Kikwete kairudisha Tanganyika!! next...?

Nimegundua kitu......baada ya hutuba ya JK jana watu wamekuwa an hasira saa.....mimi nikiwa mmoja wapo.....nafikiria kuachana kabisa na Tanzania.....
Utaenda wapi? Tutabanana humo humo na kupambana na mafisadi hadi ushindi.
 
Ni vema tu kukasirika na kukunja ndita kwenye mapaji ya nyuso zetu huku tukisonya kwa uchungu.

Wameshika mpini nasi twashikilia makali.

Katika mapambano kulemewa si dalili ya kushindwa ila ni jambo moja baya litokealo lakini lenye nia ya kutuelekeza udhaifu wetu.

Mahali penye udhaifu ndipo penye siri ya Ushindi.

Kazi yetu kubwa ni kutumia udhaifu wetu na kuufanya ngazi ya kutupeleka kwenye ushindi.
 
Jibu lako ni sahihi kwamba Tanzania ni sehemu zile zile za Tanganyika na Zanzibar kwa ujumla. Na hii ndiyo maana halisi ya Muungano.
Haziwezi ungana Tanganyika na Zanzibar na eneo la Tanzania likawa juu ya usawa wa ardhi ya South Africa na Namibia.

Nakubaliana na wewe kwa hilo lakini naomba utafakari muungano wetu. Tunaambiwa kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliunda Muungano na vyombo vya Muungano ikiwa pamoja na Rais na Bunge.

Sasa kichekesho kinakuja pale Rais wa Muungano akilihutubia Bunge la Muungano kwa masaa matatu na dakika kumi, anapozungumza mambo ya upande mmoja tu. Tafadhali fatilia hotuba utaona kuwa pale palipozungumzwa Zanzibar ilizungumzwa kwa nafsi ya tatu kama vile Rais wetu hahusiki na Zanzibar. Kwa masaa matatu hayo concentration ilikuwa kwa sehemu moja ya Muungano Tanganyika.

Sasa mtu analazimika kujiuliza jee huyu Rais ni wa Muungano au ni Rais WA Tanganyika na Jee Bunge analolihutubia ni la Muungano au la Tanganyika? Si hoja kuwepo Kina Khalifa aliyojoki nao Rais kuthibitisha kuwa Zanzibar inawakilishwa ,Issue ni yale yanayozungumzwa yanahusu upande mwengine wa Muungano?
Hapa kwa uelewa wangu mdogo ndio ulionifanya nihisi kuwa hakuna kitu Muungano Physical utakaoonyesha mipaka bali kuna DHANA tu ya Muungano kwani Rais ni Wa Tanganyika na Bunge ni la Tanganyika kwani Rais anahitaji ruhusa ya kuingilia mambo ya Zanzibar na Bunge halina nafasi na masuala ya Zanzibar. Jee hii si Dhana kuliko ukweli.?
 
Ukipanda mimea shambani ni lazima uitunze ili itoe mazao bora.
Nyumba ikijengwa, kazi haiishii hapo ukarabati wa hapa na pale ni lazima japo kupaka rangi tu.
Muungano wetu ni muungano wa kweli lakini umekosa ukarabati au matunzo ya kweli.
Hapa wote tumetumbukia kwenye shimo lile lile tunajadiri kwa munkari juu ya matokeo na kuacha kabisa kugusa chanzo cha matokeo.
Tuna muungano wenye matatizo chungu mzima.

Wengine hawapendi kujadiri matatizo ndani ya muungano kwa sababu mjadara wa aina hiyo utawafanya wengi walio wasemaji sasa kugeuka bubu.
 
Kati ya vitu ambavyo inawezekana vimewaponyoka wengi ni kuwa Rais Kikwete alipozungumzia suala la Zanzibar alijikuta ameirudisha "Nchi ya Tanganyika" kwa makusudi (haiwezekani kuwa bahati mbaya). Aliirudisha hivyo kwa kufuata reasoning yake ambayo kwa kweli naamini ina makosa na alishindwa kutaja tatizo la Katiba tu.

Kikwete alifafanua kuwa tarehe 26 Aprili nchi mbili huru ziliamua kuachilia sehemu ya mamlaka yake na kuunda nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akasema kwa kufanya hivyo "nchi ya Zanzibar" na "nchi ya Tanganyika" zikakoma kuwepo na nchi moja ya Tanzania ikazaliwa (hadi hapo hana makosa).

Akaendelea kuelezea kuwa hivyo katika mahusiano yetu ya nje na nchi nyingine sisi ni Tanzania. Hiyo ndiyo inatupa utambulisho wetu. Akasema katika "utambulisho wetu wa nje nchi ni Tanzania". Akaendelea kusema "lakini kati yetu sisi wenyewe, nchi ni Zanzibar na ya Muungano" (hapo nikahamaki.

Kama kwa sisi wenyewe "nchi ya Zanzibar" bado ipo ndani ya huu Muungano, sasa nchi ya Tanganyika iko wapi? Ndipo nikagundua kwa urahisi tu kuwa kwa mara ya kwanza Rais wa Muungano ameelezea Tanzania Bara kama ni Tanganyika. Kuwa ni nchi iliyo sambamba na Zanzibar.

Next question? Serikali ya Tanganyika iko wapi?

.... hii inanikumbusha fumbo la kikatoliki -UTATU MTAKATIFU ...baba, mwana na roho mtakatifu. Baba na roho mtakatifu ni huyo huyo!

No jokes!
 
Kati ya vitu ambavyo inawezekana vimewaponyoka wengi ni kuwa Rais Kikwete alipozungumzia suala la Zanzibar alijikuta ameirudisha "Nchi ya Tanganyika" kwa makusudi (haiwezekani kuwa bahati mbaya). Aliirudisha hivyo kwa kufuata reasoning yake ambayo kwa kweli naamini ina makosa na alishindwa kutaja tatizo la Katiba tu.

Kikwete alifafanua kuwa tarehe 26 Aprili nchi mbili huru ziliamua kuachilia sehemu ya mamlaka yake na kuunda nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akasema kwa kufanya hivyo "nchi ya Zanzibar" na "nchi ya Tanganyika" zikakoma kuwepo na nchi moja ya Tanzania ikazaliwa (hadi hapo hana makosa).

Akaendelea kuelezea kuwa hivyo katika mahusiano yetu ya nje na nchi nyingine sisi ni Tanzania. Hiyo ndiyo inatupa utambulisho wetu. Akasema katika "utambulisho wetu wa nje nchi ni Tanzania". Akaendelea kusema "lakini kati yetu sisi wenyewe, nchi ni Zanzibar na ya Muungano" (hapo nikahamaki.

Kama kwa sisi wenyewe "nchi ya Zanzibar" bado ipo ndani ya huu Muungano, sasa nchi ya Tanganyika iko wapi? Ndipo nikagundua kwa urahisi tu kuwa kwa mara ya kwanza Rais wa Muungano ameelezea Tanzania Bara kama ni Tanganyika. Kuwa ni nchi iliyo sambamba na Zanzibar.

Next question? Serikali ya Tanganyika iko wapi?

What a contradiction! Mheshimiwa huyu amekuwa Waziri wa mambo ya Nje kwa Miaka 10, sasa ni Rais.Miaka 3 baada ya kauli hizi changanyishi, bado ANAIKANA Tume alounda mwenyewe inayotaka Kuileta "NJE" Tanganyika, ambayo YEYE mwenyewe anakiri IPO! Hapa hatumwelewi. Ubaya ni kuwa kila anapolikoroga, ANAKIMBIA! Hawezi fafanua ama kulinda hoja yake!
 
Back
Top Bottom