Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Sep 8, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kesho, Jumatano, Septemba 9, 2009, atazungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku. Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zinatarajia kuonyesha mazungumzo hayo.

  Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.

  Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.

  Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.


  Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.

  Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari +255-22-2772448, +255-22-2772452 na +255-22-2772454.

  Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari 0788-500019, 0714-591589 na 0764-807683 ama kupitia kwenye barua pepe swalikwarais@yahoo.com kuanzia leo.

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM
  .

  08 Septemba, 2009
   
 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amejiandaa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wananchi? Hofu yangu ni kwamba mengine yanaweza kuwa embarrassing kwa mkuu wa nchi. Hii imekaaje? Au kuna watakaoandaliwa kuuliza maswali?
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Wameanza kuuza sura!Tumechoka kusikiliza pumba.

  Hotuba ya rais mpaka baada ya miezi kadhaa hata kama kuna mambo mazito ya nchi wapi na wapi.

  Mimi binafsi nategea nipate majibu ya ni mpaka lini mafisadi watakuwa wamefilisiwa na kufungwa gerezani? Je, tusubiri uchaguzi upite? Fedha za EPA ziko wapi?

  Maana kwa wakulima haziko kilimo kiko vilevile.Kikwete ameuza lini nchi kwa waarabu?
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Yatakuwa filtered na TBC. Si yote yatakayo ulizwa yatamfikia rais
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,390
  Likes Received: 3,719
  Trophy Points: 280
  Yasije yakawa yale yale ya yule mwanafunzi wa Mwanza. Unauliza swali halafu inaonekana umetumwa, maana kwa utashi wao wengine hawawezi kuuliza maswali ya aina ile mpaka watumwe.

  Hatukawii kuanza kufuatana na kuulizana hata pensi nyanya niliyonayo nimeitoa wapi, achia mbali kuku, gari, duka n.k. Na kwa jinsi wanavyojuwa kufuata, utafuatwa na kila aina ya nguvu waliyonayo FFU (una fujo), POLICE (mwizi, kibaka), MAGEREZA (umefungwa), TRAFIC POLICE (kama una gari, pikipiki baiskeli hadi utapaki) HAKIMU (utafungwa baada ya kuuliza swali ulilotumwa), TRA (umekwepa kodi), n.k.

  KAMA KWELI WAPO SILIAZI, WAACHE KUSUMBUA WANANCHI BILA SABABU ZA MSINGI BAADA YA KUULIZA MASWALI. HAYO MASWALI EMBARRASSING YAPO HIVYO KWA VILE WANANCHI WANA-FEEL EMBARRASSED
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Lakini Hao TBC pamoja na Ikulu wawe kama wameenda shule jamani umeona hiyo email hapo chini swalikwar...@yahoo.com hii ni freeemail toka yahoo na tena imesajiliwa leo leo dakika chache zilizopita tu wanataka wananchi watume email zao huko , waliposajili hii email walisoma terms zote za yahoo?

  Kwamba kila unapofungua au kuwasiliana na mtu kuna log huwa wanazihifadhi? Kwa kazi zao wao wenyewe yahoo? hapa kwetu tunatakiwa kumuuliza maswali raisi kwa kutumia email hiyo hiyo kwa kweli hili halikubaliki

  RAISI WAJIBISHA WOTE WALIOTENGENEZA EMAIL HII , WEWE NI RAISI UNATAKIWA ZAIDI YA
  HII UNATAKIWA KITU KINACHOKUTAMBULISHA SIO HII AIBU SANA , HIZO BAJETI KUBWA
  MNAZOPITISHA HUWA MNATUMIA KWENYE NINI ? HIZO SEMINA NA WATU WANAENDA
  KUFUNDISHWA NGAMBO MASUALA YA ICT NDIO LEO WANAKUJA NA HIKI KITU ?

  HATUTAKI RAISI WETU AZARAULIWE KIASI HICHI
   
 7. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  Salvatore Rweyemamu unafanya nini Ikulu? Huoni kuwa ni aibu kwa Mkuu wa Nchi kuwasiliana na wananchi kupitia Yahoo! Tena katika nchi ambayo leo asubuhi nimesikia habari ikitangazwa kuwa inachukua namba tano ulimwenguni kwa kuwa na wingi wa madinii ya Uranium!Tena takriban mwezi mmoja uilopita rais mwenyewe amezindua Seacom (undersea fibre optic cable ya hiper-speed broadband internet connectivity)! Maajabu! Kama umeshindwa ku-cope, Rweyemamu, itabidi urudi Uhuru!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mhhh ataweza jibu kitu kweli mambo ya Meremeta ama maswali yatawekwa kapuni!
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  ndio wale wale wababaishaji,wanafanya kazim kwa mazoea tu bila kujali haya ni najukumu ya kitaifa.......

   
 10. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo mengi ya nchi hii hayaeleweki kabisa,hapa sio suala la bajeti wala nini,huu ni uzembe wa watendaji,jamani hata kama umeingizwa kwa ki note kwenye kazi hiyo mpaka leo kweli huwezi kujua raisi wa nchi kuwasiliana kwa yahoo kuwa ni aibu!!!!
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tafadhali watanzani nisaidieni kufahamu kama kule ikulu hawana site yao ambayo wanaweza kufungua emails mbalimbali kwa shughuli mbalimbali. Salva naomba ujiuzulu kazi imekushinda, waachie vijana wabunifu. Au niseme wapo lakini Salva una assume mno cheo bila ku-decentralize??? Please, acheni aibu.

  Tanzanians we are lazy au hatuogopi kuaibika??? Hii ni aibu ya mwaka sijawahi kuona tena. Acheni mambo ya free lunches!!! Yaani yahoo ambako kila kitu ni open??? Acheni hayo!!! Shame!!

  Halafu hayo maswali ya papo kwa papo na majibu, mhhhhhhh yangu macho!!!!! Hebu to speculate some questions topics!!!

  1.Rushwa

  2.Ufisadi hasa hasa kesi za EPA

  3.Hukumu ya Kesi ya Zombe

  4.Kiwira

  5.Meremeta and Deep Green

  6. RADAR a.k.a vijisenti Chenge

  7. Richmond

  8.Fedha ze uwezeshaji wananchi (J.K Fund) -

  9.
  10.
  11.
  12 The list is endless!!

  hapo hujagusia hali ngumu ya maisha kwa mtanzania hasa vijinini

  Wana JF tusisahau kuuliza maswali maana tuna upeo mkubwa wa mambo!!! Watuhakikishie tu usalama wa maisha na visimu namba vyetu ambavyo tumeregister!!!
   
 12. B

  Boca1 Member

  #12
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "swalikwarais@yahoo.com"! anyone can register that one. I can believe this is an e-mail account for the STATE HOUSE. Comrade Rweyemamu please resign
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa vyema tusiangaike kutafuta makosa tu ohoo mara yahoo tuitimiea fursa hii adimu kumlima maswali JK wa Bagamoyo mpaka akione kiti kichungu.
   
 14. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nashukuru sana mkuu SHY umeliona; hivi hatuna IT specialist hapo state house kweli?? jamani hata ku-configure email kwenye domain ya state house mnashindwa?? mnafanya nini hapo?? hii ni kuidhalilisha nchi!! ... aibu gani hii!! eeh Mola tuepushe ...!!
   
 15. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ngongo .. i believe unaelewa unachomaanisha .. so kifupi ni kwamba tukiwa kama sovereign state kwanini tutumie free tools (which are being administered by foreigners) ku-discuss mambo yetu ya ndani?? tena ikulu?? wakati tunao watu tunaowalipa kwa kodi zetu kushughulikia mambo haya?? wtf ..!!
   
 16. s

  saikon nokoren Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As usual the President(JK) must come with plain ideas,
   
 17. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  RAISI WAJIBISHA WATENDAJI WAKO

  Mheshimiwa Raisi Toka uingie madarakani kumekuwa na jitihada nyingi sana zinazofanywa na watendaji wako katika kuhakikisha unakuwa karibu zaidi na wananchi wako kwa njia rahisi zaidi za mawasiliano .

  Toka umeingia madarakani watendaji wako wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya kimataifa yaani INTERNET kwa ajili ya kukuweka wewe karibu zaidi na wananchi wako , pamoja na jitihada hizi za kupongezwa kuna mengine yamefanyika inabidi sasa uwe macho na hawa watu .

  Miaka miwili iliyopita mlianzisha tovuti maalumu kwa ajili ya wananchi kutoa maoni yao , kipindi hicho watu mbali mbali walilalamika kuhusu gharama za tovuti hiyo hakuna aliyejali kujali kwa maana ya kutoa ufafanuzi kwa wananchi hata hivyo tovuti hii mpaka leo iko kimya .

  Baadaye mlianzisha tovuti zingine ambazo zilikuwa zinafanana na hizo za kutoa maoni , naona kuna moja bado iko lakini imeshindwa kupambana katika soko ili kuweza kutambulika itumike kiurahisi na watu wengi zaidi maana yake iko kimya .

  Halafu likaja hili la ikulu kuanzisha blogu yake ya mawasiliano ambayo ilikuwa imesajiliwa katika Google , si unakumbuka raisi ulienda kutembelea makao makuu ya google mwaka huu na wasaidizi wako ? wale ndio mlisajili blogu kwao , pamoja na kusajili imeandikwa mara chache sana mtu akitaka habari zozote inabidi atembelee blogu na mitandao mengine na sio blogu hiyo .

  Mheshimiwa hakukuwa na sababu za msururu wa tovuti zote hizi pamoja na blogu hizi zote kwa sababu raisi aliyekutangulia alikuwa na tovuti maalumu ya ikulu na nyingine iliyokuwa inaitwa statehouse ilibidi kuendeleza tovuti hizi na kuweka hivyo vyote .
  Kumbuka Ikulu sio mali yako wewe wala ya mwingine wowote yule , kiongozi aliyetoka alitambua hilo sio mali yake ndio maana akaacha tovuti hizo zenye majina ya ikulu , ili wewe ukiingia mtumie hizo na muziendeleze tofauti yake mmeziacha zote na kuanzisha zetu wenyewe hii sio tabia nzuri mheshimiwa .

  Baada ya yote hayo leo tena nimesoma Barua toka ikulu kwa vyombo vya habari inayohusu mkutano wako kesho moja ya kitu kilichonichekesha na kunihuzunisha ni hili la kuweka email ya yahoo ambayo ni swalikwarais@yahoo.com , inahuzunisha sana kwa sababu watendaji wako wameshindwa kubuni njia nzuri zaidi na bora kwa ajili ya wananchi kutoa maoni yao kwenye karne hii .

  Anuani ya barua pepe hiyo imesajiliwa leo na ninaamini wakati wanasajili hawakusoma maelezo ya ziada kabla ya kuendelea na usajili hivi ikatokea sasa mtu akafanikiwa kuingilia anuani hiyo akachukua maswali hayo pamoja na mawasiliano mengine mtafanya nini ? halafu akaamua kuifuta mtafanya nini ? na suala la usalama wako hapo umeliwekaje ? .

  Mheshimiwa kila unapotaka kusoma Ujumbe kwenye Anuani hiyo kama kweli utakuwa unaisoma , kumbukumbu zinabaki yahoo kwenyewe , kila unapojaribu kujibu maswali kutumia anuani hiyo inapoenda itajulisha ilijibiwa akiwa wapi kwahiyo uhalifu unaweza kuanza hapo na kuendelea sipendi kuona hili likiendelea

  Kwa maslahi ya usalama Wako wewe mwenyewe raisi , wasaidizi wako na wengine ambao watakuwa kwa njia moja au nyingine wanatumia anuani hiyo nawaomba kabisa muache kutumia anuani hiyo andaeni njia nzuri za mawasiliano kati ya raisi na wananchi wake na hivi vyote vinaweza kufanyika kwenye tovuti ya ikulu ikitengenezwa vizuri tu .

  Kingine mnatakiwa mfungue channel zetu kwenye tovuti zingine kama youtube hii ni kwa ajili ya video muwe mnaweka video zenu na vingine humo , Raisi wa sasa wa Marekani alisaidiwa sana na youtube katika kufanikisha mambo yake mengi .

  Mheshimiwa raisi ulizindua Mkonga wa mawasiliano siku chache tu zilizopita kwa sasa mtandao uko haraka sana hakuna matatizo kama zamani naamini wasaidizi wako wakitumia advantage hii utafika mbali hata kwenye kampeni zako za mwaka 2010 utatesa sana .

  Mwisho ni kukuomba wewe na wasaidizi wako muwe karibu sana na wataalamu wenu wa ICT katika utendaji wa kazi inawezekana hata hii ANUANI iliyotengenezwa leo pamoja na hizo BLOGU zimetengenezwa bila ridhaa ya wataalamu wenu wa ICT nah ii ni mbaya sana , hawa watu wanasomeshwa kwa pesa nyingi sana lazima tuone tofauti yao katika jamii .
   
 18. P

  Papa Sam Senior Member

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  onyesho lingine linaletwa kwetu na wasanii wakutoka kitalu namba moja.
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kama IT members wa ikulu ni akina kisare unadhani kuna kitu hapo??? ni ziro tu.
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Server yenyewe kufanya configuration mpaka wamtafute Mtui, akisafiri wako hoi. Ikulu pale ICT imelala na kuna vihiyo kibao pale. Kisare kama anabisha aseme hadharani kama kweli anaweza ku-configure linux server.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...