Kikwete has only 10 months to go

Kikwete has only 10 months to go

Ni jambo la kushukuru Jk amebakiza miezi kama 10 tu aondoke madarakani.Tumeona na kujifunza mengi kuhusu faida na hasara katika kuchagua kiongozi mkuu wa nchi.

I even wish CCM to go along with him.

Ahsante mungu kwa fadhila zako.

Ni muda mrefu sana kwa kweli. Zinaweza kuibuka ishu nyingi tu kama za escrow.
 
Umetumwa au umejituma kupima upepo? Hunipati. Njoo kivingine. Waiter hebu nipe tea masala chap!!!
 
Hivi kumzushia uwongo kiasi hiki mheshimiwa Raisi wetu mpendwa, hujui kuwa ni dhambi kubwa?, au unafikiri Mungu hakuoni kwakuwa sisi wanadam wenzako hatukuoni hapo kwenye keyboaed yako? nakuhurumia unavyoteseka kwa chuki moyoni mwako, Pole sana!

Rafiki pole sijamsingizia.Nilimsikia mwenyewe akiyaongea kuwa hana ubia na mtu, urais wake ni wakwake na familia yake.

Nenda uliza ndugu usitake tuzidi kuwaumbua.Je Si yeye aliyesema haitaji kura za wafanyakazi?

Pole lakini huo ndiyo ukweli na ukweli unauma.
 
Ni jambo la kushukuru Jk amebakiza miezi kama 10 tu aondoke madarakani.Tumeona na kujifunza mengi kuhusu faida na hasara katika kuchagua kiongozi mkuu wa nchi.

I even wish CCM to go along with him.

Ahsante mungu kwa fadhila zako.

...not 10 months to go but 10years..this is the scientifically proven overall survival from prostate cancer....or did you mean differently?...
 
Unaweza kushukuru JK anaondoka akaja rais mpya ambaye ni JK wa JK.
Tuna Rais mbovu, kwa mawazo ya baadhi yetu. Tunafurahi anakaribia kuondoka.

Hatujui anakuja nani, tusikitike?
 
Nitafurahi sana huyu jamaa akiondoka, maana amekuwa kama mtu asiyejielewa katika kuendesha nchi.
 
Tuna Rais mbovu, kwa mawazo ya baadhi yetu. Tunafurahi anakaribia kuondoka.

Hatujui anakuja nani, tusikitike?

Sana tu.

Hasa kwa sababu the real "choice" is beteeen the Lowassas, Membes and Pindas of Tanzania.

With a long shot for a CHADEMA dark horse.
 
Sana tu.

Hasa kwa sababu the real "choice" is beteeen the Lowassas... of Tanzania.
Lowassas of Tanzania ndio kina nani?

Unajuaje Lowassa hatakuwa rais bora kuliko Kikwete?
 
WE WISH ANGEPATA MIAKA MINGINE KUMI
TUNAMHITAJI sana, amefanya kazi sana kuimarisha miundombinu kama mabarabara, madaraja, mahosipitali, mashule, mavyuo n.k. hakuna rais yeyote kabla yake aliyewahi kufanya aliyoyafanya Kikwete. Pili kuhusu kuuza rasilimali zetu, mkapa ni kinara (kama wewe ni wa ile dini ya escrow huwezi ona hili) kauza, NBC, Tanesco, na mashirika karibia yote ya umma tuyajuayo (kama hujui sema nikutajie), migodi mingi imeuzwa na mkapa na ndo muanzilishi wa sisi kupata 3% tu kwenye mapato hayo. lakini pia uongozi wake uligubikwa na kashifa nyingi ila hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari kama tuvionavyo kipindi hiki. kulikuwa na scandal kama za EPA, mwananchi gold, radar, ndege ya rais, meremeta, kujiuzia mgodi wa kiwira, kujianzishia benki iitwayo anaben, rushwa za kajengo BOT, alex and stewart na upuuzi mwingi ambao sina muda wa kuulist hapa.

Inawezekana wewe ni mmoja wa waliolipwa 300,000 kwa siku ndio maana unamsujudia licha ya uongozi wake wa mashaka.
 
Lowassas of Tanzania ndio kina nani?

Unajuaje Lowassa hatakuwa rais bora kuliko Kikwete?

Lowassas of Tanzania ndio ilk ya uongozi wa CCM.

Lowassa hatakuwa rais bora kuliko Kikwete kwa sababu ana hubris. Usishangae Lowassa akiwa rais Tanzania ikaingia kwenye vita ya kijinga na Malawi na kutugubika katika lindi lingine la umaskini lisilo na sababu ya msingi.

Changanya kukumbatia rushwa kupita Kikwete na hubris unapata Lowassa.

And don't even go with Pinda. Utapata rais "msomi" wa sheria anayemaka "wapigwe tu".

It's downhill from here.
 
Natamani ingekuwa wiki Moja! Ufisadi umekithili, umasikini umejenga kibanda, hali ni mbaya kuliko hapo kwanza alipochukua nchi.
 
Lowassa hatakuwa rais bora kuliko Kikwete kwa sababu ana hubris. Usishangae Lowassa akiwa rais Tanzania ikaingia kwenye vita ya kijinga na Malawi na kutugubika katika lindi lingine la umaskini lisilo na sababu ya msingi.
Kwa hiyo umempima Lowassa kwa kigezo kimoja tu cha kuwa na hubris.

Hubris ni hulka ya mtu binafsi, hulka inayotetea kwa nguvu maslahi ya nchi dhidi ya nchi nyingine hiyo sio hubris, huyo mtu ni foreign policy hawk.

Wapo tunaotaka foreign policy hawk sawa sawa na alivyofanya Lowassa kutaka kufutilia mbali mkataba na Wamisri kwamba sisi tusitumie maji ya lake Victoria eti kwa sababu yanaenda Misri.

Tishio la vita na Malawi halimo katika issues za kitaifa zinazojadiliwa katika uchaguzi wa rais ajaye.

Afya na umri wa wagombea wanaoongelewa, mitazamo yao kuhusu Katiba mpya na Muungano, matatizo ya nishati ya umeme, thamani ya shilingi, soko la mazao ya wakulima, mustakabali wa uwekezaji wa nje haswa unaoondoa raia kwenye maeneo yao, rushwa ofisi za juu, ajira za vijana (wazee hawaongelewi), ujangili na ujambazi, mustakabali wa matarajio ya neema ya gesi na mafuta (kama kuna neema kweli), migogoro ya ardhi na umaskini wa Watanzania kwa ujumla, ndio baadhi ya masuala yanayoongelewa au yanayotakiwa kuwa msingi wa kuchambua wagombea kujua nani atakuwa bora ya Kikwete. Lowassa na wenzake wote tuwapime kwa watakavyokabiliana na hayo.

Sio hubris ya Lowassa kwa sababu eti atatuingiza vitani, hofu ya uwezekano wa vita na Malawi haupo kwenye gumzo la kitafa.
 
Kwakuwa imebaki miezi michache kabla ya JK kumalizia madaraka yake basi hatuna budi kusubiri walengwa wa ESCROW kuondoka naye.
Kuvunja baraza la mawaziri kwa sasa ni gharama kwa wananchi.

wahusika wamalize muda wao halafu ndio wahukumiwe ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha zetu.

wahisani tusameheni kwa muda huu msitubanie sana kwani tunaoumia ni sisi wananchi.
 
tukibadili mawaziri kwa sasa ni sawa na kujikomoa maana ni gharama
 
Ni jambo la kushukuru Jk amebakiza miezi kama 10 tu aondoke madarakani.Tumeona na kujifunza mengi kuhusu faida na hasara katika kuchagua kiongozi mkuu wa nchi.

I even wish CCM to go along with him.

Ahsante mungu kwa fadhila zako.

Ninamashaka kama atatoka. Kama akitoka madarakani, Bilal atafufuka, PAP ataimba, akina muongo mhongo watacheza nk. Hata kama ni mimi siwezi ruhusu mafuriko yanibebe ningali naona. Hakuna mpango huo
 
Back
Top Bottom