Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,264
- 154,352
Kwa hiyo umempima Lowassa kwa kigezo kimoja tu cha kuwa na hubris. .
Wapi nimekwambia hivyo?
Hubris ni hulka ya mtu binafsi, hulka inayotaka kutuingiza vitani kutetea maslahi ya nchi hiyo sio hubris, huyo mtu ni foreign policy hawk..
Unapimaje kwamba Lowassa hatatuingiza vitani kwa kukosa kiasi na hubris na atatuingiza kwa maslahi ya nchi?
Lowassa alishindwa kuongea na wakuu wa wilaya tu kama kiongozi anayethamini "collective responsibility" na mutual respect ethics of leadership, ataweza "foreign policy"?
Tanzania tuna "foreign policy" zaidi ya boilerplate outdated directionless Nyerereism?
Wapo tunaotaka foreign policy hawk sawa sawa na alivyofanya Lowassa kutaka kufutilia mbali mkataba na Wamisri kwamba sisi tusitumie maji ya lake Victoria eti kwa sababu yanaenda Misri. ..
Lowassa kwanza hiyo kazi hata hajafanya yeye, yeye kachukua credit tu. Kazi kubwa kafanya Anthony Diallo. Talk about when opportunism meets ignorance.
Tishio la vita na Malawi sio katika issues za kitaifa zinazojadiliwa katika uchaguzi wa rais ajaye. .
Even more reason to support my assertion that we are going downhill. The populace itself is not imaginative, how do you expect sharp candidates?
Afya na umri wa wagombea wanaoongelewa, mitazamo yao kuhusu Katiba mpya na Muungano, matatizo ya nishati ya umeme, thamani ya shilingi, soko la mazao ya wakulima, mustakabali wa uwekezaji wa nje haswa unaoondoa raia kwenye maeneo yao, rushwa ofisi za juu, ajira za vijana (wazee hawaongelewi), ujangili na ujambazi, mustakabali wa matarajio ya neema ya gesi na mafuta (kama kuna neema kweli), migogoro ya ardhi na umaskini wa Watanzania kwa ujumla, ndio baadhi ya masuala yanayoongelewa au yanayotakiwa kuwa msingi wa kuchambua wagombea kujua nani atakuwa bora ya Kikwete. Lowassa na wenzake wote tuwapime kwa hayo..
If one cannot chew gum and walk, of course adding one item to your laundry list will cause a doomsday scenario.
Sio hubris ya Lowassa kwa sababu eti atatuingiza vitani, hofu ya uwezekano wa vita na Malawi haupo kwenye gumzo la kitafa.
Kwa nini mimi niende tu na yale yaliyopo kwenye gumzo la kitaifa? Yale yaliyopo kwenye gumzo la kitaifa leo hayajawa na mwanzo pale ambapo hayakuwapo katika gumzo la kitaifa? Kwa nini una limit nini kinafaa kuzungumzwa na nini hakifai kwa msingi wa "gumzo la taifa"?
Hili "gumzo la taifa" ni la taifa gani hili ambalo mwananchi wake hawezi kuongezea kitu?
Kwa nini tishio la vita Malawi lisiwe mfano tu unaoonyesha suala zima la Lowassa kukosa kiasi na kuongoza nchi kwa munkari, jazba na inda iliyojaa kiburi cha ujuaji asionao?