Kikwete Hana Mchezo!

Leo nimependa alipogundua matatizo ya managment za nashirika yetu kuwa wanateua makada wasio na uwezo
 
Watanzania wenzangu tafadhali mnyonge mnyongeni lakini haki yake mwachieni. Kwa hili jambo alifanyalo Jakaya la kupita mawizarani na kuangalia ufanisi wa kazi anastahili pongezi kubwa sana. Watendaji ndiyo wamekuwa wakimuangusha JK na sasa kaamua kuwavalia njuga, nina imani kubwa kwamba hali ya utendaji na uwajibikaji itabadilika kwa kiasi kikubwa.

Mkuu si kuna baraza la mawaziri?kwa huko hawaulizani,kwa nini wasifokeane huko,nas tukaonana utendaji imara,AU SABABU SASA NI LIVE LUNINGANI ANAUZA SURA,.Pili watendaji kawateua yy,kama wanamuangusha c awatoe?atawafokea mara ngapi?UTENDAJI MBOVU WA SERIKALI UNAANZIA KWAKE.
 
Jamani hebu tukatae umbumbumbu na tuwe wa wazi, hakuna management style wala case study iliyoonyesha hicho anachofanya kimewahi kuleta mabadiliko yoyote wala ufanisi.Tuacha kuleta siasa kwenye swala la science, swali kuu nini lengo la ziara hizi? pili ningemshauri kama ni matembezi ya kawaida basi asikilize zaidi na asijabu kutoa ama kushauri nini kifanyike kwa sasa kwa lengo la kupata media attention. Natumaini ana washauri wake basi wachukue notes, atafanyia kazi maelezo anayopewa wakati huo yakiwa yamejumuisha na taarifa ya uchunguzi ya anachoambiwa ndipo aseme analosema. Sitaki hii style yake peke yake inayozidi kuonyesha udhaifu wake haipendezi na ashauriwe na wahusika kwamba muda wa campaign umeisha. Hawa mawaziri si watendaji, hawana uwezo, wanajua hawajachaguliwa kwa uwezo bali kwa mahusiano zaidi, wenye uwezo wakina magufuli ndio hao yeye mwenyewe aneyewakata mikono sasa hiyo ni nini? Mi nashauri hiki kipindi cha mwisho aache u rafiki na mambo ya kusema huyu si mwenzetu, badala yake atafute watanzania wenye uwezo wamsaidie walau anapoondoka awe ameache 'legacy' kipindi chake cha kwanza ameshindwa kabisa kuonyesha lolote zaidi ya kuboronga, awamu ya pili mwaka umeshakatika hajaanza hata kutoa vision yake maana hiyo ya ari zaidi.... tayari imekufa kabla ya kuanza maana huwezi kuwa na zaidi pasipo 'mpya' kwanza.
 
Nimeona kwa kifupi, TBC walikuwa wanaonesha kwa ufupi ziara ya JK kwa wizara mbalimbali, aisee huyu Mr angekuwa mkali namna hii siku zote nchi yetu ingekua mbali, waziri wa uchukuzi alikua anampiga longo longo za kitoto jamaa akamkatisha katikati ya speech halafu akatema madini ya kutosha, yaani hadi ananifanya nijiulize mara mbili mbili hivi anafanyaga makusudi tu kuwabeba watu wasio na tija au?

Kitu gani kimemsukuma sasa amewawakia, yaani sijui kama hili baraza litamaliza 5 yrs

Nasikia alikwenda Loliondo kwa babu kunywa dawa........may be sense zimerudi...
 
HAKUNA JiPYA!! NO ACCOUNTABILITY, NO TRANSPARENCY, RO RESPONSIBILTY, NO INTEGRITY. Those are pillars. Katika serikali yake ni zero!! kwa hiyo hizo ni mbwembwe za kuonekana katika TV. Hatufanyii kaZI KATIKA Luninga
 
Huyu changa la macho tu, Hana lolote. anatafuta mbuzi mwingine wa kafara ili aonekane msafi. kama alivyofanya kwa Dani yona na Mramba! ila mi namuona ni kama mtu anayenuka jasho afu anajipulizia pafyum, wakati dawa yake ni kuoga tu!!
Naendelea kushangaa maoni ya great thinkers. Very funny.
 
Ni usanii tupu. Labda zaidi kujikosha.
Ishu za kuwakoromea mawaziri wake zilitakiwa ziwe zimefanyika kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Hapa anawadanganya wasioelewa utendaji wa serikali. Istoshe angeliwafukuza kazi mawaziri wanaochemsha. Anaendelea kuuonesha ulimwengu kuwa ameimudu sanaa.

Vikao vya baraza la mawaziri ni siri , ungejuaje kuwa kawakoromea ? ni afadhali sasa afanyavyo tunajua kinacho endelea
 
sijui ngoja niendelee kumcheck hizi siku mbili tatu, blv me jamaa alikua hackeck na mtu, kawaka sana, waziri wa nishati alikua anatetemeka tu, ile haikuwa sanaa jamaa alim-mind sana yule waziri, dizaini alitaka kumchakachua halafu Kikwete akashtukia issue dah ilikua mara ya mwisho nimemuona Kikwete kachukia vile ni ile siku ya mgaya wa walimu

Sidhani kama kauli yako ni sahihi hebu waone hapa......
NGELEJA.jpg
 
Watanzania wenzangu tafadhali mnyonge mnyongeni lakini haki yake mwachieni. Kwa hili jambo alifanyalo Jakaya la kupita mawizarani na kuangalia ufanisi wa kazi anastahili pongezi kubwa sana. Watendaji ndiyo wamekuwa wakimuangusha JK na sasa kaamua kuwavalia njuga, nina imani kubwa kwamba hali ya utendaji na uwajibikaji itabadilika kwa kiasi kikubwa.

