Wapo watakao tofautiana na mimi kimtizamo lkn wenye positive mind watakubaliana kuwa JK hakupaswa hata kuwa katibu taarifa,hana kipaji cha uongozi,mtaakubaliana na mimi kuwa serikali ya kikwete imekua ikikumbwa na dhoruba nyingi kuliko awamu nyungine zozote,mfano richmond,operation tokomeza,iptl na Escrow,mpaka sasa hakuna action zaid ya wahusika kujiuzulu,Jk rais wangu utakumbukwa kwa lipi kwenye uongozi wako? Awamu yako imeuza kila kitu gas,madini,uranium,bandari nk ni nini hatma ya kizazi kijacho? Vijana wengi waliohitimu vyuo watakwenda wapi kama uwekezaji unaofanyika hautoi fursa za ajira? Ni awamu hii tumeshuhudia utekaji,utesaji na hata kuuwawa kwa watz wenzetu walioamua kupaza sauti zao kwa kuonyesha udhaifu,ubadhirifu wa serikali yako,tumeshuhudia jinsi familia yako kupitia mkwe wako ndg albert marwa,ridhwani kikwete na wengine wanavyotumia taasisi ya rais kufanya ubadhirifu ilihali ofisi yako ikiwa kimya,uliwahi kusema nanukuu"urais wangu hauna ubia ba mtu" lkn mh rais ni nini tafsiri ya kauli hii kwa kipindi hiki nchi ikiwa njia panda? Bado huna mbia kwenye urais wako? Ni ukweli ulio wazi sasa kuwa urais una ubia na watu mfano familia yako,albert marwa,rostam aziz and coy,home shopping center,patel na wengine wengi,sina hakika kama ulikuwa na tafsir kamili ya neno ubia lkn bado naamini umeganda kwenye tope
ambalo kamwe huwezi kutoka kwa sababu urais wako una ubia na wabadhirifu na wezi wa mali za umma,sitaki kuamini kuwa singasinga ambaye kenya yuko black listed mmeleta kuja kufanya ubadhirifu kachukua pesa kaondoka,nchi yetu watu wake ni masikini sana pamoja na utajir mungu aliotujalia,mh rais nimalizie kwa kusema nimechangia ujenzi wa maabara ilihali tusikia huko dsm wanabeba pesa kwa viroba,je ipo wapi haki hapa?
Mungu ibariki Tanzania