Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Mwafrika wa Kike,
Vipi mbona Italy hakuwakimbia Watanzania? Au aliona ni mapadre wengi akajua hao hawana nguvu ya kumtwanga maswali mazito mazito?
Muungwana naona kapatikana, kiti kimekuwa moto. Kuna haja ya kuendelea kuwazomea mafisadi, huenda baadhi yao wakaona kuzomewa ni kubaya zaidi ya mali wanazozipata kwa kuiba.
Ila tu tukumbuke Historia, kwasisi tuliosoma kuhusu wajamaa wa njozi (Utopian Socialism), na yale mawazo ya kwamba tuwazomee mabepari kisha watabadilika, walio wengi pamoja na kuzomewa wakaendeleza unyonyaji wao tu. Huenda ni ngumu sana kwa fisadi kubadilika, mpaka siku anapelekwa lupango.
Ah wapi,
Vasco da gama aache safari aje kushughulikia mambo ya ndani ya nchi? miezi sita iliyopita nilidhani kuwa angeweza kufanya hivyo. Baada ya hii trip yake ya mwisho ya US na yote niliyosikia na kuona yakifanyika, Kikwete hana ubavu kabisaaaa wa kuvunja baraza la mawaziri.
Hii ni kutokana na sababu mbili:
1. Kikwete na CCM wamesema kuwa issue ya ufisadi, richmonduli, kiwira, rada, BOT, ndege za rais, Buzwagi, nk ni uzushi tu toka kwa wapinzani ambao nia yao ni kuchukua madaraka tu.
Kama Kikwete akiact na kufanyia kazi hizi tuhuma basi atakuwa amesalenda kwa upinzani na kuthibitisha madai yao.
2. Serikali ya Kikwete inaongozwa kwa ushirikiano wa watu watatu ambao nao pia wana makundi yao. Kikwete ni rais ila yeye anaendeleza kazi yake ya uwaziri wa mambo ya nje, Lowasa ndiye anadeal na mambo ya ndani, wakati Rostam Aziz anashughulikia biashara zao na vyombo vya habari. Wote hawa wana watu wao katika baraza la mawaziri na wanasaidiana katika kufanya ufisadi na wizi wao.
Kuvunja baraza la mawaziri itamaanisha kuvunja nguvu na style ya kikwete ya kuongoza kitu ambacho hana bollz za kufanya!
Kikwete,
I dare you kuvunja baraza la mawaziri ili unipe sababu ya kusherekea ushindi mwingine dhidi yako baada ya ule wa wewe kunikimbia hapa USA kukwepa maswali yangu na watanzania!
Huyu Mkwere anatafunwa na njia zilizotumika kumuingiza Ikulu. Aliingia Ikulu kwa NJIA za KIFISADI iweje avunje baraza la mawaziri kwa sababu ya UFISADI.
Yeyote anayetetea UFISADi hujue yeye ni fISADI zaidi. Tunaweza kuwa tunamwangalia Karamagi kama FISADI lakini kila anachokifanya kina baraka za JK.
Lakini cha kumuuliza kikwete Je na BUtiku, John, Hassan, Mohamedi na wengineo nao ni wapinzani wake? Wanataka madaraka au ni visingizio tu?
Vile vile nafikiri JK mnaweza kumkaba koo mpaka ukamumaliza lakini hawa jamaa walivyomsaidia wakati wa kampeni ni ndoto kufanya chochote. Mawazo yangu ni kuwa hata hajawahi kuongea nao kuhusu hizo tuhuma.
Mi nimeipenda hiyo ya 'kuendeleza kazi yake ya wizara ya mambo ya nje'......inaonekana inamfaa zaidi
He jamani,
tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.
Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.
Asante
Jamani hizi subira tunaambiwa kila siku na wakati nchi inaangamia ndio zinanitisha hapa. Inaonekana Kikwete ana kiburi na dharau kama za Mkapa. Kinachoshangaza, Kikwete anazifanya awamu ya kwanza ya utawala wake. Kazi kweli kweli!
Mkuu,
ulivyotaja John,Hassan umenikumbusha Mwl,alikua aliyependa kuwaita kwa first name.
Hapo Jakaya hana la kusema,maana bila ya RA,Karamagi,EL jamaa asingefika hapo.Ila ni sisi watanzania ndio tuna silaha ya mwisho ya kuondoa huu mraba,maana nchi ni yetu sote.
He jamani,
tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.
Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.
Asante
jamani na nimesikia kiinua mgongo cha mwisho cha wabunge kinakuwa million 60,je ni kweli?