Ni kweli kufuatilia ufanisi wa watendaji ni jambo la msingi na linatakiwa kupongezwa. Ila angeweza kabisa kufuatilia utendaji kwa karibu bila ya kufanya hii sinema ya kuzungukia wizara na kupigwa picha akitoa maelekezo kwa ukali. Kitu ambacho watu hawana imani nacho ni uwezekano wa kutembelea wizara zote kisha kurudi ikulu na kuacha mambo yakiendelea kama alivyoyaacha (business as usual). Tunahitaji mfumo endelevu wa kusimamia utekelezaji wa manifesto ya chama tawala na maamuzi mengine ya msingi ya kitaifa na siyo hii approach ya nyota wa sinema za kimarekani akina Chuck Norris ambao lazima wawepo kila sehemu ili mambo yafanikiwe. Yaani bila wao mambo hayaendi.
 
Jamani hebu tukatae umbumbumbu na tuwe wa wazi, hakuna management style wala case study iliyoonyesha hicho anachofanya kimewahi kuleta mabadiliko yoyote wala ufanisi.Tuacha kuleta siasa kwenye swala la science, swali kuu nini lengo la ziara hizi? pili ningemshauri kama ni matembezi ya kawaida basi asikilize zaidi na asijabu kutoa ama kushauri nini kifanyike kwa sasa kwa lengo la kupata media attention. Natumaini ana washauri wake basi wachukue notes, atafanyia kazi maelezo anayopewa wakati huo yakiwa yamejumuisha na taarifa ya uchunguzi ya anachoambiwa ndipo aseme analosema. Sitaki hii style yake peke yake inayozidi kuonyesha udhaifu wake haipendezi na ashauriwe na wahusika kwamba muda wa campaign umeisha. Hawa mawaziri si watendaji, hawana uwezo, wanajua hawajachaguliwa kwa uwezo bali kwa mahusiano zaidi, wenye uwezo wakina magufuli ndio hao yeye mwenyewe aneyewakata mikono sasa hiyo ni nini? Mi nashauri hiki kipindi cha mwisho aache u rafiki na mambo ya kusema huyu si mwenzetu, badala yake atafute watanzania wenye uwezo wamsaidie walau anapoondoka awe ameache 'legacy' kipindi chake cha kwanza ameshindwa kabisa kuonyesha lolote zaidi ya kuboronga, awamu ya pili mwaka umeshakatika hajaanza hata kutoa vision yake maana hiyo ya ari zaidi.... tayari imekufa kabla ya kuanza maana huwezi kuwa na zaidi pasipo 'mpya' kwanza.

Marekebisho kidogo ndugu. Mwaka haujakatika kwenye awamu ya pili ya Mheshimiwa rais Dr. Kikwete.
 
Kikwete hana tofauti na Theodore "T - Bag" Bagwell wa kwenye Prison Break maana ana character kama za huyo jamaa
 
Watanzania wenzangu tafadhali mnyonge mnyongeni lakini haki yake mwachieni. Kwa hili jambo alifanyalo Jakaya la kupita mawizarani na kuangalia ufanisi wa kazi anastahili pongezi kubwa sana. Watendaji ndiyo wamekuwa wakimuangusha JK na sasa kaamua kuwavalia njuga, nina imani kubwa kwamba hali ya utendaji na uwajibikaji itabadilika kwa kiasi kikubwa.

Naomba unielleweshe, kwani hao watendaji(mawaziri) walijiteua?
 
sijui ngoja niendelee kumcheck hizi siku mbili tatu, blv me jamaa alikua hackeck na mtu, kawaka sana, waziri wa nishati alikua anatetemeka tu, ile haikuwa sanaa jamaa alim-mind sana yule waziri, dizaini alitaka kumchakachua halafu Kikwete akashtukia issue dah ilikua mara ya mwisho nimemuona Kikwete kachukia vile ni ile siku ya mgaya wa walimu

Uswe you're a great thinker mkuu achana na hizi bla bla Pliiiz!!!!!
 
Kwenda kwenye wizara na kukalipia watu hakusaidii kitu zaidi ya kumpunguzia heshima yake. Vitu vingi anavyohoji inaelekea anavifahamu, sasa kwa nini havijafaniwa kazi?? Anapokwenda huko mawizarani anasababisha kazi zisifanyike kwa ajili yake. Mimi sijawahi sikia Rais yeyote dunianai anayetembelea wizara kama JK ......................... Inaelekea anaikimbia ikuru kwa vile hajui afanye nini!!
 
Nimeona kwa kifupi, TBC walikuwa wanaonesha kwa ufupi ziara ya JK kwa wizara mbalimbali, aisee huyu Mr angekuwa mkali namna hii siku zote nchi yetu ingekua mbali, waziri wa uchukuzi alikua anampiga longo longo za kitoto jamaa akamkatisha katikati ya speech halafu akatema madini ya kutosha, yaani hadi ananifanya nijiulize mara mbili mbili hivi anafanyaga makusudi tu kuwabeba watu wasio na tija au?

Kitu gani kimemsukuma sasa amewawakia, yaani sijui kama hili baraza litamaliza 5 yrs

maigizo tu yale.mambo yote anayafahamu tangu zamani.ile ni stage perfomance ambayo anataka tuamini, hana lolote.maneno tu yale hata kwenye khanga yapo.hapa tunataka vitendo sio maigizo
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom