Kikwete has only 10 months to go

Kikwete has only 10 months to go

Mwenye nafasi za kazi hata utaniboy jamani tumsaidie huyu dogo.ametuchosha humu
 
Mh.rais, ikiwa umebaki mwaka mmoja kukabidhi kiti cha urais (kwa mujibu wa katiba).....binafsi nashauri utumie sakata la escrow (bila woga au upendeleo) kama nafasi yako ya mwisho ili kudhihirishia watanzania na ulimwengu kuwa fighting corruption is on top of your priority-list. Ukifanya hivyo, hakika utanusuru chama na historia ya nchi hii (na africa kwa ujumla) itaandika jinalako kwenye upande safi wa kurasa za historia ya Tanzania.
 
Kigugumizi cha maamuzi ya kuwaadhibu watuhumiwa wa sakata la Escrow ni kwa sababu naye anahusika.

Sidhani,kwa nafasi alonayo awalinde hao waliokula hizo pesa za Escrow na kupokea lawama zote ndani na nje ya Tanzania kama hajahusika pia.

Nachoshukuru ni kuwa hasira naanung'uniko ya wananchi yameonekana kwenye zoezi dogo la uchaguzi wa viongozi wa serikali z mtaa.

Mungu,tunakuomba uzidi kulilomboa taifa lako hili.

Amen
 
Ni jambo la kushukuru Jk amebakiza miezi kama 10 tu aondoke madarakani.Tumeona na kujifunza mengi kuhusu faida na hasara katika kuchagua kiongozi mkuu wa nchi.

I even wish CCM to go along with him.

Ahsante mungu kwa fadhila zako.
prof kikwete amepona tezi dume
 
Kitu kikubwa JK ambacho katufanyia watanzania ni kututolea uchafu wote uliokuwa chini ya carpet la Taifa kwa muda mrefu. Kwa kuruhusu free media serikari yetu imekuwa very exposed, ingawa yeye mwenyewe anakiri ana majibu yote lakini kaiweka wazi ngoma yenu ndio hiyo:

Uwezo wa viongozi wenu ndio huo kwenye kujibu changamoto za jamii si habari sijui za nani msomi, fanya wakuone watazania.

Uwezo wa vyama vya siasa kujibu hoja za wananchi kauwacha wazi viongozi wenu ndio hao tangia escrow inaanza watu kimya wanasubiri uchaguzi ndio wakurupuke kuna kamati ya ufundi kweli huko CCM au wazee wanaopokea posho tu

Sijui vijana wataweza, vijana wenyewe ndio hao sifa tupu

Serikari sijui aipati budget ya kutosha kutekeleza, watendaji wenyewe wa serikari ndio hao kazi kufuja hela za miradi

In short JK katufungua watanzania na tuione Tanzania jinsi ilivyo na sivyo kama ilivyokuwa zamani tunadhani tuna watu wa maana kumbe hatare. Raisi ajaye ndiye anapaswa kuja na walau majibu maana changamoto ziko wazi.
 
Back
Top Bottom