Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
huu ni usanii tu wa kiongozi mkuu wa nchi, hakuwa na sababu ya kutoa hii mail address, yeye asubiri tu maswali ya moja kwa moja na sio hadi apewe maswali ayafute mengine ndio aje kutujibu, pia ningependa kumuona mzee mwanakijiji naye akishiriki katika kuuliza maswali pale tbc 1
 
JK kama anataka discussion aanzishe thread humu JF!
Nina uhakika atapata michango iliyotulia kuliko hizo simu atakazokuwa anapigiwa na walewale mabingwa wa kupiga simu kina Manase Muhaha, yule Ustadh wa Tegeta, Chesco mzee wa matunda nk
 
The Farmer;577840]Buchanan, Hakuna sababu yoyote ile ya kupewa maswali in advance. Mambo yanayokera watanzania yanajulikana sitegemei kama kuta kuwa na swali ambali Rais JK atakuwa hajawahi kulisikia.
Ni kweli atakuwa anayajua. Lakini kwa nini sasa ameamua kutupotezea muda eti anataka kuongea live? Anatuzuga au zecomedy nyingine?
Kama kweli hapa rais ameamua kuongea live na wananchi tunatahadharisha tusije kukakosa line kwa sababu ya JAM kwenye mawasiliano...
Kama ulishajaribu kupiga simu kwenye vipindi live vya TV basi hutashangaa. Labda utumie simu ya mmoja wa wasaidizi wake (may be January au Salva) ili akupigie cross. Siyo jam tu, kuna uwezekano mkubwa nyingine zitakuwa "not reachable"! Hii ni Bongo Darisalam ndugu yangu!
 
habari ndio hiyo tukumbuke tuliko toka.....waasisi walikuwa hawasubiri kuongea na watz kwenye tv walikuwa wanawatembelea wananchi huko waliko na kuwasaidia kutatua matatizo yao.Hapa tunazugana tu.Kikwete kaamua kujificha kwenye tv hataki kwenda mbeya anajua hajatekeleza ahadi alizowaahidi hivyo akitia maguu tu wanapopolea mawe msafara wake...........tumepigwa chenga ya mwili hakuna rais wa kwenye tv hapa duniani hizi ni dalili za kuwaogopa wananchi.
Njoo huku kwetu vijijini tukueleze matatizo yetu......

Tutakumbuka enzi za mwalimu.......no kuandaliwa hotuba,hotuba zilitolewa kulingana na hali halisi ya maeneo na matatizo ya wananchi,huto tudakika 90 baada ya miaka4 ya kujinafasi ikulu ndio anataka kutuzuga kwa staili hii
Sidanganyiki...............
 
Hivi hamjagundua? Baada ya kuona wamechemsha kwa maamuzi ya NEC Dodoma ya kumbana Spika na kugundua wananchi hawawaungi mkono, wanajaribu kufanya ka utafiti waone je, wananchi maamuzi ya NEC yamewakera kiasi gani? Wanataka kugundua response ya watanzania. HATUDANGANYIKI!!
 
"Kwa maswali ya papo kwa papo kwa rais, naona tunadanganyana, kwa sababu hakuna mtu mwenye uwezo huo wa kukariri kila kitu asubiri tu kuulizwa papo kwa papo kisha ajibu. Tusishangae kusikia majibu mengi yakifanana na "nitafuatilia", "nimekusikia", "sina taarifa", "nasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi" nk. Au aanze kutoa majibu tata kama yale ya Mh Pinda ya kusema "Zanzibar si nchi", au kushabikia uchukuaji wa sheria mkononi (wauaji wa albino).

Kwa nini asijipe nafasi ya kufanyia utafiti maswali hayo, aje na majibu kamilifu kabisa, pengine asubiri tu maswali ya nyongeza ya kutaka ufafanuzi. Hayo ya nyongeza au ya ufafanuzi ndio yawe 'live', na wasaidizi wake wawepo kutoa details, yeye afanye tu kumalizia conclusions na uamuzi, yaani kuyatilia nguvu ya utekelezaji"


BRAVO MUKULU!!!!!
 
Mimi naomba pia Kikwete ajiunge hapa JF ili tumpatie mawazo yetu, wala hatutauliza maswali ila tutampa facts ambazo akizifanyia kazi ataweza hata kuongoza nchi vizuri.
 
Amejiandaa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wananchi? Hofu yangu ni kwamba mengine yanaweza kuwa embarrassing kwa mkuu wa nchi. Hii imekaaje? Au kuna watakaoandaliwa kuuliza maswali?

hilp pia nina wasi wasi nalo, maana jinsi wananchi walivyokuwa na hasira na serikali, sasa sijui itakuwajer. haya wacha tuone hiyo usiku
 
Duh, hizi chuki zinakwedna vipi jamani sii ndio Ya obama kutyaka kuzngumza na wanafunzi Republican wakapinga vibaya vibaya lakini wao alipohutubia Reagan na Bush mzee haikuwa shida.. Tumewaona Mwinyi, Mkapa wakizungumza tena pumba tupu lakini haikuwa na upinzani kama huu..
..
watu wanacholalamika sana ni maswali kwenda yahoo.com
swalikwarais@yahoo.com
je wewe unaona hii ni sawa
kila mtu anataka kumuona raisi akijibu maswali kwa wananchi kwa ajili huo sio utamaduni wa viongozi TZ
 
Kumbe ikulu kuna email hiyo hapo. Kwa isitumike hiyo?????????????????

inawezekana walikuwa hawakumbuki na hapo kutengeneza hiyo ya yahoo ambayo ni bure waweza kuta wameandika na imprest na watasubmit risiti, na kutakuwepo na masalia ya kugawana wao kwa wao
 
Ngongo .. i believe unaelewa unachomaanisha .. so kifupi ni kwamba tukiwa kama sovereign state kwanini tutumie free tools (which are being administered by foreigners) ku-discuss mambo yetu ya ndani?? tena ikulu?? wakati tunao watu tunaowalipa kwa kodi zetu kushughulikia mambo haya?? wtf ..!!

Kuna email address kwenye hiyo press release press@ikulu.go.tz, kwa nini hawakutumia hiyo? Au Rweyemamu ana agenda ya siri ku-cook maswali anayotaka yeye kwa raisi !!!
 
Walitakiwa wafikirie kwanza kabla ya kuanzisha mpango huu,kwasababu wananchi wengi wana hasira na nchi yao,kwahiyo na hakika maswali mengi yatakuwa ya kumdiscredt mheshimiwa kutokana na utendaji wa serikali yake,na hii inaweza msababishia stress na hasira ambazo amezitengeneza mwenyewe,ukizingatia kuwa huyu mheshimiwa hana system ya kujibu vyema since day one!!

msiwena hofu hakuna mtu atakayeweza kumuuliza swali nje ya yaliyopangwa, simu zetu zintkuwa tu zinasema number unayopiga haipatikani kwa sasa....
na ukizingatia wamepewa chance ya kujiingizia mapato leo sina shaka voda na tigo na TTCL hawataacha kurudisha fadhili .
 
Ataongea nini ambacho ni kipya hapa? Kwanza ajiulize yeye mwenye zile ahadi zake alizoahidi amezitimiza? Hali ya nchi ni mbaya and very dissapointing. Juzi kwenye hotuba yake alisema kwamba kuna Uranium imegundulika na kwamba Tanzania itakuwa among 7 countries wanaoproduce Uranium. Ana mpango gani wa kusimamia hii ili isiwe kama madini yetu yanayochimbwa kila kukicha na kuiacha Tanzania bado masikini???? Mheshimiwa Rais anatakiwa kujua kuwa Nchi yake imeshindikana. Tunahitaji muujiza wa Mungu kuweza kuikwamua Tanzania kwenye umasikini.
 
Nina uhakika atapata michango iliyotulia kuliko hizo simu atakazokuwa anapigiwa na walewale mabingwa wa kupiga simu kina Manase Muhaha, yule Ustadh wa Tegeta, Chesco mzee wa matunda nk
ahaa ahaa du! umenikumbusha redio one saa za jioni.
 
Mkuu heshima mbele, lakini hapo juu tafadhali tutake radhi! Nani ka kwambia JK hajaulizwa maswali. Ameshaulizwa sana tena sana tuu. He knows all our questions. So hizo dakika 90 aje na majibu. Ni upuuzi kusema eti raisi hajui the basic questions za watanzania sasa hivi. Utakuwa ni mzaha kabisa. Hata kama wewe makandara hujui maswali ya watanzania ambayo hayajajibiwa long agoo basi it is better tuuwe media zote tz.


Kwani ni issue ngapi amekuwa na wakati mgumu kuzi adress na watu wanajua but nothing is going on bana? Tutafute kila mbinu ya kuwakilisha? what do you mean sir?


Hata angekuwa anasikiliza maswali/maoni ya wananchi kila siku, kama hamna DHAMIRA YA UTEKELEZAJI na UWAJIBIKAJI ni bureee. Issue sio kuwa na database ya maoni au maswali, that is not the issue. Issue ni utekelezaji wa mambo. Hata kama angekuwa anapokea ushauri mmoja kwa mwezi na anaufanyia kazi effectively, ni bora zaidi kuliko huu mzaha wa kupokea malalamiko/maswali randomly kutoka kwa wananchi. This thing is not practical bwana. Inamaana watu wa kule mahenge watauliza kuhusu issue ya Zombe, wa kigoma barabara na reli, wafanyakazi PAYE kubwa... huoni huu ni mvurugano. Angetoa topic au area of focus walau the questions zingekuwa specific and focused lakini hili sioni kama kuna dhamira yeyote.
.................i'm sorry to say mi nadhani ile michezo ya kuigiza inaendelea. Nothing will come out of this. Maswali yameshapangwa....na majibu tayari yapo.......its really a waste of time to think eti kuna genuine nia ya kusikiliza maoni ya wananchi......BS
 
.................i'm sorry to say mi nadhani ile michezo ya kuigiza inaendelea. Nothing will come out of this. Maswali yameshapangwa....na majibu tayari yapo.......its really a waste of time to think eti kuna genuine nia ya kusikiliza maoni ya wananchi......BS

Nitakuwa busy na big brother huyu muungwana hana kipya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom