Kikwete hana ubavu wa kuvunja baraza la mawaziri

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
59
Ah wapi,

Vasco da gama aache safari aje kushughulikia mambo ya ndani ya nchi? miezi sita iliyopita nilidhani kuwa angeweza kufanya hivyo. Baada ya hii trip yake ya mwisho ya US na yote niliyosikia na kuona yakifanyika, Kikwete hana ubavu kabisaaaa wa kuvunja baraza la mawaziri.

Hii ni kutokana na sababu mbili:

1. Kikwete na CCM wamesema kuwa issue ya ufisadi, richmonduli, kiwira, rada, BOT, ndege za rais, Buzwagi, nk ni uzushi tu toka kwa wapinzani ambao nia yao ni kuchukua madaraka tu.

Kama Kikwete akiact na kufanyia kazi hizi tuhuma basi atakuwa amesalenda kwa upinzani na kuthibitisha madai yao.

2. Serikali ya Kikwete inaongozwa kwa ushirikiano wa watu watatu ambao nao pia wana makundi yao. Kikwete ni rais ila yeye anaendeleza kazi yake ya uwaziri wa mambo ya nje, Lowasa ndiye anadeal na mambo ya ndani, wakati Rostam Aziz anashughulikia biashara zao na vyombo vya habari. Wote hawa wana watu wao katika baraza la mawaziri na wanasaidiana katika kufanya ufisadi na wizi wao.

Kuvunja baraza la mawaziri itamaanisha kuvunja nguvu na style ya kikwete ya kuongoza kitu ambacho hana bollz za kufanya!

Kikwete,

I dare you kuvunja baraza la mawaziri ili unipe sababu ya kusherekea ushindi mwingine dhidi yako baada ya ule wa wewe kunikimbia hapa USA kukwepa maswali yangu na watanzania!
 
Mwafrika wa Kike,

Vipi mbona Italy hakuwakimbia Watanzania? Au aliona ni mapadre wengi akajua hao hawana nguvu ya kumtwanga maswali mazito mazito?

Muungwana naona kapatikana, kiti kimekuwa moto. Kuna haja ya kuendelea kuwazomea mafisadi, huenda baadhi yao wakaona kuzomewa ni kubaya zaidi ya mali wanazozipata kwa kuiba.

Ila tu tukumbuke Historia, kwasisi tuliosoma kuhusu wajamaa wa njozi (Utopian Socialism), na yale mawazo ya kwamba tuwazomee mabepari kisha watabadilika, walio wengi pamoja na kuzomewa wakaendeleza unyonyaji wao tu. Huenda ni ngumu sana kwa fisadi kubadilika, mpaka siku anapelekwa lupango.
 
....huyu mkwere is a big dissapointment,i doubt hata kama anajua anachofanya,seems he s a nice guy na hana deal chafu lakini kwa style yake ya uongozi hatutaenda popote yaani ni ushikaji shikaji tuu na maslahi ya chama mbele kuliko nchi....very soft & unambitious guy he needs to go!
 
Mwafrika wa Kike,

Vipi mbona Italy hakuwakimbia Watanzania? Au aliona ni mapadre wengi akajua hao hawana nguvu ya kumtwanga maswali mazito mazito?

Muungwana naona kapatikana, kiti kimekuwa moto. Kuna haja ya kuendelea kuwazomea mafisadi, huenda baadhi yao wakaona kuzomewa ni kubaya zaidi ya mali wanazozipata kwa kuiba.

Ila tu tukumbuke Historia, kwasisi tuliosoma kuhusu wajamaa wa njozi (Utopian Socialism), na yale mawazo ya kwamba tuwazomee mabepari kisha watabadilika, walio wengi pamoja na kuzomewa wakaendeleza unyonyaji wao tu. Huenda ni ngumu sana kwa fisadi kubadilika, mpaka siku anapelekwa lupango.

kwa kweli Mtanzania sijui nini kilitokea Italy. Ninajua tu kuwa Kikwete alinikimbia mimi na watanzania wenzangu hapa US hata baada ya kuwa tumetuma maswali yetu in advance. Huu ni ushindi wa kwanza.

Akivunja baraza la mawaziri atanipa wa pili na nitamlipa 84 cents for that. Sijui sana kama kuzomea tu kutasaidia ila pia nafarijika kuona kuwa watanzania wanafanya kitu ambacho kwa miaka mingi sana hawakuwa wakifanya.

Huu ni mwanzo mzuri.

Asante kwa challenge yako.
 
Huyu Mkwere anatafunwa na njia zilizotumika kumuingiza Ikulu. Aliingia Ikulu kwa NJIA za KIFISADI iweje avunje baraza la mawaziri kwa sababu ya UFISADI.

Yeyote anayetetea UFISADi hujue yeye ni fISADI zaidi. Tunaweza kuwa tunamwangalia Karamagi kama FISADI lakini kila anachokifanya kina baraka za JK.

Lakini cha kumuuliza kikwete Je na BUtiku, John, Hassan, Mohamedi na wengineo nao ni wapinzani wake? Wanataka madaraka au ni visingizio tu?

Vile vile nafikiri JK mnaweza kumkaba koo mpaka ukamumaliza lakini hawa jamaa walivyomsaidia wakati wa kampeni ni ndoto kufanya chochote. Mawazo yangu ni kuwa hata hajawahi kuongea nao kuhusu hizo tuhuma.
 
Ah wapi,

Vasco da gama aache safari aje kushughulikia mambo ya ndani ya nchi? miezi sita iliyopita nilidhani kuwa angeweza kufanya hivyo. Baada ya hii trip yake ya mwisho ya US na yote niliyosikia na kuona yakifanyika, Kikwete hana ubavu kabisaaaa wa kuvunja baraza la mawaziri.

Hii ni kutokana na sababu mbili:

1. Kikwete na CCM wamesema kuwa issue ya ufisadi, richmonduli, kiwira, rada, BOT, ndege za rais, Buzwagi, nk ni uzushi tu toka kwa wapinzani ambao nia yao ni kuchukua madaraka tu.

Kama Kikwete akiact na kufanyia kazi hizi tuhuma basi atakuwa amesalenda kwa upinzani na kuthibitisha madai yao.

2. Serikali ya Kikwete inaongozwa kwa ushirikiano wa watu watatu ambao nao pia wana makundi yao. Kikwete ni rais ila yeye anaendeleza kazi yake ya uwaziri wa mambo ya nje, Lowasa ndiye anadeal na mambo ya ndani, wakati Rostam Aziz anashughulikia biashara zao na vyombo vya habari. Wote hawa wana watu wao katika baraza la mawaziri na wanasaidiana katika kufanya ufisadi na wizi wao.

Kuvunja baraza la mawaziri itamaanisha kuvunja nguvu na style ya kikwete ya kuongoza kitu ambacho hana bollz za kufanya!

Kikwete,

I dare you kuvunja baraza la mawaziri ili unipe sababu ya kusherekea ushindi mwingine dhidi yako baada ya ule wa wewe kunikimbia hapa USA kukwepa maswali yangu na watanzania!

He jamani,

tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.

Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.

Asante
 
Pale kiongozi anapopata madaraka kwa njia za Ufisadi basi Ufisadi na mafisadi wanakuwa wamepata baraka zote za kiongozi huyo. Mwacheni JK na kundi lake la Mafisadi kwani kuwafukuzuza kazi ni hatari zaidi kwake kuliko kuwaacha waendeleze Ufisadi. Kilichobaki ni sisi kuwapiga chini kwa kura zetu
 
Huyu Mkwere anatafunwa na njia zilizotumika kumuingiza Ikulu. Aliingia Ikulu kwa NJIA za KIFISADI iweje avunje baraza la mawaziri kwa sababu ya UFISADI.

Yeyote anayetetea UFISADi hujue yeye ni fISADI zaidi. Tunaweza kuwa tunamwangalia Karamagi kama FISADI lakini kila anachokifanya kina baraka za JK.

Lakini cha kumuuliza kikwete Je na BUtiku, John, Hassan, Mohamedi na wengineo nao ni wapinzani wake? Wanataka madaraka au ni visingizio tu?

Vile vile nafikiri JK mnaweza kumkaba koo mpaka ukamumaliza lakini hawa jamaa walivyomsaidia wakati wa kampeni ni ndoto kufanya chochote. Mawazo yangu ni kuwa hata hajawahi kuongea nao kuhusu hizo tuhuma.

Mkuu,
ulivyotaja John,Hassan umenikumbusha Mwl,alikua aliyependa kuwaita kwa first name.
Hapo Jakaya hana la kusema,maana bila ya RA,Karamagi,EL jamaa asingefika hapo.Ila ni sisi watanzania ndio tuna silaha ya mwisho ya kuondoa huu mraba,maana nchi ni yetu sote.
 
He jamani,

tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.

Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.

Asante

Jamani hizi subira tunaambiwa kila siku na wakati nchi inaangamia ndio zinanitisha hapa. Inaonekana Kikwete ana kiburi na dharau kama za Mkapa. Kinachoshangaza, Kikwete anazifanya awamu ya kwanza ya utawala wake. Kazi kweli kweli!
 
Hakuna democratic country inafanya anayojaribu kufanya huyu bwana mkwere.Kwenye nchi inayofuata democracy ya kweli hakuna kitu chenye nguvu kama sauti ya watu..achana na pccb anayojitetea kwamba ameiachia ishughulikie huo ufisadi maana anajua hawatamwangusha.
Labda tujikumbushe yaliyotokea kwa nchi ya kidemokrasia kama japan.Mpaka sasa hivi kwa habari tulizo nazo ni kwamba wana serikali mpya kabisa baada ya chama tawala kubadilisha mawaziri mara mbili katika miezi miwili iliyopita,akiwamo waziri mkuu kuachia ngazi na kumpisha mwenzake afanye mageuzi wananchi wanayotarajia.
Pia kuna waziri aliyekatisha maisha yake baada ya media kutaka kumhoji kutokana na kutoa upendeleo wa tenda kwa kampuni fulani pamoja na ofisi kuwa na matumizi ya kama tzs 20 million ambazo hazikuwa na maelezo ya kina kwa mwaka 2005-07.Baada ya waziri kukatiza uhai siku iliyofuata wakurugenzi wawili wa yale makampuni yaliyopendelewa wakajimaliza vile vile.Hivyo media hawakufanikiwa kumhoji hata mmoja wao kwani wote walikuwa marehemu tayari. Walikatiza uhai siku moja kabla kwani familia,ndugu na jamaa wakijua umefanya ufisadi wowote wanakutenga kabisa.
Nashangaa mpaka sasa hivi bado akina karamagi et al wanaruhusiwa kuingia ofisi za umma pamoja na madudu waliyosaini ambayo tumeyashuhudia kwa kuyasoma live wala siyo uzishi kama wanvyodai kuanzia rais wa nchi.This is ridiculous.I cant believe thats whats happening in ma country!!!
 
Jamani hizi subira tunaambiwa kila siku na wakati nchi inaangamia ndio zinanitisha hapa. Inaonekana Kikwete ana kiburi na dharau kama za Mkapa. Kinachoshangaza, Kikwete anazifanya awamu ya kwanza ya utawala wake. Kazi kweli kweli!

Ndo ivo nadhani kama kuna 'magonjwa' tunayougua watanzania basi hili la subira lazima liwepo!

Subira kusubiri nini? Kila kitu kipo wazi...ripoti ya CAG kwa mfano, ilikosewa? kwa nini JK aliita makatibu wakuu, hadi wakurugenzi kuwaaambia 'waaache'? mbona yeye hakusubiri?

Sasa sisi tusubiri nini, kuhoji na kutaka uwajibikaji wa kwa nini mkataba ulisainiwa nje ya nchi ukiwa na mapungufu kibao? sahihi si tumeziona? kuna anayekanusha kama ile sio sahihi yake? tusubiri nini?

Nauliza tusubiri nini, iwapo imejulikana kama BOT kuna 'madudu', anayepaswa kusubiri ni nani, sisi wananchi tuliowapa wajibu wa kutulindia njuluku zetu kiduchu pale BoT wakati wao wakiendelea kutanua tu?

Tusubiri kwa sababu gani, kama tumesubiri kwa miaka zaidi ya arubaini, kama Musa na waisraeli jangwani, lakini walau wale waliahidiwa nchi ya maziwa na asali, na wakaifikia, sisi tumeahidiwa lakini ndo hivo hata Musa mwenywe haoinekani, tukichonga ndama wa dhahabu tutalaumiwa?

Tusubiri wakati wale tuliowaaajiri wala hawana subira hiyo hiyo linapokuja suala la maslahi yao binafsi?

dawa ya hili 'gonjwa' ni nini? maana sidhani kama wahenga waliposema 'subira huvuta heri' walikuwa na maana hii ya subira tunayotakiwa tuwe nayo,.....
 
Mkuu,
ulivyotaja John,Hassan umenikumbusha Mwl,alikua aliyependa kuwaita kwa first name.
Hapo Jakaya hana la kusema,maana bila ya RA,Karamagi,EL jamaa asingefika hapo.Ila ni sisi watanzania ndio tuna silaha ya mwisho ya kuondoa huu mraba,maana nchi ni yetu sote.

Nilikuwa na maana kuwa angefufuka Mwl basi JK angekimbilia mbali. Sina uhakika kama kweli anasikiliza hotuba za Mwalimu maana zinamstuta kweli.

Halafu anatwambia watu wampelekee majina ya wala rushwa na PCCB rukusa kuchunguza. Huku anasema wanaotuhumu mawaziri wake wanataka madaraka sasa wanachunguza nini wakati tayari ameisha toa hukumu.

Huyu ndiye aliyepata 80% nafikiri tuliliwa.
 
He jamani,

tuweni na subira kidogo. Ninauhakika Kikwete anajua kinachoendelea na atafanya kazi pale uchunguzi utakapokamilika.

Sio kila jambo linalosemwa lina ukweli. Nchi lazima sheria ifuatwe ili amani iwepo. Kikwete atapanga timu mpya pale tu muda utakapotimia.

Asante

Masaka

wakati Mzee sita amekuja na hoja ya kuwaongezea marupurupu wabunge na kusema wanapata kidogo ukilinganisha na nchi jirani, wananchi walipiga kelele sana JK alimaliza kelele kwa kusema tu ni watu wazima nafikiri wamesikia yakaisha.

Hata kama walijiongezea ilikuwa kimya kimya.

Kwa hili anajikanyaga sana namshauri washauri wake wawe wanamkumbusha anasema nini. mara Amesema suala la BoT linashugulikiwa na wahusika watashugulikiwa.

mara PCCB inashugulikia tuhuma zote.

Mara wanaoandama serikali yake wanataka madaraka hawamnyimi usingizi, nk

Haya yote yanasemwa na mtu yule yule mmoja tuchukue lipi tuache lipi?

Subira ya nini wakati yeye conclussion yake inamaanisha ameridhika kuwa kila kitu ni sawa na kusema mbona na RICE wa USA(hii ni kuwapumbaza watanzania) amesema kuwa anafanya vizuri?
 
jamani na nimesikia kiinua mgongo cha mwisho cha wabunge kinakuwa million 60,je ni kweli?

Kwa kazi ipi ya maana? Labda nalo lifanyiwe mabadiliko ndio wapewe hizo pesa. Kama ni Stempu si tupeleke hata watoto wa shule? Wakasikilize halafu wakubaliane na kila kitu?
 
Hawezi kabisa,hawezi katu kwa sababu hana huo ubavu wa kuwafukuza watu waliomuweka madarakani.Hao mafisadi wanaimaliza nchi yetu walihusika kwa njia moja ama nyingine kumuweka mkwere huyo hapo alipo.Anawalipa fadhila.Ila hizo fadhila naona sasa zinaruka mipaka,kumwacha mtu Kama Karamagi kwenye baraza la mawaziri mpaka muda huu,ameonesha udhaifu wa hali ya juu na inaonekana hakuna kitakachofanyika Tanzania kama huyu jamaa na timu yake ya mafisadi wataendelea kuwa madarakani.Natamani kungekuwa na njia nyingine mbadala ya kuwang'oa watu wote wanahujumu nchi yetu,wanaotaka kuipeleka Tanzania kuzimu,kuzimu bila chochote!!!!
Eeh Mungu isaidie Tanzania,vinginevyo itaangamia.
 
Tumesubili mpaka sasa tumechoka,Waswahili wanasema subira huvuta heri,ila hii subira ya kusubili kuwawajibisha wezi wa rasilimali za nchi yetu itakuwa "subira inayovuta Hara" badala ya heri.Ni ajabu sana,wenzetu wanapotuhumiwa na tuhuma nzito kama za kina Karamagi na mafisadi wengine hujiwajibisha,ila Mafisadi hawa wanavyopenda kushibisha mitumbo yao,hawawezi,wameng'ang'ania,na Mkwere wetu haweze kuwaondoa kwa sababu hana ubavu huo,Rais wetu anatakiwa atumie madaraka aliyopewa na katiba ya nchi kuinusuru nchi,vinginevyo kama uswahiba utaendelea hapo Ikulu,tanzania itaumia,itajeruhiwa zaidi na zaidi.
 
We we weeeeh! Shhhhhh! KIKWETE KUBADILISHA BARAZA LA MAWAZIRI?
Hilo haliwezekani kabisa sanasana Karamagi atapelekwa wizara ya Viwanda na Biashara,Mramba kwenye Uchumi na ubinafsishaji ktk kumaliziamalizia.
The Handsome boy is helling somewhere Europe....
He's about to land very soon to plan for the next trip somewhere else Asia.Atafanya kwanza mikutano na Media kuwaeleza jinsi alivyosifiwa kwa utawala wake uliotukuka wa kifisadi na jinsi miela uchwara itakavyomwagwa kwenye akaunti zake na mafisadi wengine kupitia dhamana waliyopewa na watanzania maskini i.e Wahadzabe.
Hilo la kutuletea First lady,second lady sijui what itakua siri yake.This Foreign Minister will adress very soon in a diplomatic tone.To hell with him
 
Back
Top Bottom