Kwako Rais wa awamu ya nne, mimi kama mtanzania ninasema nimekumisi sana. Japo katika uongozi wako kulikuwa na watendaji wa umma wezi wengi lakini ulijitahidi kuwakumbuka wananchi. Ulitoa ajira kwa wakati, watu walipandishwa madaraja na mishahara kuongezeka. Pia watu walipata uhamisho na biashara zilistawi.
Japo watu wengi hawakuwa wanalipa kodi ila pesa ilipatikana. Kiukweli unakumbukwa sana tu maana maisha tunayoishi sasa ni sawa na vishetani vidogodoka. Ajira hakuna sijui tatizo ni nini maana kodi zinalipwa na TRA wanakusanya mahela mengi hadi wanavuka kiwango.
Kwakweli siku hizi tunalia mitaani mkuu uliyemuachia anakamua maziwa hadi kwa ng'ombe tasa analazimisha kutoa maziwa. Baba JK salimia huko uliko maana huku uraiani tunalialia. Kama namba tumesoma hadi tumeanza kusoma alfabet sasa baada ya kumaliza namba.