwa, hivyo wakiwa wanawajibika kwao watakosa uhuru wa kufanya kazi vizuri," alisema.
  ZIARA TRA
  Akiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), rais Kikwete alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa uongozi wa mamlaka hiyo.
  Katika hatua nyingine, akiwa mlangoni akitoka ofisi hizo, alilazimika kusimama kuwasikiliza watu waliokuwa wakipaza sauti kumuomba asikilize kilio chao.
  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Joseph Mwakalinga, aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara ya magari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, alimuomba rais kuingilia kati suala la kutozwa ushuru mara mbili.
  Mwakalinga alisema TRA huwatoza kodi wanapoingiza gari kutoka Zanzibar, licha ya kuwa lilikwishalipiwa visiwani humo.
  Rais Kikwete aliwataka kuunda umoja na aliahidi kukutana nao wiki hii ili kusikiliza matatizo yao.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Plzz Mr. Presedent thnk clearly, utakuwa kilaza hadi lini? Tax Exmption ndio italeta maisha bora!? Mwanzo kulikuwa hakuna msamaha? Toka hapo magogoni tukufundishe ala!
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hivi hata Sukari inayozalishwa nchini inatozwa kodi kubwa? ndio sababu ya bei kuwa juu??
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  wamemdanganya tena najua mtasema hivyo WASAIDIZI WAKE WANAMWANGUSHA NA SI JK NI KILAZA HAHAHHA VERY FUN!
   
 5. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  THE SAME PEOPLE FROM THE SAME GOVERNMENT!Jaman mnatuchanganya.Juzi wazir wako Wasira kapewa ushaur wa kupunguza kod akajib haitawezekana maana serikal inahitaj mapato na haitaweza kuish bila kod.Just one day ,mr president unakuja kulekule.the same wazir sasa atabadik kaul in favour of boss na sio wananchi.shame on you all.
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Huyu tunaambiwa ni mchumi eti anako ka digiriii ka uchumi,au mwenzetu kasoma ka-uchumi gani kwamba hawezi kupambanua mambo madogo madogo kama sababu za inflation.Wajameni tusaidieni hapo UDSM alikuaga anaingia darasani kweli tusaidiage wajameni kaa-aibu bwana
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..huyu hafahamu kwamba Zanzibar ni nchi, yenye Raisi na mipaka yake?

  ..kwenye siasa mnataka nchi yenu, ikija kulipa kodi mnajidai nyinyi ni mkoa wa Tanganyika.
   
 8. czar

  czar JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sanaa kila pahali, wakipunguza kodi kwenye bidhaa itabidi wafidie sehemu nyingine, sasa angalia bei za bidhaa zingine wanazoita sio za lazima zitakavyopanda. PAYE pia haitaachwa. Kwenye madini aah jamaa wanapeta bure na misamaha. Hamna kitu kasema JK.
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kwa kuanzia rais yupo kwenye mstari hajakosea. tatizo la kodi kubwa Tanzania ni source ya mfumuko wa bei. Japo ukiachilia mbali hili la kupunguza kodi ya baadhi ya bidhaa ambayo ni kama 0.2% ya sababu za kuwa na maisha magumu. Matatizo yanayotukabili ambayo yanahitaji strategic actions ni

  1. Corruption, rushwa ni source ya kila kitu maana pamoja na kuumiza wananchi pia ina slow down maendeleo yao kutokana na urasimu wanaoufanya waomba rushwa. Huchelewesha mambo kwa makusudi ili kupata chochote kitu. Dili za kifisadi na ujanjaujanja zinazofanywa na watu wanaojiita wafadhili wa CCM, hawa watu wanapewa kazi zote kubwakubwa zenye malipo mazuri kwa lengo la kurudisha pesa hizo kwa mlango wa nyuma kama michango kwa CCM. Kama serikali ingekuwa inatoa miradi yake kwenye makampuni yanayochipukia ingekuwa imeweza kupunguza wasio na ajira na pia kuongeza consumer spending ambapo muuza chai atapata chake, muuza dagaa pia. Ila hawa mapapa wanaopewa hela na kuzi-swindle nje ya nchi ndiyo wanasababisha maisha na uchumi kuwa duni kila siku, HILI NI FUPA LILILOMSHINDA JK.

  2. Unemployment rate should be reduced to the lowest. Watanzania wengi hawana ajira maalum zenye uwezo wa kupatia kipato halali cha kujikimu na hali ngumu ya maisha, tulitakiwa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa viwandani pamoja na kilimo ambavyo kwa sasa ni wimbo usiochezeka.

  3. Serikali inatakiwa kupunguza discretionary spending hasa katika malipo ya wanasiasa na kuwekeza kwa wingi katika miradi ya maendeleo ambayo in a long run itakuwa ni source kubwa ya ajira kwa watanzania

  4. kuondoa mianya yote ya wakwepa kodi ambao wanajulikana kabisa, kwani wengi wa wafanyabiashara wameingia kwenye siasa ili warahisishe ukwepaji wa kodi wakishirikiana na TRA, matokeo yake kodi kubwa inaelekezwa kwa wafanyakazi ambao walitakiwa kuwa na disposable income ya kuweza ku-spend kwa wafanyabiashara wadogowadogo na hivyo kuwezesha trickle down effect kufanya kazi
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mchumi kazini. Teh teh
   
 11. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  khe khe kheheheheeeeeeeee... wewe unazungumzia yule mzee aliyesababisha ban??

  Let me tell you sir, serikali iliyopo ni hadithi ya ule mnara wa babeli, kila mtu anaongea lugha yake... we imagine na shida zote zile, waziri wa fedha yuko bubu na kipara chake (no ban intended!!!)
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  effect ya chadema hiyoooooo
   
 13. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Rais anaposema eti wizara imeshughulikia tatizo la kuchelewa mishahara sio kweli, mshahara wa mwezi wa pili watumishi wamelipwa mwezi wa tatu. Hv huyu raisi yuko serious kweli?
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa mara ya kwanza toka JK achuke kiti cha Ikulu kanifurahisha pale alipoweza kwenda ktk kiini cha kero za Watanzania..

  Binafsi sio mchumi kihivyo, lakini naamini kabisa kuwepo kwa kodi kubwa ndio sababu kubwa ya rushwa TRA pamoja na huu mfumko wa bei za bidhaa nchini.

  Kwa hiyo, nampongeza JK, kutembelea TRA ma iwe ndio mwanzo wake kutazama kero za wananchi,kwa njia hiyo. Afike Mtera, atembelee vyanzo vya nguvu za umeme, mabwawa ya maji safi kama vile Ruvu chini na kadhalika badala ya kusubiri report za wasanii wenzake, kwani kote huko ndiko atakutana na hali halisi pia wataalam wanaoweza kumpa picha pana ya kero hizi..
  Na kikubwa zaidi lazima afikirie mbinu za kudhibidi rushwa mafisadi toka juu, mbali na kupunguza ushuru uongozi mpya na bora uwekwe TRA pamoja na mbinu mpya kabisa za kuingiza bidhaa nchini kwani ukweli utabakia palepale - Huwezi kujaza pakacha linalovuja...

  Ufisadi nchini umefikia mahala tinajenga Nigeria ya kesho.. Kuendelea kuwalealea Mafisadi, sidhani kama atamaliza miaka mitano - dalili zote zimeshajitokeza na visingizio vya kisiasa au udini haviwezi kusaidia bali kuharibu kabisa hata madogo aloweza kuyafanya....
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Siasa tu!
   
 16. e

  emalau JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  At one one time the great scientist Albert Einstein said, the problem which exist in the world today can not be solved by the people who created them, likewise the problem we have in Tanzania can not be solved by the people who created them - CCM and their proxies.

  When you hear the president talking about tax exemption you wonder whether the guy deserves to be at the position he is holding. A leader is supposed to put in place mechanism which do not necessarily need to be consumer oriented pledge. What he has pledged is focusing on temporary solution.

  He should understand that there should be a long term plan of bringing the people to work, and to accomplish this carrot and stick method should be put in place to avert the status quo
   
 17. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chadema are remote controlling this country! Its all I can tell for now. Ccm are confused jamani
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Dakta Kikwete ni mpuuzi sana; hajui kutumia madaraka yake badala yake amekeaa kuwa wa kulalamikia wengine kwa kila analoshindwa. Tatizo la kodi nchini si la TRA wala la wizara ya fedha, kwa haiyo asitafute kisingizio cha kuiambia TRA na Wizara ya fedha kupunguza kodi. Kodi zinapangwa na serikali yake inayoongoza nchi kupitia sheria ya kodi , halafu wale jamaa wa TRA kazi yao ni kutekeleza sheria hiyo ya kodi. Kama kweli Kikwete yuko siriasi kupunguza kodi, (halafu asubiri pia kama wafadhili wake watakubaliana na hilo), inabidi yeye ndiye asimamie uundwaji wa shria mpya ya kodi yenye viwango anavyodhani vinafaa, halafu TRA kupitia Wizara ya fedha watatekeleza.

  Sasa hivi analalama kusudi wananchi waamini kuwa kuwa Mtukufu Rais Kikwete hapendi kodi kubwa zinazowaumiza watu, ila wabaya ni TRA na Wizara ya fedha; huo ni unafiki mkubwa sana.

  Angejifunza kwa rafiki yake Bush alivyopitisha TAX CUT kwa nguvu wakati hata waziri wake wa fedha hakubaliani na hatua hiyo kwa vile ilikuwa inalipeleka pabaya taifa kama inavyojulikana leo. Lakini Rais alisimamia lengo lakje la kupunguza kodi na akafanikiwa.
   
 19. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Ivi Tax exemption ndo kama tax reduction?
   
 20. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Kupunguza kodi sio suluhisho la kupunguza inflation, tatizo la kupanda kwa bidhaa ni sababu ya supply constraints si vinginevyo-kama napoza soda kwa jenereta unatarajia niuze mia tano thubutuu-ntauza mia nane!
   
Loading...