Kikwete has only 10 months to go

Kikwete has only 10 months to go

Watanzania wazalendo wanaopenda maendeleo, wanatamani JK aongezewe miaka mingine mitano ili aendelee kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Sijui wewe mleta mada uko nchi gani!

Makubwa yaliyofanywa na uongozi WA Kikwete, hayalingani na wingi WA rasilimali za nchi alizokabidhiwa. No input and output relationship that justifies what you purppot he has achieved.
 
Nawaasa watanzania tusirudie makosa ya kuchagua rais bubu na dhaifu kama Kikwete he never act unless being pushed.
 
Link Meles Zenawi, Ethiopian Prime Minister, Dies At 57

Link BBC News - Ghana's President John Atta Mills dies

Link Africa?s food security and the G8 summit

In addition to the G8 heads of state, four African leaders were also present for talks on the project. President John Atta Mills of Ghana, Prime Minister Meles Zenawi of Ethiopia, President Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania and President Yai Boni of Benin, who is also the current chairperson of the African Union, met with Obama to discuss this partnership.

Link BBC News - Hugo Chavez returns to Venezuela after surgery in Cuba

Link Venezuela's Chavez Preps for Surgery (Video)

Link Venezuela President Hugo Chávez To Continue Cancer Treatment Upon Return Home From Cuba
Hatujui siku, saa, dakika wala nukta ambayo mauti yatatufikia. Siyo vizuri kuwaza kuhusu kifo juu ya Rais wako, au yeyote yule kwa tofauti ya itikadi tu, ukizingatia hakuna uthibitisho wa tishio la kiafya!
 
Aliyewaza kifo ni mimi au wewe? Umejishitukizia?
 
Unataka kumaanisha kwamba viongozi wa africa walio attend hiyo summit wamekufa/watakufa?? Why??

Walioatted na wasioatted wote watakufa. Hata mimi na wewe tutakufa. Kila mtu kwa siku yake!
 
Wapi nimekwambia hivyo?
Nimekuwa nikisema Kiranga huwa humaanishi unachokisema! Hukusema kwamba Lowassa atakuwa Rais mbovu zaidi ya JK kwa sababu ana hubris itakayotuingiza vitani na Malawi? Unaruka hata yaliyoandikwa?

Unapimaje kwamba Lowassa hatatuingiza vitani kwa kukosa kiasi na hubris na atatuingiza kwa maslahi ya nchi?
Kwanza kabisa umemtathmini Lowassa based on a hypothetical, kitu ambacho bado hajijatokea wala kuelekea kutokea. Lowassa anaguswa vipi na vita vya Tanzania na Malawi ambavyo hakuna mtu duniani aliyeongelea hilo kuhusiana na mbio za urais? Lowassa katamka nini kuhusu vita na Malawi?

Kinachovutanisha nchi za Tanzania na Malawi ni maslahi ya nchi hizo, sio ya mtu binafsi, kuna maslahi gani binafsi hapa?
Lowassa alishindwa kuongea na wakuu wa wilaya tu kama kiongozi anayethamini "collective responsibility" na mutual respect ethics of leadership, ataweza "foreign policy"?
Alishindwa kuongea na wakuu wa wilayua kivipi?

Tanzania tuna "foreign policy" zaidi ya boilerplate outdated directionless Nyerereism?
Ndio tunayo. Msimamo wetu, kwa mfano, dhidi ya Malawi ndio foreign policy yetu kwenye suala hilo, foreign policy ni issue specific. Kwenye mahusiano na Misri Tanzania ime capitulate to regional pressure pamoja na peremembe za Egypt kama vile kutuletea huduma za Egypt Air. Lowassa haya aliyakataa lakini hakuwa na mamlaka ya kutosha kusimika hiyo foreign policy kulazimisha tutumie maji ya Ziwa Victoria kwa maslahi ya nchi.

Lowassa kwanza hiyo kazi hata hajafanya yeye, yeye kachukua credit tu. Kazi kubwa kafanya Anthony Diallo. Talk about when opportunism meets ignorance.
Obama hakumuua Osama wala hakujua yuko chimbo gani pasi kuambiwa, bali alitoa maamuzi. Lowassa ndio aliamua foreign policy mpya dhidi ya Misri japo alikuwa overruled.

Even more reason to support my assertion that we are going downhill. The populace itself is not imaginative, how do you expect sharp candidates?
Not the point.

Point is, you can't judge Edward Lowassa as potentially poorer president than Kikwete based on one factor of "hubris."

Kwa nini mimi niende tu na yale yaliyopo kwenye gumzo la kitaifa?
Kwa sababu, kwa vile ni hoja fringe and far-out, hai convince mtu, msamiati mpya kwenye medani za siasa wanasema haina mashiko. Hakuna anaehofia kwamba Lowassa atakuwa Rais mbaya kwa sababu atatuingiza kwenye vita na Malawi, hakuna anaeongelea hilo!

Kwa nini tishio la vita Malawi lisiwe mfano tu unaoonyesha suala zima la Lowassa kukosa kiasi na kuongoza nchi kwa munkari, jazba na inda iliyojaa kiburi cha ujuaji asionao?
Kwa sababu Lowassa hajawahi kutishia kwamba ataenda vitani na Malawi! Tishio gani la vita? Tutathmini wagombea kwa mapana zaidi ya "hubris" ya kutuingiza vitani na Malawi.

Unaongea mambo ambayo, I'm a really sorry to say, they are just not in the conversation.
 
Hivi kuna changamoto gani ambayo JK aliikuta, lakini atakapoondoka atakuwa ameishaitatua.

Matatizo ktk sekta za elimu, na afya, inaonekana yako palepale, huku wengine wakielekeza kwamba hali imekuwa mbaya zaidi.

Tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa kubwa zaidi. Sasa linaitwa bomu.

Ufisadi umekuwa mkubwa zaidi. Hali ya usalama hairidhishi. Migogoro baina ya wananchi, wafugaji vs wakulima imeongezeka.

Kuna mabadiliko ktk VITU, lakini mabadiliko hayo hayajaboresha HALI za wananchi walio wengi.
 
In short,JK is a failed president.
 
wanasema hata simba anazaa , kingine ni kwamba nimefurahishwa sana na jina lako ! Kitabu changu cha kumbukumbu kinalionyesha jina hilo kuwa ni kati ya waasisi wa usaliti kwenye vyama vya siasa .
Wewe furahishwaga kivyako, mimi ndio Jidu, jitu lenye ng'ombe wengi kanda ilee!!!!
 
Namsikitikia sana JK,anaondoka na aibu ya karne ya kuwa na mawaziri mijizi ambayo hapana shaka ameshindwa kuwawajibisha na kutia shaka pengine yeye ana uovu zaidi ya huo!
 
Aliyewaza kifo ni mimi au wewe? Umejishitukizia?

Kama siyo kuwaza kifo, kuna uhusiano gani wa muda uliobaki wa Kikwete kama rais na vifo vya Meles Zenawi, Atta Mills, na Hugo Chavez? (ref. links ulizotoa hapo kabla).
 
Nimekuwa nikisema Kiranga huwa humaanishi unachokisema! Hukusema kwamba Lowassa atakuwa Rais mbovu zaidi ya JK kwa sababu ana hubris itakayotuingiza vitani na Malawi? Unaruka hata yaliyoandikwa?

More like wewe ndiye hujui kusoma. Wapi nimeandika kwamba hubris ndiyo objection yangu pekee kwa Lowassa?

Kwanza kabisa umemtathmini Lowassa based on a hypothetical, kitu ambacho bado hajijatokea wala kuelekea kutokea. Lowassa anaguswa vipi na vita vya Tanzania na Malawi ambavyo hakuna mtu duniani aliyeongelea hilo kuhusiana na mbio za urais? Lowassa katamka nini kuhusu vita na Malawi?

Again. Hujui kusoma. Nimemtathmini Lowassa kutokana na kauli zake za jazba alizotoa awali kuhusu mambo mengi. Kuanzia vita na Malawi mpaka kuropokea wakuu wa wilaya kama wanae.

Kinachovutanisha nchi za Tanzania na Malawi ni maslahi ya nchi hizo, sio ya mtu binafsi, kuna maslahi gani binafsi hapa?

Zaidi ya maslahi binafsi, suala ni hubris. A president has got to be levelheaded, not someone who just flies on populism like a bat from hell.

Alishindwa kuongea na wakuu wa wilayua kivipi?

Lowassa katika Uwaziri Mkuu wake alikuwa haangalii ethics za collective responsibility wala mutual respect in leadership. Alikuwa anawazodoa wakuu wa wilaya kama watoto wake publicly, mpaka mjeshi mmoja akampandishia Mwanza huko. This is not statesmanlike conduct. Kashamzodoa sana John Mongella, mkuu wa wilaya, katika mkutano wa wazi, kama vile anaongea na mwanawe Freddy. We don't need egotistic dictators.

Ndio tunayo. Msimamo wetu, kwa mfano, dhidi ya Malawi ndio foreign policy yetu kwenye suala hilo, foreign policy ni issue specific. Kwenye mahusiano na Misri Tanzania ime capitulate to regional pressure pamoja na peremembe za Egypt kama vile kutuletea huduma za Egypt Air. Lowassa haya aliyakataa lakini hakuwa na mamlaka ya kutosha kusimika hiyo foreign policy kulazimisha tutumie maji ya Ziwa Victoria kwa maslahi ya nchi.

Foreign policy ya mkono wa kulia haujui mkono wa kushoto unafanya nini? Membe anakwambia anajua nyendo za kila mfanyakazi wa serikali za Tanzania na hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania aliyehusika katika kuuza silaha DRC, balozi Mahiga anasema serikali haihusiki na inachunguza kama wafanyakazi wake wamehusika kama watu binafsi?

Obama hakumuua Osama wala hakujua yuko chimbo gani pasi kuambiwa, bali alitoa maamuzi. Lowassa ndio aliamua foreign policy mpya dhidi ya Misri japo alikuwa overruled.

Kama alikuwa overruled hajaamua, alishauri. Don't overrate him.

Not the point.

Point is, you can't judge Edward Lowassa as potentially poorer president than Kikwete based on one factor of "hubris."

Yes you can. A president is supposed to be levelheaded. Lowassa is not levelheaded enough to be president. His track record shows some rash decisions, including his resignation.

If he couldn't handle being PM, why should we believe that he can handle being president?

Kwa sababu, kwa vile ni hoja fringe and far-out, hai convince mtu, msamiati mpya kwenye medani za siasa wanasema haina mashiko. Hakuna anaehofia kwamba Lowassa atakuwa Rais mbaya kwa sababu atatuingiza kwenye vita na Malawi, hakuna anaeongelea hilo!

Fringe and far out does not mean irrelevant. Pre 9/11 people did not think using commercial airliners to crash the twin towers was feasible, but it happenned. Dispute an idea on the merit, not whether it is fringe and far out.

Furthermore, that was an example to demonstrate an inner character that Lowassa has.Hubris.

Kwa sababu Lowassa hajawahi kutishia kwamba ataenda vitani na Malawi! Tishio gani la vita? Tutathmini wagombea kwa mapana zaidi ya "hubris" ya kutuingiza vitani na Malawi.

Una hakika hajawahi au ni wewe tu stuck on stupid hujafuatilia habari?

Lowassa katoa kauli hapa zimejadiliwa kwamba zimemzidi kimo na ni kauli ambazo zinatakiwa kutolewa na amiri jeshi mkuu tu, wewe ulikuwa umelala chini ya jiwe gani wakati tunajadili hilo hapa?

Unaongea mambo ambayo, I'm a really sorry to say, they are just not in the conversation.

If you have an 8 second attention span.
 
Mh Rais pole na majukumu na pia bado najua una jiuguza kama ambavyo madaktari wako wameshauri,nimeangalia kalenda hapa naona mda umetupa mkono,muda wako wa kupanga ikulu umekwisha pamoja na yote lkn bado watz wana hamu ya kujua mwisho wa sakata la Escrow ambapo baadhi ya wateule wako na hata familia yako ikihusishwa na utakatishaji wa fedha haramu,ni lini mh rais utakata kiu ya watz juu ya wizi huu wa escrow? Kutengua uteuzi na kuteua wengine siyo mworabaini wa haya yanayojitokeza kila kukicha,hata wananchi wanalalamika kuwa kwa muda sasa ofisi yako kazi kubwa inayofanya ni kuteua na kuapisha,moja ya udhaifu wa serikali yako ni kutokuchukua hatua kwa wakati ambapo imepelekea wananch kuwa na tention wakati wote,tunaomba kwa hili la escrow mh rais usiishie kuteua na kuapisha tu nenda hatua mbele zaidi ili kurudisha matumaini kwa watz,ni ukweli pesa zimeliwa je ni nini kifanyike kurudisha hela za walipa kodi ?
Mungu ibariki Tanzania
 
Ni jambo la kushukuru Jk amebakiza miezi kama 10 tu aondoke madarakani.Tumeona na kujifunza mengi kuhusu faida na hasara katika kuchagua kiongozi mkuu wa nchi.

I even wish CCM to go along with him.

Ahsante mungu kwa fadhila zako.

Alafu kama ni laana naomba tusimsahau na yule Askofu aliyeropokaga kuwa JK ni chaguo la Mungu!!
nazidi kumlaani yule kiumbe usiku na mchana kwa uropokaji usio na mantiki ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa kuiumiza hii nchi na watu wake mpaka hii leo...
 
Mkuu wewe unatisha unajua nnachowaza!!!

Hivi hukumsikia wewe Mkulu akisema amepona saratani?

Link Rais Kikwete asema amepona Saratani - BBC Swahili

Hakika Madaktari wanamfariji, Angejuwa kuwa CANCER haina kupona ila anaichelewesha tu, hakika angetuaga WaTanzania mwishomwisho angalau tumkumbuke, Yeye busy na kukusanya Mali anafikiri atazikwa nazo.

AKa muulize Chavez withj all technology na hela lakini alikwenda, TITO kocha wa barcelona with all Money na treat ment lakini hakumaliza hata mwaka.
 
Hili kosa la kuchagua tukilifanya Tena mwaka 2015 Nina uhakika hili Taifa litaingia vitani maana wanyonge watasema s's imetosha.......... Tafadhali CCM, CDM,CUF na NCCR tuwekeeni wagombea wenye sifa za kiutendaji na maadili hata kama Wana sura mbaya......Taifa na waliomo ndani yake wamechoka,hakuna hata haja ya kuwauliza,ukiwatazama tu usoni unajua kuwa wamechoka.
MUNGU IBARIKI TANZANIA TUNAPOELEKEA 2015.
 
Wapo watakao tofautiana na mimi kimtizamo lkn wenye positive mind watakubaliana kuwa JK hakupaswa hata kuwa katibu taarifa,hana kipaji cha uongozi,mtaakubaliana na mimi kuwa serikali ya kikwete imekua ikikumbwa na dhoruba nyingi kuliko awamu nyungine zozote,mfano richmond,operation tokomeza,iptl na Escrow,mpaka sasa hakuna action zaid ya wahusika kujiuzulu,Jk rais wangu utakumbukwa kwa lipi kwenye uongozi wako? Awamu yako imeuza kila kitu gas,madini,uranium,bandari nk ni nini hatma ya kizazi kijacho? Vijana wengi waliohitimu vyuo watakwenda wapi kama uwekezaji unaofanyika hautoi fursa za ajira? Ni awamu hii tumeshuhudia utekaji,utesaji na hata kuuwawa kwa watz wenzetu walioamua kupaza sauti zao kwa kuonyesha udhaifu,ubadhirifu wa serikali yako,tumeshuhudia jinsi familia yako kupitia mkwe wako ndg albert marwa,ridhwani kikwete na wengine wanavyotumia taasisi ya rais kufanya ubadhirifu ilihali ofisi yako ikiwa kimya,uliwahi kusema nanukuu"urais wangu hauna ubia ba mtu" lkn mh rais ni nini tafsiri ya kauli hii kwa kipindi hiki nchi ikiwa njia panda? Bado huna mbia kwenye urais wako? Ni ukweli ulio wazi sasa kuwa urais una ubia na watu mfano familia yako,albert marwa,rostam aziz and coy,home shopping center,patel na wengine wengi,sina hakika kama ulikuwa na tafsir kamili ya neno ubia lkn bado naamini umeganda kwenye tope
ambalo kamwe huwezi kutoka kwa sababu urais wako una ubia na wabadhirifu na wezi wa mali za umma,sitaki kuamini kuwa singasinga ambaye kenya yuko black listed mmeleta kuja kufanya ubadhirifu kachukua pesa kaondoka,nchi yetu watu wake ni masikini sana pamoja na utajir mungu aliotujalia,mh rais nimalizie kwa kusema nimechangia ujenzi wa maabara ilihali tusikia huko dsm wanabeba pesa kwa viroba,je ipo wapi haki hapa?
Mungu ibariki Tanzania

Umeandika kwa uchungu na hisia kali lakini yote ni kweli miezi iliyobaki bado ni mingi, ee Mwenyezi Mungu tujalie tusipate tena rais kama huyu
 
Jk aondoke kauza nchi na kila kitu,mikataba hii aliyoingia ni ya kinyonyaji
 
Taifa hili linakazi hata majuha nao wanahoji utendaji wa jk,kwa tarifa tu ni kwamba jk kila siku anasema mda wake ukiisha ataondoka kwa mujibu wa katiba ila kumbuka kuwa hatakuja kupatikana kirahisi mtu mpenda maendeleo kama jk japo wajinga wachache kama wewe akina mengi na mafisadi wengine ndiyo wanamkwamisha lakini hachoki kuleta maendeleo kwa watanzania.

avatar162282_3.gif

safi sana mjepo
Kikatiba kabisa bado mwaka (miezi 12) maana Uchaguzi ni Novemba matokea na kuapishana itakuwa Disemba
Wabunge walie tu kwani wao ni bado miezi 6 tu, warudi majimboni kwao ambako kumechafuka
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom