Duh, hizi chuki zinakwedna vipi jamani sii ndio Ya obama kutyaka kuzngumza na wanafunzi Republican wakapinga vibaya vibaya lakini wao alipohutubia Reagan na Bush mzee haikuwa shida.. Tumewaona Mwinyi, Mkapa wakizungumza tena pumba tupu lakini haikuwa na upinzani kama huu....
Kitu kimoja tu , sisi ni wananchi na tujipange.. Haya maswala ya kupinga kila kitu kisha keshoa JK atakuja hutubia watu hamna hata swali moja.. hakuna mtu atakaye inua kidole kuuliza swali la maana..Kipangeni Onyesheni kama kweli mna maswali ambayo yatampa shida na sii kutaka ati JK aje JF kujibu maswali... Utafikiri sisi ndio Mamwinyi wa Bagamoyo tukiagiza maswali huku tumakaa ktk vijiwe vya kahawa..
Mmeshaambiwa JK atapokea maswali hivyo, ni jukumu lenu kutafuta kila mbinu kuuyyafikisha maswali yenu hata kama akijibu Utumbo ndio wakati mzuri kwa wananchi wote tanzania kusikia Utumbo huo, lakini mkiacha na akatoka mtupu, makofi mengi kisha mnalaumu Uongozi wake, huu ni unafiki, kwa sababu mnajua fika kwamba JK atachukua tena ushindi mwaka 2010..Uvivu wa kutouliza na kuendelea kulaumu tuu wakati tunashindwa kujiwakilisha yaani to play our part ni tafisiri nzuri kabisa ya Ndivyo Tulivyo..
Muda unakwenda tungeni maswali yenu, tafuteni kila mbinu muyawakilishe hayo maswali kwa wqahusika au vyombo vya habari.. JK anatakiwa kuwa na wakati mgumu kujibu maswali na hapo ndipo wananchi hasa wa mikoani na vijijini wataweza kufikiwa na magazeti ya kesho.
Kitu kimoja tu ningeomba kuwepo na utaratibu wa kila mara kwa rais kufanya hotuba kama hizi na apokee waswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbalia mbali badala ya kuchukua maswali kiholela. Ndugu zangu tuutumie muda au nafasi hiyo kufanya japo dogo la maana kuliko kuendelea kulalamika tuu na utawala wa JK
Aibu tupu Ikulu,Ingoja wasome hii kitu labda akili zitawakaa sawa,Kwa huo upuuzi wa kutumia Yahoo.Kuna watu kesho watakua wana Password ya upuuzi.kuna watu wanajua kuichezeaMhhh ataweza jibu kitu kweli mambo ya Meremeta ama maswali yatawekwa kapuni!
Salvatore Rweyemamu unafanya nini Ikulu? Huoni kuwa ni aibu kwa Mkuu wa Nchi kuwasiliana na wananchi kupitia Yahoo! Tena katika nchi ambayo leo asubuhi nimesikia habari ikitangazwa kuwa inachukua namba tano ulimwenguni kwa kuwa na wingi wa madinii ya Uranium!Tena takriban mwezi mmoja uilopita rais mwenyewe amezindua Seacom (undersea fibre optic cable ya hiper-speed broadband internet connectivity)! Maajabu! Kama umeshindwa ku-cope, Rweyemamu, itabidi urudi Uhuru!
Kitu ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa ofisi ya Rais kutumia anawani ya kibiashara kwa email za kuwasiliana na Rais (yahoo.com) badala ya kutumia anwani ya kiofisi.
DC,
Shangaa sasa, hii inaonyesha namna gani hatupo serious na mambo yetu!
Uvivu wa kutouliza na kuendelea kulaumu tuu wakati tunashindwa kujiwakilisha yaani to play our part ni tafisiri nzuri kabisa ya Ndivyo Tulivyo....
Kwani ni issue ngapi amekuwa na wakati mgumu kuzi adress na watu wanajua but nothing is going on bana? Tutafute kila mbinu ya kuwakilisha? what do you mean sir?Muda unakwenda tungeni maswali yenu, tafuteni kila mbinu muyawakilishe hayo maswali kwa wqahusika au vyombo vya habari.. JK anatakiwa kuwa na wakati mgumu kujibu maswali na hapo ndipo wananchi hasa wa mikoani na vijijini wataweza kufikiwa na magazeti ya kesho.....
Hata angekuwa anasikiliza maswali/maoni ya wananchi kila siku, kama hamna DHAMIRA YA UTEKELEZAJI na UWAJIBIKAJI ni bureee. Issue sio kuwa na database ya maoni au maswali, that is not the issue. Issue ni utekelezaji wa mambo. Hata kama angekuwa anapokea ushauri mmoja kwa mwezi na anaufanyia kazi effectively, ni bora zaidi kuliko huu mzaha wa kupokea malalamiko/maswali randomly kutoka kwa wananchi. This thing is not practical bwana. Inamaana watu wa kule mahenge watauliza kuhusu issue ya Zombe, wa kigoma barabara na reli, wafanyakazi PAYE kubwa... huoni huu ni mvurugano. Angetoa topic au area of focus walau the questions zingekuwa specific and focused lakini hili sioni kama kuna dhamira yeyote.Kitu kimoja tu ningeomba kuwepo na utaratibu wa kila mara kwa rais kufanya hotuba kama hizi na apokee waswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbalia mbali badala ya kuchukua maswali kiholela. Ndugu zangu tuutumie muda au nafasi hiyo kufanya japo dogo la maana kuliko kuendelea kulalamika tuu na utawala wa JK..