Serikali tatu inawezekana, inatekelezeka

Mbunge

Senior Member
Aug 7, 2008
104
10
SERIKALI TATU INAWEZEKANA, INATEKELEZEKA.....


SEHEMU YA KWANZA:

Tuanze na dua ambayo ninapendekeza kwa kila mjumbe kaika bunge la katiba kuikariri na kuisoma binafsi au katika kikundi asubuhi na jioni. DUA ambayo itawafaa wajumbe wote wa Bunge la Katiba Mpya bila kujali imani ya mtu kuanza nayo kila siku:

"Mwenyezi Mungu awali ya yote mimi na wenzangu tunakutanguliza wewe mbele yetu ili utuongoze kwenye njia iliyo sahihi na siyo ya upotevu na alikojificha ibilisi. Ninakuomba wewe uliye mtoaji wa kilicho safi,kikamilifu, imara na bora uwape watu wangu na nchi yangu katiba utakayoridhika nayo na sisi tutakayoridhika nayo, itakayofaa watu na nchi yangu kwa karne moja au zaidi, lakini sio katiba ambayo mimi binafsi au chama changu au wilaya yangu au mkoa wangu au kikundi changu inayoitaka kwa maslahi yake au sababu zake binafsi. Bali tufanikishe kupatikana katiba iliyodhamiriwa kuwa ni mwamvuli wenye kivuli cha utulivu, umoja na amani tena wa kutumainiwa na Watanzania wote leo na kwa miaka mingi ijayo ili tuijengee nchi yetu heshima duniani na mbinguni ! Niongoze katika kutumia akili kufikiri na kutafakari na nikinge na jitihada za shetani kunilazimisha kufikiri kwa moyo, akili yangu ya kiovu, na nafsi na hisia zangu binafsi."




Serikali Tatu Inawezekana, Inatekelezeka na kinachokosekana ni ridhaa na utashi wa wanasiasa walioko madarakani...

Neno siasa, kimapokeo na kihistoria ni neno lenye tafsiri ya kufanya au kutenda kitu kilicho sahihi na kilichonyooka barabara kidhahnia na kivitendo. Hata hivyo, hapa Tanzania toka kuingia kwa 'glasnosti' na 'perestroika', yaani, mfumo wa vyama vingi na soko huru, neno hilo limekuwa aghalabu linatafsiriwa kama ni ujanja wa iana fulani, hadaa, urongo na uzaini kiungozi na kiutawala. Kwa sababu ambazo viongozi wa CCM waliopo na waliopita wanazijua pengine kutokana na uoga na hofu kubwa kuhusu chama chao kuendelea kubaki madarakani na sio Tanzania endapo wananchi waliofunguka kimawazo na kifikra hivi leo wa nchi hii wataamua kuchagua kuwa na serikali tatu na sio serikali mbili. Tuwakumbushe wenzetu kwamba Mwenyezi Mungu anakaririwa kusema: 'kila nafsi itaonya mauti!' je, kwa kutokubali kuwa chama chao kinaweza pia kufa kutokana na vitendo vyao au kwa wakati wake kufika ni waumini nao au ni kinyume chake. Kama sisi tutakufa, haiwezekani kwa taasisi nazo kutokuwa na siku yao ya kufa.
Toka mwaka 1990 CCM kwa shingo upande na kutokana na shinikizo la kimataifa imekuwa ikikubali kazaachia na potezea, hatua kidunchu kwa kidunchu katika kukubali na kutekeleza masharti na taratibu zinazoendana na mfumo wa vyama vingi na soko huru. Mathalani, hadi wa leo chama hicho kimeshindwa kutekeleza mambo kadhaa ambayo kimsingi ndiyo yanayoweza kuweka msingi imara wa demokrasia na soko huru nchini. Walifanya na wanaendelea kufanya hivyo kwa makosa kwa kuamini kuwa kwa kukwaza demokrasia, mfumo wa vyama vingi na haki za binadamu basi wataweza kurefusha milele maisha ya chama chao na uongozi wa CCM Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Hatua ambazo zimedhamirisa kwa makusudi kudhoofisha demokrasia na mfumo wa vyama ni pamoja na kutoruhusu demokrasia kustawi bara na visiwani, kushindwa kufutilia mbali udikteta au uimla ndani ya chama tawala, kushindwa kupeleka madaraka mikoani; kushindwa kuanzisha Tume Huru ya Uchaguzi; kushindwa uruhusu Mgombea huru: kushindwa kujizuia kutumia vyombo vya dola kukwaza wanasiasa wa vyama vya upinzan; kufeli kuruhusu ushindani wa kisiasa, kijaamii na kichumi ndani ya mikoa na kati ya mkoa na mikoa mingine; kuendelea kuminya uhuru wa vyombo vya habari; kutoruhusu uhuru wa watu kuwa na mikutano huru; kukataa kuwapa Waislamu haki ya kuabudu kwa mujibu wa sheia za dini yao kutokana na shinikizo la wakatoliki nchini (ilhali serikali ina wepesi wa ajabu katika kuhakikisha sheria zake zinafuatwa, imekuwa na uzito wa ajabu katika kuziachia dini ziweze kuendeshwa kwa mujibu wa sheria zao na mambo mengine kadhaa wa kadhaa. Isipokuwa kama tunavyojua, nyani kwa kawaida huwa haoni kundule ila huona ----- la mwenziwe.
Azma ya Watanzania walio wengi hivi sasa ni kwa wao kubaleghe na kupevuka kimawazo na kuachiwa kufikiri kwa kutumia akili zao na sio kwa kutumia mioyo yao au kufanya maamuzi kwa hisia za uoga au hofu au chuki au hawa juu ya jambo fulani. Maamuzi ya Watanzania wa miaka hii ieleweke yataendana na maslahi bianfsi ya mtu au kikundi cha watu na raia wa eneo fulani la nchi na sio vinginevyo. Kwani vinginevyo ni kuwauza unaowawakilisha na wewe ukajikuta huna mizizi wala matawi.
Hivi haiwi kweli unafiki wa hali ya juu kuwataka watu wafikiri na waamue kwa kutumia akili zao wenyewe, wakati huo huo mazingira yanajengwa kuwazunguka baadhi ya watu wasio wepesi kufikiri kwa kutumia akili washawishike kuhusu mambo fulani kwa kutumia kushangilia, kupiga vigelegele, kupiga miluzi na kunengua viuno katika shughuli ambayo inawahitaji watu kufikiri, kuwaza na kuwazua na kutafakari zaidi na sio kuigiwa na hisia za raha ya wehu wa dakika chache unaoishia kwa kuangua kwa pua na makelele na kuchezewa ngoma zisizo na mbele wala nyuma.
Kinachoonekana kutaka kufanzwa na wenzetu walioko madarkani ni kuendelea kuzitumia siasa na sera zilezile za 'naintini kweusi' kwenye miaka hii ya smarthphone na teknolojia nyengine, tarakishi milikishi, kompyuta, laputopu, facebook, twitter, habari bila mipaka na uwepo wa vijana ambao fikra zao ni tofauti kabisa na zile za wale waliozaliwa, kukua na kulelewa kabla ya ukoloni (Before Colonialism (BC)) Generation. Hili haliwezekani, kwani kila zama na watu wake, kila kizazi na mtazamo na msimamo wake. Vinginevyo, itakuwa ni vigumu kwetu kukwepa yale tunayoyaona yakitokea leo huko Russia, Syria, Misri, CAR, Congo, Burundi, NIgeria na nchi kama hizo.
Ni dhahiri kwamba kwa maneno yaliyosemwa kwa kujizuia sana lakini kwa kilichosemwa kuwa dhahiri na dua za uongo na kweli zilizoshuka kwa ghafla toka huko zilikotoka (bila kujali kuna tohara au hakuna) kwamba kuna watu wanaosimamia taasisi fulani za kiimani wenye ushawishi mkubwa kwa wanasisaa wetu walioko madarakani kuliko watu wengine.
Hilil linatia hofu kubwa miongoni mwa wananchi wlaio wengi, kwani zipo habari kwamba kuna kundi fulani la kidini linalounga mkono serikali mbili kwa sababu linaamini kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kwa imani yao kukubalika Tanzania Visiwani !



