Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
Hivi Watanzania kweli bado wanataka hotuba, maswali na majibu huku mawaziri na makatibu wakuu wako bize kama hawaibi moja kwa moja, wanashirikiana na mafisadi kuhakikisha umasikini unakolea zaidi Tanzania na kuzitumia nafasi walizonazo kujineemesha wao wenyewe, watoto wao, mbwa na paka zao ????

Mimi ninaamini hata rais awe na maneno matamu namna gani kinachohitajika sasa sio maneno bali vitendo. Tunataka vitendo ili tuone hali ya watu wetu inakuwa bora zaidi lakini sio wengi tunadidimia na wachache wanaishi kama wako peponi katika nchi hii hii !!!!


Na ni watu gani wa kumuuliza maswali ya maana jama huyo zaidi ya watu kutaka kusikika sauti zao na wale watakaopandikizwa ili asiulizwe maswali ya kumuabisha yeye, chama chake na mafisadi wake ?

Hakuna kinachozaliwa na wizi, rushwa, ubaya na tamaa kinaweza kuwa na mwisho mzuri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom