Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
Duh, hizi chuki zinakwedna vipi jamani sii ndio Ya obama kutyaka kuzngumza na wanafunzi Republican wakapinga vibaya vibaya lakini wao alipohutubia Reagan na Bush mzee haikuwa shida.. Tumewaona Mwinyi, Mkapa wakizungumza tena pumba tupu lakini haikuwa na upinzani kama huu..

Kitu kimoja tu , sisi ni wananchi na tujipange.. Haya maswala ya kupinga kila kitu kisha keshoa JK atakuja hutubia watu hamna hata swali moja.. hakuna mtu atakaye inua kidole kuuliza swali la maana..Kipangeni Onyesheni kama kweli mna maswali ambayo yatampa shida na sii kutaka ati JK aje JF kujibu maswali... Utafikiri sisi ndio Mamwinyi wa Bagamoyo tukiagiza maswali huku tumakaa ktk vijiwe vya kahawa..

Mmeshaambiwa JK atapokea maswali hivyo, ni jukumu lenu kutafuta kila mbinu kuuyyafikisha maswali yenu hata kama akijibu Utumbo ndio wakati mzuri kwa wananchi wote tanzania kusikia Utumbo huo, lakini mkiacha na akatoka mtupu, makofi mengi kisha mnalaumu Uongozi wake, huu ni unafiki, kwa sababu mnajua fika kwamba JK atachukua tena ushindi mwaka 2010..Uvivu wa kutouliza na kuendelea kulaumu tuu wakati tunashindwa kujiwakilisha yaani to play our part ni tafisiri nzuri kabisa ya Ndivyo Tulivyo..

Muda unakwenda tungeni maswali yenu, tafuteni kila mbinu muyawakilishe hayo maswali kwa wqahusika au vyombo vya habari.. JK anatakiwa kuwa na wakati mgumu kujibu maswali na hapo ndipo wananchi hasa wa mikoani na vijijini wataweza kufikiwa na magazeti ya kesho.

Kitu kimoja tu ningeomba kuwepo na utaratibu wa kila mara kwa rais kufanya hotuba kama hizi na apokee waswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbalia mbali badala ya kuchukua maswali kiholela. Ndugu zangu tuutumie muda au nafasi hiyo kufanya japo dogo la maana kuliko kuendelea kulalamika tuu na utawala wa JK..
 
Duh, hizi chuki zinakwedna vipi jamani sii ndio Ya obama kutyaka kuzngumza na wanafunzi Republican wakapinga vibaya vibaya lakini wao alipohutubia Reagan na Bush mzee haikuwa shida.. Tumewaona Mwinyi, Mkapa wakizungumza tena pumba tupu lakini haikuwa na upinzani kama huu....

Kitu kimoja tu , sisi ni wananchi na tujipange.. Haya maswala ya kupinga kila kitu kisha keshoa JK atakuja hutubia watu hamna hata swali moja.. hakuna mtu atakaye inua kidole kuuliza swali la maana..Kipangeni Onyesheni kama kweli mna maswali ambayo yatampa shida na sii kutaka ati JK aje JF kujibu maswali... Utafikiri sisi ndio Mamwinyi wa Bagamoyo tukiagiza maswali huku tumakaa ktk vijiwe vya kahawa..

Mmeshaambiwa JK atapokea maswali hivyo, ni jukumu lenu kutafuta kila mbinu kuuyyafikisha maswali yenu hata kama akijibu Utumbo ndio wakati mzuri kwa wananchi wote tanzania kusikia Utumbo huo, lakini mkiacha na akatoka mtupu, makofi mengi kisha mnalaumu Uongozi wake, huu ni unafiki, kwa sababu mnajua fika kwamba JK atachukua tena ushindi mwaka 2010..Uvivu wa kutouliza na kuendelea kulaumu tuu wakati tunashindwa kujiwakilisha yaani to play our part ni tafisiri nzuri kabisa ya Ndivyo Tulivyo..

Muda unakwenda tungeni maswali yenu, tafuteni kila mbinu muyawakilishe hayo maswali kwa wqahusika au vyombo vya habari.. JK anatakiwa kuwa na wakati mgumu kujibu maswali na hapo ndipo wananchi hasa wa mikoani na vijijini wataweza kufikiwa na magazeti ya kesho.

Nadhani reservations za wachangiaji ni effectiveness ya hii style "mpya'' ya Ki- Chavez ya kujitafutia umaarufu kwa kudai Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi WOTE WA TANZANIA kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, wakati wanajua wazi kwamba wata sensor maswali. Si chuki na sidhani kuna mtu anamchukia mh Rais wetu.

Kitu kimoja tu ningeomba kuwepo na utaratibu wa kila mara kwa rais kufanya hotuba kama hizi na apokee waswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbalia mbali badala ya kuchukua maswali kiholela. Ndugu zangu tuutumie muda au nafasi hiyo kufanya japo dogo la maana kuliko kuendelea kulalamika tuu na utawala wa JK

Hapa niko pamoja na wewe. Hata hao akina Reagan, Obama, Mwinyi, Bush, Mkapa uliowataja huwa/walikuwa wanatoa hotuba na kupokea maswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbali mbali na siyo hii innefective and populist style ya Hugo Chavez
 
Last edited:
Salvatore Rweyemamu unafanya nini Ikulu? Huoni kuwa ni aibu kwa Mkuu wa Nchi kuwasiliana na wananchi kupitia Yahoo! Tena katika nchi ambayo leo asubuhi nimesikia habari ikitangazwa kuwa inachukua namba tano ulimwenguni kwa kuwa na wingi wa madinii ya Uranium!Tena takriban mwezi mmoja uilopita rais mwenyewe amezindua Seacom (undersea fibre optic cable ya hiper-speed broadband internet connectivity)! Maajabu! Kama umeshindwa ku-cope, Rweyemamu, itabidi urudi Uhuru!


Hi kali yaani huyu bwana hana hata aibu ya kuiweka hiyo email address yake ya yahoo
 
Kama mTZ, Hako ka email ka yahoo kaminifanya niwe mdogo kama nukta na ki-ukweli hii HII NI FEDHEHA KUBWA SANA na nahisi waTZ wote TUMEVULIWA NGUO kwa huu UPUUZI. Lakini unategema nini kwa nchi ilojaa watu wasio wajibika kila kona? Ni aibu aibu aibu!
 
Mzee wa nchi na nchi na wapambe wake hawana jipya, ameshindwa kumrudi Lowasa na richmond, ameshindwa kumrudi Rostam kwa ufisadi na zaidi ameshiriki kumsulubu Sita. Anataka tumuulize maswali gani??? Labda atuambie ataondoka lini kwenye pango takatifu kutoa fulsa ya kumwingiza mtu muungwana na muadilifu
 
Wanajamvi,

Leo JK ataongea live na wananchi. Namba za simu za kuongea naye zimetolewa na pia hiyo anwani ya barua pepe. Namba za simu sijakamata vizuri.

Kitu ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa ofisi ya Rais kutumia anawani ya kibiashara kwa email za kuwasiliana na Rais (yahoo.com) badala ya kutumia anwani ya kiofisi. Lakini kitu kingine kinachonipa taabu ni kuishawishi akili yangu kwamba kweli Rais atajibu maswali yetu. Je, yatachaguliwa ili apewe yale ambayo wasaidizi wake (kwa uamuzi na mapenzi yao) wataona yanafaa? Je ataweza kujibu maswali yetu magumu ambayo tumekuwa tukijiuliza toka aingie Ikulu? Naomba wenye namba za simu wazimwage hapa ili tujaribu na sisi kwenda live.
 
Jk alipoingia madarakani alijua matatizo yote ya wananchi wake aliyaorodhesha kwa kuyataja na kuahidi kuyatekeleza kwa kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ambayo yeye binafsi naamini hataki hata kuisikia tena.Matatizo aliyoyakuta ndiyo yaliyopo,je anataka kujua nini zaidi?.Ilinipa tabu kuamini kwa haraka niliposoma hapa jf kuwa rais ataongea na watz,kwani sikuamini kama inawezwekana kuongea na kujua matatizo ya watz wote kwa muda wa dakika90 miaka minne baada ya muda wa uongozi.Zaidi ya yote nilitegemea angeongea na sisi mwanzoni mwa utawala wake ili kujua matatizo yetu.
Rais anatutega?
 
kwanza rais leo hajuiwi atasema nini? na hana jipya la kutuambia kwani nchi imeoza sana na yeye katulia sana....hakuna hata kesi moja ya mafisadi.
 
Kitu ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa ofisi ya Rais kutumia anawani ya kibiashara kwa email za kuwasiliana na Rais (yahoo.com) badala ya kutumia anwani ya kiofisi.

DC,

Shangaa sasa, hii inaonyesha namna gani hatupo serious na mambo yetu!
 
0788-500019, 0714-591589 na 0764-807683.

hizi wanasema kwa ajili ya ujumbe mfupi,

mi sijui huyu mtu anataka nini, kimsingi hatajibu chochote cha maana, dakika 90 hazitoshi. uswahili umezidi sana kwa huyu rais,
 
Leo hii Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete,atapokea maswali na maoni kutoka kwa wananchi kwa njia ya kupiga simu,ujumbe mfupi(SMS),na baruapepe(e-mail).Na tukio hili kwa siku ya leo litachukua/litatumia muda wa dakika 90 na litaanza saa 2:30 usiku kutoka studio za TBC1;si hiyo pekee tukio hili litarushwa na vyombo vyote vya habari vilivyopo hapa nchini Tanzania.

Na zifuatazo ni namba za simu:+255-22-2772448,+255-22-2772452, na +255-22-2772454.

Na zifuatazo ni namba za ujumbe mfupi wa simu(SMS):0788-500019,0714-591589, na 0764-807683.

Na baruapepe(E-mail):swalikwarais@yahoo.com

Haya sasa nafasi ya kutoa kero zenu ndiyo kama hiyo,mshindwe wenyewe
 
Tunamsubiri ajibu maswali yetu haya. 1. Kwa nini chama chake kimebariki ufisadi kupitia NEC. 2. Au huo ndio mkakati wa kulinda Kagoda (Rostam), Deep Green (Masha), Richmond (swahiba wake Lowassa)? Naingia kwenye mkutano, narudi kuweka maswali mengine...
 
Uvivu wa kutouliza na kuendelea kulaumu tuu wakati tunashindwa kujiwakilisha yaani to play our part ni tafisiri nzuri kabisa ya Ndivyo Tulivyo....

Mkuu heshima mbele, lakini hapo juu tafadhali tutake radhi! Nani ka kwambia JK hajaulizwa maswali. Ameshaulizwa sana tena sana tuu. He knows all our questions. So hizo dakika 90 aje na majibu. Ni upuuzi kusema eti raisi hajui the basic questions za watanzania sasa hivi. Utakuwa ni mzaha kabisa. Hata kama wewe makandara hujui maswali ya watanzania ambayo hayajajibiwa long agoo basi it is better tuuwe media zote tz.

Muda unakwenda tungeni maswali yenu, tafuteni kila mbinu muyawakilishe hayo maswali kwa wqahusika au vyombo vya habari.. JK anatakiwa kuwa na wakati mgumu kujibu maswali na hapo ndipo wananchi hasa wa mikoani na vijijini wataweza kufikiwa na magazeti ya kesho.....
Kwani ni issue ngapi amekuwa na wakati mgumu kuzi adress na watu wanajua but nothing is going on bana? Tutafute kila mbinu ya kuwakilisha? what do you mean sir?

Kitu kimoja tu ningeomba kuwepo na utaratibu wa kila mara kwa rais kufanya hotuba kama hizi na apokee waswali toka waandishi wa habari toka vyombo mbalia mbali badala ya kuchukua maswali kiholela. Ndugu zangu tuutumie muda au nafasi hiyo kufanya japo dogo la maana kuliko kuendelea kulalamika tuu na utawala wa JK..
Hata angekuwa anasikiliza maswali/maoni ya wananchi kila siku, kama hamna DHAMIRA YA UTEKELEZAJI na UWAJIBIKAJI ni bureee. Issue sio kuwa na database ya maoni au maswali, that is not the issue. Issue ni utekelezaji wa mambo. Hata kama angekuwa anapokea ushauri mmoja kwa mwezi na anaufanyia kazi effectively, ni bora zaidi kuliko huu mzaha wa kupokea malalamiko/maswali randomly kutoka kwa wananchi. This thing is not practical bwana. Inamaana watu wa kule mahenge watauliza kuhusu issue ya Zombe, wa kigoma barabara na reli, wafanyakazi PAYE kubwa... huoni huu ni mvurugano. Angetoa topic au area of focus walau the questions zingekuwa specific and focused lakini hili sioni kama kuna dhamira yeyote.
 

Mimi nadhani, hasa kwa wote wale wanaopinga ufisadi, hawatawatendea wananchi vyema iwapo JK hataulizwa maswali kuhusu uchotaji wa EPA, Richmond, Deep Green na tuhuma nyingine za ufisadi.

Natoa ombi kwa wapinga ufisadi, yeyote yule atayepata fursa ya kuuliza swali, amuulize JK swali lifuatalo:

“Mheshimiwa Rais, itakumbukwa kwamba mapema Agosti mwaka 2008 ulisimama Bungene kuwathutubia Wabunge, na pamoja na mada nyingine uliozozingumzia ni suala la uchotaji wa mapesa kutoka akaunti ya EPA ya BoT.

Ulitamka waziwazi kwamba pesa zote zilizochotwa kutoka akaunti hiyo zitafuatiliwa mtiririko wake hadi mtu wa mwisho ili wezi wapatikane.

Mheshimiwa Rais, katika wizi wa karibu Sh bilioni 40 uliofanywa na kampuni ya Kagoda, ilibainika kwamba pesa hizo zilitoka BoT na kuingizwa katika akaunti 6 za matawi kadha ya benki ya CRDB (namba za akaunti hizo zinajulikana) na halafu zikachukuliwa kama pesa taslimu na watu ambao hadi sasa hwajulikani. Zilichukuliwa taslimu kwa hofu kwamba kuziondoa/kuzihamisha kwa hundi mtiririko wake ungeweza kujulikana.

Mheshimiwa Rais, jee hii inawezekana kweli -- kwamba watu hao hawajulikani, na hasa kutokana na utaratibu wa kibenki wa kulipa pesa taslimu? Hivi ni kweli CRDB wameshindwa kabisa kabisa kuwatambua ni akina nani waliochukuwa pesa taslimu nyingi kama hizo over the counter?

Jee taasisi ya upelelezi iliyoko chini ya ofisi yako TAKUKURU imefanya kazi kwa udhati na undani kuhusu suala hili? Itashindwa vipi kuibana CRDB kuwabaini waliochukua pesa hizo? Jee hadi sasa umechukuwa hatua gani kuwawajibisha wakuu wa TAKUKURU kwa kushindwa kutimiza uliyoyatamka Bungeni -- kwa kukamilisha mtiririko wa uchotaji huu wa Kagoda ili kuwabaini wezi hawa?

Natanguliza shukrani, Mheshimiwa Rais.
 
Ni wazo zuri sana lakini ingekuwa vizuri zaidi kama wasahauri wa raisi wange jaribu kuomba ushauri kwa wananchi kabla ya kumuweka raisi runingani na watu wakamuuliza maswali,ninachokiamini,wapo wana nchi wenye uwezo mkubwa wa kumshauri raisi kuliko ninyi mlioteuliwa kwa sasa.kwa kuwa hata nyie wenye nafasi hizo mnahitaji ushauri kwa wananchi wengine kabla hamja mshauri raisi.angalieni kwa makini suala hili.washauri sasa mnakoelekea siko.
 
Mimi naona ingefaa apewe maswali ya wananchi kupitia njia alizotaja in advance kisha maswali hayo ayafanyie utafiti halafu atafute muda wa kutoa majibu yenye uhakika! Hayo maswali ya papo kwa hapo amwachie Waziri Mkuu Pinda akiwa Bungeni. Otherwise anaweza akajishushia hadhi kwa utaratibu huu kwa kuwa kunaweza kuwa na maswali ambayo ni embarassing!
 
Labda ndio wanajaribu kuiga kama vile Obama toka America kwa kukusanya maoni ya watu na vitu vinahusu Tanzania. duh ngoja tuone wana kitu gani cha kusema
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom