benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Mtangazaji mahiri Salim Kikeke siku ya jana aliaga rasmi, akitoa taarifa ya kuondoka katikaShirika la Habari la Uingereza baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miongo miwili (Miaka 20)
Kikeke kupitia matangazo ya Dira ya Dunia yanayorushwa na StarTV kwa hapa Tanzania aliaga rasmi kwamba matangazo ya jana ndiyo ya mwisho katika shirika hilo ambalo amefanya nalo kazi kwa miaka 20.
Kwa "experience" na "exposure" aliyoipata Kikeke kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika moja kati ya mashirika makubwa ya habari ulimwenguni nadhani ni muda wa Kikeke kurejea nyumbani, ni muda wa Taifa kufaidi matunda ya kijana wake, ni muda sahihi Rais Samia Suluhu afanye maamuzi yakayoleta mapinduzi pale TBC, ni muda sahihi KIKEKE AENDE KUHUDUMU KAMA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC).
Tumeona Zhura Yunus akipeleka ujuzi wake Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania na Charles Hillary akifanya hivyo kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Zanzibar, sasa tumtumia Kikeke pale TBC.
Haya ni maoni na mapendekezo yangu tu, wadau mnaonaje?