SEHEMU YA PILI:

KASORO KATIKA MTAZAMO NA MSIMAMO WA CHAMA TAWALA

Wazungu wana msemo kwamba ukitaka KUMUUA mbwa au paka wako basi wewe mpe jina baya. Mwiite mwizi au mchawi au mwehu na jirani zako wote watakusaidia kumuua. Hii ndiyo ajali ambayo inaikuta Tanganyika. Kwa sababu wanasiasa fulani hawaitaki tu Tanganyika basi kwa sababu wanazozijua wameamua kuhakikisha wanafanya kila wanalolifanya ili Tanhganyika isifufuliwe.
Ni wajibuu wa kila Mtanganyika kujiuliza je, katiba inayotarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 kweli itadumu bila kuwepo kwa nchi ya Tanganyika kama nchi huru iliyoungana na Zanzibar na kuzaa Shirikisho la Tanganyika. Au ndio wanasiasa walioko madarakani wameanza kutusaidia kujenga misingi ile ile mibovu ya kisiasa kama iliyojengwa na waasisi wa Yugoslavia na Urussi ambazo zilikuja kusambaratika fumba na kfuumbua ? Hali kadhalika ni vyema kujiuliza katiba hii inaandaliwa kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu au sisi ambao mguu mmoja u kaburini na mwingine duniani ?
Haiwezekani kujenga taifa imara juu ya misingi ya uzaini, uongo, hadaa, ujanjaujanja, kuwatia watu hofu, uoga, vitisho na majinamizi wa kubuni katika matumizi ya nukuu za 'maspindoctors' wa kimataifa ambao hawana hisia wala uhalisia wala uchungu na nchi yetu na watu wetu ila wanaongozwa na malipo au posho na masurufu wanayopewa na serikali iliyoko madarakani kwa njia batili na haramu. Uongo kama ni wa raia anaayepata na kubeba dhambi ni yeye raia mwenyewe, lakini uongo ukiwa ni wa wale wanaoiongoza nchi, basi dhambi inaangukia nchi nzima na hakuna anayenusurika adhabu itakapokuja. Tutahadhari sana katika hili, na kuna kitu kiovu kama kuwahadaa na kuwadangaya watu wa nyumba yako mwenyewe. Tumkurubie Mungu na tuitafute toba yake kwani siku zetu zimehesabiwa na huisha kwa kasi mno tofauti na taifa. Taifa linaweza kuishi miaka 200,300, 500 na zaidi lakini sio binadamu !
Kasoro na udhaifu wa kwanza wa kile kilichowasilishwa kwenye bunge la Katiba ni kwamba yaliwasilishwa kwenye mazingira duni ambayo hayakuwa sahihi na muafaka kwa ajili ya watu kuwa na usikivu nauelewa wa kutosha, na kwa watu wanaofikiri kwa kutumia akili na sio kutumia nafsi na mioyo yao. Kushangilia, kelele, vigelegele, kunengua viuno hayakuwa mambo yanayowafanya watu wafikiri na kutafakari kama watu wazima na wenye akili zao, ijapo ndivyo wajumbe walivyokuwa wakitafadhalishwa kufanza;
Mwasilishaji alitumia muda mwingi kuwatia uoga na hofu zisizo na msingi Wajumbe na Watanzania kwa kitu ambacho kinakitia chama chake uoga na hofu, lakini sio Watanzania walio wengi;
Ufundi wa aina fulani ulitumika katika kukemea, kubeza na kudharau kazi iliyofanywa na Tume ya Jaji Warioba huku tume ikipakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Nina hakika baada ya uwasilishwaji huo wa Machi 21, ikiwa Jaji Warioba atapewa fursa na kwa jinsi ninavyomuelewa kwamba yeye amejiweka juu ya chama na anataka Tanzania iwe na nchi wabia wawe na katiba na sheria zilizo bora na zitakazozichukua hadi karne ijayo atazipangua moja baada ya nyengine;
Hotuba ya Machi 21, haikutoa lolote jipya na la maana kuhusu wasiwasi wa Watanzania juu ya maendeleo yao ya kiuchumi na kijamii bali kukinga na kuzibeau hoja za msingi za muundo na mfumo nchi unaostahili kuwa nao. Angalau baadhi ya wachunguzi wanasema hotuba hiyo ingegusia suala la Zanzibar kuwa kisiwa chenye eneo na idadi ya watu wakati mwingine ndogo kuliko ya baadhi kama sio mikoa yote Tanzania na jinsi gani mikoa hiyo nayo kama Zanzibar inaweza kusaidiwa na katba h iyo kuwa na miikoa huru yenye ushindani ndani yake na kati yake na mikoa mingine ingechangia angalau katlili katika mustakabali mzima wa kuwa na katiba mpya inayoweza kudumu kwa karne moja au zaidi. Wenzetu wa Kenya wao wamekuja na kitu kinaitwa UGATUZI pamoja na mtafaruku walio nao kuhusu ukabila na tofauti kati ya wlaionacho na wasio nacho. sisi viongozi wetu sio tu wamekaa kimya bali wanafanza jitihada za makusudi kulipotezea jambo hili kama vile halitakuwa na athari kubwa huko tunakokwenda hasa sasa ambapo mikoa mingine inakuwa na madini au gesi na mikoa mingine wanabakia kukavu na kutupu pasipo na mali asili ya aina yoyote ile ;
Ingawa wajumbe kupitia katikati ya hotuba iliyofumwa na kusukwa kiujanja kutoonesha dhahiri kile kinchotakiwa, ilifikia mahala ikashindwa kuficha dhamira na makusudio yake, nayo yakiwa sio mengine ila kuwadhulumu vijana wa Kitanzania haki yao ya kuwa na srikali yao nao wakapata fursa ya kujifunza uongozi wa nchi kama ilivyo kwa wenzao wa Zamzibar;
Hotuba hiyo kwa bahati mbaya ilifanza kazi ya kuyatotoisha (kufanza kitu kionekane ni cha kitoto ) baadhi ya mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba, ilhali inafahamika wazi ufinyu wa muda na rasilimali walizopewa na kwamba haiwezekani katika mazingira kama hayo kuwa na kitu kisicho na kasoro. Aidha, uono unaoona mambo mengine ni ya kitoto huwa haukubaliki na watu wengine, kwani hayo hayo yanayoonekana ya kitoto leo, kesho na kesho kutwa huja kubwa makubwa kama zimwi au jini anayeweza kuchukua saizi au ukubwa wowote autakao. Hakika ukiwa na sera inyowezesha baadhi ya wananchi kuwatandika viboko wananchi wenzao kama vile ni watoro wao unahitaji hata vitu hivi vidogovidogo pia kuwemo ndani ya katiba ambayo itamlinda mwanachi huyu anaayeweza wakati wowote kugeuzwa mtoto na wale walioko madarakani;
Aidha, hotuba hiyo ilionekana wakati mwengine pengine kwa nia ya kutaka kuficha kile kilicho hasa moyoni, lakini ikashindikana, kushughulikia hoja ndogo ndogo au hoja zisizostahili kujibiwa na kuacha kushughulikia hoja zilizostahili kujibiwa;
Risala hiyo ilitumika pia kuzuga kuhusu ukweli kwamba serikali ya Tanganyika na ile ya Zanzibar zilivyokuja madarakani kila mtu anajua nazo pia hazikuwa na vyanzo vyake vya fedha. Walikuwa katika sintofahamu na iliwapasa kuwaruaia watu wao, wakoloni na wakaarimu wengine ili kuweza kujikimu kwa muda, iweje pamoja na kuwa na kipindi cha mpito ei wanshirikisho la Tanzania washindwe kukaa na kuipatia serikali ya shirikisho njia zake za uhakika za kujiendeshea masuala yake bila hofu ya kushindwa kufanya hivyo,, kama sio nia na dhamira ya mtoa risala kuwakatisha tamaa wajumbe na wananchi juu ya kitu kinachoyumkiniika, ilimradi walioko madarakani wasitumie nafasi zao kukikwaza ? Kwa maneno mengine tukitaka kuwa na seikali ya shirikisho, serikali ya Tanganyika na serikali ya watu wa Zanzibar ni kitu sio tu kinachowezekana bali kinachotekekezeka na ambacho ndio dawa na tiba mujarabu ya kuondoa matatizo yote ya muungano sio kati yetu tu bali pia na kwa nchi nyengine zitakazotaka nazo kujiunga na shirikisho la Tanzania, Afrika Mashariki.
Hotuba hiyo pia ilitumika kuwatishia wajumbe na wananchi juu ya ujio wa serikali ya kijeshi na vimbwanga vyake eti kama watakubali kuwepo kwa serikali tatu, kitu ambacho hakina uhalisia wala mashiko yenye ithbati ya kutosha ila dhihirisho la uoga na hofu juu ya kitu ambacho tulio wengi hatujaambiwa na hivyo hatukijui.
Jeshi letu lilioundwa kwa kila hali mwaka 1964 ni jeshi lililojengwa kutambua kazi na wajibu wake tofauti na majeshi mengine Afrika. Yumkini wao ni mstari wa mbele zaidi kutokupenda vita kwa sababu wamevionja na wanajua madhara yake tofauti na sisi raia. Nina hakika wao watakuwa wa mwisho kwa sababu ya njaa ya siku moja au mbili kutaka kuingia madarakani kwani wanajua fika yaliyotokea katika nchi ambazo jeshi liliacha kazi yake na kuvamia kazi ya kutaka kutawala watu na nchi.
Hotuba hiyo ilionyesha pia jitihada kubwa ya kuelewa sarufi na sintaksia lakini ikashindwa kudadavua mantiki kaitka maudhui na kile ambacho kimeachwa ili kufupisha urefu wa rasimu na presentation zake kwa wakubwa wasio na muda wa kusikiliza kila kitu;
Imedhihirisha pia kushindwa kuelewa kwamba muundo na mfumo wa serikali leo una nyufa kadhaa zinazochangia kubebwa na kupendelewa kwa vijana wa upande mmoja wa nchi kiasi cha wao kujifunza jinsi ya kuwa mawaziri au hata rais, lakini upande wa Tanganyika ukanyimwa fursa ya namna hiyo;
Hotuba hiyo imeshindwa pia kuelewa kwamba mchakato wa kaiba sio sahihi kuchukuliwa kama kitu kinachojitegemea. Pakiwa na jicho linaloangalia tu kutoka juu na kuona yote yaliyo chini ingegundulika kwamba mengi ya yale yanayopendekezwa na rasimu yatachangia pia ajira zenye uhakika kwa vijana wetu na ubunifu wa mipango na mridadi mbalmbali amabyo itachangia kuifanya Tanzania ya kesho tofauti na ile ya jana;
Aidha, kiongozi mwasilishaji kudai kwamba serikali tatu zije baada ya yeye kuondoka madarakni ni TISHO na kukosa utii na uaminifu kwa wale waliomweka madarakani na kitendo kisichodhihirisha kama yeye kwa kweli anatutataka tufanye maamuzi huru au tufuate kile yeye na walio nyuma yake wanachotutaka sisi kukifata bila hiari yetu. Uamuzi huu unafanana na ule wa Jonasi au Yunusi alipotaka kuwakimbia watu wake akihofia na yeye kuwemo katika adhabu itakayowakuta watu wake.
Serikali imetumia busara kuwaalika wazee na watumishi wastaafu kushuhudia hotuba ya kihistoria na ya kishujaa iliyoshindwa vibaya kuwaimanisha Watanzania kwamba mfumo wa serikali mbili unaweza kukidhi mahitaji yao kwa miaka 50 au zaidi ijayo; lakini ilisahau kukumbuka kuwa Katibu mwenezi wa chama tawala alishasema kwamba wazee wameshapitwa na wakati na wanachokingojea ni kufa tu. Basi angalau, ingetumia fursa hiyo adhimu kuwaeleza wazee na wastaafu hao kwamba katiba inayoandaliwa siyo yao wao wala siyo kwa kiasi kikubwa ya watoto wao bali ni ya wajukuu, vitukuu, vilembwe na vitunguu vyao na wanapaswa kutazama jambo hilo kwa macho ya kizazi kijacho sio ya kizazi chao na huko walikotoka. Katiba inayoangalia nyuma zaidi badala ya kuangalia mbele zaidi ni katiba isiyounganisha wala kuleta uadilifu, unafuu na urahisi katika maisha ya watu kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni mtazamo na msimamo unaochangia sio haba kuendelea kufanza maisha ya watu yenye utata, dhiki, taabu na ambayo ni magumu kuishi-ka!





>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>



SEHEMU YA TATU

WAJUMBE NA HOJA ZA KUJENGA MAZINGIRA MUAFAKA KWA SERIKALI TATU

Waheshimiwa wajumbe na Watanzania wenzangu, kwanza ieleweke kuwa katiba tunayoitaka hatuidai au kuililia kwa saababu ya serikali mbili au tatu. Hilo ni jambo dogo na jepesi sana na lisilo na uzito wowote katika mustakabali wetu, tumeziona nchi ngapi katika miaka ya hivi karibuni zilizokuwa zimeungana kwa zaidiya miaka 50, 100 hadi mia mbili zikisambaratika fumba na kufumbua ?
Hatufanyi hesabu hapa ya wakubwa na gharama zitakazoongezeka hayo ni masuala madogo tu ya kiuendeshaji na kiutekelezaji. Tunachopaswa kukiangalia ni vipi matatizo na changamoto zilizopo mbele yetu zinaweza kukabiiwa kwa ufanifu na ufanisi zaidi huko tunakokwenda.
Rasimu inatueleza kwamba ijapo mfumo wa serikali mbili ulitufaa huko nyuma, huko tunakoelekea ni muundo wa srikali tatu ndio utakaokidhi vyema na barabara zaidi mahitaji yetu ya kimaendeleo yanyozidi kuongezeka siku hata siku.
Ingawa Jaji Warioba hakuwa na muda wa kuongelea baadhi ya vitu, lakini nadhani katika hazina yake ya makusanyo na majumuisho ya watu pia kutakuwepo nyufa na mianya kadhaa ya kiungozi na kiutendaji iliyobainika katika muundo wa serikali mbili.
Baadhi ya nyufa hizo ni pamoja na mikoa kushindwa kuwa na ushindani huru na uongezao tija na kipato ndani na nje ya mkoa na hivyo kuimarisha jamii na uchumi wao haraka zaidi;
Kuzuia kwa namna zote kuchanganya mambo ya chama na ya serikali katika ngazi zote nchini na serikali na chama tawala kukingia kifua mafisadi na wanaoiba fedha nchini na kwenda kuzificha nchi za nje.
Aidha, fedha, ardhi, maliasili na mali za umma za nchi kutokuwa na raia huru wa kukagua na kudhibiti ; misaada toka nje kutokuwa na raia wa kuilinda na kuzidhibiti na pia deni na mikopo ya taifa kutokuwa raia au watu mahsusi wa kuvilinda na kuidhibiti ili pasiwe na wizi au ufisadi ndani yake huku maliasili zinazogunguliwa katika vijiji na wilaya na mikoa fulani zikishindwa kuchangia kuwatoa watu wa maeneo hayo kutoka kwenye umasikini wa kupindukia.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> Aidha, serikali zilizopo kushindwa kudhibiti ufisadi na rushwa;
wanachama wa chama kimojakunufaika na fedha na mikopo nchini kwa njia zisizo sahihi na halali kulko wanachama wa vyama vingine na
vyama vya kisiasa kutumia mwanya wa kuwa madarakani kuiba au kula fedha za wananchi.
Vilevile makundi fulani katika jamii kutopendelewa kimaslahi na mengine kuonewa au kupunjwa haki zao za msingi; kutovisahau vijiji na kuvigeuza jehanamu hapa nchini kama ilivyo hivi sasa na hususan kwa kukosa misaada na nafuu kwa watoto, vijana na kina mama; wilaya na mikoa yenye viongozi kupendelewa na kuwezeshwa zaidi ya mikoa isiyo na viongozi wa kitaifa.
Watoto wa vigogo na vizito kuwa na nafasi na fursa zaidi ya kujitajirisha na kujiingiza kwenye siasa kiurahisi kupitia migongo ya mama na baba zao kuliko ya watoto wa maskini na wasio na kitu.
Aidha, vijana wa Kizanzibari kupata nafasi ya bure kusomea ubalozi, ukatibu mkuu, ukamishna, uwaziri na urais lakini sio wale wa Kitanganyika; Kuvitumia vyombo vya dola kwa namna ambayo wao wanapofanya uhalifu serikali iliyopo madarakani inafumbia macho uhalifu na uchafu wao ambayo ni aina fulani ya rushwa ya ksiiasa.
Watu wa tasnia na nasaba fulani kupewa vyeo nchini na sio watu wengine;miradi mbalimbali ya serikali kuvuja na fedha zake kuliwa na wanasiasa na watu fulani; benki kuu na baadhi ya mashirika ya umma kugeuzwa shamba la bibi na wanasiasa fulani fulani, Kutumia sharti la kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume katika kuongozi wa nchi ili kuorojesha na kuchakachua masuala muhimu ya kikatiba na kiuongozi;
kutumia kutokujua kwa wananchi kufanya maamuzi ambayo yanawagharimu wananchi na kuwachelewesha wananchi kimaendeleo na husun kimaeneo, kiuchumi na kijamii.
Ni dhahiri matatizo au changamoto hizo hapo juu, Jaji Warioba ameyaona na anayajua na angeweza kuyaeleza kwa marefu na mapana yake kuhalalisha mia kwa mia kukubalika kwa serikali tatu na wale watakaokwenda kupiga kura ya maoni, lakini hakupewa fursa kama hiyo.
Ni ushahidi wa kutosha pia kwamba serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne, katika mfumo wa serikali mbili, ilishindwa kutatua matatizo haya, je, hivi kweli tunatajia bila ya mabadiliko ya msingi tutaweza kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo katika miaka 50 ijayo kiurahisi kama tunavyohadaiwa sasa ? Ifikie mahala sote tuwe na kinaya cha kuhadaiwa na kuyakabili mambo kiume katika uhalisia wake na sio kwa matamanio na dhahnia tu!



SEHEMU YA IV:
SERIKALI TATU NI KITU KINACHOWEZEKANA NA ILI KUJENGA UMOJA NA AMANI YA KWELI HAIEPUKIKI....

UKIANGALIA historia iwe ni kwa wazawa wanaoingia madarakani kwa kupewa uhuru kwenye sahani au kwa kupindua serikali iliyopo kila mtu anarudi kwenye drawing board kuangalia ambayo jinsi serikali yake mpya inavyoweza kujikimu katika masuala mbalimbali.
Nyie wajumbe wa Bunge la katiba hii ndiyo kazi yenu kubwa, yaani, kuhakikisha kuwa serikali ya shirikisho kwa kuitumia katiba kama andiko la wananchi na sio la serikali iliyopo madarakani au chama fulani inaweka bayana njia mbalmbali za serikali ya shirikisho kuwa na njia za uhakika za mapato yake na kuhakikisha haitakwama bila sababu ya msingi katika mambo yake.
Kama nilivyotangulia kusema awali, mtu akitaka kumuua mbwa au paka wake anchotakiwa kukifanya ni kumpa jina baya mbwa au paka hiyo na watoto wa jirani watakusaidia kumuua. Kwa kuwa CCM haitaki serikali ya Tanganyika na serikali tatu, imeamua kutumia uzaini hapa pia kuonesha kwamba haiwezekani kwa serikali ya shirikisho kuwa na vyanzo vyake yenyewe vya mapato. Wapo watu wenye mawazo sahihi na bora zaidi na wakipewa nafasi ya kukaa na kuanga watakuja na njia mbalimbali ambazo serikali ya shirikisho au ya muungano itakuwa ikijipatia mapato yake kiurahisi, kiuhalali na kwa wakati.
Fedha zinazoibiwa kupitia miradi njaa iliyopo sasa hivi, matumizi ya viongozi kwenda safari za n je, fedha wanazolipwa spindocrots na serikali, matumizi ya matibavu ya viongozi na wasio vingozi nchi za nje, fedha zilizofichwa uswizi na kwingineko, mabilioni yaliyoibiwa benki kuu, mianya inayoachiwa wawekzaji na watu wa madhehebu fulani fulani zinatosha kwa kiasi kkikubwa kablsa kuianzishia serikali ya shirikisho hazina ya kuitosha kwak kuanzia kama pakiwa na dhamira ya kweli kufanza hivyo.
Kama serikali kuu iliyopo hivi sasa na zile za mitaa na mikoa zinavyogaiwa fedha, ndivyo viyo hivyo nyie wajumbe wa bunge la katiba mnvyotakiwa kulitia hili kwenye katiba ili serikali ya shirikisho moja kwa moja iwe inaingiza asilimia fulani itakayotokana na uchimbwaji gesi na mafuta katika serikali ya watu wa Tanganyika na Serikali ya watu wa Zanzibar; kiasi kingine kiingie kwa dhahabu na madini mengineyo yatakayopatikana ardhini na baharini katika nchi hizo; kiasi kingine kiingie kutokana na huduma za simu za mkononi katika nchi hizo; kiasi kingine kiingie kutokana na bishara ya utalii katika nchi hizo; kiasi kingine kiingie kutokana na biashara au huduma ya usafirishaji na uchukuzi katika nchi hizo; kiasi k ingine kiingie kutokana na uuzaji wa peteroli na bidhaa dada na kadhalika na kadhalika. Kinachonekana hapa ni dhahiri kuwa serikali ya shirikisho ina kila sababu ya kupewa na katiba mpya njia na mifereji ya kudumu ya kujipatia fedha zake kwa ajili ya kujiendesha bila kukwama hata siku moja. Na njia hizo hapo juu kama nilivyosema awali ni za kuwafungua macho tu wajumbe, lakini nina hakika kina Profesa LIpumba na wenzake waliowahi kupitia kwenye mabenki ikiwemo benki ya dunia wakipewa kazi hiyo kwa siku chache tu watadhihirishia wajumbe kama serikali ya shirikisho kuwa na vyanzo vyake vya uhakika vya mapato na kuwa imara kifedha kaitka kutimiza wajibu wake wote katika masula ya fedha kama vile kuwalipo polisi, zimaamoto, wanajeshi na wapambe wa viongozi ni kitu kinahcowezekana na tena hakina sababu kabisa ya kuitia nchi na watu wake wasiwasi.
ITAKUMBUKWA kwamab wakati Watanzania walikuwa wakitaka mabadiliko na kuwa na mfumo wa vyama vingi na siasa za ushindani, waliambiwa na wanasiasa hawa hawa wakongwe maneno hayo hayo wanayozungumza leo: " MKIKUBALI DEMOKRASIA NA MFUMO WA VYAMA VINGI, BASI OLE WENU NCHI LAZIMA ITAINGIA KWENYE VITA NA UMWAGAJI DAMU WA KUTISHA.' Wakatusakazia yaliyokitokea Yugoslavia ya zamani, Russia, Kongo, Burundi na Rwanda na kwingineko.
Inasikitisha pia kuona kwamba hata viongozi wa sasa wanathubutu kutumia uzaini ule ule waliotumia watangulizi wao: ' Eti wajumbe na wananchi wakikubali serikali tatu basi jeshi litaingilia kati, Wapemaba watafanyiwa hasidi na kufukuzwa Tanganyika na kadhalika na kadhalika. Viongozi muogopeni Mungu na nafsi zenu katika kauli zenu. Sisi tunaopenda tuwe na serikali tatu, yaani, serikali ya shirikisho. serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika hatuna tofauti kabisa na wazazi walioamua kuwarithisha watoto wao zawadi ya kitu kilicho bora kabisa. Iweje leo tunawaahidi watoto wetu zawadi kama hiyo na kisha tukabadilika ghafla bin vuu na kuwaletea kikombe cha SUMU ya hemlock wanywe ? Hakika asili na nia ya mtu huwezi kuijua hadi pale anapofungua kinywa chake. Watanzania tulio wengi kweli tu masikini na tusio na kitu na kwa hiyo pengine sisi sio watu machoni mwa watu. Ndio sababu leo hii tunataka wajumbe katika baraza la Katiba mpya waitumie fursa hiyo ili kuhakikisha kwamba sisi ambao baada ya kuporwa tulichokuwa nacho kwa siasa na sera za watawala waliokuwepo jana na leo, hatimaye wanaturudishia utu wetu kwa kutupa rasimu safi na bora ya katiba na sisi kuikubali ili na sisi kupiitia kaiba mpya pamojana kuwa sio watu kwa kuwa h atuna kitu, basi tuwe watu katika nchi yetu kwa sababu katiba hiyo itakuwa ni yetu na sio ya wlaioko madarakani.

Waheshimiwa wajumbe wa Bunge la Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi yenu sio tu ni ngumu na iliyopewa muda mfupi kuliko mnaohitaji, bali pia ni kazi ya wito, uokozi na ulinzi.
Wito kwa kuwa ni ya kujitolea na ambayo inahitaji kila mmoja wenu auvue ubinafsi na uchama wake na atangulize mbele Utanzania na Uafrika wake.
Ni kazi ya uokozi kwa sababu nchi yetu kwa miaka mingi imekuwa ikishi katika kudanganywa danganywa na kupewa ahadi za uongo, ilhali tuanjua fika kwamba siku ya mwisho tutaulizwa juu ya ahadi zote tulizozitoa kwa watu wetu. Tusahiihishe kosa hilo ili tusiendelee kuingia kwenye madhanbi zaidi na nchi yetu iwe na bahati ya kulaaniwa na Muumba. Tuibadili nchi hii ili iwe ya usema ukweli sikuzote kama vile nchi ilivyoanza wakati wa chama cha TANGANYIKA AFRIKCAN UNION cha Tanganyika.
Mungu awabariki nyote, na awasaidie katika siku zote kufanya kazi bila kuchoka au kufhafilika kwa kumtanguliza yeye mbele na kuamini yumo nanyi njia nzima toka mwanzo hadi mwisho na kwamba mtafanikiwa kwa mapenzi na ridhaa yake...
 
Back
Top Bottom